OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,404
- 104,613
Tunaona reaction ya watu kuhusu mauaji ya yule ndugu anayesemwa ameuawa na Hamas. Kile sio kitendo cha kibinadamu na cha kukemewa sana.
Japo sasa kemeo linaweza kuwa halina impacts kwa sababu Hamas na Israel hawasikii chochote.
Lakini kama kinachouma ni mauaji ya mwenzetu? Tulichukua hatua gani kwa mauaji yaliyohisiwa kufanyika na serikali na vibaraka wa viongozi? Mbona hatukutoa makaripio na makemeo kama hayo? Kwamba kina Lisu waliotaka kuuwawa hadharani hawakuwa wa dhamani sana mpaka tuwe kimya?
Sisemi kwamba tubaki kimya kuhusu huyu ndugu aliyetekwa na Hamas, la hasha, bali ni kuuchuna kwa hawa ambao wapo ndani ya uwezo wetu. Polisi wanaua watu hovyo, tumewafanya nini kuanzia Rais wa nchi mpaka mkuu wa mapolisi? Je hawa tumewapa haki ya kuua?
Tumefanya nini kwa watu tunaowamudu? Kwa nini hatumii hiyo nguvu mnayotumia kwa Gaza hapa nyumbani pindi madhira kama hayo yakitokea?