Wassira amtaka Dr. Slaa aache kuita wake za watu chumbani!

Yeye Wasira alipomchukua mke wa marehemu mzee Ndege aliona fresh.Hao watoto wa ndugu yake kuchukuliwa anaona noma.Mkuu wa nchi alishasema '"KULA ULIWE"!!! sasa iko mbaya gani??!wanafuata ruzuku ya CDM hao,yaani wako kibiashara zaid!!
 
[h=3]Watoto Wa Wassira Kujiunga CHADEMA; Ufafanuzi[/h]


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI UFAFANUZI KUHUSU SISI KUJIUNGA NA CHADEMA NA MALUMBANO KUHUSU MAJINA YETU

Tarehe 30/09/2012 mimi Esther Wasira na dada yangu Lilian Wasira tulijiunga na CHADEMA na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Dr Willibrod Slaa. Tulielezea kwa kirefu sababu za sisi kujiunga CHADEMA na tukasisitiza kuwa tumeridhika kuwa CHADEMA ni chama chenye dhamira safi ya kuiongoza Tanzania na kwamba ni chama kinacholeta matumaini mapya ya kuijenga Tanzania mpya yenye neema. Waandishi wa habari walijaribu sana kutudodosa kujua tuna uhusiano gani na Waziri Steven Wasira. Tulielezea wazi kuwa mahusiano yetu ya kifamilia hayahusiki na sababu na dhamira yetu ya kujiunga CHADEMA. Hata hivyo tulielezea kuwa Waziri Steven Wasira ni baba yetu mdogo ambaye alinyang'anyana ziwa na baba yetu mzazi, wakili George Wasira. Tulidhani hiyo ilitosha na lisingekuwa swala tena la kujadili na badala yake hoja ya kujadiliwa ingeweza kuwa sababu tulizozieleza za kujiunga CHADEMA. Tunasikitishwa sana na malumbano yaliyofuata baada ya hapo kuhusu kama sisi ni watoto wa Wasira au la. Kama tulivyoeleza, tumejiunga CHADEMA kwa sababu tulizozieleza hapo awali na wala si kwa sababu nyingine yeyote. Hatujajiunga CHADEMA kumdhalilisha mtu, kumfedhehesha mtu au kukipatia umaarufu CHADEMA kwa vile tu tunatumia jina la Wasira. CHADEMA ni chama cha siasa tena chenye wanachama na wafuasi wengi Tanzania hivyo si kashfa bali ni fahari kubwa mtu kujiunga CHADEMA na tena ni ushahidi wa mtu kujitambua. Pia CHADEMA ni Chama maarufu sana Tanzania kwa sasa hata pengine ni maarufu kuliko CCM hivyo hakihitaji kujipatia umaarufu kwa mgongo wetu. Sisi tunawaheshimu sana wazee wetu na tutaendelea kuwaheshimu ila linapokuja swala la chama cha kujiunga linabaki kuwa hiari yetu kwa kuzingatia sera za chama na uwezo wa chama husika katika kujenga Tanzania tunayoitaka na hilo ndilo lililotupeleka CHADEMA. Na hii ni haki yetu ya msingi kabisa inayolindwa na Katiba ya nchi hii chini ya ibara ya 20(1). Ikumbukwe kuwa mmoja wa Waanzilishi wa CHADEMA ni Mzee Wasira. Dhamira ya kuanzisha CHADEMA ilikuwa ni kushika dola na hili ndilo CHADEMA imekuwa siku zote inajaribu kuwashawishi Watanzania kuwa sasa wamekomaa na wanastahili kuchukua dola. Kwa vile kuchukua dola ilikuwa ndio ndoto ya baba yetu mzazi Mwanzilishi wa CHADEMA, sisi kama watoto tumejiunga na M4C ya CHADEMA ili tuweze kutimiza ndoto ya baba yetu kuwa CHADEMA siku moja ichukue jukumu la kuiongoza Tanzania.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na: Lilian Wasira 0719 604156 Esther Wasira 0655 048797
 
Huyu mzee labda huwa anafanya yale mambo yake ya chumbani ofisini sasa amejisahau akidhani kila mtu ni hivyo.
 
Mimi naona ni ofisini.........sijui ''chumbani'' anakokuongelea ''PET'' WASSIRA ni wapi?

Lilian-Wassira-na-ndugu-yake-Esther-ndani-ya-CHADEMA.jpg

Namshauri mzee Wasira aanze kuala Karoti kwa wingi cause naona kama macho yake yana htilafu fulani hivi, naona kama kuna microphone tatu, moja ya ITV na zingine hizo 2 sijui ni za chombo gani, then tuna hii picha iliopigwa so i can imagine kulikua na wapiga picha zaidi ya 4, sijui ni chumba gani cha kulala hasa chanye faragha hivi kinaweza ku hold haya, also kwa utamaduni wa kwetu hapa tayari kisha watukana wanae kwamba walitaka/wamepita na huyu mzee, hizo nazo kwangu ni dalili za laana!
 
Kwa taarifa ya WanaJF, George Wassira alikuwa ni mmoja wa WanaCHADEMA wa kwanza na alichaguliwa Mwenyekiti Mkoa wa Mara.

George na mimi tulipata fursa ya kumtembelea Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, nilipokuwa Musoma nikieneza Chama; tukampelekea Katiba na Sera zetu nyumbani kwake Butiama. Nafurahi sana kwamba Lilian na Esther Wassira wamejiunga na M4C, kuimarisha ngome ya vijana wakombozi.
 
Kwa taarifa ya WanaJF, George Wassira alikuwa ni mmoja wa WanaCHADEMA wa kwanza na alichaguliwa Mwenyekiti Mkoa wa Mara.

George na mimi tulipata fursa ya kumtembelea Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, nilipokuwa Musoma nikieneza Chama; tukampelekea Katiba na Sera zetu nyumbani kwake Butiama. Nafurahi sana kwamba Lilian na Esther Wassira wamejiunga na M4C, kuimarisha ngome ya vijana wakombozi.
Asante baba Mtei, tunakukumbuka sana pamoja na mzee Ngwilulupi na Makani.
Nyie mtaendelea kukumbukwa kuwa ni watu makini.

Zinazoendelea sasa ni sisa za ushabiki tu.
 
Huyu mzee labda huwa anafanya yale mambo yake ya chumbani ofisini sasa amejisahau akidhani kila mtu ni hivyo.
Acha ofisini, huyu popote pale ni chumbani mpaka ndani ya bunge!


images


Mshuhudie hapa anavyouchapa usingizi!
Je ni chumbani au bungeni? Jibu analo!
 
Kuna watu labda hamumfahamu vizuri Wassira, ni kwamba Wassira alipigika na maisha ile kisawasawa, sasa wakati JK ankwenda kuomba baraka kwa mama Maria Nyerere, Maria Nyerere alimwambia nakubali mwanangu uwe Rais ila usimuache Wassira anaadhirika.

Wengi hili hawalijui ila kwakuwa JF ni mkusanyiko wa watu wengi najuwa wapo watakaothibisha maneno haya, Wassira mpaka leo nina uhakika hawezi kukosa sugu kwenye bega lake la kulia maana baada ya kupigigika na maisha ilibidi awe mbeba mabegi ya mawakili ili na yeye apate pesa ya kula. kwahiyo sishangazwi na lolote kutoka kwa Wassira.

matola kaka yangu wa hiari, nimekupa like kwakua umesema ukweli ila nina swali hapa, je kupigika kubeba mabegi ya mawakili na huko kuombewa na mama nmaria nyerere kuna husiana vipi na huku kusema asichafuliwe jina kwani hawa sio wanawe? binafsi nakuamni sana katika kuchambua hoja na ninalotegemea kutok kwamtu makini kama wewe ni kuijadili hoja yake kwa Dr slaa kwamba aache kugawa kadi chumbani..........................je ni kweli dr aligawa kadi chumbani? na je huko chumbani nani alikuwepo mwingine na kwanini amsemee dr NYUMA YA PAZIA LA KUVUNJA NDOA ZA WATU?
 
angalia kidole cha huyo dada anayepokea cardi kinaeleka wapi kwenye mkono wa dr. Kazi kweli kweli!!

jamani kwanini kila jambo tunalitohoa katika namna ya utusi utusi? Mara macho ya mdogo yanamtega dr mara kidole cha mpokea kadi ama kweli tumeshindwa kuwaza sasa tunawaza kwakutumia chini kwetu.
 
Hivi wasira ni jamii ya mnyama au mwanadamu.nikimuona nastuka hata sauti yake kama ya mnyama mwenye asili ya....nimesahau
 
Back
Top Bottom