Watoto kwenye ndoa sio chanzo cha furaha, jifunze furaha inatoka wapi

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Watoto kwenye ndoa sio chanzo cha furaha, na wala hawaji kuleta furaha bali wanakuja kuongeza na kuendeleza furaha iliyokuwepo baina yenu ninyi wapenzi.

Ukiona mtu anasema watoto wameleta furaha maana yake haikuwepo awali. Watoto hawawezi hata sikumoja kuchukua kureplace nafasi ya furaha ya ndoa, ndoa inafuraha yake na watoto wanafuraha yao.

Vyote hivi vinaleta ukamilifu wa furaha ya kweli. Inauma sana pale furaha ya ndoa inapokufa na mtu anabaki tu kwa ajili ya watoto, inasumbua moyo sana pale mtu anapoona hapati tena furaha kutoka kwa mume au mke wake na anaamua kuhamishia mapenzi kwa watoto.

Utamu wa asali ni wa asali na utamu wa sukari ni wa sukari ingawa vyote ni vitamu na vyote hutumika kwenye chai, kimoja kimetoka kwenye mmea na kingine kwenye mdudu. Jifunze kutofautisha na kuiheshimu tofauti iliyopo.

Nukuu ya mwaka kutoka MC Galiatano. Je kuna ukweli hapo.

 
Mtoa maada umeoa na una watoto? Maana tusije kuanza kuongea muuza matunda badala ya mla matunda
 
tatizo letu miafrika masimango wa mawifi na wakwe ila mtoto ni neema toka kwa Mungu ukipata unashukuru ukikosa unashukuru pia
 
Back
Top Bottom