Watuhumiwa wa mauaji ya M/kiti USA-River CDM wakamatwa

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Watu sita wamekamatwa na polisi wilayani Arumeru, watatu kati yao kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema, Kata ya Usa River, Msafiri Mmbwambo, na wengine kwa tuhuma za uvamizi wa mashamba ya wawekezaji.

Habari zilizopatikana jijini hapa jana na kuthibitishwa na Naibu Kamishna wa Polisi, (DCP), Isaya Mngulu, zilisema jana kuwa waliokamatwa ni wenyeviti wa vitongoji vitatu, lakini hawakubainisha kama ni viongozi wa chama gani.

DCP Mngulu hakutaka kutaja majina wala kuthibitisha kwamba waliokamatwa ni wenyeviti na wa vitongoji gani. Marehemu Mbwambo aliuawa kinyama wiki iliyopita kwa kuchinjwa na mwili wake uliokotwa kando ya makaburi wilayani humo.

CHANZO: NIPASHE
 
Hivi kweli siasa zetu zimefika huko! mpaka tutoane roho kwa sababu ya siasa! Ama kweli siasa hizi zina hitaji moyo. Haki itendeke. ukiua kwa upanga nawe utakufa kwa upanga.
 
....tusubiri taarifa zaidi ili tujue ni wa chama gani na walikuwa na sababu za kisiasa au vinginevyo. Inatisha sana!
 
Hao ni sisem tu maana wameishiwa sera yakuwaambia wananchi na wameamua kuwatishia kwa mauwaji
 
Ukute walioua ni usalama wa ccm, waliokamatwa wazururaji wakabambikiziwa kesi.
By the way, tunataka haki itendeke
 
Nasikia ni kweli ni viongozi wa magamba na wengine wamekamatwa na cm pamoja na panga so this info its true but let us wait our police for more investigation
 
ni wa ccm tu hao ila hawatatajwa!
Usiofu kama ni wenyeviti haina haja ya kuwataja majina wala vyama, maana watajulika waligombea kupitia vyama gani ili kupata uenyeviti wao, na nani mwenyekiti wa kitongoji husika.
 
Wewe shadadia tu,unaweza kukuta watuhumiwa ni wenyeviti wa Chadema...

Kwani adhabu itabadilika kwa kutegemeana na political affiliation ya mhusika?????? kwa hiyo akiwa CHADEMA adhabu yake inatakiwa iweje na akiwa CCM adhabu yake inatakiwa iweje KWA KOSA HILO HILO??????duh, kweli siasa inatawala na kuathirir adversely mawazo na akili zetu...
 
Kama vipi hao wangenyongwa tu fasta. Mambo ya kuhojiwa baadaye.
 
Back
Top Bottom