sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,486
Tangu mwezi wa tano lilipotolewa tangazo la kusitisha nyongeza yoyote kwenye mishahara ya Watumishi wa Serikalini, Watumishi hao ambao matarajio yao waliyojiwekea katika mwaka mpya wa fedha kutegemea nyongeza katika mishahara yao yamekuwa tofauti na kujikuta kukopa kwenye mabenki ili kukidhi matarajio hayo.
Benki nyingi za NMB, CRDB, NBC wakopaji ambao ni Watumishi wa Serikali wameongezeka wakiwemo wapya pamoja na wenye mikopo kuongeza mikopo.
Serikali inapaswa kuangalia upya suala la Watumishi wake kwani watumishi hao kukaa kimya na kwenda mabenki kukopa ili wasogeze siku ni kujiongezea mzigo wa ugumu wa maisha kwani hizo walizokopa zitakapoishi huku kwenye mabenki makato ni makubwa, itapelekea kudorora zaidi katika utoaji wa huduma endapo tarajio la kuboreshwa kwa mishahara halitakuwa limezingatiwa.
Hili siyo suala la kiitikadi wala chama fulani. Tutizame hatari ya huko mbele. Watumishi kujitokeza kwa wingi kwenye mabenki kukopa, ni neema kwa wenye mabenki ila ni hatari kwa mwajiri kwani mwajiri atalazimika kumwongezea kipato chake maradufu kufidia na makato ya benki maana mwajiri ndiye mdhamini wa mkopo huo, vinginevyo mkopaji atashindwa kutimiza wajibu wake kutokana na ukata wa maisha.
Nawasilisha Baba.