Warsha ya kujenga uelewa katika Sekta ya Kidigitali kuhusu Sheria, Sera na Kanuni zinazosimamia Anga ya Kidigitali Tanzania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Leo Jumanne Mei 30, 2023, Shirikisho la Wadau Wanaotetea Haki za Kidigitali Tanzania (Digital Rights Coalition Tanzania) limeandaa Warsha ya kujenga uelewa kwa Wadau katika Sekta ya Kidijitali kuhusu Sheria, Sera na Kanuni zinazosimamia Anga ya Kidijitali Nchini Tanzania pamoja na kuwezesha majadiliano ya changamoto na fursa katika tasnia husika.

Inafanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Protea (Protea by Marriot Courtyard Hotel) Jijini Dar es Salaam.

Matukio ya kinachoendelea yatakujia muda mfupi ujao;

3.JPG

Washiriki katika Warsha ya kujenga uelewa kwa Wadau kuhusu Sheria, Sera na Kanuni zinazosimamia Masuala ya Kidigitali Nchini Tanzania pamoja na kuwezesha majadiliano ya changamoto na fursa zilizopo inayofanyika katika Hoteli ya Protea Jijini Dar es Salaam, Mei 30, 2023. Warsha hiyo imeandaliwa na Shirikisho la Wadau Wanaotetea Haki za Kidigitali Tanzania (Digital Rights Coalition).

Raymond Kanegene (Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu - LHRC):
Maisha yetu ya kawaida yanasimamiwa na Sheria. Vipi kuhusu Maisha tunayohamishia Mtandaoni? Ni namna gani tunaweza kufurahia Maisha yetu katika Ulimwengu wa Kidigitali?

Raymond Kanegene (Kituo Cha Sheria na Haki za Kibinadamu-LHRC)
Digital space ni msingi wa Uhuru wa Kujieleza Duniani. Hivyo ni vyema Sheria husiana zikaakisi katika kutengeneza mazingira rafiki ya ulimwengu wa Kidigitali.

Raymond Kanegene (Kituo cha Sheria na Haki za Kibinadamu-LHRC):
Digital space ni msingi wa Uhuru wa Kujieleza Duniani. Ni vyema Sheria husiana zikaakisi katika kutengeneza mazingira rafiki ya Ulimwengu wa Kidigitali.
Ray.jpg

Raymond Kanegene (Kituo cha Sheria na Haki za Kibinadamu-LHRC):

Raymond Kanegene (Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu - LHRC):
Teknolojia ya Kidigitali ni msingi wa Uhuru wa Kujieleza. Haki hii ipo kwenye Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Raymond Kanegene( Kituo Cha Sheria na Haki za Kibinadamu - LHRC):
Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni zilianzishwa (2018) na kurekebishwa 2020 na 2022 mtawalia, lengo likiwa kuregulate aina ya maudhui yatakayo kuwa mitandaoni

Kanuni hizi zikatambulisha prohibited contents, maudhui ambayo hayatakiwi kuwepo mtandaoni. Kanuni hizi zimekuwa zikiathiri ustawi wa Digital Space Tanzania.

Raymond Kanegene (Kituo cha Sheria na Haki za Kibinadamu - LHRC):
Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni zilianzishwa 2018 na kurekebishwa 2020 na 2022, lengo likiwa ku-regulate aina ya maudhui yatakayokuwa mitandaoni.

Kanuni hizi zikatambulisha Prohibited Contents (Maudhui ambayo hayatakiwi kuwepo mtandaoni). Kanuni hizi zimekuwa zikiathiri ustawi wa Digital Space Tanzania.

Raymond Kanegene (Kituo Cha Sheria na Haki za Kibinadamu- LHRC):
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (2023) inawataka Mkusanya, Mchakata na Mdhibiti wa Taarifa kusajiliwa

Sheria hii inawataka wakusanya taarifa binafsi wote kusajiliwa kasoro Taasisi za Serikali, ambazo zimesajiliwa automatically.

Raymond Kanegene (Kituo Cha Sheria na Haki za Kibinadamu - LHRC):
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (2023) inazuia mtu yoyote kukusanya taarifa binafsi bila kusajiliwa.

Hivyo kama mpenzi wako ataingilia faragha yako kwa kukagua simu yako na ukapata athari unaweza kwenda kwenye tume ya malalamiko (itakayoanzishwa hivi karibuni) kwa ajili ya hatua za kisheria.

Raymond Kanegene (Kituo Cha Sheria na Haki za Kibinadamu - LHRC):
Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa (2016) ilitungwa kwa ajili ya kuleta Uwazi, Uwajibikaji na Ushirikishwaji wa Wananchi.

Kama Raia unaweza kwenda kwenye ofisi fulani ya Serikali au kutumia mtandao kuuliza kuhusu taarifa fulani.

Raymond Kanegene Kituo Cha Sheria na Haki za Kibinadamu - LHRC)
Kama Wadau wa Shirikisho la Wadau Wanaotetea Haki za Kidigitali, ni jukumu letu kuwezesha matukio yanayotokea ana kwa ana, mfano, Vikao na Warsha mbalimbali kuweza kufanyika kupitia mtandaoni.

Hii ni njia mojawapo ya kuziba pengo lililopo kati ya Ulimwengu halisi na Ulimwengu wa Mtandao.

Ziada.JPG

Ziada Seukindo, Meneja Programu- JamiiForums

Ziada Seukindo, Meneja Programu - JamiiForums:
Tukumbuke kuwa watu wanajipatia kipato kutokana fursa zinazopatikana mtandaoni, ambao wanaweza kuathiriwa ikiwa Sheria au 'Digital Space' haipo vizuri.

Hivyo Mkutano huu ni wa Wadau kujadili changamoto na fursa katika Ulimwengu wa Kidigitali, pia kupendekeza njia za utatuzi wa changamoto hizo ambapo baadae tutaziwasilisha kwa watu ambao tunaamini wanaweza kuzifanyia kazi.

Ziada Seukindo (Meneja Programu - JamiiForums):
Tunaangazia zaidi Sheria, hasa kwa kuwa tunaamini kwamba ndizo zitakazotoa haki mbalimbali lakini pia zitaweka mazingira rafiki ya watu kutumia vizuri fursa ambazo zipo mtandaoni.

Tunafanya uchechemuzi wa #HakiZaKidigitali kwa sababu zama hizi ambazo ambapo Watu wengi tunatumia vifaa vya kidigitali na mtandao na majukwaa ya kidigitali, utu wetu upo hatarini.

Leo hii picha zako, taarifa zako binafsi ziko mtandaoni ambapo Mtu anaweza kuzitumia kwa namna yoyote ambayo inaweza kukuathiri au kuathiri Watu wa karibu yako.
Seukindo.JPG

Ziada Seukindo (Meneja Programu -JamiiForums):
Tukumbuke kuwa Watu wanajipatia kipato kutokana fursa zinazopatikana mtandaoni, ambapo wanaweza kuathiriwa ikiwa Sheria au 'Digital Space' haipo vizuri.

Hivyo Mkutano huu ni wa Wadau kujadili changamoto na fursa katika Ulimwengu wa Kidigitali, pia kupendekeza njia za utatuzi wa changamoto hizo ambapo baadaye tutaziwasilisha kwa Watu ambao tunaamini wanaweza kuzifanyia kazi.
Ziada tena.JPG

Ziada Seukindo, Meneja Programu - JamiiForums:
Kuna changamoto mbalimbali katika Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ikiwemo Tume inayosimamia Ulinzi wa Taarifa Binafsi (The Data Protection Commission) imepewa nguvu kubwa sana ambazo zinaweza kuathiri utendaji kazi wa Taasisi au watu mbalimbali.

Tume imepewa uwezo wa kuingia kwenye jengo lolote, na kuchukua kifaa chochote ambacho wao wanahisi kina taarifa wanazozihitaji bila kuwa na kibali chochote na pia imepewa nguvu za kutozingatia Sheria zozote wakati wanatimiza majukumu yao.

1.JPG

2.JPG


Carol Ndosi (The Launch Pad):
Kuna ambayo yanafanyika tayari kuhakikisha tuna ufahamu wa Sheria.

TCRA wamekuwa na Kampeni ya kufichua utapeli Mtandaoni. JamiiForums wamekuwa wakifanya kazi nzuri sana kwa miaka na miaka kuhusu uchechemuzi wa Haki za Kidigitali na Usalama Mtandaoni.

Carol Ndosi (The Launch Pad):
Tukiangalia upande wa Sheria zinazokulinda, zinazolinda Taarifa zako na makosa mengine yanayoweza kufanyika dhidi yako Mtandaoni, ni kitu ambacho kwa Watanzania bado bado bado!

Ni kama ambavyo hakuna ufahamu mkubwa wa Haki zetu za Binadamu na jinsi ambavyo zinaathirika na mambo mbalimbali ambayo yanatokea katika Jamii yetu.

Carol Ndosi (The Launch Pad):
Sisi kutokana na shughuli zetu za uchechemuzi wa Haki za Kidigitali tumegundua ufahamu wa Watanzania kuhusu Haki hizi ni tatizo.

Sio wengi wanaofahamu Haki zao, na hii inaingiliana na kufahamu Wajibu wao kama Raia wa Kidigitali. Kuna makosa mengi sana ambayo yanafanyika Mtandaono kutokana na kutofahamu Haki na Wajibu.

Carol Ndosi (The Launch Pad):
Kama Kampuni za Simu zinaweza kututumia sisi Watumiaji Taarifa za Huduma zao mbalimbali, ina maana wanaweza wakatoa mchango katika Elimu ya Umma.

Je, inawezekana Mtumiaji wakati amenunua Sim Card yake akiwasha tu simu apate andiko fupi linalomjuza kuhusu Sheria, jinsi ya kujilinda Mtandaoni na pale ambapo anapitia unyanyasaji, wizi anaweza kwenda kuripoti wapi?

664.JPG

663.JPG

662.JPG
Wadau mbalimbali wajadili na kutoa Maoni kuhusu Sheria, Sera na Kanuni zinazosimamia Masuala ya Kidigitali Tanzania katika Warsha ya Shirikisho la Wadau Wanaotetea Haki za Kidigitali Tanzania (Digital Rights Coalition).

Baadhi ya Taasisi zilizoshiriki ni The Launch Pad Tanzania, TGNP, TAMWA, Twaweza, Nukta Africa, HakiElimu, Chuo cha Aga Khan, WiLDAF, THRDC, UTPC, Pollicy, Tai Tanzania, Her Initiative na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
661.JPG

66.JPG
 
Hapo ni upigaji tu hakuna lolote, huo uelewa wa kidijitali waupeleke kidijitali kupitia Sociial media na kila mtu atapata huo uelewa, hapo ukumbini hata watu 100 hawaji..
 
Kwamba Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (2023) inazuia mtu yoyote kukusanya taarifa binafsi bila kusajiliwa. Nani anawasajili? Anayesajili nani kamsajili?
 
Hapo ni upigaji tu hakuna lolote, huo uelewa wa kidijitali waupeleke kidijitali kupitia Sociial media na kila mtu atapata huo uelewa, hapo ukumbini hata watu 100 hawaji..
We unashauri nini badala ya kurusha lawama tu, ukute hata hujasoma ndani ukajua nini kinaendelea?
 
Back
Top Bottom