NEMC yatahadharisha Umma juu ya umuhimu wa kuchukua tahadhari kuepuka majanga

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeitaka Jamii kuchukua tahadhari kujilinda dhidi ya uwepo wa kutokea Mafuriko kwenye maeneo mbalimbali Nchini.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Menan H. Jangu amezungumza na Wanahabari na kusema “Kwa kipindi cha miezi miwili maeneo mbalimbali yamekumbwa na mvua ambazo zimeleta athari kubwa ikiwa ni pamoja na maafa yaliyojitokeza katika maeneo ya Katesh, Wilayani Hanang katika Mkoa wa Manyara.”

Amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametahadharisha umma juu ya umuhimu wa kuchukua tahadhari za kuepuka na kukabiliana na majanga haya.

Amesema taarifa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) zinaonesha mvua za viwango tofauti zitaendelea katika maeneo mbalimbali nchini, pia mvua hizo zimekuwa kubwa na kuendelea kusababisha madhara kadhaa.

Ametaja baadhi ya tahadhari hizo kuwa ni;

- Kuepuka kukaa maeneo ya fukwe za bahari pamoja na kandokando ya maziwa na mito.

- Wanaoishi kwenye milima na maeneo ya kandokando katika kuepuka athari za maporomoko ya udongo.

- Madereva wa Vyombo vya Usafiri wawe na tahadhari wakati wa safari kwa kuzingatia kuwa maeneo ya barabara yanaweza yakawa siyo salama.

- Wamiliki wa maeneo ya uchimbaji na uchenjuaji wa madini hususani kwenye mabwawa ya majitaka, topesumu na maeneo ya kutunzia miamba ya sumu kuhakikisha maeneo hayo hayaleti madhara kwa jamii na vyanzo vya maji.

- Wananchi kuwa na umakini na matumizi ya maji nyumbani na kuhakikisha tahadhari zinachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuchemsha maji ya kunywa. Aidha, Wananchi wanakumbushwa kutokutiririsha majitaka kwenye mifereji ya maji ya mvua.

- Amewakumbusha Wananchi kuzingatia Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004, Kifungu No. 57 na kuepuka ujenzi kwenye maeneo hatarishi ikiwa ni pamoja na maeneo ya kando ya mito, fukwe za bahari na maeneo ya ardhi oevu.

Akitaja baadhi ya madhara yaliyojitokeza wakati huu kuwa ni;

-Mafuriko kwenye maeneo mbalimbali hali iliyosababisha madhara kama vile makazi kuharibiwa na Wananchi kukosa maeneo ya kujisitiri.

-Maafa kutokana na mvua kubwa. Aidha, wananchi wamepoteza maisha na wengine kuumia baada ya kuchukuliwa na mafuriko.

-Miundombinu ya maji na barabara kwenye baadhi ya maeneo imeathirika na kupelekea huduma za usafiri kukwama.

-Usalama wa maji kuathiriwa kutokana na muingiliano wa maji yasiyo salama yanayotokana na mafuriko na maji ya matumizi ya nyumbani hivyo kusababisha magonjwa ya kuambukiza ikiwa ni pamoja na magonjwa ya mlipuko.

-Aidha, eneo jingine la kuzingatiwa ni miundombinu ya kuhifadhi majitaka na topesumu kwenye migodi. Aidha, mvua zinazoendelea zimepelekea miundombinu husika kujaa na mingine kuvujisha maji yenye sumu na kuathiri mazingira na hata mifugo kupoteza maisha kwa baadhi ya maeneo.

-Vilevile hali hii imeleta athari kwenye vyanzo vya maji hivyo, kusababisha maporomoko ya udongo kama ilivyoonekana huko Katesh, Hanang na kusababisha madhara makubwa ikiwa ni pamoja na vifo, makazi kuathiriwa, mifugo miundombinu ya barabara, umeme na mifumo ya maji kuathiriwa.
 
Hayo ameneo tuyaepuke vipi?

Tunataka maeneo yote yaliyokwenye mabonde, fukwe na milima nyumba ziondolewe, kama ardhi ndio waliganw hao wakurugenzi wakamatwe na kulipa fidia na wahusika wahamishwe.
 
Serikali inapaswa kuanzisha taasisi imara kabisa itakayohusika na masuala ya Majanga na Mazingira, yaani MAMLAKA YA UDHIBITI NA KUPAMBANA NA MAJANGA TANZANIA. Ndani ya Mamlaka hiyo iwepo na Idara au Kitengo Maalumu kitakachohusika na Masuala ya Mazingira.
Mamlaka hiyo ijikite ktk kutoa Mafunzo Mbalimbali kwa Wananchi ili kuwajengea Utayari wa Kupambana na Majanga Mbalimbali endapo kama yatatokea kwenye maeneo yao wanayoishi.

Serikali iachane kabisa na utaratibu wa sasa wa kuwateua Wanasiasa kuwa eti Viongozi wa Kamati za Maafa. Eti unamuona mtu mwanasiasa kama vile Mkuu wa Wilaya ambaye hajui hata kuogelea au hajui hata kuwasha mtungi wa gesi ya kuzimia moto (fire extinguisher) anateuliwa kuwa ni eti ni "Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Wilaya," Tanzania kuna maajabu mengi sana.!
 
Back
Top Bottom