Watoaji wa huduma ya majanga na maafa Nchini wametakiwa kutoa elimu Mashuleni

Apr 9, 2022
66
32
Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali zinazo jihusisha na utoaji wa huduma ya majanga na maafa Nchini wametakiwa kutoa elimu Mashuleni na katika vikundi ili kuepuka majanga mbalimbali yasiendelee kujitokeza Nchini.

Katika maadhimisho ya siku ya Ubinadamu Duniani, siku iliyotengwa kwa ajili kumbukizi ya kuwaenzi watoaji huduma hiyo Duniani ambapo katika Maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, amewashukuru Taasisi ya huduma ya kwanza Nchini Redcros na Taasisi ya kupambana na majanga RAPID Tanzania, kwa kushirikiana kuadhimisha siku hiyo.

Katika Maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila amewataka RAPID Tanzania na Redcross ziendelee kujiandaa ili kuwa tayari wakati wote kuokoa maisha ya watu, yatokanayo na Majanga ya maafa Nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya RAPID Tanzania, Maria Bilia ameiomba Serikali iweke kanuni na sheria za kukabiliana na majanga ili maafa yasijitokeze kwa kasi kubwa sana Nchini.

Hata hivyo Mratibu wa wa Redcros Kesi Ngware, amesema wanakabiliana mbalimbali ikiwamo ukosefu wa fedha na vifaa vya kutendea kazi katika kukabiliana na majanga mbalimbali.
 
Back
Top Bottom