Hoja hii ni potofu, Uvivu ni hulka ya kibinaadamu wala haijengeki kwa misingi ya Kitaifa, rangi, kabila wala Jinsia. hata walioandika THEORY X AND THEORY Y nawadhungu na walifanya utafiti kwenye Jamii zao za kidhungu, maana yake ni kwamba wavivu wamejaa na kuenea dunia nzima.
Pili unapofanya analysis kwa kuangalia wakenya 2 au mganda mmoja katikati ya watanzania 300 unakuwa unafanya kosa kubwa sana la sampling, matokeo ya utafiti wa namna hii yanakuwa yameharika kuanzia hapo. Sisi tuliofanya kazi huko huko Majumbani kwao tunajua namna na wao walivyokuwa wavivu na wajinga.
Mkuu Sangarara,
Nimefurahi sana kwa kuona mchango wako, wachangiaji wengi ni wavivu wa kufikiri lakini kwa bahati mbaya hawajui kwamba wanafikiria kivivu.
Wavivu wapo kila mahali duniani na wachapakazi wapo pia na mara nyingi uvivu unaanzia kwenye akili ya mtu mwenyewe.
Ni muhimu kuchukua tahadhari ya mawazo kama haya ya kusema watz ni wavivu generally, kwani yanaweza kuwa yamebuniwa kwa makusudi ya kuendeleza ukoloni mamboleo.
Yaweza kuwa mbinu ya kuwadumaza kiakili na pia kuhalalisha ubaguzi na dhuluma kwani ili uweze kumtumikisha mtu lazima uteke kwanza fikra zake kwa kumuaminisha kwamba yeye yu duni.
Hata hivyo yawapasa watz popote pale walipo kujua kwamba ili waendelee ni lazima kufanya kazi kwa bidii, kwa kutumia akili zao kwa faida.