SoC03 Watanzania tunufaike na nini kupitia nursery schools

Stories of Change - 2023 Competition

Tibaiwa

Member
Sep 8, 2021
50
38
Ni miongo mingi imepita huku nchi ya Tanzania ikishindwa kufanya vizuri kwenye suala la ushindani wa soko la ajira kulinganisha na mataifa mengine ya nje na yale ya jirani katika kuwasilisha “maudhui” yetu kupitia vijana wanaotumia nguvu kubwa katika kupambana na umaskini ili wajikwamue kwenye suala la uchumi yaani kujenga uchumi bora kwa kukuza vipato vyao.

Katika upembuzi wangu na kujitumia kama kisa mafunzo sambamba na wenzangu ninaokutana nao nimebaini kuwa changamoto kubwa ya kushindwa kuzalisha vijana wenye kushindana kwenye soko la ajira na kulitangaza taifa letu pendwa nje ya nchi ni “ suala la kutomudu lugha ya kiulimwengu amabayo ni kingereza.”

Tanzania tunao wataaluma wengi sambamba na wabunifu lukuki na wakubwa “kiuwezo” lakini kizingiti cha kuwafikisha mbali kupitia uwezo wao ni lugha katika kuwasilisha maudhui na ujuzi walionao kwenye ubongo wao au ndani ya fikra zao.

Baada ya muda wa masomo nilijaribu kutafuta kazi mbalimbali kulingana na taaluma yangu lakini kila nilipojaribu kutafuta kazi niliangukia pua, kila usahili niliofanya kwa lugha yangu pendawa ya kiswahili nilifanya vizuri lakini ilipokuja kwa lugha ya kingereza nilifanya vibaya “nilipuyanga” na kubwagwa chini licha ya uwezo wangu mkubwa niliokuwa nao katika kuwasilisha kile nilichokuwa nacho, “huu ni ukweli pasi kuwa mwamba ngoma” dunia ya sasa inahitaji lugha ya kiulimwengu “ambayo ni kingereza”.

Si nia yangu kukibananga kiswahili lakini tunahitaji Kufanya kazi mbili sisi kama taifa la Tanzania kwenye upande wa lugha.

Mosi ni kutafuta njia za kuifanya lugha ya kingereza kuwa nyepesi au kuwa na urahisi “sweetable” kwa watanzania iwe kwa kuiandika, kuisoma na kuiwasilisha kupitia hisia zetu na maono yetu juu ya masuala mbalimbali.

Pili kuipa chapuo lugha ya kiswahili na kuipeleka kuwa ya lugha ya kiulimwengu ili nayo iwe na kasi kama lugha zingine zinazotambuliwa kimataifa.

Katika hizi njia mbili tuchague iliyobora huku hile ya pili tukiipeleka taratibu kulingana na matakwa yanayoitajika katika ulimwengu wa sasa maana tukiipa kipaumbele lugha moja na takaitupa hile ya pili tutakuwa tumezalisha tatizo lingine linaloweza kugharimu hapo baadaye.

“Kisa mafunzo”
Mwaka 2018 hadi 2021 niliangukia pua kwenye usaili wa kufundisha shule za “nursery shool” na nilipochimbua tatizo la kushindwa majibu yalikuwa ni kutofanya vizuri kwenye kujipambanua kwa kutumia lugha ya kingereza kwenye shule zaidi ya tatu ambapo sikuwa na msingi mzuri kutoka mwanzo mimi ni zao la “santi kayumba”.

Mwaka 2021 hadi 2023 nilipohamua kujitafuta kwenye kipaji nako niliangukia pua baada ya kukutana na jopo la majaji waliotoka nje ya nchi na kuniambia kuwasilisha sanaa yangu kwa kutumia lugha ya kingereza baada ya kufanya vizuri kwenye lugha yangu ya kiswahili, lakini ilikuwa bahati mbaya kwa upande wangu baada ya “kizungu” kuniangusha na kupoteza fursa hadhimu ya kutengeneza mamilioni ya fedha miongoni mwa watanzania.

Ni wazi kuwa si mimi tu niliyekutana na changamoto hii peke yangu bali lipo jopo kubwa linalokumbana na kizingiti hiki cha lugha.

“NINI SURUHISHO YA HAYA YOTE”
Ningependekeza kwa Serikali kupitia shule hizi za nursery shools iwe na uratibu wa kufatilia vijana hawa wanaotoka kwenye shule hizi na kuwapeleka kwenye shule zile za kata kupitia msingi na sekondari kwa kazi maalumu ya kujenga stadi ya kuandika, kuzungumza na kuwasilisha mawazo yao kwa njia ya kingereza kulingana na uwezo wao walionao hiwe ni kimatendo na kimienendo au kisaikolojia kwa kuwaondolea dhana potofu wanafunzi kuwa kingereza ni kigumu na kuwafanyia wepesi wa kukimudu katika stadi za kukisoma, kukielewa, kukiandika na kisha kujipambanua kinagaubagaba bila mikwamo huku kiswahili kikizidisha kasi ya kuwa miongoni mwa lugha ya kiulimwengu.

Vile vile katika kujenga msingi mzuri wa watoto katika kukuza uwezo wao wa kujipambanua shule za sekta binafsi na umma kuanzia ngazi ya awali wawe na utaratibu wa kutembeleana “ziara” nia ikiwa ni kulisishana ujuzi na maarifa waliyonayo kwa kutumia hizi lugha mbili.

Jambo hili likitekelezwa na wizara ya elimu sayansi na teknolojia kwa kushirikiana na tamisemi katika kupanga walimu wa kujenga stadi ya kuongea na kuandika lugha ya kiingereza kwenye vituo vya kazi kwa kuangalia historia ya mwajiriwa huyo kuanzia elimu ya msingi na sekondari Tanzania itakuwa na vijana wenye uwezo mkubwa wa kufanya vizuri kwenye soko la ajira hata nje ya nchi walimu wengi wa lugha ya kingereza watoke kwenye misingi ya nursery shools nao wawe na jukumu la kujenga stadi ya kuongea na kuandika kiingereza au kila shule iwe na mwalimu mmoja au wawili kwa ajili ya kujenga stadi hizi kwa lugha ya kingereza kwa wanafunzi nao wawe ni wabobezi wazuri wa kuwajengea watoto stadi hizi. Pia pendekezo hili litaondoa mtengo uliopo kati ya shule binafsi na zile za umma kwani wote watajiona wako sawa na ni wamoja kupitia ushirikiano watakao kuwa wameujenga kutoka awali.
 
Back
Top Bottom