Wasichana wa Mbagala na Gongo la Mboto ndiyo chaguo Sahihi kwa mnaotaka Kuoa

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,262
Nakumbuka mwaka flani nilikuwa maeneo ya posta nikawa nimekutana na dada mmoja mrembo ambaye tulisoma naye kidato cha nne miaka mingi iliyopita.alikuwa bado mkakamavu mwenye nguvu,afya na uzuri wake haukuwa umepungukiwa na kitu.

baada ya kukutana maeneo ya Hotel flan pale posta nikawa sasa nimeongozana naye nikimsindikiza kituoni huku tukikumbushana mambo mawili matatu nami nikifika mbele ya posta karibu na round about kuna duka la nguo na viatu. basi tukiwa tunaongea hivi niligeuka upande wa kushoto mara moja kumwangalia jamaa mmoja aliyekuwa amejikwaa na niliporudisha macho kwa mwenzangu huku kulia sikumwona.

kilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua.jambohili lilinishtua sana na nikaanza kuwaza je nlikuwa naongea na jini?malaika?mzuka au imaginations zangu?mwili ulinisisimka sana.sikuelewa ni nini kimetokea.nikiwa katika hali hiyo ya kutahayarika huku naendelea na safari kwenye lindi la mawazo...nilisikia jina langu likiitwa na mtu aliyekuwa kwenye dala dala... shabash! alikuwa ni yule dada amekaa kwenye siti ya dirishani ananiita ili aniage ndo akanidondoshea biz card yake.

bado nikiwa mwenye mawenge kesho yake ilibidi nitie timu ofisini kwake pale uhamiaji.nikahakikishe ni yeye kweli au mzuka.nilimkuta akiwa amejaa tele amependeza anazunguka kwenye kiti na mwenye tabasamu na bashasha. baada ya maongezi nikamwambia anidokeze tu anatumia mbinu gani kupotea na kuibukia sehemu nyingine. ndo akanambia.

toka amehamia kwenye nyumba yake mbagala amejifunza ukakamavu.akanambia unapoongea na mkazi wa mbagala kama upo barabarani inatakiwa muagane mapema kabisa sababu huwa mara nyingi mnaongea huku yeye akiwa anatembeza macho kuangalia kama kuna daladala la mbagala linapita.na mara anapoliona huchangamkia fursa.hivyo hana muda wa kuagana huchomoka kama risasi na kupanda kutumia sehemu yoyote ya gari yenye uwazi.yaani kama dirishani,mlangoni,kwenye bonet n.k anasema wameshazoea hivyo kiasi kwamba usishangae hata mtu kwenye taxi aliyoiita yeye mwenyewe akaanza kusukumana na mwili wake mlangoni kuingia.

nlijifunza kitu. tabia hiyo imeendelea na kuadvance.siku moja nlikuwa natumia usafiri wa train kuelekea ubungo.wakati naelekea ndani baada ya kukata ticket mhusika mmoja akawa anamwonesha mwenzie kuwa abiria huyu ni wa ubungo,yule wa gongo la mboto...wale wawili ni ubungo n.k nlishtuka sana kuwa huyu jamaa ana kumbukumbu gani kiasi kuwa mtu ukipanda train leo kesho anakuja kukumbuka kuwa wewe unapanda la kwenda sehemu gani.nikashangaa kwa mimi ndo ilikuwa mara ya kwanza lakini aliweza nitabiria kuwa ntapanda train ya wapi.haraka nikahisi huyu jamaa atakuwa na kipawa cha ajabu.nikamsogelea na kumsabahi,kisha nikamwuliza anajuaje waendako abiria.alicheka kiasi akinionesha meno yake yasiyo na mshikamano mdomoni mwake.kisha akasema "abiria wa gongo la mboto wanaonekana tu wanapotembea macho yao yanakuwa juu juu, wana tayar tayari kwa mbio na hata uvaaji.akanambia wadada wa gongo la mboto huvaa suruali au pensi kwa ndani sababu anytime anaweza chomoka kama usain bolt kukimbilia train.

na huko anaweza panda katika mazingira magumu ili kuwahi siti.hivyo huwa wakifika stesheni wanavua michuchumio na kuvaa viatu ambavyo vitawapa nafasi ya kukimbia kwa urahisi.anasema wanaume wakifika pale huanza kukaza mikanda ili wakati wa purukushani mlango suruali isije ikabaki nje na yeye kuingia ndani.ishawahi kutokea jamaa alijikuta amefanikiwa kupanda train na kupata siti ila suruali na boksa vimebaki nje.hivyo alilazimika tena kushuka kwenda kuvichukua. acha huyo kuna ambaye wakati anapanda kumbe dada mmoja alifanikiwa kuzishikilia korodani(mapumb*) zake ili zimsaidie kupanda.jamaa alitoa ukelele mkubwa sana akiamini zimenyofolewa.kumbe bahati nzuri ni kama elastic zilivutika na ule ukelele ulimshtua dada kuwa amemshika jamaa mahali pabaya. hivyo wanakaza mikanda kiunoni na kukunja shati mikono huku wakilegeza tai kama walivaa, kujiandaa kwa mpambano wa kuwania siti kule ndani.anasema mara nyingi wanawake wameonekana kuibuka na ushindi mkubwa sana kwa kuonesha wana nguvu na mbinu kali za kivita.

nikawaza... ntampata wapi mwanamke anayejua kupambana na hali yake?kupambana na mazingira yaliyomzunguka kama wa mbagala au gongo la mboto? hawa ndo wanawake wa kiafrika wanaofaa kuoelewa. rafiki yangu ukitaka kuoa oa mwanamke wa mbagala au gongo la mboto.achana na wa masaki,oyesterbay,mikocheni,mbezi n.k hawa hawajui shida.hata kuzaa hawawezi push... watakupa gharama nying sana.
 
Nakumbuka mwaka flani nilikuwa maeneo ya posta nikawa nimekutana na dada mmoja mrembo ambaye tulisoma naye kidato cha nne miaka mingi iliyopita.alikuwa bado mkakamavu mwenye nguvu,afya na uzuri wake haukuwa umepungukiwa na kitu.

baada ya kukutana maeneo ya Hotel flan pale posta nikawa sasa nimeongozana naye nikimsindikiza kituoni huku tukikumbushana mambo mawili matatu nami nikifika mbele ya posta karibu na round about kuna duka la nguo na viatu. basi tukiwa tunaongea hivi niligeuka upande wa kushoto mara moja kumwangalia jamaa mmoja aliyekuwa amejikwaa na niliporudisha macho kwa mwenzangu huku kulia sikumwona.

kilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua.jambohili lilinishtua sana na nikaanza kuwaza je nlikuwa naongea na jini?malaika?mzuka au imaginations zangu?mwili ulinisisimka sana.sikuelewa ni nini kimetokea.nikiwa katika hali hiyo ya kutahayarika huku naendelea na safari kwenye lindi la mawazo...nilisikia jina langu likiitwa na mtu aliyekuwa kwenye dala dala... shabash! alikuwa ni yule dada amekaa kwenye siti ya dirishani ananiita ili aniage ndo akanidondoshea biz card yake.

bado nikiwa mwenye mawenge kesho yake ilibidi nitie timu ofisini kwake pale uhamiaji.nikahakikishe ni yeye kweli au mzuka.nilimkuta akiwa amejaa tele amependeza anazunguka kwenye kiti na mwenye tabasamu na bashasha. baada ya maongezi nikamwambia anidokeze tu anatumia mbinu gani kupotea na kuibukia sehemu nyingine. ndo akanambia.

toka amehamia kwenye nyumba yake mbagala amejifunza ukakamavu.akanambia unapoongea na mkazi wa mbagala kama upo barabarani inatakiwa muagane mapema kabisa sababu huwa mara nyingi mnaongea huku yeye akiwa anatembeza macho kuangalia kama kuna daladala la mbagala linapita.na mara anapoliona huchangamkia fursa.hivyo hana muda wa kuagana huchomoka kama risasi na kupanda kutumia sehemu yoyote ya gari yenye uwazi.yaani kama dirishani,mlangoni,kwenye bonet n.k anasema wameshazoea hivyo kiasi kwamba usishangae hata mtu kwenye taxi aliyoiita yeye mwenyewe akaanza kusukumana na mwili wake mlangoni kuingia.

nlijifunza kitu. tabia hiyo imeendelea na kuadvance.siku moja nlikuwa natumia usafiri wa train kuelekea ubungo.wakati naelekea ndani baada ya kukata ticket mhusika mmoja akawa anamwonesha mwenzie kuwa abiria huyu ni wa ubungo,yule wa gongo la mboto...wale wawili ni ubungo n.k nlishtuka sana kuwa huyu jamaa ana kumbukumbu gani kiasi kuwa mtu ukipanda train leo kesho anakuja kukumbuka kuwa wewe unapanda la kwenda sehemu gani.nikashangaa kwa mimi ndo ilikuwa mara ya kwanza lakini aliweza nitabiria kuwa ntapanda train ya wapi.haraka nikahisi huyu jamaa atakuwa na kipawa cha ajabu.nikamsogelea na kumsabahi,kisha nikamwuliza anajuaje waendako abiria.alicheka kiasi akinionesha meno yake yasiyo na mshikamano mdomoni mwake.kisha akasema "abiria wa gongo la mboto wanaonekana tu wanapotembea macho yao yanakuwa juu juu, wana tayar tayari kwa mbio na hata uvaaji.akanambia wadada wa gongo la mboto huvaa suruali au pensi kwa ndani sababu anytime anaweza chomoka kama usain bolt kukimbilia train.

na huko anaweza panda katika mazingira magumu ili kuwahi siti.hivyo huwa wakifika stesheni wanavua michuchumia na kuvaa viatu ambavyo vitawapa nafasi ya kukimbia kwa urahisi.anasema wanaume wakifika pale huanza kukaza mikanda na kukunja shati mikono huku wakilegeza tai kama walivaa kujiandaa kwa mpambano wa kuwania siti kule ndani.anasema mara nyingi wanawake wameonekana kuibuka na ushindi mkubwa sana kwa kuonesha wana nguvu na mbinu kali za kivita.

nikawaza... ntampata wapi mwanamke anayejua kupambana na hali yake?kupambana na mazingira yaliyomzunguka kama wa mbagala au gongo la mboto? hawa ndo wanawake wa kiafrika wanaofaa kuoelewa. rafiki yangu ukitaka kuoa oa mwanamke wa mbagala au gongo la mboto.achana na wa masaki,oyesterbay,mikocheni,mbezi n.k hawa hawajui shida.hata kuzaa hawawezi push... watakupa gharama nying sana.
chief uwe unaandika fupi fupi basi, ndefu sana hii ila naitamani kuisoma!
 
Hahaha! Mzee mkavu 'gudume' nimependa tafakari yako Hahaha!

Ila kiukweli kwa zama hizi na ugumu huu wa maisha Wanaume tunaitaji Mwanamke mkakamavu na mwenye kukabili kila hali ya mazingira, kuipambania haki yake na ya jamii inayomzunguka.
 
Back
Top Bottom