Watanzania "wanyonge" na "masikini" tutaje nafuu tuliyoipata tangu awamu ya tano iingie madarakani

Mwanangu na yeye anasoma

Juzijuzi kwa mara ya kwanza bibi yangu kashindia kiwanja alichokua anagombania na mkubwa

Tule tumatusi mtu ukiingia ofisini kidoooogo tumeisha

Kujua eti nchi yangu ni tajiri kwa kuwabudu watu kumeisha

Kauli za kufarijiana huju tunamaisha magumu zimeisha

Kale ka umwinyi mtaani naona sasa hivi tunaheshimiana

Tugharama twa maisha sasa hivi tumeshika wote

Habari ya mtu kutembea na jera mfukoni kidoooogo kumepungua

Madawati yamekua mengi huju mpaka yawwzekana watoto wakagawiwa mengine waweke akiba nyumbani

Na mwanangu toka nimnunulie yunifomu na madaftari asee naona na yeye anasoma sekondari nachojitahidi ni kuhakikisha akitoka shule afike anakula

Kwa mara ya kwanza hospitalini kwetu huku mgonjwa anahojiwa na muhudumu akiwa hayuko anachati tena kwa upoleee

Mke wangu akienda kliniki yale makofi alokua anapigwa na wahudumu sasa hivi naona kama ngeu zimepungua

Kazini kwangu bosi hajaigeuza ofisi kama kwake tenaa
 
Angalau serikali ya awamu ya tano imethubutu kuwagusa wale waliokuwa hawagusiki, kufanya yale yaliyoonekana haiwezekani. Kwa sababu hiyo maisha bora kwa Mtz yanaonekana japo kwa mbali. Tumaini jipya limezuka ndani ya mioyo ya wengi. Inajionyesha dhahiri Tz iliyonyooka inakuja na ile ya ujanjajanja inelekea kaburini. Usitake kuleta mihemuko, maskini na wanyonge tunatambua hiki ni kipindi cha mpito. Mambo mazuri yanahitaji muda na gharama.
Hao wasiogusika wanatusaidia nini sisi wanyonge na masikini? Na hali hii mpaka link maana bajeti imeshaanza kwa mwaka wa fedha 2016/2017 inamaana tusubiri zaidi na zaidi kwenye bajeti zijazo?
 
1468073939705.jpg
 
M sure the economy has contracted in the current year yet the gvt sponsored economists will paint a different picture...
 
Hao wasiogusika wanatusaidia nini sisi wanyonge na masikini? Na hali hii mpaka link maana bajeti imeshaanza kwa mwaka wa fedha 2016/2017 inamaana tusubiri zaidi na zaidi kwenye bajeti zijazo?

Unyonge Na umasikini siyo sifa nzuri bali upum..bavu WA kujitakia. A man is responsible for his own development, his family and nation acheni kukumbatia umasikini.
 
Nimetumia nusu saa kufikiri ntarudii nipo busy na tafuta ada ya dogo amekosa shule advance na vigezo anavyo et shule zimejaa :):):)
 
Maskini na wanyonge full maumivu,hospital za serikali kila kitu unalipa file,vipimo kumuona dokta,madawa na kulazwa
Hivi hao wanyonge wanasaidiwaje?
tunawaona wagonjwa hadi wa ukimwi wanazuiwa kutoka muhimbili kwa kuwa hawajalipwa bills zao sasa hatujui ni nani anaelegwa kama ni masikini sijui ni yupi,nimemuona mama mmoja itv anaomba msaada wa kulipiwa laki 6 ili mgonjwa wake aweze kuruhusiwa kutoka hospitali,alipoulizwa anasumbuliwa na nini ansema alikuwa na kansa ya koo na pia ni muadhirika.je hao si wanyonge?
 
Juzi nilinunua nyama opposite na soko la Ndizi, Mabibo kg @Tzs. 5500. Awali mwezi Februari nilinunua butcher hiyohiyo kwa bei ya kg@Tzs. 8000
 
Nimetumia nusu saa kufikiri ntarudii nipo busy na tafuta ada ya dogo amekosa shule advance na vigezo anavyo et shule zimejaa :):):)
Vigezo: alifaulu daraja gani na combination gani?
 
Kwa hapa Dar es Salaam siku hizi ninasafiri kutoka Kimara mwisho hadi Feri kununua samaki kwa Tzs. 650, nikisafiri kwa dk 40 tu (muda wa juu). Zamani nilitummia Tzs. 1000, nikitumia muda wa dk 180 (masaa 3).
 
Hata kuona serikali inaanza kukusanya kodi kwa kila anayetakiwa kwangu ni unafuhu mkubwa sana, haiwezekani udai maendeleo wakati hutaki kulipa kodi, unadai maji, unadai umeme lakini wewe kodi hutaki kutoa.

Pili, Kupatikana umeme pasipo usumbufu mkubwa sahivi, ukikuta sahivi umeme umekatika basi jua kuna tatizo kubwa sana mahala.

Tatu, Kushuka bei ya umeme majumbani, sahivi mie nalipia 10000 mwezi mzima wakati nilikuwa lazima nitoe 40000.

Nikiwa na shida sahivi kuanzia ofisi ya mtaa mpaka manispaa ni chap chap nashughulikiwa na naendelea na majukumu mengine kwa wakati.

Kwenda hospitali sahivi natibiwa tena na kundi kubwa la wahudumu kila mmoja ananiuliza najisikiaje?

Yako mengi na nategemea mengi sana pale bajeti hii ikielekea kwenye miezi ya sept na okt hasa kwenye miundombinu.

Du mkuu hii ni kweli mbona wengine hatuoni hayo Zaidi ya hilo la umeme lakini karaha za maofisini ni zile zile hakuna afadhali kabisa!!! Hospitali gani hiyo umeenda wewe...?
 
Tuambie Kwanza wewe umefanya nini kuisaidia serikali yako ifikie Malengo yake.!
 
CBG three ya 24 ....
CBG ziko shule chache sana, Ni wanafunzi wachache tu wanaochaguliwa kusomea combination subjects hizi. Hata shule za binafsi ni hivyo. Shule ni chache na wanachagua wanafunzi waliofaulu Div. 1 na kwa uhache sana 2 pekee. Jaribu Marian Boys au St. Joseph Cathedral.
 
Hata kuona serikali inaanza kukusanya kodi kwa kila anayetakiwa kwangu ni unafuhu mkubwa sana, haiwezekani udai maendeleo wakati hutaki kulipa kodi, unadai maji, unadai umeme lakini wewe kodi hutaki kutoa.

Pili, Kupatikana umeme pasipo usumbufu mkubwa sahivi, ukikuta sahivi umeme umekatika basi jua kuna tatizo kubwa sana mahala.

Tatu, Kushuka bei ya umeme majumbani, sahivi mie nalipia 10000 mwezi mzima wakati nilikuwa lazima nitoe 40000.

Nikiwa na shida sahivi kuanzia ofisi ya mtaa mpaka manispaa ni chap chap nashughulikiwa na naendelea na majukumu mengine kwa wakati.

Kwenda hospitali sahivi natibiwa tena na kundi kubwa la wahudumu kila mmoja ananiuliza najisikiaje?

Yako mengi na nategemea mengi sana pale bajeti hii ikielekea kwenye miezi ya sept na okt hasa kwenye miundombinu.
JPM Kasaidia Sana Ila Wanafiki Wachache Wanapiga Tu Kelele. Nampongeza Sana.
 
Siyo kweli, Mh. Mhongo ndiye aliyeiagiza Ewura na Tanesco kureview bei za umeme downwards, baada ya kuteuliwa na Mh. Rais kwenye nafasi yake ya Uwaziri wa wizara husika.

Pia, tanki za gesi ya kupikia za uzito wa kilo 15, kwa jiji la Mbeya ilikuwa inauzwa kwa shilingi 54,000/- Baada ya Magufuli kuingia hivi sasa ni shilingi 46,500/- Na watanzania wengi wanahamia kwenye gesi kwa kuwa ukilinganisha na mkaa (gunia Shs. 35,000/) tofauti siyo kubwa sana.

Hivi sasa hospitali za umma mtu unaulizwa tukusaidie nini? umeshahudumiwa? Watoto wanafundishwa mashuleni. Wale waliokuwa wanapenda kupiga stori makazini ndiyo wanaumia, na wapiga dili (aka miungu watu) katika ofisi za umma.

Nimepata hatii za viwanja vyangu ndani ya wiki moja. Hakuna ubabaishaji wala senti ya kulainisha mchakato. Kama unajishughulisha mambo ni mazuri, ila kama ulikuwa dalali wa huduma za serikali au mpambe wa wanasiasa, karibu shambani. Vitunguu na viazi vinalipa kwelikweli.

NB: Ukishaanzisha mada waache wengine wachangie. Kitendo cha mtoa mada kuwa ndiye commenter mkuu kinaleta picha ya mtu anayependa ligi just for the sake of it. Ukishaiweka ajenda mezani, iangalie inavyorutubishwa au kukatwakatwa kwa misingi ya uzito na ukweli wake.
Mpaka Sasa Nampongeza Sana JPM Karudisha Heshima Kwa Na Tumaini Kwa Watz.
Wanasiasa Wamekuwa Wanafiki Coz Of Pesa, Wanatengeneza Figisu Tuendelee Kuumizwa.
Piga Kazi JPM.
 
Back
Top Bottom