Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,759
- 41,624
Watanzania walio wengi wanaugua ugonjwa wa unafiki. Na hawa wanafiki ambao siku hizi wanaitwa machawa, wakati wote hutafuta vitu vidogo vidogo ili waisifu Serikali, wamsifu Rais au waisifu CCM. Hata vitu vya kawaida vikifanyika, watatoa sifa unaweza kudhani labda tumefanya ugunduzi ambao Dunia nzima ilikuwa haijawahi kufanya.
Jana tumeambiwa kuwa mlango mmoja wa bwawa la Nyerere, wa kufua umeme umefunguliwa na kuanza kuzalisha umeme. Tunashukuru kwa hilo kuwezekana maana inaweza kupunguza madhira makubwa ambayo Watanzania wamekuwa wakiyapitia kwa kuwekwa kwenye mgao mkali wa umeme kwa zaidi ya mwaka mzima. Lakini hakuna kikubwa cha kusherehekea. Bwawa hili likizalisha sawasawa, maximum generation capacity yame itakuwa 2,115MW. Ukimjulisha na generation capacity tuliyokuwa nayo ya 1,938MW, tutakuwa na total generation capacity ya 4,053MW. Huo utakuwa ndio uwezo wa mwisho wa uzalishaji kama kila chamzo na kila mtambo vikafanya kwa ufanisi wa 100%. Lakini kwa poor efficiency ya TANESCO kama zilivyo taasisi zote za Serikali, hawatazidi 70% ya capacity, ambayo ina maana haitazidi 2,837MW.
Wakati sisi tunapiga kelele na kushangilia kama vile tumefanya maajabu, nchi nyingi, tena za Afrika hii hii wanazalisha umeme kama huo na nyingine kutuzidi kwa mbali sana:
Nigeria yenye watu milioni 213 , ina installed capacity 22,000 MW.
South Africa yenye watu milioni 59 inaninsatlled capacity 58,095MW
Ghana yenye watu milioni 32 ina insatlled capacity 5,134MW
Mozambique yenye watu milioni 32 ina installed capacity 2,780MW
Kenya yenye watu milioni 53 ina installed Capacity 3,300 MW.
Zambia yenye watu milion 19 ina installed capacity 3,356MW
Ninachotaka kusema kuwa hata kama Bwawa la Nyerere litazalisha MW zote 2,115, siyo maajabu na wala haimaanishi tumetatua tatizo forever. Ikumbukwe kuwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa matano yanayoongoza kwa kuzaliana katika Africa. Hivyo muda si mrefu, kwa vile sisi ni watu ambao huwa hatuna mipango, kwa kuzingatia ongezeko la watu, ongezeko la shughuli za kiuchumi, ufanisi mbaya wa TANESCO, ukame, na udhaifu wa Serikali katika kuisimamia TANESCO, haitapita muda mrefu, tutarudi kwenye matatizo haya haya ya kukosa umeme.
Kuwashwa kwa umeme wa Bwawa la Nyerere isiwe sababu ya kupeana sifa za kupitiliza, isiwe sababu ya Serikali na TANESCO kubweteka bali muda huu utumike kufikiria na kutekeleza miradi mipya ya umeme ili angalao tufikie 10,000MW. Tulisherehekea hivyo hivyo tulivyoanza kuzalisha umeme bwawa la Mtera, Kihansi na baadaye wa gas, lakini ikawa ni sherehe ya muda mfupi.
Yatupasa kufikiria miaka 50 mbele.