Not_Yet_Uhuru
JF-Expert Member
- Oct 11, 2010
- 1,304
- 431
Akiongea katika kipindi cha DK 45 ITV. Wasira kasema kwanza anao uzoefu kwa kuwa alikuwa waziri wa kilimo enzi hizo; kwa mazao ya chakula ni tatizo kwani jirani zetu ambao tunapakana nao kama Kenya Sudan na Somalia wanapokuwa na matatizo ya vyakula hununua kwetu.............. Naomba msaada kwa wanajiographia kuhusu nchi tunazopakana nazo..........
Wala hatumshangai sana babu huyu kusema SUDAN inapakana na TZ...nahisi ndio usingizi unamtesa kwa uzee maana mara ya mwisho kumwona, alikuwa 'Zzzzzzzzz zzz, ndoto, anaota bungeni...! akili zimechoka..! Huyu Babu yupo tangu enzi Mwl Nyerere anaanza kuiongoza Tanganyika, na anajigamba kuwa alipewa Uwaziri akiwa kijana! Hata Mbunge Machali hivi Majuzi alimtolea mfano kuwa ni kati ya Matatizo ya Ajira ya Vijana maana wanashikilia nafasi hadi wafie madarakani, wakati vijana wanakosa ajira! Sasa angalia alivyo hayupo-hayupo!, ila tusisahau kuwa ni 'Mshauri wa JK'...! Je JK ataweza kuvuna toka kwa watu kama hawa??
Swali Je, endapo JK anamuuliza Mahusiano yetu na Nchi jirani yakoje, mzee huyu si aajabu akasema pia ana wasiwasi na Libya na Misri, na sidhani kama anakumbuka kuwa Gadhafi na Mubarak hawako madarakani tena... Ndio Wanaoiongoza nchi yetu hao...Kazi kweli kweli..