Watetezi Wa Kweli wa Haki za Binaadamu Tanzania ni Kina Nani?!, Jee JF Tumo?!.

Mkuu Pasco ,

Sikubaliani na wewe Dikteta(Uchwara) kumpa hadhi ya Dikteta(Mzalendo)

Tuanzie hapo tu kwanza hayo mengine tutawekana sawa

Ila nimecheka sana kwa jinsi ulivyopanga mtiririko huu
Mungu peke yake ndiye anajua uliko....nakuombea.

Pasco mtetezi wa haki za binadamu ninayemfahamu na kumwamini sana ni Jamii Forum family, hapa ndipo kuna utetezi wa kweli.
 
si kweli kila anachofanya rais ni udikteta kuna mambo mengie yalikuwa yanafanya kwa mazoea mfano no 3 na 4 ni taratibi mtumishi wa serikali anaposafiri apate kibali cha ikulu ili lilikuwa halifanyiki lakini vitu vingine anavyofanya tumemruhusu mwenyewe kupitia katiba yetu ndio maana rais wa kwanza aliwahi kuzungumzia juu ya katiba ilivyompa madaraka ambayo yangemfanya kuwa dikteta hapa tukideal na rais haitasaidi bali tupiganie mabadiliko ya katiba ili rais asiwe juu ya katiba
 
Wanabodi,

Hii ni thread ya swali kuhusu watu wanaoitwa watetezi wa kweli wa haki za binaadamu Tanzania, ni kina nani? (human right defenders). Haki za binaadamu ni jambo la kisheria, hivyo watetezi wa kweli wa haki za binaadamu, walipaswa kuwa ni wanasheria, lakini kwa upande wa Tanzania, jee wanasheria wetu tulionao ni watetezi wa kweli wa haki za binaadamu au ni watetezi wa matumbo yao kwa kisingizio cha kutetea haki za binaadamu?.

Namalizia kwa lile swali la msingi, jee watetezi wa kweli wa haki za binaadamu Tanzania ni kina nani?, Jee hawa wanasheria wetu tulionao ni watetezi wa kweli wa haki za binaadamu au ni watetezi wa matumbo yao kwa kisingizio cha kutetea haki za binaadamu?.

Wasalaam

Paskali
Hii ni rejea tuu.

P.
 
Kwenye hoja ya udikiteta wa rais Magufuli, kuna madikiteta wabaya na madikiteta wazuri au madikiteta wema.
Madikiteta wazuri ni wale ambao wanafanya vitendo vya udikiteta kwa nia njema, hata ikibidi kuivunja katiba, au kukiuka sheria, taratibu na kanuni, kwa nia njema, ni udikiteta unaokubalika, mfano katiba inaruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano, rais Magufuli anataka watu wafanye kazi na sio kuwa wazururaji kwa kisingizio cha kufanya maandamano, au kuwa ni watu wanaokaa bure tuu kwa kisingizio cha kuhudhuria mikutano ya siasa, watu wenye muda wa kuhudhuria mikutano ya siasa kila siku ni watu wasio na kazi, hivyo kama tangazo lake la kupiga marufuku mikutano ya siasa na maandamano ni ili watu wasizurure ovyo, na wasikae onyo bila kufanya kazi, then huu ni udikiteta mzuri. Dikiteta wa aina hii anaitwa a benevolent dictator.

Hata kuachiwa kwa Babu Seya, sheria hairuhusu wabakaji na wauwaji kuachiliwa kwa msamaha wa rais, kilichofanyika pia ni udikiteta, ila umefanywa kwa nia njema kuwa vipindi walivyotumikia gerezani, wamejirekebisa, na sasa ni watu wema, hivyo udikiteta is not necessarily ni udikiteta mbaya, udikiteta mwingine ni udikiteta mzuri.

Big up sana rais Magufuli.

Paskali
 
Wanabodi,
miongoni mwa watetezi wa kweli wa haki za binaadamu nchini Tanzania, ni huu mtandao wetu wa jf, watu humu wanapaaza sauti zao bila kutegemea kulipwa chochote na yeyote, na wengine sauti zao humu jf zimewaponza, zinawaponza, na zitaendelea kuwaponza, uhuru wao, haki zao, hadi maisha yao, na wengine zikiwaponza wasikamate ulaji for being too critical, kwa sababu ya kusema ukweli!, katika utetezi wa kweli wa haki za binaadamu, ipo siku JF italipwa kwa mema yote inalowafanyia Watanzania.

Wasalaam

Paskali
Hatimaye juhudi za JF katika kutetea haki za binadamu kwa Watanzania, kumeaza kuzaa matunda.

Hatua ya kwanza ni kupata recognition, JF kupitia Maxence Mellow, imepata recognition kwenye Mkutano wa AU. Soon tutatambuliw na UN, na ndipo labda tutatambulika nyumbani.

‪Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ampa heshima mwanzilishi wa mtandao wa JamiiForums kwenye mkutano wa AU‬ - JamiiForums

Hongera Max, Mike, Asha Dii, staff wote wa jf na member kwa kazi nzuri.
P.
 
View attachment 1083094

Kwa niaba ya Wakurugenzi na Watendaji wa JamiiForums nampongeza Mkurugenzi wetu Maxence Melo kwa kupata tuzo ya kinara wa Uhuru wa Kujieleza Mtandaoni kwa mwaka 2018/19(Distinguished Champion of Online Freedom of Speech in Tanzania 2018/19) iliyotolewa na Jumuiya Watetezi wa Haki za Binadamu(THRDC)

Maxence amekuwa mtetezi wa haki za kidijitali na uhuru wa kujieleza kwa zaidi ya miaka 10 kupitia JamiiForums. Tuzo hii imeangazia sehemu ya kazi zake nyingi za mtandaoni.

View attachment 1083183

Kauli mbiu ya siku hii kwa mwaka huu ni “kudai na kulinda nafasi ya kiraia mtandaoni kwa ajili ya kuboresha na kulinda Haki za Binadamu Tanzania.” JamiiForums chini ya uongozi wa Maxence, tumejikita katika kuhakikisha nafasi ya kiraia(civic space) inalindwa mtandaoni na nje ya mtandao.

Ni katika kulinda nafasi hii, Mkurugenzi wetu alifunguliwa kesi ambazo zinaendelea hadi sasa.

Tunamtakia kila la heri katika harakati za kuendelea kupigania haki za kidijitali na uhuru wa kujieleza na kuahidi kuwa team yote ya JamiiForums itakuwa naye bega kwa bega katika safari hii.

Tunawapongeza pia washindi wengine walioibuka vinara wa kutetea uhuru wa kujieleza katika nyanja mbalimbali wakiwemo CIPESA, Salma Saidi, Maria Sarungi na wengineo.
Imeanza kulipa/
P
 
Hatimaye juhudi za JF katika kutetea haki za binadamu kwa Watanzania, kumeaza kuzaa matunda.

Hatua ya kwanza ni kupata recognition, JF kupitia Maxence Mellow, imepata recognition kwenye Mkutano wa AU. Soon tutatambuliw na UN, na ndipo labda tutatambulika nyumbani.

‪Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ampa heshima mwanzilishi wa mtandao wa JamiiForums kwenye mkutano wa AU‬ - JamiiForums

Hongera Max, Mike, Asha Dii, staff wote wa jf na member kwa kazi nzuri.
P.


JF tunakwenda vizuri, baada ya AU ni CPJ sasa Max anatinga rasmi New York, Marekani siku ya Nov. 29, 2019 kupokea tuzo ya utetezi wa haki za binadamu.


P
 
We jamaa matakonini? Mbona watanzania wenzio wanapopotezwa unakaa kimya?, watu wanaotekwa hamjawahi kupaza sauti, watu wanapigwa risasi mpo kimya uzalendo ni kwenye mambo yanayomhusu magufuli pekee?? Uzalendo sio kutetea madege hayo uzalendo ni kusimamia misingi ya utawala bora, haki n.k nyie kwenu uzalendo ni kumsifia magu hata kwenye ujinga... Acha upuuzi Paskali umenikera
Karibu
P
 
Lakini miongoni mwa watetezi wa kweli kabisa na wa dhati wa haki za binaadamu nchini Tanzania, ni huu mtandao wetu wa JamiiForums au jf, watu humu wanapaaza sauti zao kutetea haki za binaadamu bila kutegemea kulipwa chochote na yeyote, na wengine sauti zao humu jf zimewaponza, zinawaponza, na zitaendelea kuwaponza, uhuru wao, haki zao, hadi maisha yao, na wengine zikiwaponza wasikamate ulaji for being too vocal or too critical to the current regime, imewa cost kwa sababu tuu ya kusema ukweli!, katika utetezi wa kweli wa haki za binaadamu, mimi naamini ipo siku iso jina, hawa unsung heroes wa JF wakiongozwa na Maxence Melo, Mike na wana jf wengine wote, na jf yetu, italipwa kwa mema yote inayo watendea Watanzania, na itakumbukwa na kuja kupewa tuzo, na hawa baadhi ya mawakili wanaojinasibu ni watetezi wa haki za binaadamu ilhali kiukweli ni watetezi tuu wa matumbo yao, nao pia watalipwa kwa utetezi wao!.
Wasalaam
Paskali
That was 2016, leo ni 2019
Lisemwalo...
Hatimaye

Habari wakuu,

Leo Mkurugenzi na Mwanzilishi wa JamiiForums, anapokea tuzo kutoka CPJ. Fuatilia hii link hapa chini kujua kinachojiri.

Asante sana kwa hii kitu
P
 
Wakuu,

Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru watanzania kwa ujumla na hasa watumiaji wa mitandao ya kijamii na kwa namna ya kipekee wanachama wa JamiiForums kwa support ambayo tumekuwa tukiipata toka kwenu tangu mwanzo wa kesi hii hadi mwisho wake.
mawakili wangu wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala wamewasilisha notisi ya kukata rufaa na imepokelewa (nakala ipo chini). Jopo la Mawakili linawahusisha Benedict Alex Ishabakaki, Peter Kibatala, Jebra Kambole na Jeremiah Mtobesya.

Wito wangu: Kwa umoja wetu, tuendelee kushirikiana kuhakikisha Uhuru wa Kujieleza unalindwa na watoa taarifa zenye nia ya kufichua maovu ndani ya jamii wanalindwa bila kupewa vitisho vya aina yoyote. Mwananchi mwenye taarifa ni nguzo muhimu kwa ukuaji wa demokrasia ya kweli.

Natambua kazi ngumu na ya kizalendo inayofanywa na Jeshi la Polisi, naheshimu sana mamlaka za dola na kutambua kuwa kuna wakati mambo mengine yanahitaji ushirikiano wetu wananchi katika kuweza kutoa huduma nzuri kwetu kama raia; lakini nadhani bila mfumo unaoeleweka wa kuchakata taarifa za watumiaji wa digital platforms, tutajikuta badala ya kuimarisha jamii inayotoa ushirikiano tunawavunja moyo wananchi hivyo wakafumbia macho maovu wanayoyaona katika jamii.

Hawa ni miongoni mwa watetezi wa kweli wa haki za binaadamu Tanzania,
P
 
Je Mkuu wadhani Mungu halipi? Ama wadhani uhalifu au udhalimu unaolindwa na wanadamu huwa haulipwi? Sihitaji kukumbusha mengi ila jiweke kwenye familia za Azory Gwanda, Ben Saanane, na wengineo wengi ambao tunawajua na tusiowajua ambao walinyanyaswa na walinyanyasika huku 'media na raia wakitazama na wengine kushangilia madhila"
Mkuu Mwanamageuko , karibu pande hizi, ili ushuhudie utetezi wa haki, sikuanza leo!.
P.
 
Wanabodi,

Hii ni thread ya swali kuhusu watu wanaoitwa watetezi wa kweli wa haki za binaadamu Tanzania, ni kina nani? (human right defenders). Haki za binaadamu ni jambo la kikatiba na kisheria, hivyo watetezi wa kweli wa haki za binaadamu, walipaswa kuwa ni wanasheria, lakini kwa upande wa Tanzania, jee wanasheria wetu tulionao ni watetezi wa kweli wa haki za binaadamu au ni watetezi wa matumbo yao kwa malipo ya uwakili kwa kisingizio cha kutetea haki za binaadamu?. Ili wakili uwe ni mtetezi wa kweli wa haki za binaadamu, inakubidi utetee bure. Jee mawakili wetu wanatetea haki za binaadamu bure?.

Nasi JF kwa ujumla wake, tunastahili pongezi na hongera za dhati kwa utetezi huu, hizi kelele tunazopiga humu kuhusu ukiukwaji wa haki za binaadamu, haki za kisiasa, uhuru wa kujieleza, uhuru wa habari, haki ya kupata habari, haziendi bure. Hivyo swali linabaki, kwa mawazo yako, jee JF tunastahili kuwamo kwenye list ya watetezi wa kweli wa haki za binaadamu, nchini Tanzania au jf ni wachafuzi tuu kwa kupinga kila kitu cha awamu hii?.

Wasalaam

Paskali
Mbona hukuwahi kuandika kabla? Kaka, hebu acha ndio maana unakosa teuzi.
Mkuu Elli Mshana , karibu pande hizi na uangalie tarehe ya bandiko!.
P
 
Wanabodi,

Lakini miongoni mwa watetezi wa kweli kabisa na wa dhati wa haki za binaadamu nchini Tanzania, ni huu mtandao wetu wa JamiiForums au jf, watu humu wanapaaza sauti zao kutetea haki za binaadamu bila kutegemea kulipwa chochote na yeyote, na wengine sauti zao humu jf zimewaponza, zinawaponza, na zitaendelea kuwaponza, uhuru wao, haki zao, hadi maisha yao, na wengine zikiwaponza wasikamate ulaji for being too vocal or too critical to the current regime, imewa cost kwa sababu tuu ya kusema ukweli!, katika utetezi wa kweli wa haki za binaadamu, mimi naamini ipo siku iso jina, hawa unsung heroes wa JF wakiongozwa na Maxence Melo, Mike na wana jf wengine wote, na jf yetu, italipwa kwa mema yote inayo watendea Watanzania, na itakumbukwa na kuja kupewa tuzo, na hawa baadhi ya mawakili wanaojinasibu ni watetezi wa haki za binaadamu ilhali kiukweli ni watetezi tuu wa matumbo yao, nao pia watalipwa kwa utetezi wao!.

Kwa maoni yangu, nadhani JF wakiongozwa na Maxence Melo na Mike ni miongoni mwa vinara watetezi wa kweli kabisa wa haki za binaadam nchini Tanzania, angalia kila uchao wanavyohangaika na kukabiliwa na mlolongo wa kesi mahakamani zisizo na kichwa wala miguu.

Nasi JF kwa ujumla wake, tunastahili pongezi na hongera za dhati kwa utetezi huu, hizi kelele tunazopiga humu kuhusu ukiukwaji wa haki za binaadamu, haki za kisiasa, uhuru wa kujieleza, uhuru wa habari, haki ya kupata habari, haziendi bure.

Wasalaam

Paskali
JF IIinyongwa na Magufuli na mlishangilia sana including you. Wewe ulibaki hai kiuandishi kwa sababu ulikuwa side ya opressor.
Mkuu kamili, hivi kweli mtu aliyeandika bandiko hili alishangilia ?.

P
 
Wanabodi,

Hii ni thread ya swali kuhusu watu wanaoitwa watetezi wa kweli wa haki za binaadamu Tanzania, ni kina nani? (human right defenders). Haki za binaadamu ni jambo la kikatiba na kisheria, hivyo watetezi wa kweli wa haki za binaadamu, walipaswa kuwa ni wanasheria, lakini kwa upande wa Tanzania, jee wanasheria wetu tulionao ni watetezi wa kweli wa haki za binaadamu au ni watetezi wa matumbo yao kwa malipo ya uwakili kwa kisingizio cha kutetea haki za binaadamu?. Ili wakili uwe ni mtetezi wa kweli wa haki za binaadamu, inakubidi utetee bure. Jee mawakili wetu wanatetea haki za binaadamu bure?.

Wasalaam

Paskali
MEI 3 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa vyombo vya habari, Mimi Pascal Mayalla, kwa niaba yangu kama mwanahabari na kwa niaba ya kampuni yangu ya PPR as chombo cha habari, niwatakie wanahabari wenzangu wote, maadhimisho mema ya siku hii, huku nikidurusu, niliwahi kusema nini kuhusu uhuru wa habari Kwa media za Tanzania yetu.

Nawatakia uhuru wa habari mwema.
Paskali.
 
Wanabodi,

Nimepandisha uzi huu baada ya kuguswa na tukio la mawakili wa Arusha, kuandamana kutetea haki za wakili mwenzao, aliyezuiliwa kule Loliondo.

Paskali
Je sisi JF, tutume our own independent team Ngorongoro?.
Kuna uwezekano mkubwa wa kabila la Kiiraqw lilopo mkoa wa Manyara kupotea kabisa au asili ya watu hawa kupotea kabisa siku za mbeleni na hasa ukizingatia na udogo wa kabila lenyewe.

Hii ni kutokana na sheria zao kali za kimila zinazoweka mazingira magumu sana ya wenyewe kwa wenyewe kuoana na kusababisha asilimia kubwa ya watu kulazimika kuoa au kuolewa na makabila mengine, sisemi kama kuna ubaya kuoa au kuolewa na makabila mengine.

Katika hili kabila kuna kitu kinaitwa DAWI, maana ya DAWI ni uhusiano wa kikoo au kidamu kati ya watu wawili, hata kama ni kitukuu wa kitukuu ambaye Bibi yake ni ukoo wako basi huwezi kumuoa au kuolewa naye kwasababu atakuwa ni DAWI yako.

Sasa kutokana na udogo wa hili kabila vijana wengi walioanzisha uhusiano wamejikuta wameingia kwenye huo mtego na kushindwa kuoana.
Hawa ndio wenye Bonde la Ngorongoro
Mwaka 1959, serikali ya mkoloni ya Mwingereza iliwahamisha Wamasai kutoka mbuga ya Serengeti, na walihamishiwa Ngorongoro, ili Serengeti wabaki wanyama tuu, na Ngorongoro, iwe na wafugaji na wanyama Pori, ila hawakuruhusiwa kulima wala kujenga makazi ya kudumu, walipewa huduma zote bure. Wamasai wakazidi kuongezeka huku wenye Ngorongoro yao wakizidi kusinyaa.

Hivyo serikali inapopanga kuwahamishia Lushoto is doing the right thing. Ila kuhama huku ni kwa hiyari hakuna ansyehamishwa kwa nguvu.
Tuiaminie Serikali yetu ina nia na dhamira njema na raia wake wote wakiwemo wana Ngorongoro.
P
 
Back
Top Bottom