Waberoya,
Hata mie nimeanza kusoma nilikuwa sijui lolote. Ila nilianzia ukurasa wa kwanza na hadi kufika mwisho, nimeshaelewa kila kitu. NA WEWE NENDA UKAFANYE HIVYO. Vinginevyo, basi unaona kile tu unataka wewe ukione. Mzee kweli maji ya shingo. Mwanzo nilifikiri akina Mtanzania wanadanganya juu ya huyu Mzee. Ila sasa nimeelewa na kwa kweli siasa kitu kibaya. Mkapa kalisha watu wengi sumu na ukichunguza sana, utagundua kuwa kuanzia juu hadi wabunge wetu, walikula ASALI hiyo ya mti wa kati.
Mtanzania nakubali sasa maneno yako. USIMWAMINI MWANASIASA.
1. Uamuzi wa kuanzishwa kwa Kampuni ya Mwananchi Gold ulitokana na nia njema ya serikali,
2. serikali iliamuru BoT na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Kampuni ya MA-CE ya Italia kuunda kampuni hiyo.
3. Baada ya uamuzi huo, serikali ilikuja kwenye ofisi yetu ya uwakili ya Nyalali, Warioba & Mahalu Law Associates ili tuisaidie kuipatia huduma ya kisheria kabla na baada ya kuundwa kwa kampuni hiyo.
hatimaye kaongea.Nilisema Warioba Fisadi. maji yanaanza kuzidi unga.
hakuna msafi hata mmoja kwenye uongozi wa CCM kwani hata wale walioonekana ni watakatifu ndio wezi wakubwa. Read btn the line. He is the big one.
Alikuwa wapi siku zote tukipiga kelele alivyoona sasa anakwenda chini anatafuta huruma ya wananchi, nail him down till death.
...hivi kwani bado hatuna health insurance ambazo ndio kazi yake kulipia matibabu ya wateja wake,matatizo mengine ni ya kujitakia tuu
[/B][/COLOR][/B]Duh, Mbona siwaelewi?
Jamani Warioba aliwaita waandishi wa Habari ili awaeleze ufahamu wake kuhusu tuhuma zinazosemwasemwa mitaani na katika baadhi ya vyombo vya habari. Sasa alichokisema ndicho alichokuwa tayari kukisema. Ndio maana anasema, kama kuna kushitakiwa yuko tayari kujibu mashitaka hayo wakati wowote.
Ndugu zangu, Jaji Warioba ni mtu makini sana. NI mtu anaefikiri kabla ya kusema. Na anasema kinachojitosheleza. Anapotaja Makampuni yenye uwekezaji katika hiyo MWANANCHI Gold anajua anachokisema. Kama unavyojua, Kampuni ina wamiliki wake, na wamiliki wanaweza kuwepo leo, kesho wakauza share zao. Hawezi kutaja tu moja kwa moja wamiliki wa hizo kampuni bila kuwa makini. Yeye kama Jaji anajua umuhimu wa kuhifadhi taarifa za watu (Kama Waziri Mkuu mstaafu, anaijua Katiba). Haikuwa nia yake kwenye kikao kile kisema majina ya watu wowote.
Pili ushiriki wake na Kampuni yake ameusema bayana. Kama unavyojua, Memorandum and Articles of Association za Kampuni yoyote huandaliwa na wana sheria. Kampuni yake ilipewa kazi ya kufanya hivyo, pamoja na ushauri mwingine wa kisheria endapo utahitajika wakati wowote kabla na baada ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo (hii ameisema vizuri katika taarifa hapo juu Sijaona mahali anaposema alikuwa mwendeshaji wa Kapuni hiyo (labda kama kuna mtu anaweza kunisaidia hilo).
Wakuu, nadhani mnajua pia kuwa Serikali imepewa mamlaka na Katiba kupitia Bunge kuanzisha Taasisi, na taratibu zimewekwa za kufanya hivyo. Serikali pia inaweza kuwa na wabia wengine (binafsi au Taasisi za serikali) katika kufikia matarajio ya uanzishwaji wa Taasisi hizo.
[COLOR="Orange[B]"][B]Nilidhani mngeshitushwa zaidi na taarifa ya kudidimizwa kwa MWANCHI GOLD ambayo inaelekea ilikuwa na nia ya kuhakikisha rasilimali (madini) yetu yanasafishwa hapa hapa nchini na kutuhakikishia kuwa hatuporwi mali hizo. Mimi kwangu ni jambo la kushtua sana kusikia serikali inakusudia kwa nguvu zote kuua shirika/Kampuni muhimu kama hiyo.
Duh, Mbona siwaelewi?
Ndugu zangu, Jaji Warioba ni mtu makini sana. NI mtu anaefikiri kabla ya kusema. Na anasema kinachojitosheleza. Anapotaja Makampuni yenye uwekezaji katika hiyo MWANANCHI Gold anajua anachokisema.
Now look at this:-
- Serikali ilimuamuru Warioba kuisaidia namna ya kuanzisha Wananchi Gold, huku ikiwa na nia njema, na kwa nia njema kabisa serikali ikaamuru kampuni ya MA-CE ya Italy, ambako balozi wetu alikuwa Mahalu, mshiriki wa Warioba kwenye shirika la sheria, ambalo serikali ililiomba kuisaidia namna ya kuanzisha Mwananchi Gold,
- Hivi wananchi wa Tanzania tunatakiwa kuwa tumelala kwa kiasi gani jamani?