Mtawala wa forum hii na wote kwa ujumla napenda kuwapa mada hii iwe kama ni ushahidi mojawapo wa sakata la BoT. Hili suala la watoto wa vigogo kuajiriwa Bot si la uongo kwani
1. Rogers Sumaye alipata ajira hata kabla hajamaliza shule Uk kwani kuna watu walianza kufanya interview za kumsindikiza.
2. Kigoda naye the same
3. Lowasa's the same
4. And many others who have brothers there or relatives
Ishu hapa sio kuwa na sifa za kufanya kazi Bot bali je walipitia usahili na taratibu za ajira serikalini?
Je, ni watu wangapi wenye sifa walifanya interview na kushinda na bado wakapigwa chini?
Inasikitisha kuona kuwa hata Gavana mpya anatetea maovu akiwa ofisini hata mwezi haujaisha ni SHIDA hii
May 30, 2008:
=======
Baadae: Watoto wa vigogo BoT wasafishwa
=======
Oktoba 07, 2012
Oktoba 23, 2012
1. Rogers Sumaye alipata ajira hata kabla hajamaliza shule Uk kwani kuna watu walianza kufanya interview za kumsindikiza.
2. Kigoda naye the same
3. Lowasa's the same
4. And many others who have brothers there or relatives
Ishu hapa sio kuwa na sifa za kufanya kazi Bot bali je walipitia usahili na taratibu za ajira serikalini?
Je, ni watu wangapi wenye sifa walifanya interview na kushinda na bado wakapigwa chini?
Inasikitisha kuona kuwa hata Gavana mpya anatetea maovu akiwa ofisini hata mwezi haujaisha ni SHIDA hii
May 30, 2008:
UCHUNGUZI uliofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuhusu ajira za upendeleo kwa watoto, ndugu na jamaa za wakubwa ndani ya Benki Kuu (BoT), umekamilika.
Kukamilika kwa uchunguzi huo kulitangazwa mbele ya waandishi wa habari jana na Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu.
Ingawa hakuwa tayari kusema kile kilichomo ndani ya taarifa hiyo kwa maelezo kuwa TAKUKURU ni taasisi inayojitegemea, Gavana Ndulu alisema, tayari BoT imeshaanzisha uchunguzi wake mwingine kufuatilia suala hilo hilo la ajira.
Gavana Ndulu alisema kuwa katika uchunguzi wake, TAKUKURU ilikuwa ikichunguza ajira za watu 14 wanaohusishwa na viongozi waandamizi kulingana na maelezo waliyopewa na ngazi husika.
Alisema baada ya kupata taarifa hiyo ya TAKUKURU, BoT nayo ikaamua kuanzisha uchunguzi wa ajira za wafanyakazi wake wote, ili kuepusha malalamiko kutoka upande fulani pamoja na kuepuka kupelekwa mahakamani.
"Wale TAKUKURU walifanya uchunguzi wa ajira za watoto wa vigogo kulingana na maelezo waliyopewa, lakini sisi tunataka kufanya uchunguzi wa ajira za wafanyakzi wote," alisema Ndulu.
Alisema kuwa ndani ya BoT kila mfanyakazi ni sawa, awe mtoto wa kigogo au wa mkulima, ndiyo maana wameamua kuwashirikisha wafanyakazi wote kwenye uchunguzi huo.
"Unajua leo hii ukifanya uchunguzi wa ajira za watoto wa vigogo pekee, kesho unaweza kujikuta hata hao watoto wa wakulima nao walipata ajira kwa njia zisizokubalika," alisema Ndulu.
Aidha, alisema uchunguzi wao utakuwa tofauti zaidi, kwani wao watafuata sheria ya mwaka 2004 (iliyobadilika), wakati TAKUKURU walitumia sheria ya mwaka 2000.
Ndulu hakuwa tayari kufafanua utofauti wa sheria hizo, lakini alidai kuwa katika uchunguzi huo, TAKUKURU haikutumia sheria iliyotumika kuwaajiri watoto hao.
"Hapa kunaweza kutokea tofauti ya kutokuelewana na jamii ikachukulia vibaya mambo haya, kwani sheria zilizotumika kufanya uchunguzi zilishabadilishwa, sasa sijui itakuwaje," alisema Ndullu.
Aidha, alisema ni vizuri jamii ikavuta subira ya kupata matokeo ya uchunguzi wa BoT kuhusiana na ajira za wafanyakzi wake na asingependa kutoa matarajio ya kazi hiyo mapema.
"Jamani nisingependa kuwaahidi nyinyi au wananchi wengine hivi sasa matarajio ya uchunguzi wetu, bali ninawaomba tungoje hayo matokeo," alisema.
Hivi karibuni, vyombo mbalimbali vya habari vilitoa taarifa na kutaja majina ya watoto wa vigogo ambao wanafanya kazi BoT, wakisadikiwa kuwa walipata kazi hizo kutokana na ushawishi au nafasi za ndugu zao.
Taarifa hizo pia zilinukuu viongozi wa TAKUKURU wakidai wanachunguza ajira za watoto hao wa vigogo kuona kama walipata ajira BoT bila kufuata taratibu zilizotakiwa.
Juhudi za Tanzania Daima kumtafuta Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Edward Hosea, kuthibitisha kukamilika kwa uchunguzi wa ajira za watoto wa vigogo hao ziligonga mwamba baada ya simu yake kutokuwa na majibu.
Taarifa kwamba kulikuwa na ajira za upendeleo ndani ya BoT kwa mara ya kwanza zilisambazwa katika mtandao wa intaneti kabla vyombo kadhaa vya hapa nchini kuripoti taarifa hizo.
CHANZO: Tanzania Daima
=======
Baadae: Watoto wa vigogo BoT wasafishwa
=======
Oktoba 07, 2012
Ona nchi yetu ilivyo
1. FILBART SUMAYE,
2. PAMELA LOWASA,
3. ZARIA KAWAWA,
4. HERIETH LUMBANGA,
5. SALAMA MWINYI,
6. RECHAL MUGANDA,
7. SALMA MAHITA,
8. JUSTINA MUNGAI,
9. KENETH NCHIMBI,
10. BLASIA W. MKAPA,
11. VAOLETH LUHANJO,
12. LIKU KATE KAMBA,
13. THOMAS MONGELA na
14. JABIRI KIGODA.
HIYO NI TIMU YA WATOTO WA VIGOGO WALIOAJIRIWA BOT BADO KATIKA BALOZI ZETU NJE YA NCHI. NCHI YETU INAFISADIWA NANI WA KUTUOKOA WENGI WAO WAMEGHUSHI ELIMU ZAO
SASA SIJUI KWAMBA NI KUJIVUNIA VIONGOZI WETU KUTUONYESHA KUWA ELIMU NI MSINGI WA MAISHA KWA KUWAPA WATOTO WAO ELIMU BORA AU NI WANANCHI KUONA HUKO NI KUPENDELEANA KATIKA AJIRA ZENYE MASLAHI MAZURI AU NI WIVU WA WATANZANIA TU?
Oktoba 23, 2012
Gazeti la Jamuhuri la October 23, 2012 Limewataja vijana wafuatao kuwa ni watoto wa vigogo waliojazana BOT: Kweli Tanzania ina wenyewe
Salama Ali Hassan Mwinyi
Filbert Tluway Sumaye
Zaria Rashid Kawawa
Blasia William Mkapa
Herriet Marten Lumbanga
Pamela Edward Lowassa
Rachel Muganda
Salma Omary Mahita
Justine Mungai
Kenneth Nchimbi
Violet Philemon Luhanjo
Liku Kate Kamba
Thomas Mongela
Jabir Abdallah Kigoda