Watu wakiuliza uhalali wa teuzi hizi tutawaona wana wivu?

yani kwanza nilipoziona hizo picha hapo nilitegemea kukuta michango ya wadau inasoma page kama sitini(60) hivi jamani hili ni kosa kubwa sana kwa kiongozi mwenye uwezo wa kumfanya mtu fulani awe kwenye nafasi flani kuwepo kwenye kitu kama hiki...! kwa viongozi waadilifu na wenye busara zao hata wakialikwa hua wanatoa excuses labda kama iwe ni kitu ya kiserikali kama mambo ya kuapishana na nini lakini kwenda kuminya bata wazeee....! yani hii inaonesha jinsi gani watanzania tuko kwenye usingizi wa ujinga

unajua watanzania wengi tuna hali kama ya kuwaabudu viongozi hivi..! hiki kitatupeleka mbali sana yani.. mbali na ulimwengu wa maendeleo..! tutarudi kulee nyuma ambapo watu walikua wanasema machifu hawakosei..!! jamani hawa nao wanakosea tu kama sisi nao wameumbwa hawajashushwa hawa....! mimi kwakweli hua nikiona mtu anakua kama anamuabudu kiongozi huwa ninakerwa sana wadau...!

hawa ni wakuawachana live tu wanapokosea....
UMESIKIA WEWE MICHELLE.......??????

Nimesikia nini tena mkuu? simwabudu kiongozi yeyote nchini,namwabudu Mungu tu...!
 
Duh! Ndo maana wanawake tunagandamizwa sana in pursuing our careers! Sasa is that party official ama? Ndo maana Michelle kasema Mindi kaandaa party mwenyewe! There is nothing professional in that party! Ni kufurahia ulaji tu, akabembee US! Vitu kama hivi kiukweli vinanifanya nione aibu kuwa a professional woman, how do I defend myself kuwa sifanyi hivi kwenye official parties?!

Aliandaa mwenyewe, akawaalika rafiki zake ambao baadhi yao ndo hao waheshimiwa na wengine wasio waheshimiwa.
 
Kwanza sielewi mentality ya mtu kusherehekea namna hii uteuzi wa kutumikia wananchi. Sherehe hizi hazionyeshi kuwa upo na furaha sana kuwa sasa utawatumikia wananchi vyema badala yake inajenga picha kuwa unafurahia ulaji tu

Uwepo wa Mawaziri pia shereheni pia kunaibua masuali zaidi. Wapo hapo kama nani? Wana uhusiano gani na mhusika?

Zaidi ya yote inatifanya tuhoji qualifications zake. Anastahili? Kuna wengine wamekiukwa ili apewe yeye?

Kwanza hiyo kazi yenyewe hata bado hajaanza, hizo fweza za sherehe kapata wapi??
 
Hizi picha zinafanana na za waziri wa uganda or rwanda alikuwa nakula bata na mabinti zikasambaa mtandaoni ikabidi aliresign. Kazi kibongo bongo kawaida tuu. Dada anastahili kwenda kupiga kazi. Mama mkubwa mama mkapa, bff ndio hao umewaona kwenye picha. mungu ampe nini tena zaidi ya diplomatic priviledges.
 
Enzi za mwl woote walioshiriki wangepigwa chini pamoja na huyo rafiki yao, us angeisoma tu magazetini na kuiona kwenye tv na mitandao
 
Kama (Iwapo) qualifications anazo, tatizo ni nini??? Kuandaa sherehe???? Kuagwa???? au nini??? Kwa wanao fahamu, lete CV zake, vinginevyo mwache afurahie matunda ya usomi wake, ambaye hajasoma, aende shule sasa.
 
Back
Top Bottom