n00b
JF-Expert Member
- Apr 10, 2008
- 1,006
- 2,667
- Wapenyeza rushwa kuivuruga
- Vigogo CHADEMA washitukia
KATIKA kile kinachoonekana mkakati wa kuupata Urais kwa gharama zozote, kigogo mmoja anayetajwa kuwania nafasi hiyo ya juu, anadaiwa sasa kupenyeza sumu ya rushwa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Taarifa za ndani ya kambi ya mgombea huyo ambaye kwa sasa amejikita ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) zinaeleza kwamba tayari amekua na mazungumzo na baadhi ya vijana ndani ya Chadema kwa nia ya kukihujumu chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Hata hivyo, taarifa zinaeleza kwamba, uongozi wa juu wa chama hicho umekua makini na njama hizo na kwa kutumia makachero wake, umejipanga kukabiliana na yeyote anayekusudia kufanya hujuma.
"Ameanza kushirikiana na Vigogo wenzanke hasa wale wenye "permanent interests" kuhakikisha wanaingiza mbegu ya rushwa ndani ya Chadema kwa kuwarubuni vijana walioko ndani ya chadema ikiwa ni pamoja na kurecruit wapya waingie kwa nia moja ya kuvuruga mikakati ya upinzani.
"Mkakati huu umeanza muda mrefu na unaanza kuota mizizi. Vijana hawa watakuwa wanapinga kwa nguvu zote kunapotokea uelekeo wowote wa baadhi ya vigogo wazito wanaoweza kuihama CCM na kujiunga na Chadema kutokana na mizengwe na rushwa," anaeleza mtoa habari ndani ya kambi ya mgombea huyo.
Tayari baadhi ya viongozi makini ndani ya Chadema wameshagundua mpango huu unaoendeshwa nje ya chama na huenda wakatoa tamko hivi karibuni kuwaweka sawa wanachama wake kuhusu mbinu hii ya kijasusi inayoendeshwa na walafi wa madaraka ndani ya chama tawala CCM.
Ni hivi karibuni muasisi wa CHADEMA mzee Edwin Mtei ameonya tabia ya baadhi ya viongozi wake kuanza kujipanga kuwania Urais mwaka 2015.
Pamoja na Mtei kutofafanua, baadhi ya watu ndani ya CCM na CHADEMA wameuelewa kwa undani mwanasiasa huyo mkongwe kutokana na angalizo ambalo linalenga kuwatahadharisha na mbinu za kutaka kuwagawa.
"Watu wamejipanga kupata Urais na wako radhi kumnunua mtu yoyote ili njia yao iwe nyeupe. Ule msemo usemao kuwa kwenye siasa hakuna uadui wa kudumu ila kuna maslahi ya kudumu umeanza kuonekana kwenye chaguzi hizi za CCM zinazoendelea.
"Ule wimbo wa kujivua gamba kwa watuhumiwa wa ufisadi umesahauliwa na badala yake wahusika hao wameonekana ni vinara baada ya kupitishwa na Vikao vikuu vya CCM vilivyoasisi falsafa hiyo ya kujivua gamba," anaeleza.
Katika kuonyesha kwa undani kinachoendelea ndani ya CCM, mtoa habari huyo anazungumzia kuwapo kundi la wana CCM wanaohofia nguvu ya Chadema baada ya 2015.
"Zile permanent interests zimeonekana dhahiri hasa pale 'wastaafu watarajiwa' wamejikuta wakiungana kimkakati katika kuwazuia wale wanaoonekana kuwa tishio pindi wakipata nafasi ya kuingia kwenye vikao vya maamuzi. Taswira halisi ni huu muenendo wa nafasi za NEC, Wenyeviti Wilaya na mikoa unaoendelea ambao umebeba sura halisi ya kuweka rushwa mbele kwa ajili ya kuweka watu wao na kusahau kabisa kuwa uongozi ni kwa maslahi ya Taifa zima na si kwa ajili ya kundi dogo la wachache," anasema.
Tayari kumekua na mwitikio mkubwa kutoka kwa wananchi mbalimbali wa mijini na vijijini kutokana na nguvu kubwa ya Chadema inayotokana na kampeni za kila siku nchi nzima za chama hicho zilizoanza na 'operesheni sangara' na sasa 'Movement for Change-M4C'.
Chanzo: Kulikoni - Oktoba 12, 2012