Wasiomjua Dr. Slaa soma mada hii, kabla ya uanasiasa na baada

Mkuu mimi ni mtanzania kama hao wengine labda kama sina haki kuielewa ; imeandikwa kwa kiwango cha chini sana labda kama iliandaliwa kwa wanafunzi wa shule za kata; kujishusha daraja siwezi game yangu nyingine kabisa wewe ndio unapaswa upandishe kiwango

Chama
Gongo la mboto DSM

hata tahira/kichaa anayeokota makopo jalalani siku zote hujiona yuko sahihi kufanya vile!!
 
Thanks, lakini hapa tunajadili hoja, ungetulitea hoja zako kupambanisha na zetu tungekuona una fanya analysis iliyotukuka, lakini kuproromosha mtusi bila hoja za kukabiliana na hoja zetu kuna dalili ya kupwaya kidogo.
Ni mtaalam wa kuanalyze matusi, usimhukumu kwani ndiyo taaluma yake. Mimi huwa sielewi unaposoma hoja nzito zenye vigezo vya uhakika matusi yanapata vipi nafasi akilini mwako.
 
Hoja za slaa ziko kikanisa zaidi na mbona ulisema tusiwaseme viongozi wa chama na wewe ni mfanyakazi wa chadema Tv na unalipwa mshahara na chama kilicho jengwa na wakina zitto. sasa unamsema zitto kwamba anahoja za kibinafsi sasa mwambie huyo mzee ajenge nyumba nyingine maana mwakani hana chake na nyumba ya tegeta kaweka jina la josephine kama ataendelea hivyo atakuwa mlinzi pale makao makuu.

Tope...
 


images

Dr. Slaa

Dr. Slaa si mtu mwenye maneno mengi, ni mtulivu na mkimya kiasi chake, lakini akipanda jukwaani na kuanza kulishambulia huku na kule huwezi kuamini kinachotoka ubongoni mwake. Kimya kingi kina mshindo.

Wengi hawamfahamu Dr. Slaa vilivyo, wengi wanamwona sasa baada ya kuingia bungeni na sasa katika majukwaa ya siasa, ukweli ni mtu mbunifu, mpenda maendeleo na mwenye kujitoa kwa ajili ya wengine bila kujibakiza. Ufahamu wangu wa huyu Dr. Slaa ni wa muda mrefu, lakini wengi wetu wanachukulia mambo ya juu juu tu bila kujua undani na utendaji uliotukuka wa mtu huyu.

Machache kati ya mengi kuhusu Dr Slaa kabla ya kuwa mwanasiasa, kuwa Mwanasiasa na hatimaye kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, ana mlolongo wa mambo mengi ambayo yanaonyesha ubunifu wa hali ya juu, na pia mwepesi kuwaelewa vijana na kuendana nao tofauti na watu wengine wa kizazi chake.

Pamoja na kuwa mwanachama wa CCM, baada ya kuombwa na Wanakaratu agombee ubunge kule baada ya kuchoshwa na mbunge aliyekuwepo wakati huo, CCM iliendelea na mizengwe ile ile kama iliyotokea juzi pale Dodoma kuwaengua watu wanaofaa kwa uongozi. Wanakaratu wakiamua hawataki longolongo, wakamsihi kwamba wameamua awe mbunge wao na wakamwomba achague chama kingine agombee kwani hawamtaki kabisa mbunge aliyepo. Kwa ridhaa ya wananchi akaamua kujitoa CCM na kujitosa kujiunga na Chadema ili agombee ubunge kuridhia matakwa ya wanakaratu.

Kabla ya kuwa mwanasiasa
kuna mengi ya maendeleo ambayo wengi tunayaona huku tusijua kama Dr. Slaa ndiye aliyebuni na kuyaendesha kama ifuatavyo.
  1. Dr. Slaa ndiye amekuwa wa kwanza Tanzania kuagiza big truck for load and unload makontena bandari ya Dar es Salaam wakati akiwa Katibu Mkuu TEC. Ilikuwa ni miaka ya 1980th, hakukuwa hata kampuni au watu binafsi waliothubutu kufanya hivyo. Truck hilo lilikuwa na crane za kupakia na kupakua bila taabu kokote linalokifkishwa container na kwa truck hilo. Baadaye makampuni yakabembeleza wauziwe gari ile, ndipo Barala La maaskofu likawauzia.
  2. Kwa mara ya kwanza baraza la Maaskofu Tanzania lilipoanza kuwa na matumizi ya computer ikiwepo ofisi yake Dr Slaa kama katibu Mkuu, na taasisi za upashanaji habari ambazo zilikuwa chini ya uongozi wake ikiwa ni pamoja na:

  • Gazeti la kiongozi kuanza kutumia mfumo wa computer katika idara ya set up
  • TMP (Tanganyika Mission Press) Kipalapala idara ya uchapishaji (printing) wakitumia Apple computers.
  • TMP Book deparment Tabora mjini) idara ya maduka ya vitabu na usambazaji vitabu wakitumia Apple computers
  • TAPRI idara ya tungo za mawasiliano vitabu TEC iliyokuwa na ofisi zake Seiminari kuu Kipalapala Tabora.

Idara hizo zilikuwa na matumizi ya computer na PageMaker & QuakExpress software ambazo kwa graphic designers ilikuwa kitu kigeni kisichozoeka bado Tanzania ukitilia maanani wakati huo tulikuwa na chuo kimoja tu cha ardhi kule Tabora kujifunzia Graphic Design kabla ya Ardhi Dar haijaanza kukamilika. Huo ni ubunifu wa Dr. Slaa kwa wakati huo wakati wengi Tanzania hawajafunguka kuhusu matumizi ya teknologia ya ulimwengu wa dot com.

NB.
Wakati huo chuo pekee cha mawasiliano (journalism) Tanzania kilikuwa ni Nyegezi-Mwanza pekee kilichokuwa kikiongozwa na AMECA (Balaza la Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati kimoja kikiwa Kitwe - Zambia, cha Nyegezi kiliendeshwa na TEC Dr. Slaa akiwa msimamizi mkuu kama Katibu Mkuu.​

Dr. Slaa atakumbukwa sana kwa makubwa aliyofanya kujenga na kuikuza TEC

  1. Makao makuu ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) tunayoona siku hizi ni matunda ya ubunifu wa Dr. Slaa alipokuwa Katibu Mkuu pale. Jengo la awali ni lile lililo upande wa mbele zinapotumika ofisi siku hizi ambapo yalikuwa madarasa ya shule ya sekondari ya Masisita Tanzania, ambayo baadaye ilihamishiwa Bigwa Morogoro kupisha kiwanja hicho kuwa makao ya Maaskofu Katoliki Tanzania, awali yalikuwa pale ofisi za St. Joseph, Dar es Salaam. TEC aliyoikuta DR. Slaa ilikuwa na jengo hilo la madarasa na jengo lilolokuwa la utawala wa shule. Dr. akabuni majengo ambayo tunayoana sasa, hata kama hayakukamilika yote waliofuata walikamilisha kazi alioyoianza.
  2. Kaone maendeleo na majengo katika jimbo la Mbulu ni jitihada za Dr. Slaa na Fr. Narda ambao kwa pamoja walifanya makubwa.
  3. Kaangalie jimboni kwake huduma za kijamii ambazo amezifanya, utachoka mwenyewe kiasi ambacho CCM imekimbiwa kabisa huko sababu utendaji wa Slaa huko na CCM ni sawa na kulinganisha mlima na kichuguu.
  4. Dr. Slaa kwa tunaomfahamu ni mwanamapinduzi na mpenda maendeleo, na pengine mengi alikuwa anayafanya yakaonekana mapya mno kwani alikuwa anaona mbali kuliko hawa wakubwa wake, ila sipendi kuliongelea sana hilo.

Chadema yaimarika baada ya Dr. Slaa kuwa mgombea urasi uchaguzi Mkuu uliopita.

Siyo siri Chadema hakikuwa na nguvu tunayoona sasa hivi licha ya kuwa na sera nzuri, lakini leo tunaona nguvu ya Chadema inayoogopewa mno na CCM ni kutokana na Chadema katika dakika za majeruhi kuamua kumwangukia Dr. Slaa agombee urasi ambao Samweli Sitta aliingia mitini baada ya makubaliano nao. Tangu hapo Chadema imekuwa na nguvu ya ajabu.

Je, vijana hao waliokuwemo ndani ya Chadema kabla ya Dr. Slaa kugombea Urais kwa nini hawakuipaisha juu Chadema kama sasa? Baada ya Dr. Slaa kuipaisha Chadema juu sasa tunakuja na kauli mbiu ya kubeza makubwa yaliyofanywa na hawa mnaowaita kizazi cha kabla ya uhuru. Hapana tuwe waungwana, pamoja na kila mmoja kuwa na haki za kugombea nafasi tusigeuze uhuru huo kuwabeza hawa ambao wametufikisha tulipo, na bado tunahitaji mchango wa ushauri, uongozi, hekima na busara zao. Uongozi bora ni kuchanganya mapya na ya kale kwani
viatu vya zamani vyaijua njia.

Ubunifu wa Chadema viongozi wakiwa mojawapo waliozaliwa kabla ya Uhuru Dr Slaa na Kamanda Mbowe:

  • Dr. Slaa ndiye mbunge ambaye baada ya kuingia bungeni alianza kuchangamcha kwa kuichambua serikali na kasoro zake kitu ambacho katika mabunge yaliyotangulia wabunge walikuwa ni rubber stamp ya serikali.
  • Chadema wakiwemo hao unaoona walizaliwa kabla ya uhuru wamebuni mapya katika shughuli na kampeni za uchaguzi Tanzania kuwa zenye mvuto kuanzia mkuktano wa ufunguzi wa kampeni uchaguzi Mkuu uliopita ulifanyika Kidongo Chekundu baada ya Dr. Slaa kushusha makumbora mazitomazito kuituhumu serikali, watendaji wa serikali na CCM, tuhuma ambazo CCM wanazidi kubabaika kuwanyoshea kidole wahusika kisha kuwakumbatia tena hivi karibuni kule Dodoma.
  • Mkutano wa Kidongo chekundu Dar es Salaam ndio ulioanza kutufungua macho na masikio Watanzania na kuanza kujifunza elimu ya uraia ambayo tulikuwa tunazibwa na CCM tusiijue.
  • Dr. Slaa ndiye aliyetufunza na kutufunua kwamba raia wanayo nguvu ya kuiadabisha serikali haki zao za msingi zinapokiukwa kwa kauli mbiu ya nguvu ya umma (peoples power).
  • Utumiaji wa chopper kufikia maeneo magumu kufikika kwa magari na kurahisisha kazi ya kampeni, CCM wakaiga.
  • Kuwa na magari yanayotumika kama majukwaa ya mikutano badala ya kupoteza gharama na muda kujenga majukwaa yatakayotumika kwa dakika chache.

Ilani ya Uchaguzi Chadema ndiyo inayotumika na yenye uzito sasa hivi:


  • Fukuto la Katiba mpya linaloendelea sasa nchini ni uzao wa ilani ya Chadema na ilani ya Dr Slaa kwamba kinachofuata baada ya Uchaguzi mkuu ndani ya siku 10
  • Kikwete kufanya mabadiliko ya barala la mawaziri mara kadhaa ni kutokana na shinikizo la wabunge wa Chadema bungeni.
  • Serikali kubana matumizi ya ziada ili kuokoa pesa za walipa kodi

Kuna mengi tu wachangiaji wengine watachangia, ni dhana potovu kuwa na fikra za aina hiyo na kuwabeza wabunifu wa mengi, waliongoza nchi hii, wenye kuturithisha mengi kwa uzoefu na busara zao na walioongoza nchi hii hadi kuwa na utulivu wa aina yake. Leo vijana mnaowasema yanayojilia ni amani kusambaratika na mauaji ambayo ilikuwa hadithi za kusimuliwa kutoka nchi nyingine, leo serikali ya CCM inayoongozwa na Rais kijana kuliko Rais mwingine aliyemtangulia imetwishwa na aibu kubwa ya kitaifa na kimataifa ya mauaji ya raia wasio na hatia.

Kuna nchi ambazo ni kielelezo cha vijana ambao mimi ningewaita watoto kukabidhiwa madaraka ya kuongozia nchi na kusababisha maafa makubwa kwa nchi husika kama Liberia, Ujerumani chini ya Hittler, na kinachoendela huko Zaire ya sintofahamu.

Vijana achaneni na uroho wa madaraka, vema kubaki watumishi na watendaji wazuri serikalini na vyamani kujifunza mbinu za uongozi na kupata uzoefu katika kuongoza nchi.

Kuongoza nchi hakuna shule wala kitabu cha kusomea au chuo. Hekima na busara ya mtu ndio kielelezo cha fanaka katika kuongoza nchi.

  • Vijana wana papara,
  • wanataka njia ya mkato,
  • pagumu wanataka kulazimisha bila busara wala kutumia akili
  • Vijana wanalipuka kama moto wa gas
  • mambo yakigeuka magumu ni mabavu hutumika.
Aya ya mwisho umepingana na Mhe. Zitto wako ambaye haoni tija yoyote katika maendeleo ambayo inaweza kuleta na wale wote waliozaliwa Kabla ya uhuru.
 
Mie namjua kuliko wewe, tulifahamiana bado yupo TEC na baada ya kuacha utumishi wa Mungu tulianzisha ofisi hapa jijini (nje kidogo ya jiji) na kufanya biashara ya halali ya export kabla ya kuingizwa siasa ghafla.
 
Mie namjua kuliko wewe, tulifahamiana bado yupo TEC na baada ya kuacha utumishi wa Mungu tulianzisha ofisi hapa jijini (nje kidogo ya jiji) na kufanya biashara ya halali ya export kabla ya kuingizwa siasa ghafla.

Shukrani, mtu hafahamiwi na mtu mmoja tu, wewe, mimi na wengine wengi. Kila mmoja atampambanua kwa uzoefu wa kufahamiana au kumfahamu yeye.
 
Hoja za slaa ziko kikanisa zaidi na mbona ulisema tusiwaseme viongozi wa chama na wewe ni mfanyakazi wa chadema Tv na unalipwa mshahara na chama kilicho jengwa na wakina zitto. sasa unamsema zitto kwamba anahoja za kibinafsi sasa mwambie huyo mzee ajenge nyumba nyingine maana mwakani hana chake na nyumba ya tegeta kaweka jina la josephine kama ataendelea hivyo atakuwa mlinzi pale makao makuu.

Martin Lutter King yule mpigania haki, usawa na ubaguzi wa rangi nchini Marekani anavyoenziwa na kuwa na siku ya holiday nchini Marekani alikuwa mwanasiasa au mtumishi wa kanisa?

Tunafahamu watu wasio na upeo katika uwepo wa Mungu na utumishi kwa Mungu huwa kujitoa kwao kuna ukomo na kukata tamaa mapema kwa sababu kichocheo ni haja na manufaa binafsi badala ya hali ya kujitoa kwa ajili ya jamii anayoitumikia.

Katika utumishi wa umma huangaliwa back ground ya mtu historia ya kutumikia umma, haijalishi anatumikia taasisi au idara gani, lakini zote zinahusu umma anaotarajia au anaoutumikia.

Inaelekea watu tunajadili kwa vionjo kile moyo ukipenda bila kujenga hoja za msingi katika mada inayojadiliwa.
 
Aya ya mwisho umepingana na Mhe. Zitto wako ambaye haoni tija yoyote katika maendeleo ambayo inaweza kuleta na wale wote waliozaliwa Kabla ya uhuru.


Kuongoza nchi hakuna shule wala kitabu cha kusomea au chuo. Hekima na busara ya mtu ndio kielelezo cha fanaka katika kuongoza nchi.

  • Vijana wana papara,
  • wanataka njia ya mkato,
  • pagumu wanataka kulazimisha bila busara wala kutumia akili
  • Vijana wanalipuka kama moto wa gas
  • mambo yakigeuka magumu ni mabavu hutumika.

Haya ya sifa za kiongozi kijana siwezi kuyafuta katu kwani historia ni mwalimu, na kuna sababu za msingi kuweka kigezo cha umri kutokana na yaliyojitokeza katika hitoria za tawala mbalimbali.

Unajana una mambo yake, ndio maana wanatakiwa kuwa watulivu na kujizoesha fadhila ya unyenyekevu, uvumilitu na ustahimilivu, la sivyo itakuwa ni vurugu tupu tangu mwanzo hadi mwisho na kuishia kumwaga damu.

Mashirika ya zamani ya usafri nchini kama shirika la mabasi ya reli au kamata haikuajiri mtu wasiyemjua kushika usukani wa magari yao. Mwenye kutaka kibarua cha udereva alitakiwa kufuatana na dereva mzoefu kwa miaka kadhaa kupata uzoefu stahiki ndipo aweze kukabidhiwa usukani aushike kwa kujiamini kutokana na uzoefu alioupata. Ndio maana ajali wakati huo halikuwa jambo la kawaida. Siku hizi ajali ni kama ukishika ushukani vyombo vya usafiri ukifika salama mwisho wa safari ni bahati kwa vile ajali ni jambo la kawaida.

Ndivyo ilivyo katika mambo ya siasa, ukitaka kuwa kiongozi bora utakayefaa siku za usoni, jitahidi kujenga dhamira ya uvumilivu, utendaji, ukakamavu, kujituma, kutokuwa mwoga wa kutanguliza wengine kuwa ngao kwako na mengineyo. Wakati mwafaka timeline itakuonyesha ndoto yako, wala hutahangaika kujitangaza kwa umma kugombea nafasi fulani, utaona sisi tunakusukuma kwa hali na mali ufanye hivyo kwa wakati unaofaa bila kukwenda kinyume cha taratibi za kichama.

Kumbuka vijana tabia za teenage haziondoki mara, huondoka kwa mwendo pole, na usije kufikiria 30th umekuwa mtu mzima, ndio maana unaona umri huo bado katika vyama vya siasa ni vijana wanaoandaliwa katika umoja wa vijana ili kuwajenga.

Vijana tujitahidi kuiva kutosha kustahimilia msukomsuko wa kukalia Ikulu, kule si lelemama.
Watu wanakimbiakimbia na kurudi kubadilisha nguo tu, ujue kiti kile ni kukalia jivu la moto.
 
Nafurahi kuona huku nako kampeni zimeanza huku Zito huku Slaa ni afya ya Demokrasia
 
Hivi kwa nini Dr Slaa asijaze pengo lililoachwa na Bob Makani aache vijana waongoze chama.
 
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe akiwahutubia wananchi na wanachama wa chama hicho waliohudhuria katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana Karatu mjini Mkoani Arusha.
 
Hivi kwa nini Dr Slaa asijaze pengo lililoachwa na Bob Makani aache vijana waongoze chama.

Atajipeleka mwenyewe wakati wananchi bado wanamhitaji. Hitoria inatueleza Slaa si wa kujipeleka au kujipendekeza, mara zote ameombwa kuingia kwenye siasa kama ilivyotokea Kuombwa na uongozi Chadema agombee urais uchaguzi mkuu uliopita.
 
Humu ndani kuna watu wengine hata uwaambie vipi hawatakuelewa na hawawezi kuelewa mpaka mwisho wa maisha yao.
'' Mh Godbless Lema alisema unaweza kufanya zinaa kwa kujificha lakini huwezi kuugua ukimwi kwa siri,'' so watu hawa ambao vichwa vyao ni vigumu kuelewa huwezi kubishana nao.
 
Humu ndani kuna watu wengine hata uwaambie vipi hawatakuelewa na hawawezi kuelewa mpaka mwisho wa maisha yao.
'' Mh Godbless Lema alisema unaweza kufanya zinaa kwa kujificha lakini huwezi kuugua ukimwi kwa siri,'' so watu hawa ambao vichwa vyao ni vigumu kuelewa huwezi kubishana nao.

Ni ujumbe mzito sana ulioutoa na umenifikirsha kwa kiwangu cha juu. Ndio maana naipenda JF.
 

  1. Kaone maendeleo na majengo katika jimbo la Mbulu ni jitihada za Dr. Slaa na Fr. Narda ambao kwa pamoja walifanya makubwa.

Ni dayosisi au jimbo la Mbulu? Kama ni dayosisi, basi siyo Nada achilia mbali Slaa, bali ni kazi ya mtu mmoja tu ambaye ni Marehemu Askofu Nichodemus Hhando, ambaye in fact ndiyo Godfather wa Nada na Slaa, na bila yeye kusingekuwa na Nada au huyo Slaa unayemjua wewe.

Marehemu Askofu Hhando ndiyo single-handedly aliyewaweka Slaa (na Nada) under his wings tokea wakiwa wadogo na hatimaye kuwa-support kwa hali na mali.

 
Back
Top Bottom