Chukwu emeka
JF-Expert Member
- Jan 12, 2018
- 23,443
- 36,664
Enzi za kadi RTD ......wakaweka kabisa live stand ya mkoa.......Bokoman Mkongoman,Wajadi fundi wajadi, binadamu mashaka 🤣🤣🤣Miaka imesonga sana, maisha yamebadilika Kwa kiasi kikubwa.Tofauti na sasa ambapo ukiwa na simu janja au tarakirishi unapata taarifa zote zilizotokea na zilizovunjika 'breaking news' , Zamani redio ilikuwa chombo muhimu ktk kupata taarifa na burudani
Leo nimewakumbuka wale watuma salamu maarufu enzi zile,ingawa hata sasa wapo baadhi ya watu ambao ni maarufu ktk vipindi mbalimbali ukisikiliza redio km clouds mfano kuna heri dereva babaji,shangwe dereva babaji, Daudi wakota nk
Enzi hizo ukisikiliza kipindi cha mirindimo asilia na Malima Nderema au salamu Kwa wagonjwa,kuna majina maarufu huwezi kuacha kuyasikia wakati wa kutuma salamu
Kuna huyu jamaa wa kuitwa Wajadi fundi Wajadi binadamu mashaka,yeye kila siku yupo safarini kuelekea mahuta shimoni,fundi Khamisi full migebuka wa mwandiga fashion sokoni kigoma
Lawena Msonda Baba mzazi kutoka chunya Mbeya
Ally Mrangi Gigiri Mresa yeye mar kila siku yupo safarini kuelekea mabibo Dar es salaam
Zakaria Ndemfoo, Issa Mzee wa urembo kutoka Moshi.Lupa tingatinga "mdau asiyechuja" ndiyo ilikuwa slogan yake
Bila kumsahau Chesko Mzee wa matunda kutoka Africa Sana
Kuna mdau akiitwa Limonga Justine Limonga na kuna huyu mama Abuu wa majani mapana.Kuna jamaa aliitwa Fikiri Dario Gakala wa GGM Geita na Filbert Kyenshambi kutoka Muleba-Nshambi,wapo wengi sn na tulikuwa tunaenjoy sn Enzi hizo
Unawakumbuka baadhi? Unazikumbuka kauli mbiu zao maarufu zilizotamba?