Watanzania Wengi ni Wavivu? The Moment of Truth!

Ungesema waZenj ningekuelewa kidogo.

Ngongo,
Napingana na wewe Wazenji wakomavu kuzidi sisi nenda Dar kaone wanavyopiga kazi kuanzia kuuza maji juice mpaka maduka, nenda Kahama kaone soko lote la mchele wamelikamata wao, Nenda Malawi, Nenda, Congo, nenda Angola, sisi wa Tanganyika ndiyo wavivu.
 
kiukweli kabisa watanzani ni wavivu hasa maeneo ya pwani yaani Tanga, zanzibar, na dar
 
mikonomiwili,

Nakuunga mikono miwili wacha mmoja.

Watanzania ni wavivu wa kutupwa. Makazini kila siku visingizio, leo kafa shangazi, kesho mjomba, kesho kutwa jirani, mtondo bibi.

Wote huo ni uvivu tu. Sasa wakifa ukienda wewe ndio watafufuka? kaa kazini ukimaliza muda wako wa kazi nenda. Ukiwaambia hivyo wanakwambia "huna imani". Sasa imani kwenye kifo?

Ndio maana hatuendelei. Ni mfumo mbaya wa kuwa kila kitu cha umma ndiyo umeua uwajibikaji.

Mijitu imekaa inataka kufanyiwa tu, viongozi wafanye hivi viongozi wafanye vile.

Mimi ningepiga marufuku hawa wagombea ubunge na wabunge wote kujidai kwenda kupeleka sijui mabati, sijui simenti, Huu mfumo ndio unauwa uwajibikaji na unaendeleza uvivu.

Leo unakuta kijiji kinauza mbao lakini hakina madesk kwenye shule zake. Huu ni uvivu wa hali ya juu.
Kwa mara ya kwanza wewe Punguani Ribosome umeongea point. JF wakirekebisha mambo desktop version ikianza kufanya kazi nitakugonga LIKE, I promise.
Tena uvivu wa wabongo unaanzia kwa presdaa kila kukicha yuko anaranda na njia tu hakai ofisini then anafuata Waziri Mkuu yeye anatoa matamko tu bila kufuatilia utekelezaji. Kifupi sisi wabongo ni wavivu wa kazi na wavivu wa kufikiri
 
Watanzania siyo wavivu, asilimia kubwa ya watanzania wavivu ni WAFANYAKAZI WA SERIKALINI ukianza na President-balozi wa nyumba kumi10.

Ulienda kwenye sekta binafsi ipi ukakuta wafanyakazi wavivu? Wakulima wapi ukakuta wana mashamba yenye rutuba lkn
hawalimi?

Hapa mleta mada alitakiwa aseme
wafanyakazi wa serikalini ni
wavivu.

Wakenya wao wana utaifa zaidi yaani kuanzia President-mwananchi wa Kenya. Serekali inafanya kazi ndiyo maana unaona wakenya wana idea mpya kila siku wana vision.

Ukienda Kenya utaona viwanda either binafsi au vya serikali, kinachofanikisha viwanda kuwepo na kusurvive ni sera nzuri na utawala bora. Ukienda mashambani wanalima kilimo cha kisasa, Wafugaji wanafuga kwelikweli si kubabaisha Compare to Tz hamna kiwanda zaidi ya Pombe, mashamba unauza kwa wazungu mzungu analeta expert toka kwao watz tunabakia kufanya kazi za kimanamba zisizolipa.
Wakenya wanasaidiana sana akiwa anafanya kazi mahali akisikia nafasi ya kazi lazima atamwambia rafiki/jamaa/ndugu yake Arusha wapo wengi kwenye mahoteli ya kitalii na kawaida wanaitana wapi uliona mtz anakuitia kazi, hatuna utaifa tuna ubinafsi wa mimi mimi.
Tatizo hapa Tz ni mfumo mbovu wa utawala Maendeleo yanaenda inversely proportional na mahitaji kila mtu anakula anavyojua. Leo hii wakenya wanakuja wanachukua maziwa hapa wanapeleka kwenye viwanda vya kwao wanapack wanarudisha hapa wanatuuzia, sasa hapo kuanzia kwa mfugaji mpaka kiwandani ni ajira ngapi zimekosekana hapo, general tyre umeua kiwanda kenya wakachukua formula sisi tumebaki kuwa walaji from ajira tumepoteza hapo sasa ni ajira/kazi ipi tutafanya sisi watz zaidi ya siasa na kuwa majizi. Watz siyo wavivu, Serikali ndiyo vivu
 
Hii statement iko general sana na haitoi picha halisi ya watanzania wengi. Kwa sababu umeongelea graduates basi ningependa kuamini unaongelea vijana walio mijini. Lakini kumbuka 80% ya watanzania wanaishi vijijini. Wanajilisha wenyewe, wanalima na kulisha huku mijini tena kwa kutumia jembe la mkono. Sasa hivi Mbeya wakulima wanalia, mazao yanaozea ndani, je, nani alilima hayo mazao, Wakenya? Serikali hii inayomiliki magari ya Tshs 5 trilion imeshindwa kujenga reli ya uhakika ili watu wasafirishe mazao yao kuja mijini! Hapo utamlaumu nani? Na mbaya zaidi, serikali inapiga kelele kuhusu kilimo kwanza lakini ni lini serikali hii ilikaa chini na watu wa vijijini na kujadili namna bora ya ku-implement kilimo kwanza? Matreka na power tillers ziko Dar, hela za kukopesha wakulima zimepelekwa TIB ambayo iko Dar, hata watu wa utabiri wa hali ya hewa wamejikita kutoa taarifa za mvua kwa watu wanaoishi mabondeni huku Dar. Wakulima wanaagalia mawingu kama 1800! Kwa kifupi watu wanaolisha hii nchi ni watanzania 80 % waliotelekezwa na serikali ya CCM. Year in year out, wakubwa wapanga mipango hapa Dar, wanaitekeleza kwa sytle wanayotaka hapa hapa Dar, wakulima wamebaki kama yatima. Lingine linaifanya nchi hii iwe kama kichwa cha mwenda wazimu ni 'weak industrial base' Wakubwa wameua viwanda na badala yake wamejigeuza mawakala wa viwanda vya nchi za nje. Kiwanda cha maziwa Arusha kimeuzwa kwa WaKenya, na matokeo wameng'oa hata mitambo na kupeleka kwao Kenya. Watanzania wamekosa ajira huku wakenya wakipata ajira. Tanganyika parkers haipo, kiwanda cha ngozi kimekufa, na ukitaka kuanzisha 'cottage industry (kiwanda kidogo) utakuta kuna mkubwa ana tenda ya vitu kama hivyo kwa bei chee toka China. Kwa mazingira haya huwezi ku-encourage watu waanzishe viwanda maana hakuna mkakati maalum wa kuwalinda. Na bado CCM wanataka kubaki madarakani!
Nakubaliana na wewe kwamba wakulima wanaangushwa na policy makers wetu. Lakini hilo hiliwaondoi wakulima na wanavijiji kwa jumla bado kwenye kundi la wavivu. Ni wanavijiji hao hao wanaofuga kuku kumi na mbuzi watatu wakati hakuna kinachowazui kufuga kuku au mbuzi 5000. Unakuta kijiji kiko kwenye barabara kuu kuelekea mjini (kwenye soko), kina maji, availability ya traditional animal feed etc. lakini mkulima kafuga kuku 10 tu. Huu ni uvivu tu. Ishu nyingine ni uvivu wa kufikiri, wananchi wavivu wa kufikiri so wanachagua watawala wavivu wa kufikiri
 
Ukiwa una compare Tanzania na nchi jirani kama kenya ama Uganda ama Rwanda utangundua kua watanzania ni wavivu kwa asilimia kubwa sana tofauti na mataifa mengine.

kunasiku Mkapa alitoa hii kauli lakini watu walimshambulia sana , lakini mimi naamini ukweli una uma na ndio maana walimshambulia. watanzania tunapenda kupiga stori tunapenda kushadadia mambo na tunachukia mambo ya kuumiza akili.

mfano mdogo tu ni unaweza kuta kijana ni graduate lakini eti ana kaa nyumbani akisingizia hana kazi na anasubiri mpaka eti kazi zitangazwe na ndipo afanye application. huyu kijana angeweza kufanya kazi yakujitolea hata sehemu yeyote ambayo ingemsaidia hata kupata kujuana na watu zaidi na hata kua na experience zaidi lakini ana oana haina maana kama kukaa nyumbani.

mfano mwingine una kuta mtu kaajiriwa ofisini lakini kufanya kwake kazi mapaka asukumwe mara kwamara . Napenda sana wakenya wanavyo fanya kazi wko so smart na hakuna mchezomchezo mara viruhusa vya hapanapale mara hayupo offisini. kusema kweli East Africa community ita tufanya tuwe watumwa wakenya kama tusipo angalia nafasi zote nyeti zitashikwa na wakenya na sisi tutabaki tunapiga kelele za umbeya na ushabiki.

Hii issue ilitokea south Africa ambapo wazungu walikua wana waajiri watu ambao walikua wanaona wana weza fanya kazi na baada ya muda ikawa wa south afrika wengi hawapo kwenye nafasi zajuu, ndo ikaja ile vita ya wahamiaji.

ukiongelea mambo ya siasa Tanzania utapata mashabiki kibao lakini ongelea swala la kumputer imetengenezwa vipi ama gari limetengenezwa vipi ama ni lini nasisi tutakua na kiwanda chetu. kusema kweli unaweza usipate mchango wowote. angalia tu ishu ya kanumba ilivyo chukua mudamrefu ikiongelewa lakini sijawahi sikia hata sikumoja kitu chochote chauvumbuzi kikiwa kinaongelewa hata kwa sikumoja.

Jamani Tanzania tubadilike tufanye kazi tuachane na uvivu. sisemi tusiongelee siasa kabisa hapana namaanisha kua angalau tuwe pia na vitu vyauvumbuzi amabavyo vitatuzaidia

kwanza nakushangaaaaaa. Kisha najiuliza hivi wewe ni mtanzania kweli? Hivi tupo wote hapa nchini kweli? Wewe fanya utafiti wa kina kisha ndio uje hapa kuongea na watu wenye fikra zao, huwezi kuchomoza kama uyoga na kudai unujua mbuyu wenye matunda kauotesha nani, wacha kupotosha. Katika kusoma kwangu nilipata kusoma somo linaitwa management, humo kuna usemi uliofanyiwa utafiti unadai kuwa binadamu hapendi kazi na kama angepata nafasi ange epuka kabisa kufanya kazi.. Unajua ni kwanini? Hiyo sio asilaya yetu, tulipewa adhabu baada ya makosa yetu kwa mwenyez Mungu. Ila hilo sio hoja sana kwa maana unaporojo zako zimenikera. Nianze hivi
1. Swala la ubunifu. We nimwongo sana, watanzania ni wabunifu na ubunifu upokila mahali isipo kua haupewi kipaumbele na serikali. Nianzie secta rasmi, hapo UDSM kitengo cha uhandisi ni hv juz tu mhadhiri wa hapo alikua akilaan utaratibu wa nchi hii kutotoa kipaumbele kwa mainjinia wake. Ataivyo pia aliongelea mchango wa maguful uliyo wezesha kutengenezwa mtreka pale, akasema pia yapo magar yameshabuniwa huku akionesha michoro ktk tv jins ya livyo na kusema kilichokua kimebakia ni uwezeshwaji tu.
B>Huku SIDO.
Jiulize mwenyewe sido inakipaumbele gan ktk serikal kwa sasa, sido ni kama imekufaa. Ukija huku mtaani kila siku wapo watu wanaibuka na ubunifu wao lakini wanapotezwa, wapo wagunduz wa kufua umeme, kutengeneza radio station na wanarusha matangazo yao na huyu mmoja nilikutana nae pale dodoma ktk maonesho ya nane nane anaitwa lamek yupo singida yeye kagundua mtambo wa kutengeneza mafuta ya biodizel kwa kutumia matunda ya miti fulani najua hadi anatoka pale ktk maonyesho lazma alishapewa onyo. Niseme serikal haina muda na wabunifu wetu.
2. Mwamko wa watu kufanya kazi. Tuanze na hawa watu wasio na elimu kubwa kama ulivyoonyesha wewe, hapa naona ni wazi hauna ushirikiano sana na maisha ya kijamii katika hali ya chini maana siku hizi hakuna kaz za jinsia, kama ni mafundi seremala, ujenz, machenical na umeme wote wapo unajua ni kwa ni nini, mwamko uko juu.
Kwa upande wetu wasomi ndio machozi yananilenga lenga, hivi unajua kama haujuan na mtu hata hiyo kaz ya kujitolea bure haupati. Hivi unajua vituko vinavyoendelea hapa nchini juu ya swala la ajira. Mwaka jana niliitwa ktk usaili pale UDOM lakin kabla ya kumaliza usaili tuligundua na ilikua kweli kwamba zile nafasi zilikua na watu tena walifanya usaili kabla yetu lakin tulituma maombi pamoja. Na usaili uliyofanyika chuon muccobs umesikia yaliyojiri pale, uongo ktk tarehe ya usaili ktk gazeti, kupewa vigezo vya usaili gafla kabla ya kuingia ktk vyumba vya usaili na kutokua na muda halisi wa kufanyika usaili.
Naomba tuje kuongelea jambo hili baada ya ukomboz wa hii nchi na ndio maana tunao mwamko zaidi katika siasa, we ajira inatangazwa ni vigezo vya uzoefu miaka sio chini ya mitatu hadi kumi na tano, graduet tukapate wapi huo uzoefu? Mama kabaka nae katangaza eti kazi za nje zipo uarabun lakin za ndani ya u house boy/girl, ndio wasomi wakazifanye?.
 
Mvivu ni wewe baba yako mama yako wajomba zako na jirani zako!
Watanzania wanafanya kazi sana tena sana, tunayo mifano mingi tu ya utendaji mzuri wa watanzania nchini tanzania. Tatizo lililopo ni mifumo mingi haijakamilika ya kitechnolojia ya kuweza kubaini nani anafanya kazi nani hafanyi kazi. Mfano we nenda ofisi nying ulaya utakuta ukiingia ofisini kuna sehemu unagusisha kadi, na inaerkodi muda, the ukitoka hivyo hivyo na hii inapelekea hata hao unaowaita wanafanya kazi kuwa wafanya kazi hata kama ni wavivu. Nakupatia mfano mwingine, nchi kama Norway wafanyakazi wanalindwa na sheria nyingi sana, wavivu wengine hutumia hizo sheria zinazowalinda kuchkua likizo ya ugonjwa hata mwaka mzima, na huyo mvivu anaendelea kulipwa mshahara wote kwa kipindi chote, je naye utamuitaje?? Usijilinagnishe na kenya hao ni mabebari, mifumo ya mabebari ni unyonyaji, kazi kubwa anakulipa msharara kidogo ili uendelee kumtumikia. Tanzania ni nchi yenye neema na watu wake ni wema na wanachapa sana kazi! nenda sehemu ambazo watanzania wameajiliwa kama Barrick uone kazi, nenda hata Bank of africa uone, acha ujinga kijana wa kuwadharau watanzania!!

Kweli wanafanya kazi sana na bado ni mafukara mno
 
Hata kidogo Watanzania Sio Wavivu Siasa Zetu zimetufanya kuwa watulivu sana mpaka Mnadhani ni Wavivu

Toka wewe Umezaliwa Umesha wahi kuishi bila chakula? labda bila pesa lakini ukilinganisha na hizo nchi ulizozitaja zote

zina matatizo ya Vyakula, Sisi ng'atu hata kidogo pamoja na wao kuwa na big farmers kama Kenya.

Ukiangalia hizo Nchi zilikuwa zinaendeshwa kibepari, sisi tulikuwa wasocialist hapo labda tulikuwa tunazuia Maendelea au

Ubunifu wa Wafanya Biashara wadogo lakini Sio Uvivu. HATA KIDOGO WATANZANIA SIO WAVIVU; LABDA WEWE!!!

Huu ndio mchango wa mtu mvivu, a typical tanzanian....naendelea kufuatilia wachangiaji wa uzi huu...
 
hilo ni sahihi kabisa.sio huko vijiweni tu hata hapa JF pia.mijadala ya siasa inawachangiaji wengi sana.jamaa mmoja aliwahi niambia tz inaongoza kwa wasomi wa political sciance kuliko taaluma zingine.

Idadi ya wasomi wa political science inalingana na ile ya WACHAMBUZI WA MPIRA MIGUU!
 
Mvivu ni wewe baba yako mama yako wajomba zako na jirani zako!
Watanzania wanafanya kazi sana tena sana, tunayo mifano mingi tu ya utendaji mzuri wa watanzania nchini tanzania. Tatizo lililopo ni mifumo mingi haijakamilika ya kitechnolojia ya kuweza kubaini nani anafanya kazi nani hafanyi kazi. Mfano we nenda ofisi nying ulaya utakuta ukiingia ofisini kuna sehemu unagusisha kadi, na inaerkodi muda, the ukitoka hivyo hivyo na hii inapelekea hata hao unaowaita wanafanya kazi kuwa wafanya kazi hata kama ni wavivu. Nakupatia mfano mwingine, nchi kama Norway wafanyakazi wanalindwa na sheria nyingi sana, wavivu wengine hutumia hizo sheria zinazowalinda kuchkua likizo ya ugonjwa hata mwaka mzima, na huyo mvivu anaendelea kulipwa mshahara wote kwa kipindi chote, je naye utamuitaje?? Usijilinagnishe na kenya hao ni mabebari, mifumo ya mabebari ni unyonyaji, kazi kubwa anakulipa msharara kidogo ili uendelee kumtumikia. Tanzania ni nchi yenye neema na watu wake ni wema na wanachapa sana kazi! nenda sehemu ambazo watanzania wameajiliwa kama Barrick uone kazi, nenda hata Bank of africa uone, acha ujinga kijana wa kuwadharau watanzania!!

Huyu hapa ni mvivu mwingine, kutoona ukweli ni uvivu pia! Naendelea kupitia utetezi wa wavivu.
 
Watanzania wanafanya kazi bhana,,,sasa mtoa mada ukitaka kuamin wanafanya kazi angalia kundi la vijana na akina mama wanaohangaika kuitafuta pesa barabarani as wamachinga,nenda bugurun,nenda tandale nenda tandika angalia mijini vijana wanavyohangaika na wamachinga....twende vijijin kuna jamaa amekwambia vizuri tu hapo juu kwamba huko vijiji kuna watu wanapiga kazi mdau acha tu,,,,
twende kwa graduates,hawa jamaa bwana wanakabiliwa na changamoto nyingi,hasa mfumo wa elimu lakini pia mitaji,,,amemaliza shule ana shahada ya ujasiriamali lakini hana mtaji,ameandika business plan lakin hana assets za kumfanya apate mkopo,,,pia tatizo la kupata information...HILI NALO NI TATIZO KUBWA SANA,,,,VIJANA WA KITANZANIA KWAKWELI TUNA TATIZO LA KUPATA TAARIFA,,,,WAPI KUNA NINI NA KIAS GANI

Kuumwa ni tatizo, lakini kukataa kuwa huumwi ni tatizo kubwa....wewe pia ni miongoni mwa wavivu....I hate excuse!
 
Watu wanafanya kazi bana angalia mashamba wanavyohangaika kulima wakishapata mazao serikali inapanga bei lakini wakati huo serikali imesema soko huria nafikiri hujasikiliza bungeni wanavyolalamika kuhusu pembejeo na mbolea srikali inaleta feki hata mbegu pia feki.
Kuna vitu vinachangia uvivu uwe umesoma mnafanya kazi mahali hakuna mpangalio tena siku hizi kuhusu mishahara unaweza kuwa form six ya 1990 ukaanza kazi lakini atakuja wa form 4 akaanza kufanya kazi 2011 na wewe lakini amekuzidi mshahara....angalia mikopo ukitaka hata kama una vitu vyote lakini lazima uhonge kila mahali ..
angalia kilimo kwanza hakuna cha maana zaidi ya maneno ya viongozi angalia matrekta yalio letwa yapo yamepaki kwenye halimashauri yamekaa tu

Kwa mtazamo wako hayo ni matatizo makubwa sana? Ardhi ingekuwa jangwa au mafuriko ungesemaje? Kungekuwa na vita kama Somalia! Wewe pia ni sawa na wanaosubiri neema inyeshe kama Mana!
 
mimi kua mvivu sikatai ndo maana nikasema asilimia kubwa , sijasema watanzania hawafanyi kazi . uwe unaelewa sentenzi . Nahizo kadi unazo sema unagusisha mlangoni sionje tu hata hapa zipo makampuni makubwa yanazo na ndiko niliko toa hizo data sizungumzi kutoka hewani.

Ukweli una uma na maranyingi hatupendi kuambiwa ukweli sis ni wavivu kulinganisha na wengine . huko vijijini mnakosema vijana wangekua wanafanya kazi kama inavyo paswa tungekua tupo mbali sana , lakini wao nikunywa pombe sikunzima . nina ushahidi wa hii sikuandika tu from no ware

ndio najua huku andika from no where, lakin sikubaliani na wewe kwamba ni asilimia kubwa, kwa sababu najua sasa hivi asilimia kubwa ya watanzania wanapigania mabadiliko ili waeze kutumia fursa tulizo nazo hapa nchini kujiendeleza wenyewe, 'movement for the change' itakapotimia ndio tutajua je sisi ni wavivu au sio. Unajua kipindi cha mkapa vijana walio kuawamejiajiri ktk migodi ni wangapi wamepoteza ajira zao na wengine kufa kwa risasi za police wake? Huku akisema nguvu za maskini ni nguvu zake mwenyewe.. Mi'niseme mfumo wa sasa ndio tatizo, kule moshi kahawa ziling'olewa nyanya zikaoteshwa kwa nini? Je ni uvivu? Jibu utakuta ni hapana wakulima walichoka kunyonywa na serikal wakaona bora walime kile kinacho wasaidia papo hapo.
TUNAITAJI MABADILIKO KATIKA MFUMO MZIMA WA UONGOZ HAPA NCHINI.
 
Unajuwa kuna watu wanaangalia hali ya Tanzania na kukumbilia majibu rahisi kuwa ni wavivu. Niseme hivi, siasa, ni mahindi, siasa ni sukari, siasa ni maji, na kubwa ziadi siasa ni elimu. Hapo kwenye elimu, inaweza kuwa elimu ya ufundi stadi, au main stream. Siasa ndio inatoa guidelines za kila kitu kinachogusa maisha ya raia na nchi kwa jumla.

Ukiangalia siasa ya Tanzania specifically, utendaji wa serikali ya CCM ni vigumu kujua wanataka kujenga taila la aina gani? Tuna dira ya taifa (Vision 2025) inasema wazi by 2025 Tanzania itakuwa kwenye kundi la uchumi wa kati na watu wake watakuwa wana elimu bora. Na tunajua bila elimu (ufundi or mainstream) hatuwezi kupiga hatua yoyote. Kama taifa hatuwezi kufikia malengo ya Vision 2025 kupitia shule za Kata! Hatuwezi. Mtoto aliyesoma kwenye shule za kata unategemea kweli aanze kuongea magari yanatengezwa wapi? Nani asiyejua hali ya shule za kata?

Lakini tuje kwenye mitaala. Juzi nilisoma thread moja hapa kuhusu Mzee Makamba kuwa anazindua vitabu vyake viwili. Moja ya vitabu hivyo kinagusa mambo ya maandamano. Lakini pia Mzee Makamba alishaandika kitabu na serikali ilikubali kitumike kufundishia. Mzee Makamba anawe kuwa uwezo mkubwa sana kwenye mambo mengi, lakini kwa hakika kama tunategemea watunzi wa vitabu vya kufundishia watoto wetu wawe na thinking ya Mzee Makamba hatuwezi kufikia malengo ya Vision 2025.

Na hapa ndipo Waziri wa Elimu (mwanasiasa) anatakiwa awaeleze elimu inayotolewa kwenye shule zetu ni sahihi kwa malengo ya nchi? Ni elimu inayomwezesha mtoto wa Kitanzania kuwa na uwezo sahihi katika nyanja mbalimbali. Wakati Mzee Makamba anatunga kitabu chake hicho alikumbuka Vision 2025? Kukaa kwa vijana vijiweni ni kielelezo tosha kuwa siasa yetu as a foundation ya kuongoza nchi imefeli kabisa. Vijiweni ni matokeo sio sababu! Tukiweza kutambua hilo basi tutatua mzizi wa tatizo na sio matokeo.

Na hili liko kila sekta, kuanzia kilimo, afya, reli .. everything. Huwezi kutenganisha siasa na elimu. Huwezi kutenganisha siasa na reli, huwezi kutenganisha siasa na jua kali. Watu wengi wanajadili siasa kwa msingi huo!

mdau umekuja na analysis nzuri sana bhana
 
Naungana na mtoa hoja, kwa kusema watanzania..kweli kabisa watanzania wavivu! Lakini si wote..naweza kusema KUNDI MOJA la watanzania ndilo wavivu..'WASOMI'..hawa bwana ndio wavivu balaa,pamoja na kusoma na kupata diploma,degree etc wao wamekuwa wategemezi wa kuajiriwa! It is a shame..jamaa akimaliza degree anachowaza ni kupata kazi tu..! Yani hawa wasomi ndio wanarudisha nyuma maendeleo ya tanzania kwa uvivu wao..mikataba iliyoandikwa kizungu wasoma wao but wanamislead na kuleta hasara kubwa kwa kuiuza nchi, ma-engineer wanajenga majengo yanayoboka baada ya muda mfupi, waandishi makanjanja, watunga sera wabovu..huu wote uvivu. Yani tangu a-graduate mpaka anapokuwa kazini..'MSOMI' wa Tanzania mvivu sana.
 
ndio najua huku andika from no where, lakin sikubaliani na wewe kwamba ni asilimia kubwa, kwa sababu najua sasa hivi asilimia kubwa ya watanzania wanapigania mabadiliko ili waeze kutumia fursa tulizo nazo hapa nchini kujiendeleza wenyewe, 'movement for the change' itakapotimia ndio tutajua je sisi ni wavivu au sio. Unajua kipindi cha mkapa vijana walio kuawamejiajiri ktk migodi ni wangapi wamepoteza ajira zao na wengine kufa kwa risasi za police wake? Huku akisema nguvu za maskini ni nguvu zake mwenyewe.. Mi'niseme mfumo wa sasa ndio tatizo, kule moshi kahawa ziling'olewa nyanya zikaoteshwa kwa nini? Je ni uvivu? Jibu utakuta ni hapana wakulima walichoka kunyonywa na serikal wakaona bora walime kile kinacho wasaidia papo hapo.
TUNAITAJI MABADILIKO KATIKA MFUMO MZIMA WA UONGOZ HAPA NCHINI.

nakatiza maeneo ya bugurun hapa saa hiz ndo kumekucha,,,vijana wanauza nguo(mitumba) na specialmviatu,matunda tena wametandika chini,sasa hali hii ipo kuanzia bugurun,kariakoo,magomen mikumi,magomen hospt,moroko hoteli,MKWAJUN NDO KUMEKUCHA ,STUDIO,MANYANYA,B,KANISANI HADI MOROKO......
KATIZA MWENGE SAA HIZI NDO KUNA MIANADA,NA WANAOCHAKALIKA AIDHA VIJANA AU AKINA MAMA,,,,,HAWA WOTE HAWAJATAFUTIWA SOKO RASMI
 
Naungana na mtoa hoja, kwa kusema watanzania..kweli kabisa watanzania wavivu! Lakini si wote..naweza kusema KUNDI MOJA la watanzania ndilo wavivu..'WASOMI'..hawa bwana ndio wavivu balaa,pamoja na kusoma na kupata diploma,degree etc wao wamekuwa wategemezi wa kuajiriwa! It is a shame..jamaa akimaliza degree anachowaza ni kupata kazi tu..! Yani hawa wasomi ndio wanarudisha nyuma maendeleo ya tanzania kwa uvivu wao..mikataba iliyoandikwa kizungu wasoma wao but wanamislead na kuleta hasara kubwa kwa kuiuza nchi, ma-engineer wanajenga majengo yanayoboka baada ya muda mfupi, waandishi makanjanja, watunga sera wabovu,no new innovations..ni pombe na starehe tu.

Tz, esp city areas, Bar zote wamejaa hawa wanaojiita elite, WASOMI, wanaji-boast kweli kweli..but hakuna lolote!.

Yani tangu a-graduate mpaka anapokuwa kazini ni uvivu tu..aaaggrhhh..'MSOMI' wa Tanzania mvivu sana. I could shoot them down kama ningekuwa na....!
 
Naungana na mtoa hoja, kwa kusema watanzania..kweli kabisa watanzania wavivu! Lakini si wote..naweza kusema KUNDI MOJA la watanzania ndilo wavivu..'WASOMI'..hawa bwana ndio wavivu balaa,pamoja na kusoma na kupata diploma,degree etc wao wamekuwa wategemezi wa kuajiriwa! It is a shame..jamaa akimaliza degree anachowaza ni kupata kazi tu..! Yani hawa wasomi ndio wanarudisha nyuma maendeleo ya tanzania kwa uvivu wao..mikataba iliyoandikwa kizungu wasoma wao but wanamislead na kuleta hasara kubwa kwa kuiuza nchi, ma-engineer wanajenga majengo yanayoboka baada ya muda mfupi, waandishi makanjanja, watunga sera wabovu..huu wote uvivu. Yani tangu a-graduate mpaka anapokuwa kazini..'MSOMI' wa Tanzania mvivu sana.

changamoto nyingine hii,,,
unawakilisha kundi letu la wakulima nini?????
 
watanzania sio wavivu ila serikali yao na mifumo ya kiutawalo ndo mivivu. Makazini watu wanakatishwa tamaa na mishahara midogo kufanya kazi kwa bidii. Kwa mfano kima cha chini cha mshahara kwa walimu wa Kenya ni 700,000 ila Kima cha chini cha mshahara cha mwalimu wa TZ ni 180,000 na mfumko wa bei wa 20% sasa we unadhani mwalimu wa tz atajituma kufanya kazi km wa kenya. Hivyo basi watanzania si wavivu ila maslahi wanayopata kutokana na kazi wanazofanya yanakatisha tamaa kujituma katika hizo kazi
 
Twaweza kusema sio wote lakini ukweli ni kuwa majority ya watanzania ni wavivu kwa kweli na zaidi ya hapo pia ni waongo na wenye tabia ya wizi wizi. Nikisema waongo ni pale kwenye tabia za kucheat mitihani hadi vyeti na wakipata kazi bado watacheat kazini sometimes kusababisha hasara na hata katika jamii. Wizi ni pale wanapokosa uaminifu kwenye masuala mazima ya pesa za mahala pa kazi na hata katika jamii na huu ndo ufisadi... Hili ni tatizo na liko katika familia zetu ndio maana viongozi wetu waliopo madarakani wengi wao ni hovyo kabisa.... Tuombe sana Mungu halii hii isiendelee bali iishe maana majirani zetu wanatucheka na baadhi ya organisations haziajiri watanzania wengi bali wakenya au waganda n.k. kutokana na ujinga huu...
 
Back
Top Bottom