KCMC na TPC waungana kutoa huduma za kitabibu

Jun 20, 2023
55
52
MADAKTARI BINGWA KCMC KUTUOA HUDUMA ZA KIBINGWA HOSPITAL YA TPC

Moshi.

Hospital yenye hadhi ya nyota nne inayomilikiwa na kiwanda cha Sukari cha TPC,ipo katika hatua za mwisho kukamilisha mchakato wa kuingia makubaliano ya ushirikiano na Hospital ya Rufaa ya KCMC kwa ajili ya kutumia madaktari wake bingwa na wanafunzi wa shahada ya pili ya udaktari ,shahada ya uuguzi kwa ajili ya kutoa huduma katika hospital hiyo.

Mpango huo utaiwezesha hospital hiyo kubwa inayohudumia aslimia kubwa ya wananchi wanaoishi kuzunguka kiwanda hicho na maeneo jirani hasa wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara,kutoa huduma za kitabibu za kiwango cha juu .

Mpango huo umetangazwa hivi karibuni na meneja wa Hospital hiyo,Razaro Urio katika hafla fupi ya uzinduzi wa jengo la kisasa la huduma kwa wagonjwa wan je(OPD) uliofanywa na mkuu wa wilaya ya Moshi,Kisare Makore hivi karibuni.

Katika taarifa yake kwa mkuu huyo wa wilaya,meneja huyo amesema kuwa,TPC wametumia kiasi cha zaidi ya Bilioni moja kwa ajili ya upanuzi wa Hospital hiyo pamoja na ukarabati wa majengo ikiwa ni mkakati wa kampuni hiyo kuboresha Huduma za afya kwa Wananchi wanaoishi kuzunguka kiwanda hicho.

Amesema kiasi hicho cha pesa pia kimetumika katika kujenga majengo mapya,kuboresha yaliyopo,kununua vifaa tiba pamoja na vya kutolea Huduma ikiwamo ujenzi wa wodi ya daraja la kwanza,wodi maalumu kwa ajili ya magonjwa ambukizi pamoja na jengo la mama na mtoto.

Mengine ni kuboresha wodi zote ikiwamo wodi ya kina mama,wodi ya wanaume,wodi ya watoto pamoja na kununua vifaa muhimu vya kutolea Huduma ikiwamo gari la wagonjwa,mashine kwa ajili ya chumba cha upasuaji.Utra Sound machine,kiti cha Huduma ya meno, kuongeza wataalamu wa tiba bobevu na kuboresha jengo hilo la OPD,

Meneja huyo amesema kuwa,TPC pia imefadhili ujenzi wa zahanati tano katika vijiji vya Mserekia,Loondoto,Mawala,Kiyungi,Chemchem na kuboresha zahanati ya ya kijiji cha mikocheni ikiwa ni mkakati wa kiwanda hicho kufikisha Huduma kwenye vijiji vilivyopo mbali na TPC.

Katika hatua nyingine uongozi wa kiwanda hicho umefungua milango kwa wakandarasi wake kutumia Hospital hiyo kutibu watumishi wao kwa kutumia fao la SHIB lililopo mfuko wa Hifadhi ya Jamii(NSSF)mpango utakaowezesha wananchi zaidi ya 4,500 kupata huduma katika Hospital hiyo.

Akizindua jengo hilo,mkuu wa wilaya ya Moshi, Kisare Makore alipongeza juhudi kubwa zinazofanywa na kiwanda hicho kwenye nyanja mbali mbali ikiwamo Huduma za afya kwa jamii inayozunguka kiwanda hicho .

Alisema serikali inathamini mchango unaotolewa na sekta binafsi katika kuwahudumia Wananchi na kwamba suala la afya ni moja ya kipaumbele kwa serikali na kusisitiza serikali itaendelea kutoa ushirikiano hasa katika suala la afya na maeneo mengine.

Amesema serikali kwa kutambua umhimu wa suala la afya katika mwaka wa fedha 2023/2024 imetoa bilioni 1.8 kwa ajili ya upanuzi na ukarabati wa Hospital ya wilaya iliyopo kata ya mabogini,shilingi milioni 870 kwa ajili ya uboreshaji wa huduma kituo cha afya cha Uru kusini,milioni 500 kituo cha afya Kahe na Milioni 500 zimeenda kituo cha afya Marangu.

Hospital hiyo inahudumia,wafanyakazi wa kiwanda cha sukari, wananchi wanaoishi kuzunguka kiwanda hicho pamoja na maeneo ya Msitu wa tembo wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara na baadhi ya maeneo ya Nyumba ya Mungu wilaya ya Mwanga.

Mbali na kuwekeza kwenye sekta ya afya, kiwandahicho cha sukari cha TPC pia kimekuwa kikitoa ufadhi kwenye Nyanja ya elimu kwak ukarabati majengo ya zamani na kujenga mapya kuanzia shule ya awali,msingi hadi sekondari kwenye vijiji vilivyopo ndani ya eneo la kiwanda hicho na maeneo ya jirani.

MWISHO.
 
Back
Top Bottom