Watanzania wengi kuwania ubunge sababu hii hapa

Kisendi

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
699
178
“INASHANGAZA, tumepewa shilingi milioni 90 za magari kwa wabunge wote, huku bungeni tunajadili Bajaj kuwa ’ambulance’ (gari ya kubebea wagonjwa)”. Ni kauli ya Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema kule Dodoma hivi karibuni.

Alikuwa kwenye uzinduzi wa tawi la CHADEMA, eneo la Mipango, Kata ya Miyuji mkoani Dodoma. Wabunge waliohudhuria uzinduzi huo walionyesha kushangazwa na hatua ya Rais Jakaya Kikwete kuweka pikipiki za magurudumu matatu kuwa moja ya vipaumbele vyake ili zitumike kubebea wajawazito wakati wabunge wanalipwa mamilioni ya shilingi!

Lema alisema anaomba wake wa viongozi wanapopata ujauzito na kuumwa uchungu, wapakiwe katika pikipiki (Bajaj) hizo wanapopelekwa kujifungua ili waone adha ya usafiri huo itakavyokuwa.

Kama kila mbunge katika wabunge 360 anapewa shilingi milioni 90 kununulia gari binafsi ‘kwa shughuli za kibunge’ ni mke wa mheshimiwa gani atakayepandishwa kwenye Bajaj ilhali n-nje kuna ‘shangingi linalosubiri kupakiwa?

Ubunge una utamu wake bwana. Mshahara usiopungua shilingi milioni sita kwa mwezi mbali ya msururu wa marupurupu; zaidi ya shilingi laki moja (100,000) kila siku wanapohudhuria vikao vya Bunge, shilingi milioni 90 kwa kila mbunge za kununulia gari, (hata kama analo alilonunua miaka mitano iliyopita), mshahara wa dereva na malipo ya mafuta kila siku.

Kuwekewa bima za afya, kutibiwa katika hospitali binafsi humu nchini na inaposhindikana kupelekwa n-nje ya nchi kwani hospitali za serikali hazina huduma nzuri; ndio sababu wenye uwezo huzikimbia. Pia kila mbunge kulipwa si chini ya shilingi milioni 50 anapomaliza kipindi cha miaka mitano bungeni.

Marupurupu kama hayo ni nani atakayeyaacha? Labda zumbukuku (mtu ambaye hana uwezo wa kufahamu undani wa mambo.) Kumbe ndio maana wahenga walisema; ”akutanguliaye chanoni hukuzidi tonge?” ’Chano’ ni sinia kubwa ya ubao kinachotumiwa kupakulia chakula.

’Tonge’ ni mmego mmoja wa chakula kwa mkono. Kwa hiyo anayekutangulia kuupeleka mkono wake chanoni hupata tonge kubwa zaidi.

Maana yake ni kwamba mtu aliyepata nafasi kabla yako huweza kufaidika na kukutangulia katika mambo mengi. Hatuwezi kushindana na mtu mwenye nafasi nzuri kuliko sisi. Je, wapiga kura waliolitumikia taifa hili kwa miaka 40 na zaidi walipostaafu walilipwa kiasi gani?

Walilipwa kiduchu, tena kwa mbinde na wengine mpaka kesho hulipwa shilingi elfu 60 kila baada ya miezi sita! Wafikirie watumishi wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wanavyohenyeshwa kwa miongo mitatu na wengine wakiwa wageni wa Mwenyezi Mungu hivi usomavyo.

Sasa tunajua ni kwa nini wanaogombea ubunge hutumia fedha nyingi kwa kuhonga, kununua shahada za wanaoonekana kuwa wapinzani, kwenda kwa waganga na hata kuua kimazingara ili waingie ’mjengoni’.

Si hayo tu kwani mtu anapokuwa ’mjengoni’ na kupewa jina la ’mheshimiwa’, hata pasi yake ya kusafiri huwa tofauti na ya akina sisi na kila anaposafiri kwa ndege, hapitii mlango wa kina ’kajamba nani’ bali hupitia chumba maalumu kwa watu mashuhuri, wenyewe wanaita VIP (Very Important Persons).

Haishangazi basi kuona watu wenye kazi walizosomea kwa miaka mingi wakizitelekeza na kuingia kwenye siasa inayolipa mabilioni ya fedha kwa muda mfupi. Tunao madaktari, wanasheria, mainjinia na wengineo wanaohitajika sana katika nyanja zao lakini kwa kuwa fani zao ’hazilipi vizuri’ wameamua kuingia kwenye siasa.

Kwa hiyo upo uwezekano mkubwa kwa wahitimu wa vyuo vikuu na wasomi wengine kuzikimbia fani zao na kutafuta njia ya mkato katika siasa. Hali ikiwa hivi tutakosa wataalamu wanaohitajika mno nchini.

Ni muhimu kwa waheshimiwa wetu kutekeleza wajibu wao ipasavyo kama walivyowaahidi wapiga kura. Wana wajibu wa kukaa na kuishi na wananchi ili kujua matatizo yanayowakabili.

Wananchi wana matatizo mengi sana vijijini: kutokuwa na maji salama, kuzuiwa kuuza mazao n-nje ya mikoa yao kwa lengo la kupata fedha za kujikimu, shule kukosa madawati na walimu wa kutosha, ukosefu wa zahanati, vituo vidogo vya Polisi.

Kwa wabunge, haya ni mambo wanayopaswa kushirikiana na wapiga kura wao ili kuyapatia utatuzi wa kufaa. Haipendezi kuona wabunge wakitumia muda mwingi mijini wakifanya shughuli binafsi huku waliowachagua wakiendelea kuteseka.

Imekuwa kawaida wabunge kukimbikilia mijini na kurudi kwenye majimbo yao karibu na uchaguzi mkuu. Wanapokuwa hawaonekani majimboni, wananchi nao hujaribu kutafuta watu watakaowawakilisha vema bungeni na kuanza kuwatambulisha.

Cha kushangaza ni kwamba Wabunge waliopo wanaporejea majimboni mwao na kupata habari hizi hulalamika wakidai kuingiliwa kwenye majimbo yao!

Ni mbunge gani mwenye hatimiliki ya jimbo analolisimamia hata alalamike kwa kuingiliwa katika ’jimbo lake?’ ’Jimbo’ hilo alilianzisha lini na katika ardhi ipi ya Tanzania?

Fedha wapewazo wabunge kusaidia majimbo yao huzifanyia kazi gani? Fedha wanazopewa kwa ajili hiyo zitumike kwa malengo yaliyowekwa. Wasizibanie kwani si mali yao.

Ni wachache mno wanaochangia maendeleo ya majimbo yao na wengi wao hutoa fedha kiduchu zisizotosheleza mahitaji ya miradi iliyopangwa na majimbo yao.

Wabunge watatenda haki kama wakitangaza fedha walizopewa kusaidia maendeleo ya majimbo yao na kuweka wazi mgawanyo wa fedha hizo kwa kila kata.

Baadhi hudai kuwa fedha hizo zinatoka mifukoni mwao kumbe si kweli! Huu ni ulaghai (tabia ya udanganyifu wa kutumia maneno; utapeli).

Ubunge si ufalme au usultani bali ni utumishi kwa umma. Kwa hiyo Wabunge wanapaswa kuonyesha mfano kwa kushirikiana na wananchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo majimboni mwao badala ya kukimbilia mijini na kuwaacha wapiga kura wakihangaika peke yao.

Huo si uwakilishi unaotakiwa; na Wabunge wa aina hii ndio wanaosinzia bungeni wasijue yanayoendelea!
Source: tzdaima
 
Godbless Lema baada ya kutoa hiyo siri AMECHUKIWA mpaka na wabunge wenzake wa CHADEMA! Sh. Bilioni 33 kwa ununuzi wa magari tu na karibu Billioni 5 kwa ajili ya kuya-operate ni fedha nyingi sana.

Tunavyolia kuhusu Dowans we have to cry for things like this where our MPs seems not to care about!hizi fedha ni asilimia 35 ya fedha za dowans, it means in other similar issues we have many dowans surrounding us everyday

wakati wapenzi wa vyama vya upinzani mkiwa vipofu wa reality......huu ni ukweli mwingine ambao hata hao mnaowaita wapinzani HAWAKO TAYARI KUZIKOSA HIZO FEDHA.. tunaposema muwe wakali na kamwe upofu wa mapenzi kwa hivi vyama usiwatawale huwa hamsikii.

Hii taarifa inauma kuliko dowans, swali je managapi kama haya yanafanyika...nani yuko tayari kuyasema????

Lema kasema simply kwa sababu mtoto wa mjini, ana fedha, hamuogopi mtu na tunajua historia yake vizuri.....wengine wapinzani wanayasema haya.....au kupeana moyo tu/......''tutafika''

kama wapinzani wengi wako hivi... je CCM??

kweli! "akutanguliaye chanoni hukuzidi tonge?"
 
Lema yupo sahihi.
Endelea Kama Lema.
ni kweli baadhi ya wabunge wa chadema na ccm wamechukizwa na kauli hiyo ya Lema.
 
mi mwenyewe nina mpango huo wa kugombea,jimbo flani kusini tanzania
 
mimi naona ubunge kwa tanzania sio tena kazi ya kuudumia umma na kutetea maslahi ya wananchi au kupeleka matatizo yao bungeni, bali ni moja wapo ya ujarisilia mali na ufujaji wa mali za umma, hata kama kuna wachache wanaoenda kutetea kwa ajili ya wananchi walio wachagua bado mishahara na posho wanazopewa hazilingani na hali halisi ya uchumi wetu na uchumi wa mpiga kura wakawaida na kazi wanayo ifanya. badala ya kupunguza mishahara yao wao wana pigia debe wahisani kuchangia bajeti ya serekali., tunaonekana watu wa ajabu sana. mbunge more than 3 to 4 million a month lakini katika jimbolake kuna shule za kata zaidi ya 5 walimu wote katika shule hizo mishahara yao haifiki hiyo hela
 
kugombea ubunge ni dili siku hizi....tena huna hata haya ya kusema chochote bungeni.....ukikaa kimya hata hawakuongelei bungeni.....muda wa uchaguzi ukifika, ukajifananisha na walioongelewa vibaya kwenye media, we unaonekana mzuri.....unaendelea kula.
 
Kuna wabunge wengine wanaingia bungeni ili kulinda mali zao kama kukwepa kodi, kupata tenda kirahisi nk. huo mshara na marurupu ni pesa kidogo mno ukilinganisha na miradi yao. Mfano watu kama Aziz Abood(abood companies moro),NChambis(mombasa raha shy),LOWASA(alpha companies),ROSTAM(vodacom,mtanzania,dowans etc) na wengine kibao nafikiri unaweza kuona wengine ni kama kuchota maji Indian ocean unaweka Meditiranian sea.
Af kingine huyu kijana wa arusha asilete usnitch kama ameguswa na tatizo la kina mama nafikiri huu ndo ungekuwa wakati wa kutoa mfano angechukua hizo 90mls atoe kidogo af ananue ambulance moja sio kuchukua pesa af unaponda tu toa vitendo isiwe kama pinda anaangiza magari af anakataa la kwake. Hii haina tija kwa taifa
 
Back
Top Bottom