Watuhumiwa wa mauaji ya M/kiti USA-River CDM wakamatwa

....tusubiri taarifa zaidi ili tujue ni wa chama gani na walikuwa na sababu za kisiasa au vinginevyo. Inatisha sana!
Jamani, kama ni hao Wenyeviti wa vijiji ndo wamehusika basi sioni kama kuna sababu ya kujiuliza kama haya mauaji si ya kisiasa! Wangekuwa wamehusika Mapadre watatu au Masheikh watatu, tungejua ni mauaji ya Kidini. Msikwesekwepese!
 
jamani haijalishi ni chama gani au ni mtu gani hata kama angekuwa babake anyongwe kwani uhai wa mtu ni kitu kingine.mtu afe kwa mapenzi ya Mungu.na sio awaishwe
 
Wakithibitika basi nao wanyongwe publically ili iwe fundisho.

Sheria ichukue mkondo wake, Ni unyama ulioje! Watanzania tunaelekea wapi? hata kama sio siasa huu sio ubinadamu hata kidogo; damu yake na iwe juu ya vichwa vyenu popote muendapo na kibali kiondoke juu yenu kwa kila mtu aliye mbele yenu au nyuma yenu kama ilivyokuwa kwa Kaini! Mtaishia kuwa wa kutanga tanga. KIBALI KIMEONDOKA JUU YENU KWA JINA LA YESU KRISTO. Amen.
 
DON'T BE biased
kwa wale wakazi wa USA river karibia na eneo la tukio, fanya kauchunguzi kidogo tu.
tafuta wenyevit wote wa vitongoji vya jiran, ambao hutawaona ndo waliokamatwa!!
tubandikieni majina yao hapa.
au kama mwenyekit wa kitongoji chako haonekani tuambie!

au km kuna mtu anafanya kazi tigo aangalie mtu aliempigia marehem kwa mara ya mwisho!!!!!!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom