Wasiomjua Dr. Slaa soma mada hii, kabla ya uanasiasa na baada

Mungu amjalie slaa aendelee kuwa na rekodi yake safi "kiuongozi"...tofauti na ya watumishi wenginewa mungu ktk siasa afrika ambao rekodi zao ni utata mtupu...
 
Mungu amjalie slaa aendelee kuwa na rekodi yake safi "kiuongozi"...tofauti na ya watumishi wenginewa mungu ktk siasa afrika ambao rekodi zao ni utata mtupu...

Huyo Slaa alianza kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wake wa zamani Rose Kamili wakati bado aki-enjoy nafasi ya upadri na cheo cha Ukatibu Mkuu wa TEC miaka ile ya 80, pale nyumba ya dayosisi ya Mbulu Ngarenaro. Alikuwa akifanya mapenzi na Rose Kamili ndani ya hiyo nyumba wakati akiwa padri na Katibu Mkuu wa TEC huku watu wakimuona. Kwa hiyo jamaa siyo malaika au perfect kihivyo kama wengi wanavyofikiri. He's shown himself to be as gullible and corrupt as any man when in a position of power.
 
images

Kabla ya kuwa mwanasiasa

Kwa mara ya kwanza baraza la Maaskofu Tanzania ...ofisi yake Dr Slaa kama katibu Mkuu, na taasisi..

Balaza la Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati kimoja kikiwa Kitwe - Zambia.... Slaa akiwa msimamizi mkuu ...

Makao makuu ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ....ubunifu wa Dr. Slaa alipokuwa Katibu Mkuu pale.
Unaruka kipengele hapo, chama kinakwepa kukisema, ndo maana anakosa some credibility and votes: Slaa aliondokaje kanisani?

Usitueleze habari ya Slaa aliagiza ma truck ya kanisa, tunajua alichofanya Slaa bungeni ndio maana tukampigia kura Wilbrod Slaa kuwa rais, kuagiza ma truck cha mtoto. Slaa aliondolewa uongozi kanisani baada ya kutenda dhambi zipi?
 
Ni dayosisi au jimbo la Mbulu? Kama ni dayosisi, basi siyo Nada achilia mbali Slaa, bali ni kazi ya mtu mmoja tu ambaye ni Marehemu Askofu Nichodemus Hhando, ambaye in fact ndiyo Godfather wa Nada na Slaa, na bila yeye kusingekuwa na Nada au huyo Slaa unayemjua wewe.

Marehemu Askofu Hhando ndiyo single-handedly aliyewaweka Slaa (na Nada) under his wings tokea wakiwa wadogo na hatimaye kuwa-support kwa hali na mali.

Yes, alikuwa mkubwa wao, askofu wao, lakini unakumbuka askofu ni kichwa na baba ambaye ana watu watendaji katika jimbo wanasaidia kulisimamisha jimbo? Askofu kwa kazi yake si mchumi, anakuwa na mtendaji wa jimbo (procurator) mwenye uwezo wa kubuni mipango ya maendeleo kiutaalamu na kufikisha kwenye mashirika ya misaada na kuweza kuyashawishi kwa mipango yenye kuwavutia kwa utekelezaji wenye umahiri mkubwa.

Askofu kama rais anategemea timu ya waandamizi aliowaaminisha kazi utendaji wake. Ndio maana unaona rais akiona mambo hayaendi analazimika kufanya mabadiliko kuwaondoa wanaomharibia utendaji. Uongozi wa jimbo katika kanisa katoliki hauna tofauti kubwa kiutendaji na mfumo wa utendaji serikalini.

Dr. Slaa na Fr. Narda nawafahamu vema walikuwa kiungo kizuri cha maendeleo ya jimbo la Mbulu. Uwezo aliokuwa nao Dr. Slaa jimboni Mbulu na baadaye kule TEC ndivyo vilivyo mwezesha kuwa na miradi ya maendeleo huko Karatu akiwa mwanasiasa, na alikuwa na njia za kupata kutoka kwa mashirika ya misaada ni kutokana na ukweli na utendaji, uwazi na uhakiki wa matumizi ya miradi iliyofadhiliwa. Uzoefu wa kazi zake za uchumi na maendeleo jimboni na TEC ndivyo vilivyomjengea uwezo wa kubuni, kuratibu na kuiendesha kwa ufanisi mkubwa miradi ya maendeo kimboni mweke Karatu. Ukiona majimbo fulani ya kanisa hayana ufanisi kama huo ni kutokana na watendaji katika idara za maendeleo kuwa mbumbumbu.

Mashiririka mengi ya misaada kutoka nchi za ulaya kama Miserior, Miva na mengine hawa ndio waliokuwa kiungo na wanafahamika kutokana na uwezo waliokuwa nao kuandika takwimu sahihi za mahitaji ya miradi ya maendeleo jimboni, kuweka mchanganuo mzuri ambao ulisaidia wahisani kufikisha misaada ya maendeleo katika ujenzi wa jimbo na huduma za jamii kwa kuamini uwazi na utendaji hali kadhalika usimamizi wao.

Askofu hayajui hayo, askofu anategemea utendaji wa watu hawa. Majimbo mengi yanashindwa kufanikiwa katika hilo kwa kutegemea Askofu ndiye afanye kila kitu.

Rais Kikwete alienda kufungua miradi ya umeme huko Mkoa mpya wa Njombe katika jimbo katoliki Njombe linaloongonzwa na Akofu Alfred Maluma. Lakini mtendaji mkuu katika miradi hiyo mwenye uzoefu kwa miaka mingi kuanzia askofu mstaafu Raymond Mwanyika ni Padre Peter Wella. Huyu anajua kuwaweka sawa wahisani kwa umahiri wake wa kupanga vizuri mipango ya maendeleo, kuendeza maendeleo kwa wananchi, na kuhakiki matumizi ya miradi kwa usahihi na hivyo kuwavutia wahisani kujenga zaidi miradi wanayoombwa.

Sema jingine nikufafanulie zaidi yakhe?
 
Unaruka kipengele hapo, chama kinakwepa kukisema, ndo maana anakosa some credibility and votes: Slaa aliondokaje kanisani?

Usitueleze habari ya Slaa aliagiza ma truck ya kanisa, tunajua alichofanya Slaa bungeni ndio maana tukampigia kura Wilbrod Slaa kuwa rais, kuagiza ma truck cha mtoto. Slaa aliondolewa uongozi kanisani baada ya kutenda dhambi zipi?

Pole sana, labda niendelee kukupooza zaidi.
Mada yangu historia ya Dr. Slaa katika kupanga mipango ya maendeleo kwa wananchi, na namna alivyofanikiwa katika mipango hiyo, lakini hicho unachouliza ni sawa na kukuuliza wewe kwa nini kwanza ulisema ulibadilisha taaluma yako ya uhasibu na kuingia uanasiasa kama yule Mwigulu Mchemba toka Bank Kuu na kwenda kujinadi ubunge jimboni.

Dalili za kushindwa hoja za msingi ndio hizi, unapozidiwa unatafuta pa kutokea, maana yake umebanwa mbavu. Umesoma hoja yangu ya mada hii ni ipi?
 
Huyo Slaa alianza kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wake wa zamani Rose Kamili wakati bado aki-enjoy nafasi ya upadri na cheo cha Ukatibu Mkuu wa TEC miaka ile ya 80, pale nyumba ya dayosisi ya Mbulu Ngarenaro. Alikuwa akifanya mapenzi na Rose Kamili ndani ya hiyo nyumba wakati akiwa padri na Katibu Mkuu wa TEC huku watu wakimuona. Kwa hiyo jamaa siyo malaika au perfect kihivyo kama wengi wanavyofikiri. He's shown himself to be as gullible and corrupt as any man when in a position of power.

Personal attack hutumiwa na wanaozidiwa hoja. Je, unahoja za kushindana na CV ya utendaji kiuchumi na kimaendeleo ya Dr. Slaa? Mambo unayoongelea hapa ya kijiweni, si ya great thinkers na kati hayamtoi nyoka pangoni. Ndio maana hata msaafu wa biblia Yesu aliwaambia mafarisayo waliomleta mke mzinifu mbele yake kwa mtego, "ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumrushia jiwe huyu mama." Mafasayo waliondoka mmoja mmoja kuanzia na mkuu wao baada ya dhamiri zao kujishtaki kwamba bora yule mama kuliko madhambi wayafanyayo.
 
TOKA SASA MBONA UNACHANGIA MADA.....NDO MANA NAKUAMBIA UMEJITOA AKILI, kama mada ni ya kata tuache tuijadili sisi wa kata.... WEWE FUATA MAMBO YAKO

Hamkufundishwa na namna kujenga hoja kwenye shule za kata?

Chama
Gongo la Mboto SDM
 
Personal attack hutumiwa na wanaozidiwa hoja. Je, unahoja za kushindana na CV ya utendaji kiuchumi na kimaendeleo ya Dr. Slaa? Mambo unayoongelea hapa ya kijiweni, si ya great thinkers na kati hayamtoi nyoka pangoni. Ndio maana hata msaafu wa biblia Yesu aliwaambia mafarisayo waliomleta mke mzinifu mbele yake kwa mtego, "ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumrushia jiwe huyu mama." Mafasayo waliondoka mmoja mmoja kuanzia na mkuu wao baada ya dhamiri zao kujishtaki kwamba bora yule mama kuliko madhambi wayafanyayo.

Si umeuliza "wasiomjua Dr. Slaa", au siyo? Basi kuna wanaomjua Dr. Slaa. Mambo ya Yesu na Mafarisayo muulize Dr. Slaa aliyekuwa Padri na anayejuwa msahafu mzima wa biblia maradufu zaidi ya wewe. Ukweli unabakia palepale kuhusu morals za huyo Dr. Slaa na mwenzake Padri John Nada. Na usijifanye unawafahamu vyema Slaa na Nada.

Huyo Nada mwenyewe miaka ya 90 alikumbwa na kashfa ya kufilisi mamilioni ya pesa za Dayosisi akidai katepaliwa na mganga wa kienyeji Arusha kwenye dili ya kuzalisha pesa. Padri mzima anaenda kwa mganga wa kienyeji kutafuta namna ya kuzalisha pesa ambazo amekabidhiwa na kuaminiwa na Wakubwa zake ndani ya kanisa kwa njia za ushirikina?!
 
awa wacheza viduku kama nape ndo wabsh! Huruz hata bibi yngu kijiji anajua dr.slaa nijembe
 
Yes, alikuwa mkubwa wao, askofu wao, lakini unakumbuka askofu ni kichwa na baba ambaye ana watu watendaji katika jimbo wanasaidia kulisimamisha jimbo? Askofu kwa kazi yake si mchumi, anakuwa na mtendaji wa jimbo (procurator) mwenye uwezo wa kubuni mipango ya maendeleo kiutaalamu na kufikisha kwenye mashirika ya misaada na kuweza kuyashawishi kwa mipango yenye kuwavutia kwa utekelezaji wenye umahiri mkubwa.

Askofu kama rais anategemea timu ya waandamizi aliowaaminisha kazi utendaji wake. Ndio maana unaona rais akiona mambo hayaendi analazimika kufanya mabadiliko kuwaondoa wanaomharibia utendaji. Uongozi wa jimbo katika kanisa katoliki hauna tofauti kubwa kiutendaji na mfumo wa utendaji serikalini.

Dr. Slaa na Fr. Narda nawafahamu vema walikuwa kiungo kizuri cha maendeleo ya jimbo la Mbulu. Uwezo aliokuwa nao Dr. Slaa jimboni Mbulu na baadaye kule TEC ndivyo vilivyo mwezesha kuwa na miradi ya maendeleo huko Karatu akiwa mwanasiasa, na alikuwa na njia za kupata kutoka kwa mashirika ya misaada ni kutokana na ukweli na utendaji, uwazi na uhakiki wa matumizi ya miradi iliyofadhiliwa. Uzoefu wa kazi zake za uchumi na maendeleo jimboni na TEC ndivyo vilivyomjengea uwezo wa kubuni, kuratibu na kuiendesha kwa ufanisi mkubwa miradi ya maendeo kimboni mweke Karatu. Ukiona majimbo fulani ya kanisa hayana ufanisi kama huo ni kutokana na watendaji katika idara za maendeleo kuwa mbumbumbu.

Mashiririka mengi ya misaada kutoka nchi za ulaya kama Miserior, Miva na mengine hawa ndio waliokuwa kiungo na wanafahamika kutokana na uwezo waliokuwa nao kuandika takwimu sahihi za mahitaji ya miradi ya maendeleo jimboni, kuweka mchanganuo mzuri ambao ulisaidia wahisani kufikisha misaada ya maendeleo katika ujenzi wa jimbo na huduma za jamii kwa kuamini uwazi na utendaji hali kadhalika usimamizi wao.

Askofu hayajui hayo, askofu anategemea utendaji wa watu hawa. Majimbo mengi yanashindwa kufanikiwa katika hilo kwa kutegemea Askofu ndiye afanye kila kitu.

Rais Kikwete alienda kufungua miradi ya umeme huko Mkoa mpya wa Njombe katika jimbo katoliki Njombe linaloongonzwa na Akofu Alfred Maluma. Lakini mtendaji mkuu katika miradi hiyo mwenye uzoefu kwa miaka mingi kuanzia askofu mstaafu Raymond Mwanyika ni Padre Peter Wella. Huyu anajua kuwaweka sawa wahisani kwa umahiri wake wa kupanga vizuri mipango ya maendeleo, kuendeza maendeleo kwa wananchi, na kuhakiki matumizi ya miradi kwa usahihi na hivyo kuwavutia wahisani kujenga zaidi miradi wanayoombwa.

Sema jingine nikufafanulie zaidi yakhe?
Dr. Slaa mchango wake mkuu kwa Dayosisi/Jimbo la Mbulu ulikuwa ku-exploit nafasi yake kama Padri na Katibu Mkuu wa TEC kumpiga miti Rose Kamili kwenye nyumba ya Dayosisi ya Mbulu pale Ngarenaro, Arusha. Bora mara elfu mchango wa John Nada kwa Dayosisi (au sijui "Jimbo" la Mbulu)
 
images

Dr. Slaa

Dr. Slaa si mtu mwenye maneno mengi, ni mtulivu na mkimya kiasi chake, lakini akipanda jukwaani na kuanza kulishambulia huku na kule huwezi kuamini kinachotoka ubongoni mwake. Kimya kingi kina mshindo.

Wengi hawamfahamu Dr. Slaa vilivyo, wengi wanamwona sasa baada ya kuingia bungeni na sasa katika majukwaa ya siasa, ukweli ni mtu mbunifu, mpenda maendeleo na mwenye kujitoa kwa ajili ya wengine bila kujibakiza. Ufahamu wangu wa huyu Dr. Slaa ni wa muda mrefu, lakini wengi wetu wanachukulia mambo ya juu juu tu bila kujua undani na utendaji uliotukuka wa mtu huyu.

Machache kati ya mengi kuhusu Dr Slaa kabla ya kuwa mwanasiasa, kuwa Mwanasiasa na hatimaye kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, ana mlolongo wa mambo mengi ambayo yanaonyesha ubunifu wa hali ya juu, na pia mwepesi kuwaelewa vijana na kuendana nao tofauti na watu wengine wa kizazi chake.

Pamoja na kuwa mwanachama wa CCM, baada ya kuombwa na Wanakaratu agombee ubunge kule baada ya kuchoshwa na mbunge aliyekuwepo wakati huo, CCM iliendelea na mizengwe ile ile kama iliyotokea juzi pale Dodoma kuwaengua watu wanaofaa kwa uongozi. Wanakaratu wakiamua hawataki longolongo, wakamsihi kwamba wameamua awe mbunge wao na wakamwomba achague chama kingine agombee kwani hawamtaki kabisa mbunge aliyepo. Kwa ridhaa ya wananchi akaamua kujitoa CCM na kujitosa kujiunga na Chadema ili agombee ubunge kuridhia matakwa ya wanakaratu.

Kabla ya kuwa mwanasiasa
kuna mengi ya maendeleo ambayo wengi tunayaona huku tusijua kama Dr. Slaa ndiye aliyebuni na kuyaendesha kama ifuatavyo.
  1. Dr. Slaa ndiye amekuwa wa kwanza Tanzania kuagiza big truck for load and unload makontena bandari ya Dar es Salaam wakati akiwa Katibu Mkuu TEC. Ilikuwa ni miaka ya 1980th, hakukuwa hata kampuni au watu binafsi waliothubutu kufanya hivyo. Truck hilo lilikuwa na crane za kupakia na kupakua bila taabu kokote linalokifkishwa container na kwa truck hilo. Baadaye makampuni yakabembeleza wauziwe gari ile, ndipo Barala La maaskofu likawauzia.
  2. Kwa mara ya kwanza baraza la Maaskofu Tanzania lilipoanza kuwa na matumizi ya computer ikiwepo ofisi yake Dr Slaa kama katibu Mkuu, na taasisi za upashanaji habari ambazo zilikuwa chini ya uongozi wake ikiwa ni pamoja na:

  • Gazeti la kiongozi kuanza kutumia mfumo wa computer katika idara ya set up
  • TMP (Tanganyika Mission Press) Kipalapala idara ya uchapishaji (printing) wakitumia Apple computers.
  • TMP Book deparment Tabora mjini) idara ya maduka ya vitabu na usambazaji vitabu wakitumia Apple computers
  • TAPRI idara ya tungo za mawasiliano vitabu TEC iliyokuwa na ofisi zake Seiminari kuu Kipalapala Tabora.

Idara hizo zilikuwa na matumizi ya computer na PageMaker & QuakExpress software ambazo kwa graphic designers ilikuwa kitu kigeni kisichozoeka bado Tanzania ukitilia maanani wakati huo tulikuwa na chuo kimoja tu cha ardhi kule Tabora kujifunzia Graphic Design kabla ya Ardhi Dar haijaanza kukamilika. Huo ni ubunifu wa Dr. Slaa kwa wakati huo wakati wengi Tanzania hawajafunguka kuhusu matumizi ya teknologia ya ulimwengu wa dot com.

NB.
Wakati huo chuo pekee cha mawasiliano (journalism) Tanzania kilikuwa ni Nyegezi-Mwanza pekee kilichokuwa kikiongozwa na AMECA (Balaza la Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati kimoja kikiwa Kitwe - Zambia, cha Nyegezi kiliendeshwa na TEC Dr. Slaa akiwa msimamizi mkuu kama Katibu Mkuu.​

Dr. Slaa atakumbukwa sana kwa makubwa aliyofanya kujenga na kuikuza TEC

  1. Makao makuu ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) tunayoona siku hizi ni matunda ya ubunifu wa Dr. Slaa alipokuwa Katibu Mkuu pale. Jengo la awali ni lile lililo upande wa mbele zinapotumika ofisi siku hizi ambapo yalikuwa madarasa ya shule ya sekondari ya Masisita Tanzania, ambayo baadaye ilihamishiwa Bigwa Morogoro kupisha kiwanja hicho kuwa makao ya Maaskofu Katoliki Tanzania, awali yalikuwa pale ofisi za St. Joseph, Dar es Salaam. TEC aliyoikuta DR. Slaa ilikuwa na jengo hilo la madarasa na jengo lilolokuwa la utawala wa shule. Dr. akabuni majengo ambayo tunayoana sasa, hata kama hayakukamilika yote waliofuata walikamilisha kazi alioyoianza.
  2. Kaone maendeleo na majengo katika jimbo la Mbulu ni jitihada za Dr. Slaa na Fr. Narda ambao kwa pamoja walifanya makubwa.
  3. Kaangalie jimboni kwake huduma za kijamii ambazo amezifanya, utachoka mwenyewe kiasi ambacho CCM imekimbiwa kabisa huko sababu utendaji wa Slaa huko na CCM ni sawa na kulinganisha mlima na kichuguu.
  4. Dr. Slaa kwa tunaomfahamu ni mwanamapinduzi na mpenda maendeleo, na pengine mengi alikuwa anayafanya yakaonekana mapya mno kwani alikuwa anaona mbali kuliko hawa wakubwa wake, ila sipendi kuliongelea sana hilo.

Chadema yaimarika baada ya Dr. Slaa kuwa mgombea urasi uchaguzi Mkuu uliopita.

Siyo siri Chadema hakikuwa na nguvu tunayoona sasa hivi licha ya kuwa na sera nzuri, lakini leo tunaona nguvu ya Chadema inayoogopewa mno na CCM ni kutokana na Chadema katika dakika za majeruhi kuamua kumwangukia Dr. Slaa agombee urasi ambao Samweli Sitta aliingia mitini baada ya makubaliano nao. Tangu hapo Chadema imekuwa na nguvu ya ajabu.

Je, vijana hao waliokuwemo ndani ya Chadema kabla ya Dr. Slaa kugombea Urais kwa nini hawakuipaisha juu Chadema kama sasa? Baada ya Dr. Slaa kuipaisha Chadema juu sasa tunakuja na kauli mbiu ya kubeza makubwa yaliyofanywa na hawa mnaowaita kizazi cha kabla ya uhuru. Hapana tuwe waungwana, pamoja na kila mmoja kuwa na haki za kugombea nafasi tusigeuze uhuru huo kuwabeza hawa ambao wametufikisha tulipo, na bado tunahitaji mchango wa ushauri, uongozi, hekima na busara zao. Uongozi bora ni kuchanganya mapya na ya kale kwani
viatu vya zamani vyaijua njia.

Ubunifu wa Chadema viongozi wakiwa mojawapo waliozaliwa kabla ya Uhuru Dr Slaa na Kamanda Mbowe:

  • Dr. Slaa ndiye mbunge ambaye baada ya kuingia bungeni alianza kuchangamcha kwa kuichambua serikali na kasoro zake kitu ambacho katika mabunge yaliyotangulia wabunge walikuwa ni rubber stamp ya serikali.
  • Chadema wakiwemo hao unaoona walizaliwa kabla ya uhuru wamebuni mapya katika shughuli na kampeni za uchaguzi Tanzania kuwa zenye mvuto kuanzia mkuktano wa ufunguzi wa kampeni uchaguzi Mkuu uliopita ulifanyika Kidongo Chekundu baada ya Dr. Slaa kushusha makumbora mazitomazito kuituhumu serikali, watendaji wa serikali na CCM, tuhuma ambazo CCM wanazidi kubabaika kuwanyoshea kidole wahusika kisha kuwakumbatia tena hivi karibuni kule Dodoma.
  • Mkutano wa Kidongo chekundu Dar es Salaam ndio ulioanza kutufungua macho na masikio Watanzania na kuanza kujifunza elimu ya uraia ambayo tulikuwa tunazibwa na CCM tusiijue.
  • Dr. Slaa ndiye aliyetufunza na kutufunua kwamba raia wanayo nguvu ya kuiadabisha serikali haki zao za msingi zinapokiukwa kwa kauli mbiu ya nguvu ya umma (peoples power).
  • Utumiaji wa chopper kufikia maeneo magumu kufikika kwa magari na kurahisisha kazi ya kampeni, CCM wakaiga.
  • Kuwa na magari yanayotumika kama majukwaa ya mikutano badala ya kupoteza gharama na muda kujenga majukwaa yatakayotumika kwa dakika chache.

Ilani ya Uchaguzi Chadema ndiyo inayotumika na yenye uzito sasa hivi:

  • Fukuto la Katiba mpya linaloendelea sasa nchini ni uzao wa ilani ya Chadema na ilani ya Dr Slaa kwamba kinachofuata baada ya Uchaguzi mkuu ndani ya siku 10
  • Kikwete kufanya mabadiliko ya barala la mawaziri mara kadhaa ni kutokana na shinikizo la wabunge wa Chadema bungeni.
  • Serikali kubana matumizi ya ziada ili kuokoa pesa za walipa kodi

Kuna mengi tu wachangiaji wengine watachangia, ni dhana potovu kuwa na fikra za aina hiyo na kuwabeza wabunifu wa mengi, waliongoza nchi hii, wenye kuturithisha mengi kwa uzoefu na busara zao na walioongoza nchi hii hadi kuwa na utulivu wa aina yake. Leo vijana mnaowasema yanayojilia ni amani kusambaratika na mauaji ambayo ilikuwa hadithi za kusimuliwa kutoka nchi nyingine, leo serikali ya CCM inayoongozwa na Rais kijana kuliko Rais mwingine aliyemtangulia imetwishwa na aibu kubwa ya kitaifa na kimataifa ya mauaji ya raia wasio na hatia.

Kuna nchi ambazo ni kielelezo cha vijana ambao mimi ningewaita watoto kukabidhiwa madaraka ya kuongozia nchi na kusababisha maafa makubwa kwa nchi husika kama Liberia, Ujerumani chini ya Hittler, na kinachoendela huko Zaire ya sintofahamu.

Vijana achaneni na uroho wa madaraka, vema kubaki watumishi na watendaji wazuri serikalini na vyamani kujifunza mbinu za uongozi na kupata uzoefu katika kuongoza nchi.

Kuongoza nchi hakuna shule wala kitabu cha kusomea au chuo. Hekima na busara ya mtu ndio kielelezo cha fanaka katika kuongoza nchi.

  • Vijana wana papara,
  • wanataka njia ya mkato,
  • pagumu wanataka kulazimisha bila busara wala kutumia akili
  • Vijana wanalipuka kama moto wa gas
  • mambo yakigeuka magumu ni mabavu hutumika.
CV YAKE IMEKAA VIZURI SANA, HATA MIMI NATAMANI MKUMUONA AKIWA RAISI WA NCHI HII . NATAKA NIONE Atapambanaje na hali ya aukosefu wa ajira,ulinzi wa pesa za umma,na uhuru wa mahama kuu kuwa huru. Halafu, je atakubali kuweka kifungu cha raisi ashitakiwe mara akifanya vibaya madarakani? Mimi pia napenda sana kuona bunge likiwa huru na kumsuta raisi aliye madarakani. Je ataweza kukubali kujiweka chini ya bunge na mahama kuu?

Hakuna kitu kinachonikela mimi kama vile kuogopa kwa viongozi wetu kutembelea Israel kuomba misaada kwa ajiri ya wananchi, eti kwa kufanya hivyo tutawaudhi waarabu. Hii kasumba ya kujifanya kuwa taifa la kiarabu likonewa basi tumeonewa sisi na likifanikiw akiuchumi basi hiyo ni faida yao. Huu kweli ni utumwa mbaya sana . Sasa je Dr slaa tatatutoa na kasumba hiyo ?

Tanznaia mara nyingi sana imekuwa ina ilaani Israel kwa kuwapiga wapalestina lakini hamna hata siku moja ikailaani Hamas au Hisbollah kwa kurusha maroketi ndani ya Israel, hii kasumba inatuabisha sana ktk nyanja za kimataifa. Nadhani Dr slaa, hata kubali kumaliza muda wake bila kuweka ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Israel. Kabwe hawezi kufanya haya ila Dr slaa anweza bila woga.

Halafu kasumba nyingine ya serikali ya IRan kujiingiza sana katika jamii yetu na kutaka kutogombanisha ki didni wakati serikali yetu haifanyi lolote lile kwa kukemea Iran. Je Dr Slaa atweza kuikemea Iran na kuipiga stop kujiingiza katika siasa za tanzania?

Nikiiangalia shepu yake , kweli jamaa huyu anaonekana anaweza sana kututoa na kasumba ya kushikama na na nchi za kiarabu dhidi ya kuwachukia merekani Ulaya magharibi na Israel.
 
Si umeuliza "wasiomjua Dr. Slaa", au siyo? Basi kuna wanaomjua Dr. Slaa. Mambo ya Yesu na Mafarisayo muulize Dr. Slaa aliyekuwa Padri na anayejuwa msahafu mzima wa biblia maradufu zaidi ya wewe. Ukweli unabakia palepale kuhusu morals za huyo Dr. Slaa na mwenzake Padri John Nada. Na usijifanye unawafahamu vyema Slaa na Nada.

Huyo Nada mwenyewe miaka ya 90 alikumbwa na kashfa ya kufilisi mamilioni ya pesa za Dayosisi akidai katepaliwa na mganga wa kienyeji Arusha kwenye dili ya kuzalisha pesa. Padri mzima anaenda kwa mganga wa kienyeji kutafuta namna ya kuzalisha pesa ambazo amekabidhiwa na kuaminiwa na Wakubwa zake ndani ya kanisa kwa njia za ushirikina?!
Hayo ya mganga wa kienyeji sisi hatuyajui, sisi tunaongelea mambo ya siasa za Chadema na utumishi wao, ya babu wa loliondo na wengineo tuwaachie wanaoamini, nami hayana nafasi wala kuuzumbua ubongo wangu kwa ambo kama hayo. Kama unayapenda na kuyaendekeza we fanya, ila mada yangu yahusu niliyoongelea,
 
Unaanza kufyata kiaina. Aliyewaleta na kusifia mafanikio ya Slaa na Nada Dayosisi/Jimbo la Mbulu ni nani kama siyo wewe?
 
Watanzania lazima tuishukuru sana Marekani na rafiki zake kwa kuutokomeza ukomunisti hapa duniani. Sasa hivi kila mtanzania ana nafasi sawa ya kutawala na kuikosoa nchi bila ya woga, lakini wakati wa ujomunisti hatukuweza kabisaa kupata wala kama DR Slaa na kutusaidia kukemea uozo wa nchi. Kweli marekani imetukomboa sana , haswaa katika nynja za uhuru wa vyombo vya habari na vyama vya upinzani.

Raisi wa Tanznaia, siku hizi haimbiwi kwaya wala kusifiwa magazetini. Kila kukicha utakuta raisi anakosolewa hadharani bila woga, kitu ambacho enzi za chama chashika hatamu hatukuweza kabisaa kukifanya. Tulikuwa kama vile wafungwa ambao wnalzimishwa kutii amri za Gehhena.

Baada ya kufa kwa ujamaa na kujitegemea leo hii shule nyingi za secondari zimejengwa, vyuo vya ualimu navyo vimejengwa sana, vyuo vikuu vimejengwa sana na vijana wengi wahitimu wa kidato cha sita wameweza kwenda vyuo vikuu kwa kupitia bodi ya mikopo. hii yote ni kwa sababu ya marekani kuwaliza wakomunisti na kufuta ujamaa na kujitegemea. Leo hii nitasikitika sana nikiona mtanzania eti anichukia marekani .

Tukija fanikiwa kuandika katiba imara ambayo ni ya matakwa ya wananchi, kuweka mahakam kuu kuwa huru na Bunge kutomuogopa raisi, basi tutajenga nchi vizuri sana na watoto wetu watanufaika na ujasiri wetu huu. Mungu ibariki Tanznaia.
 
Ukweli na uchambuzi wako umeweka wazi ambayo watu wanaitazama Marekani kwa mtazamo tofauti sababu ya ubabe wake kimataifa bila kuangalia kunufaika na jitihada zao za kuuweka ulimwengu huru.

Pamoja na kwamba mfumo wa mawasiliano wa kizazi cha dot.com wigo wa demokrasia umepanuka zaidi kwa kurahisisha mawasiliano, yote yanatokana na mfumo wa net work ambayo imeasisiwa na hawa wamarekani, na makampuni makubwa ya server ya net work ni huko huko.

Kuibeza Marekani ni sawa na kumtukana aliyekupikia chakula unachokula, unamtumtukana huku mkononi umeshika mkate wake ukijiandaa kutia mdomoni wakati mwingine unaumeza.
 
Na wewe pia sentensi yako ya kwanza "inatia kichefuchefu" kwani wee mwenyewe una "bias" kiasi kwamba bado unang'ang'ania kuwa Slaa bado ni "padri" kitu ambacho si kweli. Check yo self before you wreck yo self, fool!

Ex padri slaa...

Happy now
 
Back
Top Bottom