X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,610
- 1,810
Watu watatu (3), walinunua mikate, mmoja alinunua mikate mitano (5) na mwinginee mitatu (3) jumla wakawa na mikate minane (8), na mwenzao wa tatu yeye hakununua chochote...!
Wote watatu, wakala kwa vipimo sawa, hakuna aliyezidisha wala kupunguza, kisha yule wa tatu akatoa shiling elfu nane (8,000), akawagawia wale wenzake wawili wagawane.
Ugomvi ukawa katika kugawana zile pesa. Yule aliyenunua mikate mitano (5) akataka kuchuwa shilingi elfu tano (5,000), na shilingi elfu tatu (3,000) ampatie mwenzake. Yule mwenzake akataka wagawane sawa kwa sawa, yaani kila mmoja achukuwe shilingi elfu nne (4,000).
Wakashtakia kwa hakimu... Maamuzi ya hakimu yakawa hivi:
Aliye nunua mikate mitano (5) achukuwe shilingi efu saba (7,000) na aliyenunua mikate mitatu (3) achukuwe shilingi elfu moja (1,000).
Aliyenunua mikate mitatu (3), alipo fahamishwa akakubali na kuridhika. Je hakimu alitumia fomula gani katika kugawa haki?
fafanua...