Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,845
Mkuu, unayejiita mtoto wa mjini, mbona unajiumbua? Hakuna kitu kama SINSEI. Karibu na daraja la salenda palikuwa na Italian Club. Mbele kidogo palikuwa na San Sui. San Sui ilikuwa kwenye hoteli ya Sea View ambayo siku hizi imebadilishwa kuwa Courtyard Hotel. Hata sisi wakuja tulikuwa tunajimwaga humo. Commodores ( Easy n.k.), Santana, Millie Jackson, Brass Construction n.k. mtindo mmoja. Hamna bolingo wakati ule.
Fundi Mchundo inaonekana mwenyeji sana mitaa ya Upanga mashariki, sea view na vitongoji hivyo, ile Etiennes mbele ya Seaview iliishia wapi? palikuwa panachomwa kuku safi sana pale.
Salender Bridge Club baada ya Disco Sansui, nadhani walifuatia Disco Biribi la Joseph Kusaga, au Jetset Dj Ratchie Cutty (Raph Chambo)
Sehemu nyingine za kujiburudisha katikati ya wiki ilikuwa Railways Club Gerezani, mwisho wa wiki Gymkhana Club, enzi hizo Movie za James Bond ndio zinatamba, au nyama choma na utumbo BOT club, Jumapili mchana kule mtoni.
Mind you, sehemu nyingi zilikuwa Members Only