Warioba: Mimi na Salim urais basi

Kiujumla hakuna kiongozi mbaya kama kiongozi neutral, tunahitaji kiongozi mwenye misimamo thabiti na iliyowazi kuwa anatetea kipi na anakemea kipi,

Salim anakosa sifa hii, career yake ya diplomasia ni ya u neutral, kupatanisha sehemu mbili haihitaji uwe na msimamo wa upande wowote bali hata kama unajua mkosaji unatakiwa kumung'unya maneno tu na kufumbia macho.

Wakuu, Salim anafanana kabisa na JK, ni mtu anaetaka kupendwa na kila mtu, ni mtu asiye na uwezo wa kukemea jambo kwa nguvu(strongly condeming) na ni mtu asiye na uwezo wa kufanya maamuzi magumu. Kulipatia taifa kiongozi kama salim ni sawasawa na kulizika kabisa.
 
Kiujumla hakuna kiongozi mbaya kama kiongozi neutral, tunahitaji kiongozi mwenye misimamo thabiti na iliyowazi kuwa anatetea kipi na anakemea kipi,

Salim anakosa sifa hii, career yake ya diplomasia ni ya u neutral, kupatanisha sehemu mbili haihitaji uwe na msimamo wa upande wowote bali hata kama unajua mkosaji unatakiwa kumung'unya maneno tu na kufumbia macho.

Wakuu, Salim anafanana kabisa na JK, ni mtu anaetaka kupendwa na kila mtu, ni mtu asiye na uwezo wa kukemea jambo kwa nguvu(strongly condeming) na ni mtu asiye na uwezo wa kufanya maamuzi magumu. Kulipatia taifa kiongozi kama salim ni sawasawa na kulizika kabisa.


Basi mpe dr slaa iyo 2015

Mimi nitampa Dr Salim Ahmed Salim..
 
Kwa jinsi siku zinavyopita, Kuna hatari ya nchi kupata Rais 2015 ambaye ni bogus zaidi ya Marais waliopata kuliongoza Taifa tokea tupate uhuru. Jamii kwa sasa imeanza kuona Rais bora ni yule mwenye imani ya dini kama wao bila kujali uwezo wake. Taifa limeanza kuonyesha dalili zote za kuelekea Taifa Mfu. Kwa Watanzania wengine wenye upofu wa fikra, Mwanasiasa mahili ni yule anayepiga kelele majukwaani bila hata ya kujua mipaka ya matamshi yake. Unfortunate, Salim Ahmed Salim hayupo kwenye haya makundi na siyo ajabu, kwa sasa ameanza kuzodolewa kwa sababu kwao, anaonekana hana vazi la Urais.

SAS ni mwanadiplomasia, na msingi mkuu wa kuwa mwanadiplomasia mahili ni kuwa CALM, COLLECTED AND ON BALANCE.

Ni kitu cha kushangaza pale watu wanamtaka aende sokoni kujiuza kama wanaSiasa wengine wanavyofanya kwa sasa. Salim Ahmed Salim hahitaji kwenda sokoni kujiuza kwa sababu kazi hiyo aliisha ifanya siyo kwa Tanzania tu bali hata katika mataifa. Pale alipopewa kazi ya kufanya katika nchi au mataifa, aliifanya kwa uadilifu na ufanisi mkubwa. What more you want!!.

Please Candid Scope , usichanganye bidhaa za kisiasa zinazojiuza kwa sasa na bidhaa iliyojipambanua tayari ndani ya soko la kisiasa.
 
Kwenye hoja za kisiasa za kumpima mtu tujaribu kuondao kipengele cha udini.Otherwise safari hii iwe zamu ya Mpagani.Maana chochote kitakachojadiliwa kwa nini baadhi yetu wanaweka kipengele cha udini.TUjitahidi kujifunza either kukubali hoja ya mtu ,kuikataa kwa hoja au kukubali katika kutokubaliana.

Tanzania kwanza mengine baadaye.

lamba 'like"
 
Aaah Wapi,

Mmeshaanza siasa zenu za majitaka sasa,,

Hebu niambie wewe sasa.humpendi huyu kwa chuki zako binafsi au humpendi kwa kuwa yuko CCM??

Akisimama huyo 2015 hatuna budi kumpatia nchi hii,mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni..

Au kwa kuwa ni Muislam??

SIASA ZA MAJITAKA.
Mkishindwa tu! Mnakimbilia udini.
Mbona sijaona alipoandka muislamu?
Mtu wa namna yako maranying ujiona inferior.
Acha udini. Hujakua bado?
Udini utakutafuna hadi kuzimu.
Hebu badilika, mkubwa wewe.
 
Sioni sababu ya ukimya kama inamantink.....

Bora raisi akawa mtu ambaye si maarufu kwan anaweza fanya makubwa zaidi....chukulia mfano mwakyembe hakuwa anajulikana lakin baada ya report ya richmond watu walifahamu utendaji wake wa kazi

Afu tuchukulie mfano wa Ben alikuwa kimya sana na hakuwa maarufu wa jukwaan lakin alifanya makubwa....

Kwan ww mtoa thread hii unadhan umaarufu wa kisiasa jukwaan unaweza ukamfanya mtu awe bora kiutendaji???????

Chukulia mfano sugu na Dr salim nan maarufu jukwaan??? Je unaweza kuwalinganisha kiutendaji????

Tunataka raisi mpiga kazi si maarufu wa majukwaaaa????





Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Umetolea mf. Wa watu wachache kama Mwakyembe. Lakin angalia nyadhifa alizoshka Salim mf.Uwazir mkuu. Nan anakumbuka alichowahi kukifanya Salim kilichochema kwa Taifa kias cha kumuamin?
Nisawa na kumpa Mizengo ashke nchi, unadhan tutapona? Wote hawa hawana msimamo. Ni fuata upepo.
 
Hilo ndilo ninaloliona mimi. Unaweza kuona akina Lowasa, Sitta na wengine hujaribu kuonyesha misimamo yao, lakini huyu Salim ni usindikizaji tu.

Hana jipya atatupoteza tuu. Liko wapi chaguo la mungu jk kama walivyosema viongozi wa dini wakati ule?
 
Kwanza kwa hali ya afya yake sidhani kama SAS anataka kutafuta Urais tena. Naona wakati wake umeisha pita,na ni vema akajitokeza mapema akatoa msimamo. Bila hivyo atachafua hata hiyo heshima kiasi iliyobakia. Pili siyo SAS tu ndani ya CCM ambaye yupo kimya wakati taifa linapopata misukosuko ambayo tungetarajia hawa jamaa wanaojiita wasafi ndani ya CCM tusikie msimamo wao. Wote wapo kimya. Kwangu maoni yangu kama Tanzania inataka kuondoka hapa tulipo kwama,hakuna budi kuiondoa CCM na watu wake ili tuanze upya!

Ndg. Timbilimu,
Kuiondoa CCM madarakani lingekuwa jambo jema sana lakini nafikiri hadi hivi sasa, hatuna chama ambacho kinachokubalika kila kona ya nchi licha ya Watanzania wengi kuichoka CCM. Ubinafsi wa viongozi wa vyama vya upinzani ndio unaoendelea kuiweka CCM kileleni hadi hivi sasa. Kwa hiyo kwa hivi sasa, bado natarajia CCM kubakia madarakani.
  1. Hivyo basi, kwangu mimi Dr. Salim A. Salim bado anafaa sana na ana sifa zote za kubadili huu uozo tulionao hivi sasa ingawa sidhani kama watamteua. SAS ni mchapa kazi, muona mbali, anajua administration, kitu ambacho ni muhimu sana kuijenga serikali upya baada ya JK na pia anauelewa ulimwengu vema. Wengine ndani ya CCM ninaoona wanafaa ni Mama Tibaijuka, Membe, Mama Migiro, Mwakyembe na mzee Cleopa Msuya.
  2. Mzee Msuya angefaa kwa angalau miaka 5 tu hivi ili asafishe uzembe atakaoacha JK. Msuya ni mchapa kazi kupita kiasi na yeye pia anaelewa administration. Tatizo lake umri wake umesonga sana, 81 hivi sasa. Lakini angepewa miaka 5 tu hivi, nchi ingenyooka. Bahati nzuri afya na akili yake bado sio vibaya lakini sidhani kama kuna atakayemfikiria kwani umri umesonga sana.
  3. Mwakyembe anaonekana na uchungu sana na nchi, lakini sidhani kama ana uzoefu wa administration ambayo itahitajika sana kuweka mambo sawa, maana chini ya JK, kila kitu kimevurugika. Wababaishaji ndio viongozi na hakuna anayejali utendaji na miundo yake.
  4. Mama Migiro ninamchagua zaidi kutokana na kazi yake ya UN ambayo kwa vyovyote vile itakuwa imemfungua macho juu ya nini wenzetu wanafanya kujiendeleza. Lakini kuwa kwake karibu sana na wanamtandao ni jambo la kutilia wasiwasi.
  5. Membe napenda sana elimu yake ya John Hopkins University na madaraka aliyowahi kuyashika ikulu na hasa wizara ya nje. Hata hivyo, Membe anaonekana kutokuwa mbunifu au kuwa na mawazo makubwa ya kimaendeleo, huu ni mtazamo wangu tu. Kwa hiyo sidhani kama atabadilisha muundo wa utendaji serikalini kwa kiasi kikubwa kinachohitajika.
  6. Halafu hatimaye kuna Mama Tibaijuka. Kwa mtazamo wangu, huyu mama angefaa sana kuwa raisi wetu mpya. Kwanza ni mchapa kazi sana, halafu anao uzoefu wa administration tena kimataifa, anajua miundo ya kimataifa tunayohitaji kushirikiana nayo, ni mbunifu na sio mwoga kufanya maamuzi yanayowachukiza watu kama alivyofanya akiwa UN-HABITAT. Zaidi ya yote, sidhani kama yuko karibu na wanamtandao na hadi hivi sasa sijasikia kama amehusishwa na rushwa ya aina yeyote. Zaidi ya yote, nafikiri akina mama wangetufaa sana wakati huu wa rushwa za waziwazi kwani wengi wao hawana tamaa binafsi kama akina Lowasa.

Kwa hiyo kwa kifupi, kwa hawa niliowataja, kama ingekuwa ni chaguo langu, ifuatayo ndio ingekuwa list yangu kulingana na ubora wao;
1. Salim
2. Msuya
3. Tibaijuka
4. Mwakyembe
5. Migiro​
6. Membe
 
Binafsi sikufikiria jambo hilo la kuwamo ndani ya kamati ya kuratibu katiba mpya. Nalo laweza kuwa tatizo la kujenga mazingira ya kusafisha magogo atakamotandika mataluma ya reli ya kuingilia Magogoni.

Hakuna ubaya wa kujenga nyumba atakayekuja kuishi,
 
Bahati mbaya sifahamu kama Candid Scope ni mwanataaluma ya habari au lah, kama siyo-tunashukuru kwa mada yako lakini kama NDIYO, mkumbuke hawa ndiyo walioleta MAJANGA ya Nchi hii. Tasnia ya habari haitakwepa matatizo ya nchi hii kwani wao pekee ndiyo "waliotuchagulia" Rais wa sasa kupitia mabandiko kama haya. Mungu atupe hekima mara hii ili tupate ujasiri wa kuwapuuza waandishi wa habari.
 
aaah wapi,

mmeshaanza siasa zenu za majitaka sasa,,

hebu niambie wewe sasa.humpendi huyu kwa chuki zako binafsi au humpendi kwa kuwa yuko ccm??

Akisimama huyo 2015 hatuna budi kumpatia nchi hii,mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni..

Au kwa kuwa ni muislam??



dr salim sio muislamu.

Ni mkomunist
 
Binafsi natamani tupate kiongozi yeyote ambaye atakuwa Dikteta wa Kiuchumi-I know we will suffer a lot, but our guys wll come to enjoy more!
 
Aaah Wapi,

Mmeshaanza siasa zenu za majitaka sasa,,

Hebu niambie wewe sasa.humpendi huyu kwa chuki zako binafsi au humpendi kwa kuwa yuko CCM??

Akisimama huyo 2015 hatuna budi kumpatia nchi hii,mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni..

Au kwa kuwa ni Muislam??

Uislamu umeuona wewe, Mtoa uzi hajasema hivo!!! Kwani huko CCM hakuna watu wengine wanaofaa U-Rais? Mbona vijana wapo wengi tu? Ni lazima "Mchekeche makapi ili kupata vipunje vya mchele?" TAFAKARI
 
Dr. Salim ni kiongozi aliekuwa na uwezo wa kuongoza nchi kwa kufuata katiba na na sheria za nchi.. Na ndie aliekuwa chaguo la Mwalimu 1995 bahati mbaya majukumu ya kimataifa (kutokana na uzoefu wake kimataifa aliombwa kuisimamia AU ambayo wakati ule ilikuwa kwenye transitional toka OAU kwenda AU) yalimuondoa kwenye rada za Mwalimu.. Baada ya kujeruhiwa na JK 2005 naona aliona siasa imekuwa uadui na akaamua kukaa pembeni.. Akawa anajishughulisha na Taasisi aliokuwa anaiongoza ya Mwalimu Nyerere Foundation.. Kama mtakumbuka alikuwa anakemea vitendo vibovu vya serikali akishirikiana na Jaji Warioba na Joseph Butiku.. Makamba Snr aliwahi kuwatukana hawa kwa kuwaita wajinga na wenye wivu wa kushindwa kutokana na wao (pamoja na Dr. Salim) kushindwa uchaguzi na JK.. Baadae kukatokea vitisho vya kuwatisha hawa na kwa wanaokumbuka ilifikia wakati Jaji Warioba alitaka kufunguliwa kesi ya wizi kwenye kampuni ya Mwananchi Goldmine (sijui kama nimelipatia hilo jina).. Yote ikiwa ni njia ya kuwanyamazisha hawa..
Kwa hiyo sio kweli kama Dr. Salim alitulia kimya bila ya kusema yale mabaya..

Ila kwa hali ilivyo sasa na mfumo huu tulionao sidhani kama Dr. Salim ataweza kuingoza nchi.. Njia pekee ambayo inaweza kuniamisha kwamba ataweza kuwa raisi mzuri ni kutoteuliwa kugombea na mfumo uliopo sasa wa ccm.. mgombea yeyote ambae atateuliwa na mfumo uliopo sasa ndani ya ccm hatakuwa raisi mzuri kwa nchi yetu kwa kuwa atakuwa anawatumikia hawa wa mfumo kwanza na Tanzania baadae.. Na wote tunajua athari za mfumo..
Swali Jee Dr. Salim anaweza kuteuliwa kugombea chini ya mfumo mwingine..?
 
dkt salim ni muungwana. muungwana ni vitendo. kwa bahati mbaya kizazi cha sasa hawaelewi utendaji wake. alifanya mambo mengi lakini ikumbukwe kuwa MWL NYERERE HUKUPENDA JINA LA MTU MMOJA MMOJA LIPANDE. ALIPENDA SANA KUTUKUZWA YEYE. HAKUWAPA MAWAZIRI WAKE FURSA YA KUAMUA NA KUTENDA KAMA WANAVYO FANYA AKINA MAGUFULI NA MWAKYEMBE hivi sasa. nilipokua chuoni, profesa mmoja aliwahi kutuambia kuwa mwalimu amelifanyia taifa letu mengi lkn hakupenda mawaziri wake wasifiwe au waonekane kuwa wanatenda. alipenda mipango ypte apelekewe yeye ili yeye ndiyo aitekeleze. marehemu sokoine aliwahi kukwamishwa na mwalimu katika kasi yake ya kuirekebisha nchi yetu. hii ni kutokana na kumuonea wivu. vilevile alimuona kama HATARI kwa utawala wake. mwalimu alipenda anaeharibu ahamishiwe sehemu nyingine lkn sokoine aliaumuru anaeharibu afukuzwe. hiyo siyo mada ya leo tuachane nayo.

dkt salim ni mtu makini azungumzapo na atendapo. hotuba aliyoitoa chimwaga mwaka 2005 wakati anaomba kuchaguliwa kugombea urais kwa tiketi ya ccm ni kielelezo kuwa uwezo na dira anavyo. hana asili ya kupayuka. kuna watu wanadhani kupayuka ndiyo utendaji. la hasha. kuna mabadiliko makubwa ambayo wakurugenzi wa nsssf na nhc wameyafanya lkn licha ya utendaji wao mzuri, siyo watu wa kujitokeza kujisifu ili waonekane.

dkt salim aliongoza oau ktk mazingira magumu. viongozi wengi walisema kuwa oau haifai kuwepo kwa sababu nchi nyingi zimeshapata uhuru. dkt salim alijitahidi kuzihamasisha kuwa chombo hicho ni muhimu na lazima nchi zichangie ili kukifanya kiwepo. baadaye aka andaa dira ya kubadilisha oau kuwa AU. yakaundwa malengo mapya ya au. LA MSINGI ZAIDI SALIM NI MTU SAFI. HANA KASHFA YA RUSHWA KATIKA UTENDAJI WAKE. mwl nyerere aliwahi kusema kuwa "kimataifa mtanzania namba moja ambaye ameifanya TZ ijulikane na kuheshimika ni dkt salim. alijenga hoja UN akifafanua self reliance (kujitegemea) ambayo tanzania inaifuata. aliiongoza oau na kuifanya kiwe chombo cha kuaminika".

kwa ccm ya sasa, salim ni chaguo bora kwa sababu hayumo katika makundi yanayo chafuana. amekua kimya kwa miaka 8 kwa sababu alichafuliwa sana mwaka 2005 na JK. aliona kuwa njia salama ya kumfanya awe na amani, ni kukaa kimya. alichafuliwa sana!

akipitishwa lowassa lazima akina sitta, membe nk..... hawatomuunga mkono. na kinyume chake ni sahihi. akipitishwa salim, wote watamuunga mkono kwa sababu amepewa mtu ambaye hayumo vitani. kinacho onesha kuwa hapendi rushwa, mwaka juzi kamati anayoiongoza ya MO IBRAHIM iliamua kuwa hakuna kiongozi mstaafu mwenye sifa ya kupewa tuzo. salim alisema wasubiri hadi miaka 2-3 ijayo.

kiafya salim bado ana nguvu na anaonekana vizuri. lowassa sasa hivi ni dhaifu kiafya. slaa ana nguvu lkn mkono naona umeshalemaa! lipumba amechokwa, mrema hoi na mbatia amekiua chama. tukiweka uzalendo pembeni, salim is the right choice to be the fifth president of TZ
th
th
th
 
Nakumbuka hata Mkapa alikuwa hana umaarufu kihivyo, gazeti la Mfanyakazi liliansdika¨ Mkapa naye achukua fomu!¨ kwambwa ilikuwa inashangaza, So kwa Salum sioni tatizo
L.Col_Members_SalimSalim.jpg
images

Dr. Salim Ahamed Salim (Tanzania) and Henry A. Kissinger (USA)

Dr. Salim Ahmed Salim ana jina kubwa nchini na kimataifa katika masuala ya kimataifa. He is a diplomatic figure. Naweza kumlinganisha na baadhi ya wanadipolamasia kama Henry Kissinger pamoja na umaarufu wao kimataifa hawakufaa kushika dola katika taifa.

Majukumu mazito aliyowahi kuyafanya kitaifa na kimataifa ni pamoja na:
  • Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa
  • Katibu Mkuu Umoja wa nchi Za Afrika
  • Mgombea Ukatibu Mkuu umoja wa Mataifa - hakupita
  • Nafsi ya juu aliyowahi kuishika Tanzania ni kuwa Waziri Mkuu
Pamoja na umaarufu alioweza kuwa nao katika masuala ya kimataifa na kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania:

  1. Hajaonyesha msimamo wake katika masuala ya kitaifa,
  2. Hayuko wazi
  3. Mkimya asiye weza kushirikisha aliyo nayo.
  4. Pamoja na kwamba ni mwana CCM sijawahi kuona ushirikishaji wa uongozi wake kwa CCM zaidi ya kuwa mhudhuriaji.
  5. Anaonekana kupokeleka zaidi kwa sura badala ya vitendo na fikra.
  6. Anaonekana kufaa shughuli za kiofisi zaidi kuliko siasa za majukwani.

Kwa mtazamo huu ana dira gani katika kuongoza Tanzania ya leo kama atagombea urais?
Je, Tanzania tuendelea kunadishwa majina makubwa ya wagombea urais pasipo kuonyesha uwezo wao?
 
Hivi Slaa anafaa kwa lipi kuongoza hii nchi? Au mbowe anautaalamu gani wa kupewa nafasi ya urais? Na Viongozi wenu wote wa CDM wamefanyanya jambo gani la maana kuwa na sifa ya urais?

Mtu ameshika ubunge miaka 10 anakuja kusema anauwezo wa kuwa Rais wa hii nchi, si ni kichekesho tu.
Slaa= ubunge na upadri
Mbowe =UDJ na ubunge
Zitto= ubunge
Sasa hawa kweli mtaweza kuwafananisha na Salim ahmed Salim?
 
Hivi Slaa anafaa kwa lipi kuongoza hii nchi? Au mbowe anautaalamu gani wa kupewa nafasi ya urais? Na Viongozi wenu wote wa CDM wamefanyanya jambo gani la maana kuwa na sifa ya urais?

Mtu ameshika ubunge miaka 10 anakuja kusema anauwezo wa kuwa Rais wa hii nchi, si ni kichekesho tu.
Slaa= ubunge na upadri
Mbowe =UDJ na ubunge
Zitto= ubunge
Sasa hawa kweli mtaweza kuwafananisha na Salim ahmed Salim?


Kweli kabisa..

Umeongea kweli kabisa..
 
Back
Top Bottom