Watu wakiuliza uhalali wa teuzi hizi tutawaona wana wivu?

Wana JF,

Kweli Does this make any sense kusheherekea kwenda fanya kazi Officen kweli sheherekea una graduate huko, hii inaonyesha ignorance kwa sisi watanzania mfanyakazi wa kawaida tu balozini washeherekea hii ndio taswila kamili ya kutumia matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi even if it was her money yet repercussion
yake kwa society yetu ni inastahajabisha pia.

 
Wana JF,

Kweli Does this make any sense kusheherekea kwenda fanya kazi Officen kweli sheherekea una graduate huko, hii inaonyesha ignorance kwa sisi watanzania mfanyakazi wa kawaida tu balozini washeherekea hii ndio taswila kamili ya kutumia matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi even if it was her money yet repercussion
yake kwa society yetu ni inastahajabisha pia.


Kinachosherehekewa hapo ni kupangiwa kazi Marekani!

Angepangiwa kazi Malawai wala asinge throw party.
 
Inaelekea kuna ulaji ubalaozi wa Tz Washington USA kama ni hivyo?

Ama ni furaha ya kutembea tu?

La ulaji sina uhakika.

Ila ubalozi wetu DC ukilinganisha na tuseme ubalozi wetu Ouagadougou, prestige hailingani kabisa.
 
Duh! Ndo maana wanawake tunagandamizwa sana in pursuing our careers! Sasa is that party official ama? Ndo maana Michelle kasema Mindi kaandaa party mwenyewe! There is nothing professional in that party! Ni kufurahia ulaji tu, akabembee US! Vitu kama hivi kiukweli vinanifanya nione aibu kuwa a professional woman, how do I defend myself kuwa sifanyi hivi kwenye official parties?!

Huu utamaduni umejengeka sana Tanzania.Tusimlaumu Mindi bali mfumo mzima unaoanza na wale waliokomaa katika madaraka/nafasi. Mtu akipata ubunge, uwaziri au cheo chochote kile , utaona maandalizi makubwa sana ya kusherehekea.

Tujiulize, kama mtu kapewa kibarua cha kutumikia wananchi, sherehe huwa za nini? Labda sherehe zingekuwa za kutoa shukrani kwa Mungu na kumwomba Mungu awape busara, afya na nguvu za kutenda kwa uaminifu tungeelewa.Anyway, labda hatujajua madhumuni ya sherehe hizo.Wenye kujua watuambie.
 
Hofstede kwa kumbukumbu zangu ni mtaalamu wa umuhimu wa culture in doing business internationally, na Binti huyu Mindi anaielewa culture ya USA, kwa maoni yangu kwa uelewa huo kunampa nafasi yeye au mwingine yeyote mwenye uzoefu wa pamoja na mambo mengine uelewa huu wa utamaduni wa Marekani. Vigezo vya kuteuliwa -sheria ya utumishi wa umma!

Mimi sija-question qualifications zake hata kidogo maana nilikuwa simjui. Nilicho question ni utata unaoonekana kwenye picha. Kama aliandaa sherehe hiyo ni private issue suala hapa kuna mawaziri wawili - viongozi wa umma, picha inayokuja hapo hata kama siyo ni kwamba huyu dada hakupata hiyo kazi kwa merits tu bali kuna more than that. Tusitumie ofisi za umma kugawiana vyeo kwa kuwa tunafurahishana faragha.

Premise yangu ya kwanza ni kuwa
  1. Atakuwa na undugu na mtu ambaye ana nafasi kubwa ya kushawishi uteuzi wake
  2. Hao walio hudhuria watakuwa ama shemeji zake kwa yeye kuwa nyumba ndogo ya mnene
  3. Mmoja kati ya hao mawaziri wawili atakuwa ni mwandani wake
  4. Kapelekwa US kwa sababu binafsi na si za kutumikia taifa hata kama ana qualifications hizo

Maswali haya na mengine mengi ya NEPOTISM yasingeulizwa kama kusingekuwa na picha hizi. Tuache kuendesha nchi kama kampuni binafsi. Mtu kama huyo akiboronga unadhani atawajibishwa?. Halafu teuzi kama hizi ndiyo vyanzo vya uzembe maana watu wanakuwa wavivu kutimiza majukumu yao wakijua kuwa hakuna wa kuwauliza. Kwao wao no ACCOUNTABILITY!.
 
Huu utamaduni umejengeka sana Tanzania.Tusimlaumu Mindi bali mfumo mzima unaoanza na wale waliokomaa katika madaraka/nafasi. Mtu akipata ubunge, uwaziri au cheo chochote kile , utaona maandalizi makubwa sana ya kusherehekea.

Tujiulize, kama mtu kapewa kibarua cha kutumikia wananchi, sherehe huwa za nini? Labda sherehe zingekuwa za kutoa shukrani kwa Mungu na kumwomba Mungu awape busara, afya na nguvu za kutenda kwa uaminifu tungeelewa.Anyway,
labda hatujajua madhumuni ya sherehe hizo.Wenye kujua watuambie.

Anasheherekea kuteuliwa kwenda kufanya kazi ubalozi wa Tanzania USA!
 
Hii ni hatari sana. Ndiyo maana tz imekosa kila kitu hapa duniani hasa toka kipindi cha awamu ya nne ilipoingia madarakani. Vyeo na nafasi mbalimbali zimekuwa zikitolewa kama zawadi kwa wapenzi, ndugu, marafiki na hata kuzingatia mambo ya dini bila kuangalia uwezo wa anayeteuliwa.

Hapa swala ni kwanini mawaziri wawepo kwenye sherehe hiyo, that is obvious kwamba hao ndiyo waliofanikisha huo uteuzi. Hii ni hatari sana, kwani nani asiyefahamu ukaribu kati ya nchimbi na lukuvi na rais?
Yaani hii nchi imefikia kipindi itawaliwe na dictator lkn ana nidhamu ya kazi na taaluma na zaidi awe na vision.

Kwa hakika kwasasa, tz hatuna viongozi. Ni wasiwasi sana na nafasi ya nchi itakavyokuwa economically and socially by october 2015.

Dictator Kama Hitler hivi, Mussolini... YAANI awe hacheki na kima Mbona watu watapiga kazi na Kuwa na ufanisi, YAANI ukizingua tu unawajibishwa na adhabu Kali. Kwa Hali ilivyo Sasa serikali legelege wananchi wako hoi bin taaban hata hatujitambui YAANI inatakiwa kiongozi wa kutupeleka speed tujitambue
 
Kupangiwa Marekani dili. Sidhani Kama angepangiwa Msumbiji angefurahia hivyo!
arifu kupelekwa mtoni ni bonge la dili........si umeona hata watoto wa vigogo hawako kenya au nigeria.......hapo huyu binti lazima kuna shukrani lazima azilipe ...soon tutasikia safari ya jk majuu....
 
Dah! Kumbe hata Mimi nilipopangiwa post ya kwenda kufundisha sekondari mikoani ilitakiwa nifanye bonge la party???? Maana siku hizi watu wanapangiwa utumishi wa umma wanafanya sherehe... Huu ni utamaduni wa kishenzi kabisa, na mbaya zaidi unafanywa na professionals :censored: Zao!!! Wote
 
Na kinachotia mashaka zaidi waalikwa ME ni wawili 2. Tujiulize uhalali wa yeye kuchaguliwa na sherehe iliyofanywa.
 
hivi huyu binti ndo mtoto wa dada yake na mama Anna Mkapa aliyegombea ubunge moshi maarufu ka mama Mindi?
 
Haya mauchafu ya ku-throw party mtu akiteuliwa kushika nafasi yenye ulaji au kujirusha yanafanyika sana bongo. Na hao mawaziri wawili kuhudhuria such a party lazima mjiulize uteuzi huo umezingirwa na vitu gani... Mbaya zaidi jamaa wa ile blog yetu ndiye kaharibu kabisaaa alipizitundika hizo picha hadharani 'wakidhania ni ujiko tutachekelea na kufurahia', mara he!!!! zimeondolewa... Jiulize kwa nini zimeondolewa ghafla???? Yaaani nimewadharau kishenzi hao jamaa, what a shame!!!!!!
 
Simfahamu Mindi, umesema huhoji uhalali wa qualification zake...ishu ni hao viongozi kujirusha na vimwana, kwa mantiki hiyo hapo Mindi angekuwa na wakina Sophia Simba na Zakhia Meghji na vinywaji na huduma zikawa hiyo hivyo kusingekuwa na tatizo sio??

Hoja iwe uwezo wake kufanya kazi ubalozini, kwa hela ya walipa kodi wa Tanzania na si walioenda kumuaga, sherehe kaandaa Mindi,wao wamealikwa.

Kwa kawaida mtu kwenda kufanya kazi ubalozini inatakiwa aajiriwe Wizara ya Mambo ya nje na afanyekazi hapo si chini ya miaka minne (otherwise kuna kama kuna dharura). Huyu dada hajamaliza hata mwaka tangu aajiriwe hapo wizarani na leo kapangiwa kwenda posting ili hali kuna watu hapo wana miaka zaidi ya saba na hawajapangiwa kwenda kufanayakazi ubalozini. Kwa kifupi kuna kitu kisicho sahihi kuanzia ajira yake mpaka hiyo posting.
 
Back
Top Bottom