Uduni na unafiki wa watanzania: Walimu wana Mchango Mkubwa

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,555
41,066
Kiuhalisia, uduni wa jamii ya Watanzania, upo katika fikra duni, ubunifu duni, uadilifu duni, unafiki, kutojiamini na kukosa ujasiri.

Umri wa utoto mpaka kufikia umri wa sekondari, ni umri muhimu sana unaoweza kuamua huyu mtoto atakuwa ni mtu wa namna gani hapo baadaye. Umri hjo unahitajika sana kumjenga mtoto. Na wakati huu ndio ambao mtoto anakuwa na wazazi wake, lakini muda mwingi anakuwa na walimu. Hii ndiyo sababu ya baadhi ya mataifa, hasa ya watu wanaojitambua, kuipa umuhimu mkubwa sana fani ya uwalimu.

Kwa bahati mbaya, kwa Tanzania, tumeifanya fani ya uwalimu ni kwaajili ya watu wenye uwezo mdogo wa akili na na uwezo mdogo wa kumudu masomo. Na polisi tukaifanya ni fani kwaajili ya walioshindwa kabisa masomo. Ndiyo maana kuna wakati mzazi akiambiwa mtoto wake hakufanya vizuri kwenye masomo, anauliza, "ina maana hawezi kupata hata nafasi ya kusomea uwalimu?", akiambiwa kuwa hawezi, anasema, "basi itabidi aende polisi"

Kwa kipindi kirefu, waliokuwa wakienda kusomea uwalimu wa shule ya msingi walikuwa ni wale waliopata division 4 (daraja la mwisho la ufaulu), na polisi ambaye tunataka awe msimamizi wa sheria za nchi na usalama wa raia na mali zao, ikawa ni fani ya walioshindwa kabisa masomo (division 0, maana yake ni watu wasiofundishika).

Yaani mtu mwenye uwezo mdogo wa kimasomo na akili, ndiyo unampa majukumu ya kulitengeneza Taifa. Taifa ni watu. Taifa linatengenezwa na Walimu. Halafu unampa mtu duni kutengeneza Taifa, unatarajia nini? Mwalimu duni ni lazima atawafanya watu wengi kuwa duni. Ni wachache sana, wale super intelligent waliofundishwa na mwalimu duni ndio, kwa uwezo wao binafsi watamudu kutengeneza maisha yao bila ya kuurithi uduni wa mwalimu.

Matokeo ya walimu duni ndiyo haya sasa tunasikia malalamiko kila mahali. Na kwa upande mwingine, fani ya uwalimu ndiyo yenye watu wengi wasiojielewa, wasioweza kujitetea wala kupigania chochote licha ya uwingi wao. Wengi wamebakia kujikomba kwa watawala waminyaji wa haki na uhuru wa watu ili tu angalao matumbo yao yawe na uhakika wa kushiba.

Leo, kwa mfano kule bungeni, katibu mkuu wa chama cha walimu, amethubutu kusema kuwa eti wakuruugenzi waendelee kusimamia uchaguzi mkuu, na waziri wa TAMISEMI aendelee kuwa msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa, huku akitoa sababu za kijinga kabisa kuwa eti kwa sababu mkurugenzi anayafahamu mazingira ya Halmashauri; kama vile msimamizi wa uchaguzi anaenda kutatua matatizo ya huduma za jamii husika. Sasa huyu mwenye fikra duni na unafiki wa kiwango hiki, ndiyo kiongozi wa walimu, je hao anaowaongoza watakuwaje?

Tukitaka nchi hii kuwepo na mabadiliko chanya, mabadiliko yaanzie na namna walimu na polisi wanavyopatikana. Badala ya kuzifanya fani hizi ni za watu wenye uwezo mdogo wa kimasomo, tuzifanye kuwa ni fani zinazohitaji watu wenye uwezo mkubwa wa akili, na hilo liendane na maslahi bora kabisa ili watu wenye uwezo mkubwa wa akili waende huko. Tuige mifumo ya mataifa kama ya UK.
 
Umemaliza kila kitu.
 
Kuwaona walimu wote ni wapuuzi kwa sababu ya wrong perception ya huyo mchumia tumbo Maganga ambaye kwa makusudi ameamua kujikomba kwa watawala ni kutowatendea haki walimu.Sababu za huyo katibu mkuu king'ang'anizi kwamba wakurugenzi wasimamie uchaguzi kwa sababu wanaijua jiografia ya eneo wanaosimamia haina mashiko kwa sababu hata nao si wazaliwa wa maeneo hayo wanayofanyia kazi
 
Mnawasingizia walimu bure.

Nchii hii watu wake wengi ni zaidi ya mazombie.

Sio walimu madokta manesi wakunga mainjinia wala wanasiasa humo mote kumejaa watu wasiojielewa.

Kama walimu wanaonekana ni kundi la wasiojielewa hao wanaojielewa mainjinia matabibu madaktari kuna kipi cha maana wamekifanya kuisaidia nchi?

Kwanini lawama apewe mwalimu?

Kwanini mwalimu apewe jukumu la kuikomboa nchi pekee?

Mainjinia madaktari ambao wana akili kwa mujibu wa mtoa mada hao kazi yao nini?
 
Hao wote unaowataja, kwenye hatua fulani, wametoka mikononi mwa Walimu. Ukitaka kulibadilisha Taifa, anzia na walimu ili wawabadilishe watoto. Watoto wakijengeka katika kuhoji, wakijengeka katika ujasiri, wakijengeka katika uhuru wa fikra; tabia hizo, walio wengi watakua nazo, na kuwa sehemu ya maisha yao. Hao watoto kuna wakati ndio watakuwa wazazi, viongozi, madaktari, n.k. Watakapokuwa wazazi, viongozi au wakuu wa taasisi mbalimbali hawataona tatizo la kubishana kwa hoja, kukosolewa au kuchangia mawazo yao wakiwa na uhuru wa fikra na siyo uchawa.
 
Back
Top Bottom