Watuhumiwa wengine watatu wa Sakata la ESCROW wafikishwa mahakamani leo

Najaribu kutafuta uwiano wa hizi kesi na zile porojo za mtaalam wetu mkuu wa mambo ESCROW pale Diamond Jubilee na hitimisho lake kwamba PESA HAZIKUWA ZA UMMA.

NAPATA UTATA!

Naomba nikusaidie bwana great thinker mwenye uvivu wa kufikiri, leo ukiwauzia TRA vifaa vya computer, wakakulipa, lakini kesho ikaonekana mfanyakazi wa TRA aliyeidhinisha malipo kwako umemuingizia fedha bank katika account yake, basi huyo mfanyakazi wa TRA pamoja na wewe mtashtakiwa kwa Rushwa pamoja na kwamba hiyo pesa sio ya Uma, ni ya kwako
 
Mramba, Yona na Mgonja hadi leo ikiwa ni zaidi ya miaka saba kesi yao bado inaendelea na akiondoka Kikwete watakuwa huru mtaani huku wakiibua kesi mpya dhidi ya Serikali kutaka kulipwa fidia....

Haya yanawezekana kwa nchi kama Tanzania pekee ambako WATAFUNAJI hawaguswi ila WAKUSANYAJI WA MAKOMBO ndiyo wanaoishia kubebwa mzobemzobe ati ndiyo walaji... aibu!!!!!!....

Hiyo ilikuwa ni gelesha tu ya Kikwete .......................... angekuwa amedhamilia ingekwisha. Mbona ya Mahalu imekwisha na ilihitaji ushahidi toka nje ya nchi!! Mazingaombwe tu ya Kikwete hayo!!
 
Teh teh teh...hii haina tofauti na wale wanaoshia kukamata kenge airport ili hali twiga,faru,chui, simba na hata tembo wakipitishwa kiulaiiini.....

Looo, kuna ukweli, kwani twiga wastani wa uzito ni kilo 1,190 wakati kenge wastani wa uzito ni kilo 15 tu. Hivyo twiga ni mzito mara 80 kumzidi kenge. Cha ajabu kenge kupitishwa airport kaonekana wakati twiga hakuweza kuonekana. Maajabu!!
 
Nitafurahi sana kiongozi wangu wa dini askofu Methodius Kilaini kama atafikishwa mahakamani pia. Katutia aibu sana hatutaki double standards

Rushwa inakuwa rushwa pale mtoaji anapotarajia kunufaika na hasa kisiasa kutoka kwa mpokeaji. Ukimpa rushwa hakimu una matarajio ya kunufaika na hasa kama una kesi mahakamani, ukimpa rusha kiongozi wa kisiasa una matarajio ya kunufaika kisiasa, hivyo hivyo kwa mkuu wa mkoa, wilaya, mkurugenzi wa halimashauri, mwenyekiti au mjumbe wa bodi nk. Ukimpa rushwa msitaafu unataka kunufaika kwa umaarufu wake. Ukimpa rushwa padre sina hakika sana kama unatarajia kunufaika kisiasa au kimaisha, labda unataka akuombee kwa Mungu jambo ambalo si lazima sana utoe rushwa maana kazi ya msingi ya kiongozi wa dini ni kuwaombea watu kwa Mungu. Ukimpa rushwa ili akuombee kwa Mungu unajipendekeza tu. Sioni ni kwa vipi TAKUKURU watampeleka Askofu Kilaini mahakamani kwa sababu sioni ni kipi ambacho mtoa rushwa anatarajia kupata kutoka kwa Askofu kama malipo ya rushwa aliyompa.
 
Watuhumiwa watatu wa sakata la akaunti ya Tegeta Escrow wasomewa mashitaka leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Watuhumiwa hao ni pamoja na Mkurugenzi wa Fedha wa benki ya BOT Julius Angelo ambaye Amekosa dhamana, Ofisa Mwandamizi wa TANESCO Steve Urassa na Leonard Lutabingwa wa TRA anayeshitakiwa kwa makosa manne.

Hivyo bado ni vidagaa, tunataka na mapapa yafikishwe mahakamani
 
Mkurugenzi watanescoyukowapi??huu o usanii wamesikia makelele yaIMF,,binafsi nisingeshauri kuona ofisa was bot maana tangu epa wotemaafisa. frm down to an wameachiwa huru mnaenda kutupelekeausanii mtupu wapi dompo
 
Kwani kilaini ni mtumishi wa umma? Halafu utamshitaki kwa kipi chenye mashiko.

Kwani wala rushwa ni watumishi wa umma tu?Kilaini ni mtu kama wewe huo upadri ni ajira tu,wacha wapelekwa mahakamani huko ndio watathibitka kama wamekula rushwa au la,je kama Kilaini ni memba board wa Mukombozi na yeye ndie alishinkiza Mukombozi watoe hela kwa waliofungua akaunti?ni mesema hivyo kama mathalani.
 
Naomba nikusaidie bwana great thinker mwenye uvivu wa kufikiri, leo ukiwauzia TRA vifaa vya computer, wakakulipa, lakini kesho ikaonekana mfanyakazi wa TRA aliyeidhinisha malipo kwako umemuingizia fedha bank katika account yake, basi huyo mfanyakazi wa TRA pamoja na wewe mtashtakiwa kwa Rushwa pamoja na kwamba hiyo pesa sio ya Uma, ni ya kwako

Kwa kweli u great thinker wa kufananisha swala la ESCROW na huo mfano wako pia sina Mkuu.
 
sisi kina gogo la shamba tunayaona yote hayo yanaoendelea kufanyika ni kuzidi kudhalilisha serikali ya ccm
 
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini tanzania TAKUKURU imewafikisha Mahakamani watuhumiwa wengine watatu kwa tuhuma zaa rushwa katika sakata la Tegeta Escrow na hivyo kufikia jumla ya watuhumiwa watano ambao hadi sasa washafikishwa mahaka ya kisutu jijini Dar es salaa.

Chanzo:ITV

Vigogo waliyotajwa na kamati ya hesabu ya bunge, mbona hawaprlrkwi mahakamani? Akina MUHONGO na wenzake.
 
Bangi zinawapeleka puta sana vijana wa ufipa hadi mnashindwa kujua mnapigania nini... kilaini kafanya kosa gani hadi aende mahakamani? Ana maslahi gani na sakata la escrow? Kuna ubaya gani kupewa hela na washirika wako, ndugu au jamaa na marafiki?


Kafanyeni kazi za ujenzi wa taifa badala ya kushinda kwenye keyboard mnaandika upuuzi... kumbuka fainali uzeeni.

Wanaotaka Askofu KilAINI ashtakiwe ni wapumbavu. Sadaka tunazotoa makanisani viongozi wanajuaje kama ni safi au chafu? Sio kzi ao kujuasource ya Sadaka. uaa eti kwa nini aliiiwaatikakaunti yake binafsi hlo ilifafanliwaa kanisa vizuri.

Usomi uakuwa na maana pale mtu anapofikiri nakutafakai jambo badala ya kurupuka kishabiki.

Kwanza Rugemalira ana haki ya kuuza mali yake na hakuna ubishi alikuwa anamiliki kihalali 30 % ya IPTL na pia walikubaliana kihalali na Sing singa kuuziana umiliki.
 
Looo, kuna ukweli, kwani twiga wastani wa uzito ni kilo 1,190 wakati kenge wastani wa uzito ni kilo 15 tu. Hivyo twiga ni mzito mara 80 kumzidi kenge. Cha ajabu kenge kupitishwa airport kaonekana wakati twiga hakuweza kuonekana. Maajabu!!

Mashine za ukaguzi kwenye viwanja vyetu vya ndege, pamoja na maafisa usalama waliopo kwenye viwanja hivi hawawezi kuona twiga wala kifaru wakipitishwa ila mitambo hiyo hiyo na maafisa hao hao wanaweza kuona kenge,nguchiro,sungura au hata panya buku wakipitishwa......serikali makini na sikivu imejaribu katika jambo hili,imeweza na sasa inasonga mbele!
 
Huku ni kujifanya eti serikali ya Tanzania ya awamu ya nne inazingatia good government. Hiyo rushwa waliopewa ni kwa ajili ya nini kwa mtoa rushwa? ESCROW ni fedha ya umma au ya IPTL?! Kama IPTL kwa nini waende mahakamani? Chenge anafikishwa lini?

Jambo hili la kufikisha watu mahakamani na liwe la wote waliohusika na ESCROW kwa kuanzia watendaji wa juu kabisa kama akina JK, Pinda, Ndullu, n.k. Hii njia ya kuwadanganya wananchi wakati wa kampeni kuwa CCM inauchungu na mali ya nchi ndio maana inawashughulikia wala rushwa!!!
 
kwa hiyo wewe ulitaka jee?? Wafungwe bila kuwapeleka mahakani, mahakam ndio waamuzi wa mwisho,

Labda wangepelekwa mahakama ya jeshi lakini kama ndio hii ya kisutu ambayo majaji wamevuta mzigo wa escrow hii ni danadana mpaka kihama.
 
Back
Top Bottom