Wasomi wengi watafariki kwa kung'ang'ania mishahara na hisani zisizowaacha na amani

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Kwa mfumo unavyokwenda Sasa hivi tutegemee wasomi na viongozi wetu waandamizi wengi kupoteza maisha kutokana na kuajiriwa au kupewa madaraka ambayo kwa kiasi kikubwa hayawaruhusu kumaliza siku wakiwa na amani, awatumii taalumu zao na awazalishi kwa ajili ya nchi kama walivyotamani kufanya kwa sababu mbili kuu;

1. Hawa watu na familia zao wanalipwa kuwatesa Watanzania kupitia maamuzi mabaya au kumsikiliza na kumuunga mkono kiongozi bila kujali ubaya wake. Kwa kuwa moyoni wanajua ubaya wao na kwakuzingatia kwao wanaimani, wanapata msongo wa mawazo nakudondoka. Hii ndiyo imepelekea miaka ya hivi karibuni tumepoteza viongozi wengi Sana. Wamepewa madaraka makubwa na wanajua chakufanya kitakachowapa furaha wananchi na nchi lakini hawafanyi hivyo, matokeo yake wanakaa na vitu kifuani nakulalamika ndani kwa ndani hadi hivyo vijimamambo vinawanyonga wanapotea.

2. Viongozi wengi wa Tanzania wanaishi maisha ya watu watatu, maisha ya Mhe. Rais ( anavyowaza ndivyo wanavyowaza japo awataki kuwaza hivyo) , wanaishi maisha ya dola( profesa/judge anasikiliza rpc au igp ameelekeza Nini na yeye anatekeleza then akiwa ofisini anajadili reality, akifanya maamuzi anafuata dola) na Viongozi wa dini, chochote anachosema kiongozi wa dini tunakichukua na kukiweka rohoni na kwenye matendo bila kutumia akili zetu kufikiri Kama kinatoka kwa Mungu au kinatoka kwa wanadamu. Matokeo yake watu wa aina hii wamedhani wanatafuta ugali wa watoto lakini baadaye watoto wanabaki yatima. Tunajitia kitanzi kwa ajira tunazopewa na wanasiasa tukiamini kwamba pesa ni Bora kuliko uhai wetu.

Haya mambo mawili yamewaua viongozi wetu wengi, wanasumbuliwa na msongo wa mawazo. Mawaziri Awana amani, makatibu wakuu hawana amani, wakurugenzi na majaji Hali ni mbaya. Wanabebeshwa maamuzi ambayo yapo kinyume na imani na elimu zao, yakiwazidi unasikia wameanguka, wameugua ghafla wamefariki nk. Haiwezekani Kama Taifa tupoteze viongozi wengi hivi na tusijue tatizo, tatizo kuu viongozi wetu Wana hofu na tutawapoteza wengi kwa sababu tiba ya hofu Ni amani.

Mfumo usio na haki na ambao tukumbuke hatukuuzoea utatumalizia viongozi wetu, nchi ambayo asubuhi Hadi jioni watu wanalalamika na kuwalalamikia viongozi hata ingejenga miradi gani bado tu wanaolalamikiwa watapoteza maisha kwa kukosa amani kutokana na kuona jamii inavyomwona.

Mfano: Tumepoteza wasomi wazuri sana kwa kuaminishwa kwamba nchini hakuna covid, hivyo watu viongozi wakikaa nyumbani wanaelezana Kuna covid ila wakikutana na bosi Mwenye nchi msimamo wao hakuna covid.Unajiuliza mtu wa aina hii asiyethamini hata afya yake alisoma ili Nini?

Sasa hivi tumeanza kujazwa ujinga kwamba hataitaji katiba mpya, Malalamiko yanayoendelea yameliondoa taifa kwenye kujadili maendeleo vyombo vyote ikiwemo polisi, mawaziri, mahakama, na hata ofisi ya mkuu wa nchi agenda inayojadiliwa ni Chadema ambayo Chadema yenyewe umeshikilia mitandao na kupitia mitandao wanaongea na kukosoa hadi tumepoteza focus, hii hofu waliyonayo watawala na stress zakupanga kupambana na Chadema unadhani zitawaacha na afya njema.

Wote wanajua umuhimu wa Katiba maana katiba mpya itadhibiti hata utumbuaji usio na tija, tunawamaliza viongozi kwa ujinga wao wakutotafuta amani ya moyo wanajikita kufanya kazi kwa stress mwisho wake mkiondoka kwa msongo wa mawazo na magonjwa ya moyo watu wanashnagilia maana wanapata ajira.

Niwaombe viongozi wetu jaribuni kutafuta amani ya moyo Duniani tunapita, msipambane na manyanyaso ya wenzenu maana namna unavyomnyanyasa mwenzako ndivyo unavyonyanyasika zaidi.
 
Umeandika mambo magumu ambayo kwa akili za Kiongozi aliyepo kwenye nafasi flani sidhani kama atakuelewa. Ila kwa kiongozi anayeelewa au kwa tajiri na binadamu mwingine yeyote aliyeelimika ataelewa umuhimu wakuishi kwenye jamii yenye amani.

Tunapokea watalii wengi si kwa sababu wanaipenda Tanzania Bali wanakuja kupumzika na kujitenga kidogo na msongo wa mawazo wa ofisi.

Lakini kwetu hapa viongozi wameteseka for five years, badala watengeneze mfumo wakuwapa amani wamefukua mfumo mbaya zaidi wakupambana na Watanzania. My friends, huu mfumo wakutengeneza maadui madhara yake ni kwamba ukiwa kiongozi utakosa Uhuru wa kula, Uhuru wa kunywa na mwisho utakosa Uhuru na jamii.

Kama mnataka mfurahie mishahra yenu, tengenezene jamii ya kazi na bata achaneni na kazi iendelee. Tunahitaji kula raha Kama taifa Wakati tukiendelea kujenga
 
Back
Top Bottom