Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,503
113,616
Wanabodi
Hii ni makala ya Jumapili ya leo.
Hili ni bandiko mwendelezo wa bandiko hili Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
Makala Jumapili ya leo 7.10.23.png

Kufanya mabadiliko yoyote ya sheria iliyotokana na vifungu vya katiba, bila ya kufanya kwanza mabadiliko ya katiba, ni sawa na kula bila kunawa!. Je Watanzania tuna njaa sana, na tuna haraka sana na uchaguzi ujao, hadi tukimbilie kula bila kunawa?​


Dini zote zinatufunza kuwa na shukrani kwa yote, hivyo kikao cha Bunge kijacho, kitapokea miswada kadhaa ya mabadiliko ya sheria za Uchaguzi, Tume ya uchaguzi na Ofisi ya Msajili wa vyama, japo bado sijajua ni sheria zipi zitafanyiwa mabadiliko, hivyo hatua ya kwanza ni kushukuru kwa mabadiliko hayo.

Lakini kufanya mabadiliko ya sheria zilizotokana na katiba, bila kutanguliwa na mabadiliko ya katiba, ni superficial changes!.

Kwa muda mrefu, tumepigia sana sheria kandamizi za uchaguzi na sheria batili zilizochomelewa kiubatili ndani ya katiba yetu!, maadam sasa something is going to be done, let's be appreciative for whatever is going to be done regardless how little it is.

Hapa ni baadhi ya sheria hizo
  1. Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?
  2. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
  3. Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
  4. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
  5. Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza?
  6. Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
  7. Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
  8. Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
  9. Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
  10. Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
  11. Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?
  12. Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa
  13. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
  14. Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!

Paskali
 

Attachments

  • 1696749954710.png
    1696749954710.png
    153 bytes · Views: 7
Mimi ninachofahamu Serikali ya CCM inafanya tu maigizo na kuwachezea shere wapinzani, na mwisho wa siku hakuna kitakachopatikana.

Na hii yote ni kwa sababu haiko tayari kuruhusu uwepo wa Uchaguzi huru na wa haki, uwepo wa Katiba yenye maslahi mapana kwa wananchi badala ya wao wenyewe na chama chao, nk.

Kiufupi CCM na Serikali yake hawana nia njema ya kuifanya hii nchi kupiga hatua katika nyanja za kisiasa na kiuchumi kutokana na ubinafsi wao uliopitiliza.
 
Na hao wapinzani watakaokubali utahira huo ndio viini macho vya vyama mbadala... Wtz tunapaswa kupima nafasi ya vyama Kama chadema kupitia hili Jambo!. Kuna kila dalalili ya chadema kuwa "CCM B"
 
Heri nusu shari kuliko shari kamili. Unaweza kubadilisha sheria husika na vile vifungu vya katiba vinavyotawala uchaguzi moja kwa moja.
Ingependeza zaidi kuja na katiba mpya lakini kama muda haupo basi teende kwa hatua.
Bado naamini kwa uchaguzi wa 2025 katiba mpya ingewezekana kama mshika mpini angetaka lakini dalili zinaonyesha hawako tayari. Kumbuka walianza na katiba baada ya uchaguzi 2025, na sasa wanasema wananchi wapewe mafunzo ya katiba ya miezi kadha. Yote yanaonyesha bado sana.
 
Kwangu mm nikiona kitu fulani kinafanyika hua nawaza hatua 3 Miele,hii ninayoiona nimaanisha nini huko mbeleni.
Kwa mtazamo wangu ukiona kunabadiliko la jambo la kisheria kazini kwako or serikalini jua kuna jambo wanatakakulifanya na hio sheria ndio itawalinda/kinga kwao soma vzr sana hayo mabadiliko uyaelewe nakuyafanyia kazi otherwise kuna siku yatakudhuru.
In short hio ni kinga Kwa wakubwa kaka Pascal Mayalla
 
Tatizo viongozi wetu baada ya kuwakasimisha mamlaka huwa wanajisahau sana na kufikiri wao ndiyo mamlaka hiyo.

Katika nchi ya asili "natural state" kila mtu ana mamlaka " war of all against all"..Kazi ya Serikali ni kuleta utaratibu " to bring orders out of chaos" na siyo kupoka mamlaka ya wananchi.

Katiba ni mamlaka au nguvu ya mwananchi mmojammoja na siyo watawala tu. Katiba ni haki ya kila mtu kwa asili na siyo haki ya kikundi au mtu mmoja.

Katika mazingira ya asili kabisa kila mtu ana mamlaka na Katiba ni haki ya asili.
 
Hapo sijalaumu bali nimekumbusha tu.

CCM inajifanya kama vile hakujawahi kuwapo kwa mchakato wa kupata Katiba mpya, wakati siyo kweli.

Kumkumbusha hilo CCM ni sawa na Mimi hapa kukumbusha wewe kuwa:

"CCM inajifanya kama vile hakujawahi kuwapo kwa mchakato wa kupata Katiba mpya, wakati siyo kweli."

Unadhani wanahitaji kukumbushwa jambo wanalolijua na ambalo kwa hakika ni walilodhamiria (kweli kweli) kutoriridhia (no matter what)?
 
Back
Top Bottom