Watu wameendekeza tamaa kwa kisingizio cha usasa

Wewe dini gani mkuu??
Au dini haikuja na ngozi nyeupe??
Dini ni utamaduni wako??
Dini zipo nyingi mkuu sio ukiristu na uislaam pekee na hata kabla ya kuja kwa izo dini tulikuwa na imani zetu(dini) ambazo zilituongoza katika maadili ambayo wazazi wetu walikuzwa nayo na kutukuza na sisi

Kuongelea maadili kuna gharama sana kwakuwa waliolewa na usasa ni wengi na hawashauriki endeleeni kutetea "ufuska"
 
Kila zama zina mambo yake ya kishenzi. Enzi za mababu kulikua na ukeketaji, pia watoto wa kike kuchukuliwa kama vile sio binadamu. Kuna makabila walikuwa wanawekea booking mimba kwamba kama atakayezaliwa ni wa kike basi namchumbia. Binti alikuwa anaolewa akiwa mdogo sana tena na mtu aliyechaguliwa. Mimi kiukweli kwa yale mambo yaliyokuwepo enzi hizo naona bora wakati huu tuliopo. Mababu walikuwa na ishu za kiboya sana. Kama ni udangaji ulikuwepo tangu enzi za Nuhu.
 
Jamaa haelewi aisee.
Yeye nadhani kila anaevaa nguo fupi basi intention yake ni kuwatega wanaume ili wamtongoze.
Wewe unavaa nguo fupi ili ufanyeje? Na kama wewe ni (me) hebu waite hao wavaa nguo fupi na vi-tight waje hapa watuambie intention yao ni nini?
 
Kwanini usichukulie hilo kama ni maendeleo badala yake wewe unasema ni mmomonyoko wa maadili??
Huoni kua kuna fursa nyingi kuliko kushikilia huo utamaduni wako usiokunufaisha na chochote!!

Ndio maana nikakuuliza huo utamaduni wako uliokua nao kabla hata ya mkoloni umekusaidia nini??
Nikakupa faida kiduchu za huo unaoita usasa ila wewe hujaleta faida yoyote ya huo utamaduni wako.
Nimekuuliza kwamba ili jamii ionekane au ione imeendelea kiutamaduni ni kuvaa tight, kuvuta bangi, kuongeza matako na kuwa mashoga? Hayo ndio maendeleo ya kiutamaduni?
 
Kila zama zina mambo yake ya kishenzi. Enzi za mababu kulikua na ukeketaji, pia watoto wa kike kuchukuliwa kama vile sio binadamu. Kuna makabila walikuwa wanawekea booking mimba kwamba kama atakayezaliwa ni wa kike basi namchumbia. Binti alikuwa anaolewa akiwa mdogo sana tena na mtu aliyechaguliwa. Mimi kiukweli kwa yale mambo yaliyokuwepo enzi hizo naona bora wakati huu tuliopo. Mababu walikuwa na ishu za kiboya sana. Kama ni udangaji ulikuwepo tangu enzi za Nuhu.
Mkuu kwaiyo kukeketa na kufanya transgender ni bora transgender?

Binti kuchaguliwa mchumba na kuolewa ni ushenzi?

Kutolewa mahari na kuolewa na hongo kwa wadangaji kwa kigezo cha feminism ni bora hongo?

Huo uhuru wa kujifanyia mambo(usasa) ndio unapelekea jamii yetu kuwa ya hovyo sana vijana wanaiga kila ovu linalofanyika duniani na mzazi asiwe na chakufanya

Mila zilikuwepo ili kulinda maadili ya jamii husika na pia kulinda jamii isipoze uhalisia(utamaduni) wake

Hatuwezi kupoteza utamaduni wetu kwa kuiga tamaduni za watu wengine
 
Hapa nilichogundua ni kwamba hoja ya mleta mada imekutana na hoja thabiti za Wadau na imekufa kifo cha Mendez. Kilichobaki ni ubishi tu ilimradi tu kubisha.
 
Unaweza ukawa sahihi maana nimekuja na hoja ya nyama nikaitumbukiza kwenye mafuta yanayochemka
 
Hasa pale kijana anapopata Admission ya chuo fulani, wengi kila kitu uanza kuwa tofauti
 
Mkuu kwaiyo kukeketa na kufanya transgender ni bora transgender?

Binti kuchaguliwa mchumba na kuolewa ni ushenzi?

Kutolewa mahari na kuolewa na hongo kwa wadangaji kwa kigezo cha feminism ni bora hongo?

Huo uhuru wa kujifanyia mambo(usasa) ndio unapelekea jamii yetu kuwa ya hovyo sana vijana wanaiga kila ovu linalofanyika duniani na mzazi asiwe na chakufanya

Mila zilikuwepo ili kulinda maadili ya jamii husika na pia kulinda jamii isipoze uhalisia(utamaduni) wake

Hatuwezi kupoteza utamaduni wetu kwa kuiga tamaduni za watu wengine
Kwa hiyo kukeketa unaona ni jambo dogo?
 
Na transgender ni jambo dogo mkuu?
Umeleta ishu ya transgender kama kujitetea. Ila nitasimama na kauli yangu kwamba kila zama zina ushenzi wake. Na pia hakuna tabia mpya chini ya jua. Labda kwa sasa tunaziboresha tu. Tangu enzi za Sodoma watu walifanya upuuzi.
 
Kabisa mkuu
Halafu izo mambo zilivokuwa na nguvu kundi kubwa linatetea na kuona sawa tu

Kuna baadhi ya wazazi wanaona bora watoto wao wasisome kabisa maana mtu kalelewa vizuri akienda chuo tu akirudi wazazi wote anawaona mafala tu na waliopitwa na wakati
 
Umeleta ishu ya transgender kama kujitetea. Ila nitasimama na kauli yangu kwamba kila zama zina ushenzi wake. Na pia hakuna tabia mpya chini ya jua. Labda kwa sasa tunaziboresha tu. Tangu enzi za Sodoma watu walifanya upuuzi.
Sio transgender tu mkuu habari ya mjini asaiv ni ushoga, kuvimbisha makalio, kutembea na vi-top, usagaji na maovu yote yanayofanyika kwa wazungu

Na jopo la wasanii na akina nyie ni kupigia upatu

Hatuwezi kuiacha jamii ikaangamia namna hii kwa kigezo cjui cha zama zinazoitwa za kisasa
 
Ushoga haukuwepo zamani?
 
Dini zipo nyingi mkuu sio ukiristu na uislaam pekee na hata kabla ya kuja kwa izo dini tulikuwa na imani zetu(dini) ambazo zilituongoza katika maadili ambayo wazazi wetu walikuzwa nayo na kutukuza na sisi

Kuongelea maadili kuna gharama sana kwakuwa waliolewa na usasa ni wengi na hawashauriki endeleeni kutetea "ufuska"
acha kukwepa swali.

wewe ni dini gani?

Kama unaabudu mizimu sema..
Kama huamini kua Yesu ni mwokozi wa maisha yako sema pia.

Kama huamini kua mtume Mohammad (S.A.W) sio mtume wako wa mwisho pia semaa.

Mbona unakwepa kijana, wewe dini gani au unaabudu mizimu??
 
Back
Top Bottom