Serikali: Iweje mtoe elimu Katiba iliyopitwa na wakati?

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Ni wazi kabisa kwamba Serikali ya CCM haina nia thabiti kutuletea katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu 2025.
Kama ni elimu kwa raia,tayari raia walikwishaipata kupitia tume ya Jaji warioba na hata baadhi ya wazee wastaafu nchini akiwemo Jaji Warioba mwenyewe.
Wametoka na kupinga mpango huo wa serikali.

Mfano:namnukuu Jaji warioba kupitia gazeti la mwananchi.
"Jaji Warioba aungana na wadau wengine kuhoji hatua ya Serikali ya kutaka kutoa elimu ya Katiba Mpya kwa muda wa miaka mitatu, akisema hakuna sababu ya kufanya kwa sababu wananchi wana uelewa kuhusu mchakato huo".
Mwisho wa kunukuu.
Mbali ya kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za serikali ambazo ni jasho halisi la walipa kodi wa nchi hii.
Kama serikali ina nia thabiti ya kutoa elimu ya katiba.
Kwanini isilete katiba mpya kwanza, na kisha itumie hizo pesa kuwaelimisha raia kuhusu katiba hiyo mpya pamoja na haki zao za msingi kikatiba?

CCM acheni kucheza na akili za watanzania.
 
KATIBA mpya haijawahi kuletwa na sirikali sababu hayo Si majukumu Yao,

KATIBA ni mkataba kati ya waongoza (Waajiriwa, sirikali) na waongozwa(bosses).

Wananchi ndo tunatakiwa tuoneshe Kwa vitendo lini tupate Katiba mpya.

NB: Bila tume HURU ya UCHAGUZI na KATIBA mpya hapatakuwa na uchaguzi wowote wa HAKI.

Tusubiri.
 
Ni wazi kabisa kwamba Serikali ya CCM haina nia thabiti kutuletea katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu 2025.

Kama ni elimu kwa raia,tayari raia walikwishaipata kupitia tume ya Jaji warioba na hata baadhi ya wazee wastaafu nchini akiwemo Jaji Warioba mwenyewe.

Wametoka na kupinga mpango huo wa serikali.

Mfano:namnukuu Jaji warioba kupitia gazeti la mwananchi.

"Jaji Warioba aungana na wadau wengine kuhoji hatua ya Serikali ya kutaka kutoa elimu ya Katiba Mpya kwa muda wa miaka mitatu, akisema hakuna sababu ya kufanya kwa sababu wananchi wana uelewa kuhusu mchakato huo".

Mwisho wa kunukuu.

Mbali ya kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za serikali ambazo ni jasho halisi la walipa kodi wa nchi hii.
Kama serikali ina nia thabiti ya kutoa elimu ya katiba.

Kwanini isilete katiba mpya kwanza, na kisha itumie hizo pesa kuwaelimisha raia kuhusu katiba hiyo mpya pamoja na haki zao za msingi kikatiba?

CCM acheni kucheza na akili za watanzania.
Nakubaliana naww ✔️ issue ya katiba itapigwa danadana mpaka rais amalize muda wake then amuachie mwingine. Nae atakuja na priority zake na sio katiba mpya so hawa jamaa nia hiyo hawana cz wanajua fika ikifanyika revolution ya katiba itawa cost wao na kuwabana kweny madili na uchaguzi. Kitu ambacho hawako tayar!!!
 
Ni wazi kabisa kwamba Serikali ya CCM haina nia thabiti kutuletea katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu 2025.
Kama ni elimu kwa raia,tayari raia walikwishaipata kupitia tume ya Jaji warioba na hata baadhi ya wazee wastaafu nchini akiwemo Jaji Warioba mwenyewe.
Wametoka na kupinga mpango huo wa serikali.
Mfano:namnukuu Jaji warioba kupitia gazeti la mwananchi....
"Jaji Warioba aungana na wadau wengine kuhoji hatua ya Serikali ya kutaka kutoa elimu ya Katiba Mpya kwa muda wa miaka mitatu, akisema hakuna sababu ya kufanya kwa sababu wananchi wana uelewa kuhusu mchakato huo"...
Mwisho wa kunukuu.

Mbali ya kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za serikali ambazo ni jasho halisi la walipa kodi wa nchi hii.
Kama serikali ina nia thabiti ya kutoa elimu ya katiba.kwa nini isilete katiba mpya kwanza, na kisha itumie hizo pesa kuwaelimisha raia kuhusu katiba hiyo mpya pamoja na haki zao za msingi kikatiba?

CCM acheni kucheza na akili za watanzania.
Naunga mkono hoja yako 100%...kwamba

Ni wazi kabisa kwamba Serikali ya CCM haina nia thabiti kutuletea katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu 2025.

Kama ni elimu kwa raia,tayari raia walikwishaipata kupitia tume ya Jaji warioba na hata baadhi ya wazee wastaafu nchini akiwemo Jaji Warioba mwenyewe.

Wametoka na kupinga mpango huo wa serikali.

Mfano:namnukuu Jaji warioba kupitia gazeti la mwananchi.

"Jaji Warioba aungana na wadau wengine kuhoji hatua ya Serikali ya kutaka kutoa elimu ya Katiba Mpya kwa muda wa miaka mitatu, akisema hakuna sababu ya kufanya kwa sababu wananchi wana uelewa kuhusu mchakato huo".

Mwisho wa kunukuu.

Mbali ya kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za serikali ambazo ni jasho halisi la walipa kodi wa nchi hii.
Kama serikali ina nia thabiti ya kutoa elimu ya katiba.

Kwanini isilete katiba mpya kwanza, na kisha itumie hizo pesa kuwaelimisha raia kuhusu katiba hiyo mpya pamoja na haki zao za msingi kikatiba?

CCM acheni kucheza na akili za watanzania.
Ni wazi kabisa kwamba Serikali ya CCM haina nia thabiti kutuletea katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu 2025.

Kama ni elimu kwa raia,tayari raia walikwishaipata kupitia tume ya Jaji warioba na hata baadhi ya wazee wastaafu nchini akiwemo Jaji Warioba mwenyewe.

Wametoka na kupinga mpango huo wa serikali.

Mfano:namnukuu Jaji warioba kupitia gazeti la mwananchi.

"Jaji Warioba aungana na wadau wengine kuhoji hatua ya Serikali ya kutaka kutoa elimu ya Katiba Mpya kwa muda wa miaka mitatu, akisema hakuna sababu ya kufanya kwa sababu wananchi wana uelewa kuhusu mchakato huo".

Mwisho wa kunukuu.

Mbali ya kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za serikali ambazo ni jasho halisi la walipa kodi wa nchi hii.
Kama serikali ina nia thabiti ya kutoa elimu ya katiba.

Kwanini isilete katiba mpya kwanza, na kisha itumie hizo pesa kuwaelimisha raia kuhusu katiba hiyo mpya pamoja na haki zao za msingi kikatiba?

CCM acheni kucheza na akili za watanzania.
Naunga mkono hoja yako kwa 100%....

Kimsingi,si serikali ya mkoloni wala hii ya sasa...zote hazijawahi kuruhusu wananchi wajitengenezee katiba inayotakona na mawazo na utashi wao.

Kwa serikali ya kikoloni kutoruhusu katiba....ni suala linaloeleweka kwa sababu ingekuwa kioja kumpa uhuru unayemtawala eti ajipangie mwongozo anavyotaka atawaliwe.

Lakini baada ya uhuru,serikali za viongozi wote waliopita wa Tanzania hazijawahi kuwapa fursa wananchi kutoa maoni yao kuhusu aina na muundo wa katiba wanayoitaka.

Na kutokana na hilo sasa ni wazi kwamba siyo rahisi kwa wananchi wengi kujua yaliyomo katika katiba zilizopita na ambazo zimefanyiwa marekebisho kidogo tu na kuzaa katiba hii ya sasa kwa vile yaliyomo ndani yake hayatokani na mapendekezo yao.

Serikali imesema eti inataka kwanza kutoa elimu kwa wananchi kwa miaka 3 kuhusu katiba ya sasa ili waielewe ndipo mchakato wa katiba mpya uendelee.

Serikali imesema nusu ya watu,hawajawahi hata kuiona katiba ya sasa....,kwa hilo serikali iko sahihi.

Lakini walitakiwa kujua jambo moja kwamba,hakuna mwananchi anataka kupoteza muda kuielewa katiba isiyotokana na mawazo yao,..na ndo maana walipopata nafasi ya kutoa maoni yao kupitia tume ya Warioba, maoni na fikra zao yalitofautiana kwa kiasi kikubwa na maudhui ya katiba ya sasa.

Serikali itambue pia,kwamba wananchi hawataki kuelimishwa,..wanataka kutoa mapendekezo na maoni yao kuhusu kuhusu katiba mpya....,maoni ambayo walishayatoa kupitia tume ya Warioba.

Wananchi wanauliza maoni na mapendekezo waliyotoa yamefichwa wapi?

Wanachi wanajua kulitumika mabilioni ya shilingi ya hela zao za kodi ili kupata maoni yao hayo,..sasa nani huyo mwenye jeuri ya kuficha na kuharibu maoni yao yasifanyiwe kazi?

Wananchi wanauliza hizo gharama zitakazotumika kwenda kuwapa elimu ya katiba ya sasa ambayo hawaitaki,itatoka katika mfuko wa kodi zao tena?

Kwa serikali yenye kufikiri sawia,itasikiliza wananchi na mahitaji ya fikra zao.
Ahlan wa salaan.
 
Nakubaliana naww issue ya katiba itapigwa danadana mpaka rais amalize muda wake then amuachie mwingine. Nae atakuja na priority zake na sio katiba mpya so hawa jamaa nia hiyo hawana cz wanajua fika ikifanyika revolution ya katiba itawa cost wao na kuwabana kweny madili na uchaguzi. Kitu ambacho hawako tayar!!!
Huo ndio ukweli.ni kituko kutumia mamilioni ya pesa kutoa Elimu ya katiba ambayo unaenda kuiondoa na kuleta mpya!
Huu ni mchezo mchafu unaandaliwa hapo.
 
Wanapoteza muda tu ufike mwakani uchaguzi wa serikali za mitaa kisha uje uchaguzi mkuu, hawana lolote la maana kusema wanatoa elimu leo kwa Katiba ya mwaka 1977, ni wapuuzi tu.
 
Tukiacha yote wana point japo miaka mitatu ni mingi,
Kipindi jaji warioba anapita ilikuwa ni 2013, miaka 10 nyuma,
Mtoto wa miaka nane kipind kile alikuwa hajui nini kinaendelea, leo ana miaka 18 na atatoa maoni kwenye katiba mpya, kwa hio ni lazima watu hawa wapewe elimu ili wajue madhaifu ya katiba iliyopo
 
Tume ya Warioba hiyo ya 2013 haikupewa kazi ya kuwaelimisha watu ili waielewe katiba ya sasa,..yenyewe ilikuwa na kazi moja tu,kukusanya maoni ya wananchi kuhusu aina ya katiba wanayoitaka....,mathalan,tume ilisikiliza maoni ya watu kuhusu muundo wa muungano waliouhitaji kati ya muundo wa serikali moja,mbili au tatu.
Ninachopinga hapa ni kupoteza muda na fedha bila sababu kwa kuwaelimisha watu juu ya katiba ambayo haikutokana na maoni yao kabisa.
Isitoshe tume ya Warioba ilifanya hiyo kazi ya kukusanya maoni kwa muda mfupi sana...,na siyo hiyo miaka mitatu wanatoisema.
 
Back
Top Bottom