Watanzania tunajifunza nini kwa wenzetu wa Kenya?

Pax

JF-Expert Member
May 3, 2009
268
87
Kenya hatimaye imeandika ukurasa mpya katika historia yake, wenyewe wanasema new republic imezaliwa. Pamoja na mambo mengine wameondoa mikoa na kuleta majimbo ambayo yana madaraka ya kujiamulia mambo yake. Zaidi ni kuwa katiba yao imegusa mambo mengi ya msingi. Jambo kubwa nililojifunza ni kuwa wenzetu wa Kenya wanajua katiba yao. Je ni watanzania wangapi angalao wamewahi kuiona katiba yetu? Nimeshaisoma mara kadhaa katiba yetu na hakika pamoja na kwamba haikidhi mahitaji, ni kuwa haifuatwi. Inafuatwa pale tu viongozi wapotumia madaraka yao lakini yale wanayotakiwa kuwafanyia wananchi wao hawafanyi. Na kwa kuwa wananchi hawaijui katiba na hawajui hata haki zao basi ndio maana viongozi wetu wanawekaga viraka tu wakitaka.

Wakenya wametuonyesha nini maana ya katiba kuwa ndio kioo cha kuleta maendeleo, bila katiba nzuri kuendelea ni ndoto.
 
tunatakiwa kujifunza kenya ni kwamba wenzetu wakenya wanajua maana ya kupiga kura na umuhimu wa kura so watanzania tujaribu kubadilika
 
kama tunataka katiba mpya Tanzania cha kwanza ni kuing'oa CCM itoke. Kenya wamefanikiwa kwa sababu hatua ya kwanza waliing'oa KANU, lakini chini ya utawala kandamizi wa CCM katiba mpya tusahau hadi kiama.
 
Back
Top Bottom