Watetezi Wa Kweli wa Haki za Binaadamu Tanzania ni Kina Nani?!, Jee JF Tumo?!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,181
Wanabodi,

Hii ni thread ya swali kuhusu watu wanaoitwa watetezi wa kweli wa haki za binaadamu Tanzania, ni kina nani? (human right defenders). Haki za binaadamu ni jambo la kikatiba na kisheria, hivyo watetezi wa kweli wa haki za binaadamu, walipaswa kuwa ni wanasheria, lakini kwa upande wa Tanzania, jee wanasheria wetu tulionao ni watetezi wa kweli wa haki za binaadamu au ni watetezi wa matumbo yao kwa malipo ya uwakili kwa kisingizio cha kutetea haki za binaadamu?. Ili wakili uwe ni mtetezi wa kweli wa haki za binaadamu, inakubidi utetee bure. Jee mawakili wetu wanatetea haki za binaadamu bure?.

Nimepandisha uzi huu baada ya kuguswa na tukio la mawakili wa Arusha, kuandamana kutetea haki za wakili mwenzao, aliyezuiliwa kule Loliondo. Mawakili hao, wamejiita ni watetezi wa haki za binaadamu, swali ni jee ni watetezi wa kweli wa haki za binaadamu, au utetezi huu umekuja kwa vile tuu wakili mwenzao ameguswa?, hivyo wanachopigania mawakili hao ni haki za binaadamu, au wanapigania haki za wakili mwenzao aendelee kuvuta malipo ya uwakili kwa ajili ya matumbo yao?.

Naungana na mawakili wasomi wote ambao hutetea haki za binaadamu wote bure bila malipo na bila ubaguzi, kikiwemo kitengo cha msaada wa kisheria cha chuo kikuu cha Dar es Salaam lakini siungi mkono utetezi wa haki za binaadamu kwa sababu tuu aliyeguswa ni wakili mwenzao, hivyo siungi mkono maandamano ya mawakili Arusha, kumtetea wakili mwenzao as if huyo wakili haki zake zikivunjwa, ndio aandamaniwe, lakini kila siku haki za wananchi wengine wengi wa kawaida, zinavunjwa kila siku, sijawahi kuwasikia mawakili hawa hata wakikohoa tuu, achilia wakiandamana!. Hivyo kuandamana kule, mimi nakuchukulia ni kuandamana kwa kupeleka machozi ya mamba (crocodile tears), kwa kisingizio cha kutetea haki za binaadamu, ila kinachoandamaniwa ni matumbo yao kwa malipo ya uwakili na sii haki za binaadamu!.
Tangu Mhe. rais Dikiteta (Mzalendo), Dr. John Pombe Magufuli, ameingia madarakani, amefanya vitendo vingi vya kidikiteta, uvunjaji wa katiba, sheria taratibu na kanuni, kwa kauli na matendo, ikiwemo kuivunja katiba au kuiweka pembeni, sijasikia hao wanaojiita mawakili wasomi, au watetezi wa haki za binaadamu, wakikemea au kuandamana!, leo wakili kaguswa ndio waandamane?, nasema no!.

Hivi ni baadhi ya vitendo vya kidikiteta vya Mhe. Rais, Dr. John Pombe Magufuli, amevifanya vikikiuka katiba, na haki za binaadamu, lakini badala la mawakili wasomi hawa kukemea, kwa kutumia vifungu vya kisheria, ndio kwanza wamekaa kimya!, leo wakili mwenzao kaguswa ndio waje na utetezi hadi wa maandamano?, wanaandamania haki za binaadamu au haki ya wakili mwenzao aendelee kuvuta malipo ya uwakili hivyo wanaandamania matumbo yao?.

1. Alivunja katiba kwa kuingilia uhuru wa watu kujipumzikia siku ya uhuru na kuwalazimisha kufanya kazi!. Mtu yuko huru kuamua kufanya kazi, au kutofanya kazi yoyote, hivyo kumlazimisha mtu kufanya kazi, ni kuingilia uhuru wake binafsi!. Sikuona watu wakikemea!, sisi humu jf, tulikemea!.
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...

2. Alilazimisha watu kufanya kazi ya usafi kwa lazima!. Kila mtu yuko huru, kufanya kazi yoyote anayoipenda!, kitendo cha kuwalazimisha watu kufanya kazi fulani ni kinyume cha haki za binaadamu na kinyume cha sheria za kimataifa za uhuru wa kazi za ILO, sikuona watu wakikemea, humu jf tulikemea!.
Amri ya Rais Kuifuta Siku ya Uhuru Haijataja Usafi!. Jee Usafi ni ...

3. Alipotoa amri ya kuwataka maofisa wote wa serikali, kuomba kibali kwake kusafiri nje ya nchi, kitendo hiki kimekwenda kinyume cha haki za binaadamu kwenye freedom of movement, sikuona watu wakikemea, humu tulikemea!.
Je, Huu Sio Uvunjaji wa Haki Za Msingi za Binaadamu Unaofanywa na ...

4. Rais ni mkuu wa mhimili mmoja tuu wa dola, the executives, amri ile ya kutosafiri, kwa mihimili yote kuomba ruhusa kwake, ilikiuka haki za mihimili mingine na kuingilia uhuru wao kinyume cha kanuni ya checks and balance, na the separation of powers, hakuna aliyepigia kelele hili. Humu jf, tulipigia kelele!.
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki ...

5. Katika hotuba yake alilaani wanaopata mishahara mikubwa, akaiita ni mishahara ya peponi, akaahidi hakuna mtumishi atakayelipwa zaidi ya TZS 15.M!, rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa yoyote ambao ulikisha pangwa na vyombo husika!, kauli hiyo ni kinyume cha haki ya the right to renumeration, hakuna aliyepigia kelele kauli hii, humu jf, tuliipigia kelele!.
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote ...

6. Katika baadhi ya tumbua tumbua majipu, zoezi hilo lilifanyika kwa masifa, papara na kukurupuka, kinyume cha sheria, taratibu na kanuni, lakini pia kinyume cha msingi mkuu wa utoaji haki, ikiwemo, "no one is condemned unheard" watu wanatuhumiwa na kuhukumiwa papo kwa papo kwa kutumbuliwa bila kupewa haki ya kusikilizwa!, hakuna waliokemea hili, sisi humu jf tulikemea!.
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ...

7. Utekelezaji wa baadhi tumbua tumbua umefanyika kwa udhalilishaji mkubwa wa utu wa mtu, huku ukifanyika kwa double standards za hali ya juu, kwa wengine kutumbuliwa kwa heshima "kupangiwa kazi nyingine", huku wengine "uteuzi wao ukisitishwa", "ukitenguliwa" na kuna waliofukuzwa kama mbwa!, hakuna waliokemea ukiukwaji huu mkubwa wa haki za binaadamu, sisi hapa jf tulipigia kelele!.
Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...
Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili ...

8. Rais wa JMT ni rais wa nchi, na pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama, hivyo kuna kauli akitoa, kauli hizi huwa ni amri na hazina mjadala!. Alipowaamuru polisi, kumalizana na majambazi wanaotumia silaha, "wasiinuke", hakuna waliopigia kelele kauli kama hizi, za vitisho, kidikiteta na kinyume cha utawala wa sheria, hakuna watetezi wa haki za binaadamu waliopigia kelele hili, sisi humu jf, tumelipigia kelele.
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...

9. Jeshi letu la polisi limekuwa likifanya brutality ya hali ya juu, hao wanaojiita watetezi wa haki za binaadamu, siwaoni wakilipigia kelele hili, sisi humu jf tumelipia kelele sana tuu!.
IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality ...
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa ...
Waziri Nchimbi na IGP Mwema, Mnasubiri Nini Kujiuzulu ...

10. Ukandamizaji wa freedom of expression, freedom of association, freedom of movements, utumiaji wa barbaric laws, uminyaji wa uhuru wa vyombo vya habari, haki ya kupata habari, freedom of assembly, rights to privacy, kila siku vinakiukwa lakini watetezi wa haki za binaadamu, hatuwaoni wakipigia kelele vitendo hivi, lakini sisi humu jf tunavipigia kelele huku tukifanya maandamano ya threads, sasa nani ni watetezi halisi wa haki za binaadamu nchini Tanzania kati ya wanasheria wajua haki, ambao walipaswa kutetea na wananchi wa kawaida wasio jua kitu, lakini wakipaza saudi zao kupigia kelele vitendo hivi?!.
Mifano hiyo na mingine mingi ni ushahidi tosha kuwa wengi wa wanaojiita ni watetezi wa haki za binaadamu nchini Tanzania , kiukweli sio watetezi halisi wa haki za binaadamu, bali ni wapigania matumbo yao kwa mwamvuli wa haki za binaadamu, wakiishashibishwa fedha za wafadhili, hupaaza sauti zao sana tuu kuhusu ukiukwaji wa haki za binaadamu ili tuu wafadhili wawasikie, lakini ndani ya mioyo yao, ndani ya nafsi zao na ndani ya dhamira zao, hakuna utetezi wowote wa kweli wa haki za binaadamu zaidi ya kupigania matumbo yao!, kwa sababu mawakili au wanaharakati, wengi wao ni watu wa mshahara!.

Lakini miongoni mwa watetezi wa kweli kabisa na wa dhati wa haki za binaadamu nchini Tanzania, ni huu mtandao wetu wa JamiiForums au jf, watu humu wanapaaza sauti zao kutetea haki za binaadamu bila kutegemea kulipwa chochote na yeyote, na wengine sauti zao humu jf zimewaponza, zinawaponza, na zitaendelea kuwaponza, uhuru wao, haki zao, hadi maisha yao, na wengine zikiwaponza wasikamate ulaji for being too vocal or too critical to the current regime, imewa cost kwa sababu tuu ya kusema ukweli!, katika utetezi wa kweli wa haki za binaadamu, mimi naamini ipo siku iso jina, hawa unsung heroes wa JF wakiongozwa na Maxence Melo, Mike na wana jf wengine wote, na jf yetu, italipwa kwa mema yote inayo watendea Watanzania, na itakumbukwa na kuja kupewa tuzo, na hawa baadhi ya mawakili wanaojinasibu ni watetezi wa haki za binaadamu ilhali kiukweli ni watetezi tuu wa matumbo yao, nao pia watalipwa kwa utetezi wao!.

Kwa maoni yangu, nadhani JF wakiongozwa na Maxence Melo na Mike ni miongoni mwa vinara watetezi wa kweli kabisa wa haki za binaadam nchini Tanzania, angalia kila uchao wanavyohangaika na kukabiliwa na mlolongo wa kesi mahakamani zisizo na kichwa wala miguu.

Nasi JF kwa ujumla wake, tunastahili pongezi na hongera za dhati kwa utetezi huu, hizi kelele tunazopiga humu kuhusu ukiukwaji wa haki za binaadamu, haki za kisiasa, uhuru wa kujieleza, uhuru wa habari, haki ya kupata habari, haziendi bure. Hivyo swali linabaki, kwa mawazo yako, jee JF tunastahili kuwamo kwenye list ya watetezi wa kweli wa haki za binaadamu, nchini Tanzania au jf ni wachafuzi tuu kwa kupinga kila kitu cha awamu hii?.

Namalizia kwa lile swali la msingi, jee watetezi wa kweli wa haki za binaadamu Tanzania ni kina nani?, Jee jf tumo?, Jee hawa wanasheria wetu tulionao ni watetezi wa kweli wa haki za binaadamu au ni watetezi wa matumbo yao kwa kisingizio cha kutetea haki za binaadamu?.

Wasalaam

Paskali
 
Namshukuru walau Mzee wa Upako kwa kujitokeza na kukemea yanayoendelea katika hii serikali maana watu wengine wakiwemo wasomi kama hao mawakili,viongozi wa dini,viongozi wa vyama vya wafanyakazi,viongozi wastaafu na hata waandishi wa habari kwa kiasi fulani wote wako kimya kwenye swala zima la kukosoa hii serikali.

Wazalendo wa nchi hii wako JamiiForums na kwenye vyama vya upinzani.
 
Mkuu Pasco ,

Sikubaliani na wewe Dikteta(Uchwara) kumpa hadhi ya Dikteta(Mzalendo)

Tuanzie hapo tu kwanza hayo mengine tutawekana sawa

Ila nimecheka sana kwa jinsi ulivyopanga mtiririko huu
Mkuu Ben Saanane, kwenye hili la udikiteta mzalendo, bora tukubaliane kutokukubaliana, kwa sababu, wengi wanaangalia tuu, rais Magufuli anafanya udikiteta gani, lakini ni wachache tunaoangalia the motive behind udikiteta huu!, kwa kumsikiliza Magufuli kwa kauli na matendo, he is very genuine, anayafanya hayo yote kwa nia njema na moyo safi, wa kuikomboa Tanzania, kwa sababu, haki, utawala wa sheria, utawala bora ndio vimetufikisha hapa tulipo, usimwite ni dikiteta uchwala, Magufuli ni dikiteta kweli ila ni mzalendo!, kitu ninachokubaliana na wewe, ni the dividing line between dikiteta kweli na dikiteta mzalendo ni very thin!, na madikiteta wote duniani walianza hivi hivi, kwanza kwa kuwa populist leaders, kisha dikiteta mzalendo na mwisho wa siku kugeuka kuwa a real dictator!.

Pasco
 
Mkuu chukua like za kutosha!!!
 
Mm nmeshangazwa na sheria za Utumishi wa Umma kuvunjwa na ikulu....kada kuwa DAS!! Na maadhi ya watumishi wa CCM kuwa na cheque number za utumish yaani mishahara yao inatoka utumishi.
 
Jf imekuwa sehemu ya watetezi Wa haki za binadamu kusemea watanzania wengi wazalendo imekuwa sehemu ya kusemea jf ni watetezi Wa haki za binadamu wengi tunapaza sauti kupitia jf
 
Kinachonipa furaha na matumaini mema ni kuwa, kwa sasa hatuongelei tena au kulalamika kuhusu wizi wa mali za asili za taifa au ufisadi ndani ya serikali ambao serikali inaufumbia macho.

Hatuongei na kulalamika kuhusu udhaifu wa serikali wakati mali za asili zinaibwa.

Kwa sasa tumebaki kwenye hoja kama udikteta ambazo mtazamo wake unatofautiana kati ya mtu na mtu au nchi na nchi.

Wengine wanadai udikteta uchwara, wengine wakidai udikteta uzalendo huku wengine wakisema hakuna udikteta bali ni usimamizi madhubuti wa sheria zilizotungwa na chombo halali ambazo zinajenga mazingira ya kidikteta.

Haya ni mafanikio makubwa sana kwa kipindi kifupi.
 
Magufulu sio dictector bali ana walk tha talk, hajawai kuvunja sheria za nchi yote anayoyafanya ndio watanzania tumekuwa tukililia kwa muda mrefu sasa yy kaamua kutenda so kwa vile ww umpendi ndo umuite dictator at the end utajua tu unapoteza muda
 
Wanabodi,

Nimeguswa na tukio la mawakili wa Arusha, kuandamana kutetea haki za wakili mwenzao, aliyezuiliwa kule Loliondo. Mawakili hao, wamejiita ni watetezi wa haki za binaadamu, swali ni jee ni watetezi wa kweli wa haki za binaadamu, au wapigania matumbo yao kwenye malipo ya uwakili?!.

Naungana na mawakili wasomi kutetea haki za binaadamu wote bila ubaguzi, lakini siungi mkono maandamano ya mawakili Arusha, kumtetea wakili mwenzao as if huyo wakili haki zake zikivunjwa, ndio aandamaniwe, lakini haki za wananchi wengine wengi zinavunjwa kila siku, sijawahi kuwasikia mawakili hawa hata wakikohoa tuu, achilia wakiandamana!. Hivyo kuandamana kule, mimi nakuchukulia ni kuandamana kwa kupeleka machozi ya mambo kwa kisingizio cha kutetea haki za binaadamu, ila kinachoandamaniwa ni matumbo yao na sii haki za binaadamu!.

Tangu Mhe. rais Dikiteta (Mzalendo), Dr. John Pombe Magufuli, ameingia madarakani, amefanya vitendo vingi vya kidikiteta, uvunjaji wa sheria kwa kauli na matendo, ikiwemo kuivunja katiba au kuiweka pembeni, sijasikia hao wanaojiita mawakili wasomi, au watetezi wa haki za binaadamu, wakikemea au kuandamana!.

Hivi ni baadhi ya vitendo vya kidikiteta vya Mhe. Rais, Dr. John Pombe Magufuli, amevifanya vikikiuka katiba, na haki za binaadamu, lakini badala la mawakili wasomi hawa kukemea, walikaa kimya!.

1. Alivunja katiba kwa kuingilia uhuru wa watu kujipumzikia siku ya uhuru na kuwalazimisha kufanya kazi!. Mtu yuko huru kuamua kufanya kazi, au kutofanya kazi yoyote, hivyo kumlazimisha mtu kufanya kazi, ni kuingilia uhuru wake!. Sikuona watu wakikemea!, sisi humu jf, tulikemea!.
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...

2. Alilazimisha watu kufanya kazi ya usafi kwa lazima!. Kila mtu yuko huru, kufanya kazi yoyote anayoipenda!, kitendo cha kuwalazimisha watu kufanya kazi fulani ni kinyume cha haki za binaadamu na kinyume cha sheria za kimataifa za uhuru wa kazi za ILO, sikuona watu wakikemea, humu jf tulikemea!.
Amri ya Rais Kuifuta Siku ya Uhuru Haijataja Usafi!. Jee Usafi ni ...

3. Alipotoa amri ya kuwataka maofisa wote wa serikali, kuomba kibali kwake kusafiri nje ya nchi, kitendo hiki kimekwenda kinyume cha haki za binaadamu kwenye freedom of movement, sikuona watu wakikemea, humu tulikemea!.
Je, Huu Sio Uvunjaji wa Haki Za Msingi za Binaadamu Unaofanywa na ...

4. Rais ni mkuu wa mhimili mmoja tuu wa dola, the executives, amri ile ya kutosafiri, kwa mihimili yote kuomba ruhusa kwake, ilikiuka haki za mihimili mingine na kuingilia uhuru wao kinyume cha kanuni ya checks and balance, na the separation of powers, hakuna aliyepigia kelele hili. Humu jf, tulipigia kelele!.
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki ...

5. Katika hotuba yake alilaani wanaopata mishahara mikubwa, akaiita ni mishahara ya peponi, akaahidi hakuna mtumishi atakayelipwa zaidi ya TZS 15.M!, rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa yoyote ambao ulikisha pangwa na vyombo husika!, kauli hiyo ni kinyume cha haki ya the right to renumeration, hakuna aliyepigia kelele kauli hii, humu jf, tuliipigia kelele!.
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki ...

6. Katika tumbua tumbua majipu, zoezi hilo lilifanyika kwa masifa, kinyume cha sheria, taratibu na kanuni, lakini pia kinyume cha msingi mkuu wa utoaji haki, ikiwemo, "no one is condemned unheard" watu wanahukumiwa na kutumbuliwa bila kupewa haki ya kusikilizwa!, hakuna waliokemea hili, sisi humu jf tulikemea!.
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ...

7. Utekelezaji wa baadhi tumbua tumbua umefanyika kwa udhalilishaji mkubwa wa utu wa mtu, huku ukifanyika kwa double standards za hali ya juu, kwa wengine kutumbuliwa kwa heshima "kupangiwa kazi nyingine", huku wengine "uteuzi wao ukisitishwa", "ukitenguliwa" na kuna waliofukuzwa kama mbwa!, hakuna waliokemea ukiukwaji huu mkubwa wa haki za binaadamu, sisi hapa jf tulipigia kelele!.
Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...
Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili ...

8. Rais wa JMT ni rais wa nchi, na pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama, hivyo kuna kauli akitoa, kauli hizi huwa ni amri na hazina mjadala!. Alipowaamuru polisi, kumalizana na majambazi wanaotumia silaha, "wasiinuke", hakuna waliopigia kelele kauli kama hizi, za vitisho, kidikiteta na kinyume cha utawala wa sheria, hakuna watetezi wa haki za binaadamu waliopigia kelele hili, sisi humu jf, tumelipigia kelele.
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...

9. Jeshi letu la polisi limekuwa likifanya brutality ya hali ya juu, hao wanaojiita watetezi wa haki za binaadamu, siwaoni wakilipigia kelele hili, sisi humu jf tumelipia kelele sana tuu!.
IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality ...
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa ...
Waziri Nchimbi na IGP Mwema, Mnasubiri Nini Kujiuzulu ...

10. Ukandamizaji wa freedom of expression, utumiaji wa barbaric laws, uminyaji wa uhuru wa vyombo vya habari, haki ya kupata habari, freedom of assembly, freedom of associations, rights to privacy, kila siku vinakiukwa lakini watetezi wa haki za binaadamu, hatuwaoni, sisi jf angalau angalau, sasa nani ni watetezi halisi wa haki za binaadamu?!.

Mifano hiyo na mingine mingi ni ushahidi tosha kuwa wengi wa wanaojiita ni watetezi wa haki za binaadamu, kiukweli sio watetezi halisi, bali ni wapigania matumbo yao kwa mwamvuli wa haki za binaadamu, wakiishashibishwa fedha za wafadhili, hupaaza sauti zao ili wafadhili wawasikie, lakini ndani ya nafsi zao, hakuna utetezi wowote wa haki za binaadamu zaidi ya kupigania matumbo yao!, kwa sababu mawakili au wana harakati, wengi wao ni watu wa mshahara!.

Lakini mtetezi wa kweli wa haki za binaadamu ni jf, watu wanapaaza sauti humu bila kutegemmea kuipwa chochote na wengine sauti zao humu jf zimewaponza, wasikamate ulaji, kwa sababu ya kusema ukweli!.

Hongera sana jf kwa utetezi wa kweli wa haki za binaadamu!.

Hongera jf, viva jf.

Pasco

Pasco umeandika vizuri, mawakili siku zote ni wavhumia tumbo.wabadirike
 
Mkuu Ben Saanane, kwenye hili la udikiteta mzalendo, bora tukubaliane kutokukubaliana, kwa sababu, wengi wanaangalia tuu, rais Magufuli anafanya udikiteta gani, lakini ni wachache tunaoangalia the motive behind udikiteta huu!, kwa kumsikiliza Magufuli kwa kauli na matendo, he is very genuine, anayafanya hayo yote kwa nia njema na moyo safi, wa kuikomboa Tanzania, kwa sababu, haki, utawala wa sheria, utawala bora ndio vimetufikisha hapa tulipo, usimwite ni dikiteta uchwala, Magufuli ni dikiteta kweli ila ni mzalendo!, kitu ninachokubaliana na wewe, ni the dividing line between dikiteta kweli na dikiteta mzalendo ni very thin!, na madikiteta wote duniani walianza hivi hivi, kwanza kwa kuwa populist leaders, kisha dikiteta mzalendo na mwisho wa siku kugeuka kuwa a real dictator!.

Pasco

Pasco stop that! Hakuna dikiteita mwema. Mpaka hapa watu wanaumia kwa kukosa haki zao bila kusikilizwa. Hilo tu linatosha. Please Pasco stop that
 
Nimemkumbuka Ben.

Paskali
Paskali umepotea. Tunataka kusikia kaulu yako kuhusu kupotea kwa Ben. Hatujui kapoteaje lakini kuna hisia nyingi. Nadhani umezisikia. Ebu tupe philosophical analysis of those rumors!
Leo kapotea huyu , hayanihusu, kesho itakuwa wewe maana wewe ni mwandishi hujui kesho ukiandika utamuudhi nani? Ni vitu vya kukemea.
 
Mkuu Retired, kuhusu kutoonekana kwa Ben, sio tuu kwamba tumeisha sema humu, bali pía we don't rule out, the possibility of an inside job.

Paskali
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom