Watanzania Wawili wakamatwa South Africa na Madawa

pole yao, ila ni bora walivyokamatwa tupunguze hili janga
Jamani wana jamvi usiombe familia yako ikakumbwa na mteja.........ni janga.

wafungwe tuu na wengine wakamatwe zaidi
 
stay tuned wema sepetu
ana jeuri ya pesa while hakuna biashara au chochote kinachoonesha vyanzo vya mapato yake watakuwa ndo mabegi(wanaobebeshwa ngada hao)
MUNGU tuokoe vijana tunakufa kwa ngada na pia tunapotea kwa ngada
R.I.P NGWEAR
R.I.P LANGA
acha kula madawa TID
acha kula madawa RAY C
acha kula madawa QCHILA
acha kula madawa MSAFIRI DIOF
acha kula madawa BANZA STONE
acha kubeba madawa NYANDU TOZI
acha kubeba madawa MR BLUE
acha kubeba madawa SUMA LEE
 
Hii habari haijanistua(tumezoea sasa) lakini yaliyojadiliwa humu na akina Matola yamenichosha!

Cc Muuza Sura
 
Last edited by a moderator:
Hii inaonyesha jinsi gani maofisa wetu walivyo wazembe kiutendaji,haiwezekani huku madawa yasikamatwe kule yakamatwe.This is a lesson to our officers
 
Halafu Maboss wenyewe wametulia tuliii huko Masaki wakiendesha magari ya bei mbaya na kujisifu FB.

Kibaya zaidi unaweza kukuta wakitoka nje, wanadaiwa gharama za madawa hayo na itabidi warudi tena kuwa Punda.
There are so many ways nowadays to make money.

So why sell dope or be used as mule by anyone?

That's juts stupid.
 
Wakikamatwa zao, zikiuzwa pesa zet tunagawana.....wataozea jela! Nabaki na shilingi zangu tu mtaani miye
 


Tuesday, July 9, 2013 | 1:30 PM




HATIMAYE wale Wanawake wawili walionaswa na madawa ya kulevya Afrika kusini wametambuliwa kuwa ni mabinti wa KITANZANIA ..


Mabinti hao wanadaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

Akizungumza na mwandishi wetu jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.

Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald (MASOGANGE) ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.

Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.

Jumapili iliyopita mtandao huu ulipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.

Taarifa hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania.

Wanawake hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.

HUYU DEMU SHULE HANA, ujanja hana..kazi kushobokea tu mabrazameni...ela ni jambo la msingi kabisa katika maisha lakini pia isikufanye ukajishusha utu wako au ukaiabudu...
Wanataka vitu vizuri alafu hawataki kazi, ndo matokeo yake sasa..mi nilijua hana ishu ya maana anayofanya sauzi...huwa ni ukahaba au biashara haramu tu!!!!
 
Kama Mamlaka za Tanzania na vyombo vya habari vinachukulia jambo hili kimzaha basi tujiandae na janga kubwa sana mbele ya safari.

Kwanza kibano cha kwanza kianzie hapa kwetu waliwezaje kutoka na shehena yote hiyo? maana ninavyofahamu mimi biashara ya unga inasafirishwa kwa njia ya tumbo ndio njia salama iliyobakia (ingawa ni risk ya uhai wako)

Kama watu wanaweza kupita madawa kwa njia ya pecking mimi hili haliniingi akili hata kidogo kwa sababu najuwa know how za biashara hii.

Something wrong somewhere na msitalajie lolote kutoka ubalozi wa Tanzania pale Pretolia, wamejaa vilaza watupu kuna siku nilitaka kumtandika makofi Dada mmoja wa kibongo anafanya kazi pale ubalozini baada ya kuniletea majibu ya Manzese wakati yeye yuko pale kwa ajili yetu.

hapo ndio utajua tanzania ni nchi ya ajabu sana na niwazi ma Agent wako wanacheki mchezo na hawezi kuwataja na yule anatumiwa kabisa na ni wakubwa wana husika kwenye hili swala ndio maana wanaweza kupitisha mzigo mkubwa kiasi hiki na tanzania ni nchi ya kupiga kelele bila vitendo vyovyote. huyu msichana waliomtuna na anao shirikiana nao wengine wapo tanzania kabisa na wanamcheck tuu.
 
Matola bado nina wasi wasi na hayo madawa yaliyo andikwa hapo, ngoja nianze kufatilia
 
Last edited by a moderator:
Kama ni kweli pole sana Agnes:mad:
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1373384121714.jpg
    uploadfromtaptalk1373384121714.jpg
    12.4 KB · Views: 220
anyongwe kabisa ili iwe fundisho kwa wapenda mtelezo bila jasho, haina haja ya kumhurumia
 
Hivi ni rais gani vile aliyesema anawajua wauza unga tena vigogo? na akasema atawataja? na kwa nini hawataji wakati wanawaponza vijana wadogo namna hii na kuwapotezea dira zao?

Mungu ni samehe huwa nina wasi wasi na mali za wema sepetu ni kilinganisha na kazi zake.
 
Hivi tanzania agness gerard ni mmoja tuu hamna wengina nan anapicha za usibitisho kuwa ni huyo video qeen...nawasilisha
 
Hii inaonyesha jinsi gani maofisa wetu walivyo wazembe kiutendaji,haiwezekani huku madawa yasikamatwe kule yakamatwe.This is a lesson to our officers
Hakuna uzembe mkuu ni rushwa tu inatawala. hebu tujiulize wanapitaje hapa uwanja wa ndege , ina maana kama kuna uzembe wa wanaoenda nje, je wanaoingia si wanaingiza kirahisi kabisa. Na kipindi hiki hii biashara imekithiri mno yaani kila mara utasikia mtz kakamatwa nchi flani na unga. Hebu tujiulize inakuaje watu wanaendelea kuthubutu kuendelea na biashara wakati tayari kuna wengi tumewaona kwenye vyombo vya habari wakikabiliwa na janga la aina hii nje ya nchi ie wamekamatwa na madawa. Nadhani kuna mkono wa watu nyuma ya mabinti wa aina hii, haiwezekani ikawa wako peke yao . Nadhani wanatumika kama wasafirishaji tu naa huenda hata mmiliki hawamjui. Tumefika pabaya watanzania sasa hivi tutakua tunaogopwa tunaposafiri inataka kua kama Nigeria.
 
Back
Top Bottom