Warioba: Tutarajie Katiba ya watawala

Kageuka

JF-Expert Member
Jun 22, 2012
241
59
Jaji Warioba amenukuliwa leo na gazeti la Raia Tanzania akisema kitakachopendekezwa na Bunge la Katiba Dodoma ni Katiba ya watawala na si Katiba ya wananchi, anatoa mifano juu ya kinachoendelea yaani Sitta anakusanya maoni ya vikundi vya kiutawala kama ALAT.

Je, yuko sahihi? Wananchi wataambulie chochote cha maana katika katiba hiyo?
 
It is absolutely true

Katiba inayoandaliwa Dodoma hivi sasa ni ya watawala na chama chao cha magamba, kwa kuwa katiba yenye maoni ya wananchi, yaliyokusanywa na Tume ya Warioba, ilishatiwa kapuni mara tu ukawa waliposusia bunge la katiba, mwezi wa 4!
 
Cha msingi tuhamasishane kuikataa tu endapo itapenya na kufikia hatua ya kupigiwa kura!
 
Hii inchi tunaelekea kubaya sana yaani Sita ni mjinga sana anapata wapi nguvu ya kuunda tume nyingine?
 
Inakera sana kumuona mtu mzima anajitoa ufahamu na kutetea na hata kuusimamia upuuzi ili tu kukidhi matakwa yao, INAKERA SANA.
Kinachoendelea Dodoma kwa sasa ni upuuzi usio mithilika, kwa kitendo cha wale wanaojiita waheshimiwa kushupaa na kufanya wanayoendelea kuyafanya kana kwamba hawasikii kelele zinazopigwa huku nje, Hii ni ishara ya mtu mzima kujitoa ufahamu.

Wanatambua wazi kuwa wanachoendelea kukijadili sio maoni ya waTanzania, lakini wanaendelea tena kwa nguvu kubwa; na hiki cha kuendelea kukusanya maoni as if hayo makundi hayakuwepo wakati Tume iliyoundwa kisheria kufanya hivyo ilipokuwa inazunguka nchi nzima kwa kazi hiyo.Hicho wanachokifanya ni kujaribu kuuhadaa umma kuwa wananchi "wengi" wanataka hicho walichopanga kukipitisha...NI UPUUZI MKUBWA HUU.

Mie nangojea kwa hamu kubwa siku watakayoanza kuwasilisha huo upuuzi wao.
 
CCM wanajidanganya sana, wanafikiri watatawala nchi hii milele thats why wanatunga katiba ya kuwa-protect as watawala wa milele.
 
Huyo Sitta na wabunge wake wa CCM, waliobaki kwenye bunge la katiba, wanataka kuipeleka nchi hii kubaya.

Yaani hadi sasa, eti wanaendelea kukusanya maoni ya wananchi!

Ina maana zile bilioni 60, pesa za walipa kodi wa nchi hii, zilizotumika na Tume ya Warioba kukusanya maoni ya wananchi, nchi nzima, ni kama vile, pesa hizo zimetumbukia 'msalani'!!
 
Sheria inawaruhusu na wananchi anaridhika ndiyo maana makundi mbalimbali yanaenda kupeleka maoni kama:
- Wasanii
- Baraza la habari Tanzania
- Wakulima na wafugaji
- Hata yeye Warioba amepeleka maoni mengine hivi karibuni
 
Mara ya mwisho uliugua lini kichaa cha mbwa? sheria ipi unayoisema? hayo maoni yanakusanywa kwa mujibu wa sheria ya mwaka gani ? ilitungwa na nani?
 
Nimesikia kuna maoni ya watu yalitiwa kapuni na tume ya Warioba. Baadhi ndo hao wanaokwenda bungeni sasa. Sina hakika kama kanuni au sheria zinaruhusu ama la.
 
Nakumbuka kabla tume haijatoa rasimu ya kwanza, Chadema walipaza sauti zao wakiituhumu tume kuwa inaandaa rasimu yenye maslahi ya CCM, ikafika kipindi hadi wakamkashifu Jaji Warioba. Baada ya rasimu ya kwanza na ya pili kutoka wakala matapishi yao kwa kuipongeza tume. Sasa hivi wajumbe wa bunge maalumu la katiba wapo Dodoma wakiendelea na mapitio ya rasimu iliyowasilishwa na tume. Kama kawaida Chadema akiongoza kundi la Ukawa, pamoja na watu wengine wamerudia staili ileile kwamba kinachotengenezwa Dodoma ni katiba ya CCM. Nashangaa kuona hata Jaji Warioba yupo mstari wa mbele kusema ni katiba ya CCM. Tuwe wawazi na wakweli, mrejesho wa kilivchoamriwa kwenye bunge haujatolewa, tunapata wapi ujasiri wa kusema ni katiba ya CCM? Nashindwa kuelewa hata utashi wa Jaji Warioba umepotelea wapi kiasi kwamba ameamua sasa kuwa mwanasiasa. Sioni sababu ya kufanya mahitimisho wakati hata ripoti hatujapewa. Isitoshe hata kama hao CCM wataweka yao, wahusika wa mwisho na wenye maamuzi ni sisi wananchi wenyewe, kama tutaona haitufai tutaikataa, CCM si Mungu kwamba wao wanachokisema lazima sisi tukifuate.
 
kuna watu humu sijui hawana akili au ni monkeys kama wassira,hivi kweli bado kuna watu kabisa wanawatetea ccm,hivi watu kama hawa si wa kuua tu
 
kuna watu humu sijui hawana akili au ni monkeys kama wassira,hivi kweli bado kuna watu kabisa wanawatetea ccm,hivi watu kama hawa si wa kuua tu

Wewe dogo changia hoja acha mitusi ya rejareja. Waungwana wanajadili na kupinga au kukubali hoja. Arfi aliwahi kusema kati ya sheria za hovyo kuwahi kutungwa duniani ni sheria ya mabadiliko ya katiba. Je, ni sahihi kimantiki sheria hiyo kuipa idhini tume kuhodhi maoni ya wananchi na kuchagua yale yanayowapendeza na kuyaweka katika rasimu, kama wao wanayo ruksa hiyo kimantiki kwa nini Bunge ambalo ni matokeo ya uwakilishi lisiwe na ruksa hiyo? Arfi yuko sahihi kwamba akina Lissu na wenzake walitunga sheria mbovu kuwahi kutokea duniani?
 
Nakumbuka kabla tume haijatoa rasimu ya kwanza, Chadema walipaza sauti zao wakiituhumu tume kuwa inaandaa rasimu yenye maslahi ya CCM, ikafika kipindi hadi wakamkashifu Jaji Warioba. Baada ya rasimu ya kwanza na ya pili kutoka wakala matapishi yao kwa kuipongeza tume. Sasa hivi wajumbe wa bunge maalumu la katiba wapo Dodoma wakiendelea na mapitio ya rasimu iliyowasilishwa na tume. Kama kawaida Chadema akiongoza kundi la Ukawa, pamoja na watu wengine wamerudia staili ileile kwamba kinachotengenezwa Dodoma ni katiba ya CCM. Nashangaa kuona hata Jaji Warioba yupo mstari wa mbele kusema ni katiba ya CCM. Tuwe wawazi na wakweli, mrejesho wa kilivchoamriwa kwenye bunge haujatolewa, tunapata wapi ujasiri wa kusema ni katiba ya CCM? Nashindwa kuelewa hata utashi wa Jaji Warioba umepotelea wapi kiasi kwamba ameamua sasa kuwa mwanasiasa. Sioni sababu ya kufanya mahitimisho wakati hata ripoti hatujapewa. Isitoshe hata kama hao CCM wataweka yao, wahusika wa mwisho na wenye maamuzi ni sisi wananchi wenyewe, kama tutaona haitufai tutaikataa, CCM si Mungu kwamba wao wanachokisema lazima sisi tukifuate.

Mkuu unaupotosha umma. Siyo watu wote ni wafuasi wa vyama ila wanataka Taifa liwe na ueledi. Mambo yanayofanyika hayawavutii watu wengi
 
wala msiwe na wasiwasi kwasababu hakuna katiba mpya akidi ya kupitisha hayo wanayoyajadili katika kamati kwasasa haipo hivyo mchakato huu hautokamilika abadani bila ukawa kurudi bungeni!!!
 
Kiweke hicho kifungu kutoka katika sheria ya mabadiliko ya katiba kinachomhalalisha Sita kupokea maoni!!!

Sheria inawaruhusu na wananchi anaridhika ndiyo maana makundi mbalimbali yanaenda kupeleka maoni kama:
- Wasanii
- Baraza la habari Tanzania
- Wakulima na wafugaji
- Hata yeye Warioba amepeleka maoni mengine hivi karibuni
 
Mkuu unaupotosha umma. Siyo watu wote ni wafuasi wa vyama ila wanataka Taifa liwe na ueledi. Mambo yanayofanyika hayawavutii watu wengi

Siipotoshi umma mkuu. Huwezi kutoa conclusion wakati hujapewa final result. Ndio maana nimetolea mfano wa Chadema walivyokuwa wanaiponda tume. Ningetaraji watu wasubiri waone nini kitaletwa mezani na hao wajumbe waliojifungia Dodoma ndipo tupate nafasi nzuri ya kukosoa na kupongeza tukiwa na ushahidi mikononi.
 
Back
Top Bottom