Wazalendo waliodhulumiwa na serikali!!

kipumbwi

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
3,056
8,717
MZALENDO ALIYEDHULUMIWA KIWANDA AMEKUFA HAJAONA HAKI

NAKUMBUKA mwaka 1999. Mara ya kwanza naingia chumba cha habari. Business Times Ltd (BTL).

Newsroom yenye hadhi. Nilivutiwa na chumba kikubwa cha wachoraji. Kizuri sana, kiliundwa kwa vioo. Kila kijana mwenye kipaji cha kuchora, alipaona nyumbani.

BTL, nyumba ya magazeti ya Business Times, Majira, Spoti Starehe, Sanifu, Dar Leo na Maisha. Mamia ya Watanzaia waliajiriwa direct. Maelfu indirect.

Kila kitu kilianza na fikra zilizoishi mbele ya muda, za wazalendo Richard Nyaulawa na Rashidi Mbuguni. Hatimaye, wote sasa ni marehemu.

Nyakati sekta binafsi ikitafsiriwa kuwa mtoto wa haramu, Nyaulawa na Mbuguni walithubutu na waliibeba kwa ujasiri na mawazo yenye ujazo mkubwa.

Kampuni yao, Business Care Limited (BCS), ikazaa BTL, iliyosajili na kuchapa gazeti la kwanza binafsi Tanzania, Business Times. Mwaka 1989.

Wakati wowote, historia ya vyombo vya habari binafsi Tanzania ikiandikwa, majina ya Nyaulawa na Mbuguni, yanastahili wino wa dhahabu.

Gazeti la Business Times, lilizaa Majira mwaka 1992. Baada ya hapo, magazeti zaidi ya kampuni binafsi yalizaliwa, kisha redio na televisheni. BTL ya Nyaulawa na Mbuguni, ilifungua njia.

Nyaulawa na Mbuguni, walianzisha kampuni ya uchapaji ya Business Printers Limited (BPL). Kiwanda cha BPL kilikuza mno tasnia ya habari.

BPL, haikuchapa magazeti ya BTL pekee, bali yote ya kampuni binafsi wakati huo. Vilevile vitabu, majarida na machapisho mbalimbali. Nyaulawa na Mbuguni ni wazazi na walezi wa kila gazeti lililozaliwa miaka ya 1990.

Uchaguzi Mkuu 1995, Nyaulawa na Mbuguni, waliandaa mdahalo wa kihistoria wa wagombea urais. Tukio hilo halijawahi kujirudia nchini.

Nyaulawa na Mbuguni ni Watanzania wa kwanza kuonesha kuwa sekta binafsi inaweza kushirikiana na Serikali, kutatua changamoto za wananchi.

Kupitia BCS, walianzisha miradi ya kushughulikia kero za maji, mikoa mbalimbali nchini. Baadaye, kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (Sida), Nyaulawa na Mbuguni, waliendesha Mpango wa Afya kupitia Maji Salama (Hesawa) kwa zaidi ya miaka 10.

Kupitia Hesawa, Nyaulawa na Mbuguni, waliwezesha Watanzania zaidi ya milioni tano wa vijijini, hususan Kanda ya Ziwa, kupata maji safi na salama.

Nyaulawa na Mbuguni, walijenga hamasa ya mtaji kwa Watanzania, na wakashawishi wachache kutoka nje, wakaanzisha Benki ya Biashara ya Akiba – Akiba Commercial Bank (ACB), mwaka 1997.

Desemba 1998, Nyaulawa na Mbuguni, walifanikisha kuileta Tanzania, taasisi ya kimataifa ya Junior Achievement Worldwide, yenye makao yake makuu, Colorado, Marekani.

Junior Achievement (AJ), hufundisha vijana elimu ya biashara na uwekezaji. Tangu kuwasili Tanzania, AJ imetengeneza maelfu ya vijana kuwa wafanyabiashara stadi.

Vicoba ni maarufu hivi sasa. Asili yake ni Vibindo. Nyaulawa na Mbuguni, walianzisha Vibindo mwaka 2002, kuwezesha Watanzania kuweka, kukopa na kusaidiana katika vikundi. Vibindo ndio sasa Vicoba.

Nyaulawa na Mbuguni ni waasisi wa Taasisi ya Utafiti na Kuondoa Umaskini (Repoa), ambayo tafiti zake zimekuwa mwanga kwa Serikali, Bunge na taasisi za kimataifa, katika kukabili umaskini Tanzania.

Mwaka 1990, Nyaulawa na Mbuguni, waliratibu mafunzo ya kilimo cha mwani (seaweed) kwa mara ya kwanza, kwa akina mama wa Zanzibar. Wataalamu hao walitoka Ufilipino.

Hivi sasa, mwani inashika nafasi ya tatu Tanzania kwa usafirishwaji nje ya nchi, ni namba tatu kwa mapato Zanzibar, na inachukua hadi asilimia 90 ya huduma za usafiri wa maji Zanzibar kwenda nje.

Nyaulawa na Mbuguni ndio waasisi wa biashara za kutembeza mkononi, yaani umachinga. Waliasisi hilo kupitia kuuza magazeti mikononi. Wakawa na mtandao wa vijana waliozunguka Dar es Salaam. Mtindo huo ukaitikiwa kwa ukubwa. Hivi sasa, mtindo huo umekuwa mtandao mpana wa ajira.

Kwa tafsiri yoyote, Nyaulawa na Mbuguni ni wazalendo wa nchi. Ni nuru ya sekta binafsi. Mageuzi ya ujamaa hadi uchumi wa soko, yana kurasa nyingi za Nyaulawa na Mbuguni. Bila swali, Nyaulawa na Mbuguni ni historia ya Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, amewahi kunieleza kuwa partnership ya Nyaulawa na Mbuguni haina mfanowe Tanzania. Walifanya mengi kibiashara na kwa nchi, kwa upacha wa hali ya juu.

Mzalendo Nyaulawa alifariki dunia mwaka 2008, akamwacha Mzalendo Mbuguni, akiendeleza waliyoyaanzisha pamoja.

Mwaka 2016, BPL chini ya Mbuguni, ilichukua mkopo benki za NMB na ECO. Fedha hizo zilitumika kununua mitambo na kufanya uwekezaji mkubwa kwenye kiwanda chake cha uchapaji. Kiwanda kikawa kipya kabisa.

Mwaka 2017, task force ya Rais wa Tano, Dk John Magufuli, ilivamia BPL. Wamiliki waliondolewa. Kiwanda kikawa chini ya usimamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kuanzia hapo, magazeti ya CCM, Uhuru, Mzalendo na Burudani, ya Serikali, Daily News, Sunday News na Habari Leo, kwa nyakati tofauti, yalichapwa bure BPL.

Magazeti mengine, Tanzanite, Fahari Yetu, La Jiji, Tanzania Perspective, The Echo, Observer na mengine mengi, yaliyoitwa ya kimkakati, yalichapwa bure BPL.

Kura za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020, zilichapwa BPL.

Wakati yote yakifanyika, Mbuguni na familia ya Nyaulawa, walipitishwa kwenye moto unaounguza. Mali zao, ikiwemo nyumba, kupigwa minada. Presha kubwa ya mikopo ya NMB na ECO.

Haitoshi, task force ya Magufuli, ilimtishia Mbuguni kumfungulia mashitaka ya uhujumu uchumi, vinginevyo alipe mamilioni kwa kushirikiana na familia ya Nyaulawa.

Kwa hofu ya kesi ya uhujumu uchumi, walikubali kulipa kwa awamu. Ajabu, wakaelekezwa kulipa benki kwenye akaunti ya mtu binafsi. Na wakalipa.

Nilimshuhudia Mbuguni akiwa kwenye mahangaiko, akipigania kiwanda chake. Panda shuka bila mafanikio.

Julai 15, 2023, Mzalendo Mbuguni, aliitikia wa wito wa mauti. Naam, kila nafsi itaonja mauti.

Mbuguni amefariki dunia akiwa bado anasotea haki yake. Kiwanda chake ambacho hakurudishiwa tangu kilipoporwa mwaka 2017.

Mtanzania aliyetenda mengi kwa nchi. Aliyebadili maisha ya maelfu kupitia mipango na ajira za moja kwa moja, nyakati za mwisho za uhai wake, zilijaa maumivu makali kwa sababu ya dhuluma. Amekufa maskini na mufilisi.

Julai 17, 2023 Mzalendo Mbuguni amezikwa makaburi ya Kisutu. Sala ya maiti, imefanyika Msikiti wa Maamur, Upanga, Dar es Salaam.

Sisi Sote ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake Tutarejea.

Ndimi Luqman MALOTO
 
Kumbe zile kura za uchafuzi wa 2020 zilichapwa baada ya kiwanda kutekwa na majambazi, mwanzo nilidhani mwenye kiwanda alishirikiana na majambazi kufanya ule uharamia wao.

Na yale magazeti ya kina Musiba nayo yakawa yanachapwa bure baada ya kiwanda kutekwa na majambazi pia, nikadhani wale majambazi kwasababu walikuwa na pesa za utapeli za Plea Bargain walikuwa wanalipia ile huduma..

Kumbe pesa za Plea Bargain wanachukua wanakula, na wakienda kwenye huduma napo wanachukua huduma bure, kama ambavyo Sabaya alikuwa akifanya kule Kaskazini, mpaka kula bure kwenye hoteli za watu, nguo madukani, mpaka wake za watu..

Aisee, tulitawaliwa na majambazi mpaka 2021, baada ya hapo amechukua usukani msaliti, aliyetugeuza watumwa ndani ya mipaka ya nchi yetu, watanganyika tunaishi kwa mitihani kila siku chini ya utawala wa CCM.

RIP Mbuguni.
 
Kumbe zile kura za uchafuzi wa 2020 zilichapwa baada ya kiwanda kutekwa na majambazi, mwanzo nilidhani mwenye kieanda alishirikiana na majambazi kufanya ule uharamia wao.

RIP Mbuguni.

Nami nilikua nikishangaa kuna magazeti ya propaganda ya CCM na serikali ambayo hayauzi hata nakala 100 kwa nchi nzima na bado kila siku yapo kwenye meza za wauzaji!!

Kumbe yanachapwa bure na kusambazwa bure,naamini pia kua wachuuzi wa magazeti huwa wanalipwa na dola kwa ajili ya kuyapokea kila siku na kuyaweka ubaoni ili yaonekane!!

Magazeti kama Machinga,Jamvi,Tanzanite na ndugu zake kibao,haachukuliwi hata kwenye kufungia vitafunio,yamejaa najisi ya propganda!!
 
MZALENDO ALIYEDHULUMIWA KIWANDA AMEKUFA HAJAONA HAKI

NAKUMBUKA mwaka 1999. Mara ya kwanza naingia chumba cha habari. Business Times Ltd (BTL).

Newsroom yenye hadhi. Nilivutiwa na chumba kikubwa cha wachoraji. Kizuri sana, kiliundwa kwa vioo. Kila kijana mwenye kipaji cha kuchora, alipaona nyumbani.

BTL, nyumba ya magazeti ya Business Times, Majira, Spoti Starehe, Sanifu, Dar Leo na Maisha. Mamia ya Watanzaia waliajiriwa direct. Maelfu indirect.

Kila kitu kilianza na fikra zilizoishi mbele ya muda, za wazalendo Richard Nyaulawa na Rashidi Mbuguni. Hatimaye, wote sasa ni marehemu.

Nyakati sekta binafsi ikitafsiriwa kuwa mtoto wa haramu, Nyaulawa na Mbuguni walithubutu na waliibeba kwa ujasiri na mawazo yenye ujazo mkubwa.

Kampuni yao, Business Care Limited (BCS), ikazaa BTL, iliyosajili na kuchapa gazeti la kwanza binafsi Tanzania, Business Times. Mwaka 1989.

Wakati wowote, historia ya vyombo vya habari binafsi Tanzania ikiandikwa, majina ya Nyaulawa na Mbuguni, yanastahili wino wa dhahabu.

Gazeti la Business Times, lilizaa Majira mwaka 1992. Baada ya hapo, magazeti zaidi ya kampuni binafsi yalizaliwa, kisha redio na televisheni. BTL ya Nyaulawa na Mbuguni, ilifungua njia.

Nyaulawa na Mbuguni, walianzisha kampuni ya uchapaji ya Business Printers Limited (BPL). Kiwanda cha BPL kilikuza mno tasnia ya habari.

BPL, haikuchapa magazeti ya BTL pekee, bali yote ya kampuni binafsi wakati huo. Vilevile vitabu, majarida na machapisho mbalimbali. Nyaulawa na Mbuguni ni wazazi na walezi wa kila gazeti lililozaliwa miaka ya 1990.

Uchaguzi Mkuu 1995, Nyaulawa na Mbuguni, waliandaa mdahalo wa kihistoria wa wagombea urais. Tukio hilo halijawahi kujirudia nchini.

Nyaulawa na Mbuguni ni Watanzania wa kwanza kuonesha kuwa sekta binafsi inaweza kushirikiana na Serikali, kutatua changamoto za wananchi.

Kupitia BCS, walianzisha miradi ya kushughulikia kero za maji, mikoa mbalimbali nchini. Baadaye, kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (Sida), Nyaulawa na Mbuguni, waliendesha Mpango wa Afya kupitia Maji Salama (Hesawa) kwa zaidi ya miaka 10.

Kupitia Hesawa, Nyaulawa na Mbuguni, waliwezesha Watanzania zaidi ya milioni tano wa vijijini, hususan Kanda ya Ziwa, kupata maji safi na salama.

Nyaulawa na Mbuguni, walijenga hamasa ya mtaji kwa Watanzania, na wakashawishi wachache kutoka nje, wakaanzisha Benki ya Biashara ya Akiba – Akiba Commercial Bank (ACB), mwaka 1997.

Desemba 1998, Nyaulawa na Mbuguni, walifanikisha kuileta Tanzania, taasisi ya kimataifa ya Junior Achievement Worldwide, yenye makao yake makuu, Colorado, Marekani.

Junior Achievement (AJ), hufundisha vijana elimu ya biashara na uwekezaji. Tangu kuwasili Tanzania, AJ imetengeneza maelfu ya vijana kuwa wafanyabiashara stadi.

Vicoba ni maarufu hivi sasa. Asili yake ni Vibindo. Nyaulawa na Mbuguni, walianzisha Vibindo mwaka 2002, kuwezesha Watanzania kuweka, kukopa na kusaidiana katika vikundi. Vibindo ndio sasa Vicoba.

Nyaulawa na Mbuguni ni waasisi wa Taasisi ya Utafiti na Kuondoa Umaskini (Repoa), ambayo tafiti zake zimekuwa mwanga kwa Serikali, Bunge na taasisi za kimataifa, katika kukabili umaskini Tanzania.

Mwaka 1990, Nyaulawa na Mbuguni, waliratibu mafunzo ya kilimo cha mwani (seaweed) kwa mara ya kwanza, kwa akina mama wa Zanzibar. Wataalamu hao walitoka Ufilipino.

Hivi sasa, mwani inashika nafasi ya tatu Tanzania kwa usafirishwaji nje ya nchi, ni namba tatu kwa mapato Zanzibar, na inachukua hadi asilimia 90 ya huduma za usafiri wa maji Zanzibar kwenda nje.

Nyaulawa na Mbuguni ndio waasisi wa biashara za kutembeza mkononi, yaani umachinga. Waliasisi hilo kupitia kuuza magazeti mikononi. Wakawa na mtandao wa vijana waliozunguka Dar es Salaam. Mtindo huo ukaitikiwa kwa ukubwa. Hivi sasa, mtindo huo umekuwa mtandao mpana wa ajira.

Kwa tafsiri yoyote, Nyaulawa na Mbuguni ni wazalendo wa nchi. Ni nuru ya sekta binafsi. Mageuzi ya ujamaa hadi uchumi wa soko, yana kurasa nyingi za Nyaulawa na Mbuguni. Bila swali, Nyaulawa na Mbuguni ni historia ya Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, amewahi kunieleza kuwa partnership ya Nyaulawa na Mbuguni haina mfanowe Tanzania. Walifanya mengi kibiashara na kwa nchi, kwa upacha wa hali ya juu.

Mzalendo Nyaulawa alifariki dunia mwaka 2008, akamwacha Mzalendo Mbuguni, akiendeleza waliyoyaanzisha pamoja.

Mwaka 2016, BPL chini ya Mbuguni, ilichukua mkopo benki za NMB na ECO. Fedha hizo zilitumika kununua mitambo na kufanya uwekezaji mkubwa kwenye kiwanda chake cha uchapaji. Kiwanda kikawa kipya kabisa.

Mwaka 2017, task force ya Rais wa Tano, Dk John Magufuli, ilivamia BPL. Wamiliki waliondolewa. Kiwanda kikawa chini ya usimamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kuanzia hapo, magazeti ya CCM, Uhuru, Mzalendo na Burudani, ya Serikali, Daily News, Sunday News na Habari Leo, kwa nyakati tofauti, yalichapwa bure BPL.

Magazeti mengine, Tanzanite, Fahari Yetu, La Jiji, Tanzania Perspective, The Echo, Observer na mengine mengi, yaliyoitwa ya kimkakati, yalichapwa bure BPL.

Kura za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020, zilichapwa BPL.

Wakati yote yakifanyika, Mbuguni na familia ya Nyaulawa, walipitishwa kwenye moto unaounguza. Mali zao, ikiwemo nyumba, kupigwa minada. Presha kubwa ya mikopo ya NMB na ECO.

Haitoshi, task force ya Magufuli, ilimtishia Mbuguni kumfungulia mashitaka ya uhujumu uchumi, vinginevyo alipe mamilioni kwa kushirikiana na familia ya Nyaulawa.

Kwa hofu ya kesi ya uhujumu uchumi, walikubali kulipa kwa awamu. Ajabu, wakaelekezwa kulipa benki kwenye akaunti ya mtu binafsi. Na wakalipa.

Nilimshuhudia Mbuguni akiwa kwenye mahangaiko, akipigania kiwanda chake. Panda shuka bila mafanikio.

Julai 15, 2023, Mzalendo Mbuguni, aliitikia wa wito wa mauti. Naam, kila nafsi itaonja mauti.

Mbuguni amefariki dunia akiwa bado anasotea haki yake. Kiwanda chake ambacho hakurudishiwa tangu kilipoporwa mwaka 2017.

Mtanzania aliyetenda mengi kwa nchi. Aliyebadili maisha ya maelfu kupitia mipango na ajira za moja kwa moja, nyakati za mwisho za uhai wake, zilijaa maumivu makali kwa sababu ya dhuluma. Amekufa maskini na mufilisi.

Julai 17, 2023 Mzalendo Mbuguni amezikwa makaburi ya Kisutu. Sala ya maiti, imefanyika Msikiti wa Maamur, Upanga, Dar es Salaam.

Sisi Sote ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake Tutarejea.

Ndimi Luqman MALOTO
Naomba lijamaa huko lilipo life Tena...then ligeuke Kuni za kuwachoma wenzake waliopo huku
 
Dah….
At least nimepata history ya Mbuguni
Nilikuwa namsikia kuna sehemu ka play part kubwa but Nilikuwa Simjui
Thanks… Ila yupo ataendelea kuishi
 
Kama ilivyo kwake yeye umemnasibu kwa mema yake na mabaya yake umeyaacha ndo ivo ivo na hayati pia tutamkumbuka kwa mazuri yake na mabaya yake tutamwachia mwenyewe, kwenye kila kisa kuna mengi nyuma ya pazia ambayo mimi na wewe hatufahamu.
 
REST IN PEACE RASHID MBUGHUNI . Nilifanya nae kazi miaka 6 toka 1999 nikiwa Private Sector Initiative na Juniour Achievement alikuwa kama chairman wa Board. Alinifundisha vitu vingi sana. He was my mentor kwakweli.
 
Kumbe this is things ended??? Mbuguni iliwahi kusoma makala yake [inayomhusu yeye] and I was real astonished na kuvutiwa na UZALENDO wake...

Sikuwahi kujua kumbe mambo yalikuwa hivi...
 
the Best people never die,..
since their IDEAS lives forever,..
once killed,live..and once die, lives forever..
GOD BE WITH THEM....
 
Dhuluma nchi hii kamwe haita iacha nchi salama

Wananchi wa Dodoma Nkuhungu broad acre ,Matuli na Mbwanga wanadhulumiwa wazi wazi naJiji la Dodoma kupitia mabadiliko ya matumizi yaeneó uliona wapi Eneo lililokuwa limepangiwa matumizi na hati kutolewa linakatwa asilimia 30 wakati mh Raisi katoa pesa za mipango mijl hiyo asilimia 30 CAG ataona wapi?
Wizimtupu wamepandikiza Eneo limevamiwa kwaniSheria hazipo
 
Kama ilivyo kwake yeye umemnasibu kwa mema yake na mabaya yake umeyaacha ndo ivo ivo na hayati pia tutamkumbuka kwa mazuri yake na mabaya yake tutamwachia mwenyewe, kwenye kila kisa kuna mengi nyuma ya pazia ambayo mimi na wewe hatufahamu.

Hakuna asiefahamu kua mwendazake zake alikua ni evil like 😈!!
 
Back
Top Bottom