Watu wa vijijini ndiyo huwa wanalipa mikopo nchi hii, wanatakiwa kupewa kipaumbele kwenye matumizi ya hiyo mikopo

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,238
12,751
Karibu asilimia mia moja ya mikopo ya nchi hii inalipwa na toka uhuru imekuwa inalipwa na watu wa vijijini. Unapoenda kulipa mikopo lazima utumie fedha ya kigeni, yaani dola. Sasa nchi yetu inapataje dola?

Ni kwa kuuza bidhaa nje ya nchi. Wazalishaji wa viwanda vya ndani ambao wanauza humuhumu hawaleti dola nchi. Wafanyabiashara wakubwa wakariakoo wanaujumlisha vitu hawaleti dola nchini. Ni wafanyabiashara wachache sana wanaoexport ndiyo huleta dola nchini.

Wakulima na wachimba madini wa vijijini ndiyo waingizaji wakubwa wa fedha za kigeni nchi. Hao ndiyo ambao nguvu zao zinatumika kulipa mikopo hii mikubwa tunayokopa. Wakulima wa korosho, chai, kahawa, vanilla, kokoa na mazao mengine ya biashara ndiyo walipa mikopo.

Na ndiyo maana serikali inanyonya sana wakulima hawa hadi kufikia kuua vilimo vya mazao hayo sababu ndiyo source yake kubwa ya dola za kigeni. Hao ndiyo wanalipa mikopo yake.

Hivyo basi, tunapokopa tukumbuke sana walipaji.
 
Back
Top Bottom