Uchaguzi 2020 Watano wakamatwa Kampeni za CHADEMA na CCM

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Watu watano wanashikiliwa na Jeshi la polisi Mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kufanya fujo, kujeruhi na kusabababisha uharibifu wa mali,wakati msafara wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na chama cha Mapinduzi (CCM) walipokutana njiani wakitoka kwenye mikutano ya kampeni.

Vurugu hizo zilitokea jana majira ya saa moja jioni wakati msafara wa mgombea ubunge wa CCM Patrobas Katambi na mgombea ubunge wa CHADEMA Salome Makamba kukutana eneo la Japanise Corner nakuibua fujo ikiwemo kuharibu magari.

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni Ramadhan mohammed(20), Yuda Kanoku(22), Frank Chiza(20), Timoth Amos(20) na Mussa Luhende(21) wote wakiwa wakazi wa Mkoa wa Shinyanga.

Pia Kamanda huyo amesema kuwa katika vurugu hizo Hasani Masanja(28) mkazi wa Mtaa wa Majengo alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali kidevuni huku gari ya matangazo ya mgombea ubunge CCM lilivunjwa vioo vyote na magari mengine mawili yaliharibiwa pamoja.

Aidha kamanda Magiligimba ametoa wito kwa wanasiasa pamoja na wafuasi wao kuacha kufanya maandamano baada ya mikutano ya kampeni.
 
Vijana under 25 washadanganywa hapo kuna nchi ya ahadi yenye mito ya asali na maziwa, wanafanya fujo tu.

Chadema ni Sacco's ya kisasa tu.
 
Vijana under 25 washadanganywa Hapo Kuna nchi ya ahadi yenye mito ya asali na maziwa,wanafanya fujo tu.

Chadema Ni Sacco's ya kisasa tu
Hapo imetajwa CDM peke yake? Hao vijana unaosema si ndio CCM imewanyima ajira na kuua sekta binafsi ili waendelee kutegemea kuishi maisha yakutegemea watu wengine.

Jifunzeni kuheshimu vijana namuwatengenezee mazingira bora, miaka 59 tangu tupate Uhuru, huku nchi Ikiwa imejaa utajiri wakila aina, halafu kunasehemu watu wanakosa tu maji Safi?. Kweli heri CORONA kuliko CCM.
 
Hapo imetajwa CDM peke yake?. Hao vijana unaosema sindio ccm imewanyima ajira na kuua sekta binafsi ili waendelee kutegemea kuishi maisha yakutegemea watu wengine. Jifunzeni kuheshimu vijana namuwatengenezee mazingira bora, miaka 59 tangu tupate Uhuru, huku nchi Ikiwa imejaa urajiri wakila aina, halafu kunasehemu watu wanakosa tu maji Safi?. Kweli heri CORONA kuliko CCM.
Bado unasubiri nchi ya asali badala ya kufanya kazi ujenge Taifa.

Kazi yako kuweka genge la mapambio ktk Sacco's yenu.

Hakuna mdanganyika Sasa hivi,hao vijana miaka 22 hawakupiga kura 2015 wengi wakijua watoto,wakiwajua Tena 2025 hakuna atakayeshughulika na nyinyi walaghai wa nchi.

Bora CCM mbivu kuliko Sacco's yenu hyo kilimanjaro
 
Waliokamatwa ni vijana wa CHADEMA wakati maelezo yanaonyesha kuwa walifanyiana fujo na vijana wa CCM.
 
Mbona waliokamatwa ni vijana wa umri mdogo na hata sidhani kama wanajielewa hata kufikia hatua ya kujilipua kwenye mambo ya siasa!
 
Wahusika na wasiohusika wote wamekamatwa au waliohusika hawajakamatwa.
 
Vijana wengi sana watampigia kura Lissu awamu hii. Vijana ni wengi mno wamenyimwa fulsa za kimaendeleo kwa miaka 5 ya CCM ya Magufuli.
Vijana hawa walijifanya hawana muda wa kujiandikisha, hawana chamkufanya zaidi ya Fujo zao
 
Bado unasubiri nchi ya asali badala ya kufanya kazi ujenge Taifa.

Kazi yako kuweka genge la mapambio ktk Sacco's yenu.

Hakuna mdanganyika Sasa hivi,hao vijana miaka 22 hawakupiga kura 2015 wengi wakijua watoto,wakiwajua Tena 2025 hakuna atakayeshughulika na nyinyi walaghai wa nchi.

Bora CCM mbivu kuliko Sacco's yenu hyo kilimanjaro
Naona uko kwenye ajira ya buku 7 leo
 
Watu watano wanashikiliwa na Jeshi la polisi Mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kufanya fujo, kujeruhi na kusabababisha uharibifu wa mali,wakati msafara wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na chama cha Mapinduzi (CCM) walipokutana njiani wakitoka kwenye mikutano ya kampeni.

Vurugu hizo zilitokea jana majira ya saa moja jioni wakati msafara wa mgombea ubunge wa CCM Patrobas Katambi na mgombea ubunge wa CHADEMA Salome Makamba kukutana eneo la Japanise Corner nakuibua fujo ikiwemo kuharibu magari.

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni Ramadhan mohammed(20), Yuda Kanoku(22), Frank Chiza(20), Timoth Amos(20) na Mussa Luhende(21) wote wakiwa wakazi wa Mkoa wa Shinyanga.

Pia Kamanda huyo amesema kuwa katika vurugu hizo Hasani Masanja(28) mkazi wa Mtaa wa Majengo alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali kidevuni huku gari ya matangazo ya mgombea ubunge CCM lilivunjwa vioo vyote na magari mengine mawili yaliharibiwa pamoja.

Aidha kamanda Magiligimba ametoa wito kwa wanasiasa pamoja na wafuasi wao kuacha kufanya maandamano baada ya mikutano ya kampeni.

Wote watoto hao
 
Vijana wengi sana watampigia kura Lissu awamu hii. Vijana ni wengi mno wamenyimwa fulsa za kimaendeleo kwa miaka 5 ya CCM ya Magufuli.
Na vijana hao mil 18 tayar ni wanachama wa ccm, wa kifupi 70% Tanzania ni ccm
 
Back
Top Bottom