Watumishi KCMC wahojiwa na Polisi kwa kudai Posho zao mtandaoni

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro, kitengo cha makosa ya kimtandao, linawahoji wafanyakazi kadhaa wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC ya mjini Moshi kwa tuhuma za makosa mbalimbali ya kimtandao.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Simon Maigwa ambaye yuko safarini kikazi nje ya mkoa, alipoulizwa juzi alithibitisha kuwapo kwa uchunguzi, lakini hawezi kutoa taarifa za uchunguzi huo kwa sasa.

“Niko nje ya mkoa, lakini hata hivyo unatoaje taarifa ambayo uchunguzi wake unaendelea na bado kukamilika?” alisema Kamanda Maigwa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) aliomtumia mwandishi wetu kwa njia ya Whatsapp.

Taarifa za baadhi ya wale wanaotajwa kuhojiwa au kutafutwa na polisi kwa ajili ya mahojiano hayo, zinadai kiini cha tatizo hilo kilianzia kwa wafanyakazi wanaodai posho ya kufanya kazi saa za ziada, ambayo ni malimbikizo ya miezi mitatu.

“Ila jambo lipo hivi hapa KCMC sisi wafanyakazi hatulipwi hela zetu za overtime (saa za ziada) na hela ya bima kwa wakati. Jambo hili likatulazimu kufungua space huku Twitter mara kadhaa na kuwasema hospitali ili watulipe stahiki zetu”

“Hili limefanya wao wanaona yanayoendelea juu ya hospitali yao ikawauma na kuanza kuwatumia mapolisi kuanza kutafuta na kuhoji ni akina nani walioanzisha jambo hili huku mitandaoni,”unaeleza ujumbe wa mmoja wa wafanyakazi hao.Alipotafutwa na gazeti hili jana, Ofisa Uhusiano wa hospitali hiyo, Gabriel Chisseo alikiri kuwa na taarifa ya baadhi ya wafanyakazi kuhojiwa na polisi kwa matendo, ambayo alisema hayahusiani na madai yao, na kwamba madai yao yanashughulikiwa.

“Ni kweli kuna ambao wanadai malimbikizo ya malipo ya hizo posho unazosema na sisi tulishalipa hadi mwezi Juni, kwa hiyo wanadai kama miezi mitatu hivi na tumeshakaa nao kama mara mbili tukawaeleza hali halisi.Hebu wewe (mwandishi) nikuulize hivi tuseme unanidai Sh100,000 na nimepitisha siku za kukulipa inakupa haki ya kuingia mitandaoni na kunitukana?alihoji.

"kuzusha tuhuma za uongo mitandaoni?Kunahalalisha kutenda kosa la jinai”alihoji.

Mbali zaidi unaitiasha mgomo,unataka watu wasiende ibada mbali zaidi unatukana na kudhalilisha utu wa mtu na familia yake sidhani kama hili ni sawa na ukumbuke unaitisha mgomo nje ya utaratibu wa vyama vya wafanyakazi

Chisseo alisema anachofahamu, polisi wanachunguza tuhuma za jinai za baadhi ya wafanyakazi walizozitenda kwa kutumia majina bandia huko kwenye mitandao ya kijamii na hakuna hata mmoja aliyeshikiliwa bali walihojiwa na kurejea kazini.

Sheria ya makosa ya kimtandao ya 2015 kifungu cha 16, kinasema ni kosa kwa mtu kuchapisha katika wa mfumo wa kompyuta ambayo ni ya uongo, udanganyifu, kupotosha au isio sahihi kwa nia kukashifu, kutishia, dhuluma, matusi, kudanganya au kupotosha umma.

Chini ya sheria hiyo, mtu anapotiwa hatiani na mahakama, atatozwa faini isiyopungua Sh5 milioni au kifungo kisichopungua miaka mitatu jela au hadi anaweza kuhukumiwa adhabu zote hizo mbili kwa wakati mmoja.

MWANANCHI
 
Sasa hivi kuna trend kubwa sana ya kutumia vyombo vya dola ku-silence madai ya wafanyakazi, which is totally unfair. Kwan vyombo vya dola havina miongozo yao ili kukwepa politics za makazini?

Mtumishi akinunua tu kagari, kesho takukuru na polisi hao hapo, Je, lengo ni kujua staffs wanavaa chupi au boksa zipi? Manake katika chunguzi nyingi hamna cha maana wanachogundua

Proper channels must be adhered.
 
Back
Top Bottom