Watumishi wa umma Zanzibar wapata nauli, wale wa muungano hali ya uchumi haijatulia

Retina

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
1,039
1,156
Yawezekana watanganyika wananyonywa hasa na wazanzibar, watumishi wa umma wa muungano wanailisha zanzibar, juhudi zao za kazi, maarifa na jasho linalovuja sio kwa ajili yao tu bali hata kwa watanganyika.

Mikopo inayokopwa na wakuu wa muungano sio kwa watanganyika tu bali hata kwa wazanzibar lakini walipaji ni watanganyika kupitia TRA iliyopo upande wa muungano.

Ukitafakari sana unaona bora kungekuwa na serikali tatu.Inawezekanaje watumishi wa umma wa Zanzibar waongezewe mshahara kila mwaka japo mwaka huu wamesema nauli,ina maana uchumi wao uko juu, hali ambaya watumishi wa umma wa Tanganyika kupitia muamvuli wa muungano,wakubwa wanasema wataongezwa hadi uchumi utulie, hawahawa wafanyakazi ndio wanailisha Zanzibar, inakuwaje serikali ya muungano imelemewa na kuilisha Zanzibar na watanganyika.

Nilitegemea Wafanyakazi wa Tanganyika chini muungano wangelipwa vizuri zaidi kuliko wale wa Zanzibar.
 
Back
Top Bottom