Watoto wa Mjini Dar

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Najua ni sehemu ya siasa lakini Mods we need something for a change at least for a weekend then mnaweza kuihamisha jumapili ikisha

Haya watoto wa mjini hebu tuambieni kuna sehemu inachai nzuri kama K-TEA SHOP?

Najua kuna watu na wake zao wana ugomvi kila kukicha kisa hawanywi chai home
 
Last edited by a moderator:
Mambo Chief Pride opposite pale kwa Mzee Abdul, nin miss kweli chai yao na yule mzee wa kindengereko anatukana kichizi.
 
Nimegundua watoto wa mjini tuko wachache sana humu

halafu kuna watu wanataka kutufundisha mambo....very unfortunate kuwa ES hayupo lakini najua yule baharia atakuwa anapajua tuu pale

Of course nina uhakika Mwanakijiji hapajui wala hawezi kuelewa whats the big fuss
 
kijiwe cha michongo yote mjini, kimechukua nafasi ya the former Salamander.

You name it EPA, Cheki zilizopigwa, TC feki, Dhahabu feki, Waungwana, watu wa kazi, halafu kachumba kenyewe kadogoo. Kijiwe cha J. Lukaza, Alex Massawe, Papaa msofe, n.k, n.k, n.k....

HQ ya madili yoote ya mjini. Mpaka Richmond kuna waliokula hela yake pale.
 
wengi wao itakuwa Dar exit au mijitu ya kufugwa....!

Yournameismine, si kweli kuwa sisi ni Dar exit. Wengine ni watu tuliopanda Ma-Ikarus yaani unapanda mabasi mawili na kulipa thumni. Sijui hata kama unaelewa nini maana yake. Nyie mtakuwa ni vijana mliozaliwa wakati wa Mwinyi. Wengine tuliona shamra shamra za Yanga kuifunga Simba mwaka 1974 ingawa mechi ilikuwa Mwanza. Wewe wakati huo sijui hata kama ulishakuwa kwenye YAI. Sanasana ndiyo baba yako alikuwa anabarehe na mama anavunja ungo. Haya maeneo yatakua mapya.
Hivyo next time heshima kwa wazee. Ehhh, na sisi tulikuwa na fashion zetu. Kigari cha kuuza Ice Cream. Kikitokea pale kwetu Ilala Flats utajua tu na wimbo wao ule ule "wewe wajifanya, usiwe kidomidomi, utakuja adhirika mama, ulimwenguni humu ...... siwezi tena mama, endelea...." Sisi haooo na senti ishirini zetu. Duuu, kweli nimshukuru Mungu, nimekula chumvi ....
By the way, namtafuta jamaa mmoja alitupiga picha tukiwa watoto. Jamaa alikuwa anavaa koti refu ingawa alikuwa akiishi Dar na joto lile. Jamaa alikuwa mzinga wa mtu na alijulikana kwa jina la MWAMBA. Picha hadi leo ninayo. Kama sikosei alikuwa akiishi hizi flats za Ilala, upande wa pili wa Shule ya Bomani na kama si hapo basi ni nyumba za Ilala KOTA.
 
mzee sikonge,
bila kusahau halaiki mazoezi national stadium na maziwa kwa mikate buuure.
na vikundi vya six batallion, jackson 8 nk.
nauli ya dmt kuanzia senti ishirini halafu inakadiriwa kwa umbali.
aah, acha ninyamaze mie.
 
Mshaanza kuharibu thread

hii ni thread ya sehemu za maakuli sasa haya mambo yenu ya na Ikarus hayahusiani after all akina ES walishaiongelea sana tuu

that said

hii mnajua kama Pilau tamu kuliko yote linauzwa pale oteli ya BUTIAMA pale magomeni?

basi unachukua ndizi zako kwa jamaa pale mlangoni kisha waingia ndani kuagizia mindi weee

kama ndio ukitaka WALI MCHUZI basi pale juu kuna sinia zimejaa samaki walokaushwa basi oooooh

Ukitoka pale huyooooo unaingia kwa bitebo kushevu huku wapiga soga na kama juma mosi basi si haba kwenda kwa babu mtama mchungu kupiga simu za nje maana kule muhimbili noma

now top that
 
game theory,kabla sijalikwaa pipa kuelekea alaska,pilau bab kubwa lilikuwa tawakal hotel,pale livingstone inapokutana na barabara ya msimbazi.ukiingia tuu hotelini waiter anakucheck kama wewe wa kuja au la,mara unamsikia mletee huyu wali jaa mchuzi tele.basi wewe kama mjini wa kuja unaona yes nimepewa priority napewa wali mwingi,kumbe lile neno jaa,maana yake wakuja huyu mletee wali wa jana
 
mzee sikonge,
bila kusahau halaiki mazoezi national stadium na maziwa kwa mikate buuure.
na vikundi vya six batallion, jackson 8 nk.
nauli ya dmt kuanzia senti ishirini halafu inakadiriwa kwa umbali.
aah, acha ninyamaze mie.

Tulivaa mizula na milosis!
 
LOL.....lazima utakuwa wakuja, maana naona hiyo Dar exit imeku-touch ile mbaya!:D

Hujanikuna, ila umenikumbusha mbali. Nilivyosoma nikakumbuka na mie nilivyokuwa nikicheka ndugu zangu nikirudi Sikonge. Wanasema nilikuwa naongea Kiswahili cha Kizaramo "...... n'likuwepo nakula pilau ...." Nakumbuka nililazwa Muhimbili na jioni chakula kilikuwa kizuriii. Asubuhi chai ya maziwa na mikate. Mchana ukaja tena wali na chuzi zito. Nikakataa kula kwa kujua mchana watakuja nichukua na nyumbani ntakuta msosi mkali sana. Mhhh, nilikuta ugali kwa maharage :)
 
haya basi, mie pia mtoto wa flats za Ilala...la kwetu lile ambalo mbele kuna ule uwanja wa kuchezea watoto!! nilikuwa na mradi wa ashkrimu za ukwaju...LOL

Kile kishule cha vidudu? Mie nilikataa kusoma hapo miaka hiyo kwani nilijua nikirudi kijijini, kaka zangu watanicheka sana kuwa nilisoma shule ya VIDUDU na mie pia ni kidudu.
SIdhani kama utakuwa unanifahamu kwani sikuwa mwenyeji sana zaidi ya jamaa wa Block 4 kama akina Rashidi, Mohamed, Deo na kaka zake, Ray, nk. Kwa mbali bwana Nguvu, kijana Paul na miwani yake, dada yake na wadogo zake. Mhh, zile chips za Mangi na soda zake tamu si kawaida. Ila baadaye mama wa kiarabu(mama Halidi-Marehemu) akaweka Kiosk chake chini ya dirisha letu la jikoni.... Block IV hiloooo baba, miaka hiyo wanaliita ghorofa la watu wanaoshindana. Ukiweka AC, wanajibu, ukiweka antena ya TV, wanakujibu, ukanunua gari, wanakujibu. Kiboko yao ni yule Msomali, ila mkewe alikuwa anatumia sijui mi LADYGAY?? Akipita basi unafeel Oxygen imekwisha. Sijui alikuwa anawezaje kupumua na hiyo harufu?
Nilikuwa pale mwezi wa tatu, nilipotea. Pamebadilika sana. Ikabidi nianze kutafuta nyumba yetu. Mungu bariki nikamuona mama Sembuli (dada ya Marehemu Sembuli wa Yanga)........, heee,kamaliza Chuo kikuu na degree yake ukutani. I was too proud of her. Wamepanda miti na nyuma ya Block IV, nasikia mama Mkapa kanunua lile eneo na ghorofa la Posta na wako busy kuweka jengo hapo. Too sad maana jamaa walikuwa wakicheza mpira hapo jioni (wazee) huku watoto wakichezea huku kwenye shule ya vidudu. Ilikuwa saa nne usiku na sikuonana na watu zaidi ya majirani wa karibu. Sikurudi tena pale. Miaka 10 sasa tangu niwe pale mara ya mwisho na karibu miaka 17 tangu niondoke........... Kumbe yule Mzaramo karibu na Wasabato walimuhamisha na wakajenga kanisa jipya ..... too much change.....
 
Tulivaa mizula na milosis!

Duuu, FM, Mizula siyooo. Umenikumbusha marehemu kaka yangu miaka hiyoo. Miaka hiyo mtu anavaa suruali ya wagonjwa wa matende na shati la mdogo wake. Miaka ya 80 ikawa mtu anavaa suruali ya mdogo wake - TINABUU na shati la baba yake, linakatwa huku chini kuweka kijiko..... halafu chini unakula RABA MTONI.
 
Ishue ni K-Tea Shop. Kama unaijjua unachangia kitu kuhusu hiyo K-Tea Shop. Kama huijui unajinyamazia.

K-Tea Shop is not just a tea shop, its more than just a tea shop. Its a a rendevuu ya aina yake na chai yake sio chai ili mradi chai bali ni chai yenye something more than just tea. It has the goodwill of tea legacy ukinywa you really feel it.
K-Tea Shop ilikuwepo kabla ya uhuru. Nyerere amekunywa chai hapo. Jumbe, Kawawa na Mwinyi wamekunywa chai hapo. Sina hakika na Mkapa bali JK amekunywa hapo kabla hajaukwaa upresedaa.

Wamiliki wa sasa ni watoto wa mmiliki original. Kachumba kenyewe kadogo na kuna maduka mengine 6 ya chai yamekizunguka tena ya kisasa hayajai ila bado watu wanafoleni na kusubiri ndani ya magari yao wakisubiri nafasi ya kukaa ndani ipatikane. Hayo yote sii bure, lazima liko jambo. Hata wahudumu ni wazee. There is some good rich history behind.
 
Ishue ni K-Tea Shop. Kama unaijjua unachangia kitu kuhusu hiyo K-Tea Shop. Kama huijui unajinyamazia.
K-Tea Shop is not just a tea shop, its more than just a tea shop.

Wee Pasco vipi? Kwanza unaanza na "ishu hapa ni K-Tea shop". Baadaye unaongeza "K-Tea shop is more thab tea shop". Ila sisi tukiweka maelezo zaidi ya hiyo K-TEa shop unatuambia shut-up kwenye rupabliki lwa watu. Usiwe mtumwa wa ishu. Ishu na sheria huwekwa ili zivunjwe. Binadamu si kama Train. Hata Train wakati mwingine huacha njia ila sema linakoishia who knows? Binadamu yuko free kama atoms za OXYGEN. So don't tell us to be like Atoms of Solid elements. Next time ndiyo wewe ujifunze kuandika.
At the end of the day, hizi si ndiyo story za hapo kijiweni?
 
game theory,kabla sijalikwaa pipa kuelekea alaska,pilau bab kubwa lilikuwa tawakal hotel,pale livingstone inapokutana na barabara ya msimbazi.ukiingia tuu hotelini waiter anakucheck kama wewe wa kuja au la,mara unamsikia mletee huyu wali jaa mchuzi tele.basi wewe kama mjini wa kuja unaona yes nimepewa priority napewa wali mwingi,kumbe lile neno jaa,maana yake wakuja huyu mletee wali wa jana

Ntakujibu baadae
maana bado naendelea kucheka

wot about ile SINAI bara bara ya uhuru iko opposite shule ya msingi ya Uhuru?

unajua mwenye ile sinai ya kariakoo na ile nyingine kule Temeke Changombe karibu na polisi ile kona ya kuelekea Tandika ni mmoja
yule ni mzee mmja wa kiarabu na mwenye lile gorofa pale magomeni mapipa

ushanikumbusha ukakumbuka ile stendi ya mabasi ya kwenda T.A ...nazungumzia Tawfiq yaliyoandikwa ATAKALO MOLA?

basi jirani pale kuna duka laitwa SOMETHING SPECIAL khabari za pale ni ndefu saaanaaaaa

ntakutafuta baadein
 
Hujanikuna, ila umenikumbusha mbali. Nilivyosoma nikakumbuka na mie nilivyokuwa nikicheka ndugu zangu nikirudi Sikonge. Wanasema nilikuwa naongea Kiswahili cha Kizaramo "...... n'likuwepo nakula pilau ...." Nakumbuka nililazwa Muhimbili na jioni chakula kilikuwa kizuriii. Asubuhi chai ya maziwa na mikate. Mchana ukaja tena wali na chuzi zito. Nikakataa kula kwa kujua mchana watakuja nichukua na nyumbani ntakuta msosi mkali sana. Mhhh, nilikuta ugali kwa maharage :)

Talk about Muhimbili

Hivi ALI MAPILAU bado yuko pale au?
 
haya basi, mie pia mtoto wa flats za Ilala...la kwetu lile ambalo mbele kuna ule uwanja wa kuchezea watoto!! nilikuwa na mradi wa ashkrimu za ukwaju...LOL

ilala flat kwa akina CHAGU na KALEONI?

ebwana unamkumbuka ZAWIYA? nasikia anazidi kuwa mzuri,

nasikia flats kila mtu kakimbilia READING na jamaa wengine ndio hivyo tena
 
Kile kishule cha vidudu? Mie nilikataa kusoma hapo miaka hiyo kwani nilijua nikirudi kijijini, kaka zangu watanicheka sana kuwa nilisoma shule ya VIDUDU na mie pia ni kidudu.
SIdhani kama utakuwa unanifahamu kwani sikuwa mwenyeji sana zaidi ya jamaa wa Block 4 kama akina Rashidi, Mohamed, Deo na kaka zake, Ray, nk. Kwa mbali bwana Nguvu, kijana Paul na miwani yake, dada yake na wadogo zake. Mhh, zile chips za Mangi na soda zake tamu si kawaida. Ila baadaye mama wa kiarabu(mama Halidi-Marehemu) akaweka Kiosk chake chini ya dirisha letu la jikoni.... Block IV hiloooo baba, miaka hiyo wanaliita ghorofa la watu wanaoshindana. Ukiweka AC, wanajibu, ukiweka antena ya TV, wanakujibu, ukanunua gari, wanakujibu. Kiboko yao ni yule Msomali, ila mkewe alikuwa anatumia sijui mi LADYGAY?? Akipita basi unafeel Oxygen imekwisha. Sijui alikuwa anawezaje kupumua na hiyo harufu?

Nilikuwa pale mwezi wa tatu, nilipotea. Pamebadilika sana. Ikabidi nianze kutafuta nyumba yetu. Mungu bariki nikamuona mama Sembuli (dada ya Marehemu Sembuli wa Yanga)........, heee,kamaliza Chuo kikuu na degree yake ukutani. I was too proud of her. Wamepanda miti na nyuma ya Block IV, nasikia mama Mkapa kanunua lile eneo na ghorofa la Posta na wako busy kuweka jengo hapo. Too sad maana jamaa walikuwa wakicheza mpira hapo jioni (wazee) huku watoto wakichezea huku kwenye shule ya vidudu. Ilikuwa saa nne usiku na sikuonana na watu zaidi ya majirani wa karibu. Sikurudi tena pale. Miaka 10 sasa tangu niwe pale mara ya mwisho na karibu miaka 17 tangu niondoke........... Kumbe yule Mzaramo karibu na Wasabato walimuhamisha na wakajenga kanisa jipya ..... too much change.....

Basi tumekubali

hivi unajua SAIDI MOLEL yuko wapi?

Hivi ni kweli Ray alikamatwa Umangani?

halafu unakumbuka kile kijiwe cha lile block la kule kama unaelekea kwa WANYALUKOLO? kijiwe kile kilikuwa cha machizi wanaotaka kwenda SAUZI tuuuu
 
Back
Top Bottom