Warioba afichua siri nzito

Aliwataja wanahisa wa Kampuni ya Mwananchi Trust, ambayo ipo ndani ya Mwananchi Gold Company Ltd kuwa ni Umoja Entertainment, VNB, WM Holding inayomilikiwa na Yusuph Mushi, na CCM Trust Company.

Alisema katika Kampuni ya Mwananchi Trust, aliyekuwa na hisa nyingi ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichokuwa na hisa 15.

Kampuni ya Umoja inamilikiwa na familia ya Warioba, kampuni ya VMB inamilikiwa na familiaya Mahalu, kampuni ya YM inamilikiwa Yussuf Mushi, kampuni ya CCM Trust wenye hisa ni Warioba na Yussuf Mushi na si wadhamini wa CCM. Kazi kwenu
 
Duh, Mbona siwaelewi?

Jamani Warioba aliwaita waandishi wa Habari ili awaeleze ufahamu wake kuhusu tuhuma zinazosemwasemwa mitaani na katika baadhi ya vyombo vya habari.

Sasa alichokisema ndicho alichokuwa tayari kukisema. Ndio maana anasema, kama kuna kushitakiwa yuko tayari kujibu mashitaka hayo wakati wowote.

Ndugu zangu, Jaji Warioba ni mtu makini sana. NI mtu anaefikiri kabla ya kusema. Na anasema kinachojitosheleza. Anapotaja Makampuni yenye uwekezaji katika hiyo MWANANCHI Gold anajua anachokisema. Kama unavyojua, Kampuni ina wamiliki wake, na wamiliki wanaweza kuwepo leo, kesho wakauza share zao. Hawezi kutaja tu moja kwa moja wamiliki wa hizo kampuni bila kuwa makini. Yeye kama Jaji anajua umuhimu wa kuhifadhi taarifa za watu (Kama Waziri Mkuu mstaafu, anaijua Katiba). Haikuwa nia yake kwenye kikao kile kisema majina ya watu wowote.

Pili ushiriki wake na Kampuni yake ameusema bayana. Kama unavyojua, Memorandum and Articles of Association za Kampuni yoyote huandaliwa na wana sheria. Kampuni yake ilipewa kazi ya kufanya hivyo, pamoja na ushauri mwingine wa kisheria endapo utahitajika wakati wowote kabla na baada ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo (hii ameisema vizuri katika taarifa hapo juu Sijaona mahali anaposema alikuwa mwendeshaji wa Kapuni hiyo (labda kama kuna mtu anaweza kunisaidia hilo).

Wakuu, nadhani mnajua pia kuwa Serikali imepewa mamlaka na Katiba kupitia Bunge kuanzisha Taasisi, na taratibu zimewekwa za kufanya hivyo. Serikali pia inaweza kuwa na wabia wengine (binafsi au Taasisi za serikali) katika kufikia matarajio ya uanzishwaji wa Taasisi hizo.

Nilidhani mngeshitushwa zaidi na taarifa ya kudidimizwa kwa MWANCHI GOLD ambayo inaelekea ilikuwa na nia ya kuhakikisha rasilimali (madini) yetu yanasafishwa hapa hapa nchini na kutuhakikishia kuwa hatuporwi mali hizo. Mimi kwangu ni jambo la kushtua sana kusikia serikali inakusudia kwa nguvu zote kuua shirika/Kampuni muhimu kama hiyo.

Kwanza ujue mimi sina chuki na Mzee Wetu , bali nina chuki na Ufisadi, Pili inaonekana unatetea kitu kwa sababu labda ya maslahi yako moja kwa moja au indirectly, kwa sababu umeshindwa kuwa- objective, au kwa kuwa unamapenzi na mzee kama sisi sote tulivyo na mapenzi nae, kinacho tutatanisha ni kuwemo kwenye kundi la kenge wakati yeye ni samaki.

Msingi wa hili suala ni utata wa uanzishwaji wake, maana kama ni kitu cha srekali kinatakiwa kiwe published in Government Gazette, kuna azimio la serikali towards it, kama alitengeneza hiyo memo na articles , sasa iweje akaendelea kuwemo humo, kama mwenyekiti, na shareholder, tatu yeye kama Mwanasheria Mkuu wa Serekali anajua taratibu au articles na memo za BOT kuhusu kutoua mikopo , tatu alipoona serekali anayo dai ilianzisha na serikali, na serikali hiyo hiyo ikaamua wachimbaji or what ever wa export raw gold, si angeamua kujitoa kwenye kampuni kama hiyo, ili kulinda jina lake zuri na pensheni yake nzuri kama mstaafu.
 
Kampuni ya Umoja inamilikiwa na familia ya Warioba, kampuni ya VMB inamilikiwa na familiaya Mahalu, kampuni ya YM inamilikiwa Yussuf Mushi, kampuni ya CCM Trust wenye hisa ni Warioba na Yussuf Mushi na si wadhamini wa CCM. Kazi kwenu

hivi ndio vitu alitakiwa kuviongea kwa uwazi si kujificha ficha kwa nia nzuri ya serikali wakati nia halisi ni kujitajirisha yeye binafsi na kundi lake. kwa kuwapatia wananchi kiduchu ya kile atakacho pata
 
Kampuni ya Umoja inamilikiwa na familia ya Warioba, kampuni ya VMB inamilikiwa na familiaya Mahalu, kampuni ya YM inamilikiwa Yussuf Mushi, kampuni ya CCM Trust wenye hisa ni Warioba na Yussuf Mushi na si wadhamini wa CCM. Kazi kwenu

Mzee Warioba anahusika hapa, maelezo yake na sakata zima lilivyo inaonyesha bila shaka kwamba Mzee amefanya ufisadi. Namheshimu sana Mzee Warioba, lakini si katika hili. Mzee Warioba bora awe muungana wa kwanza kukubali kuhusika na ufisadi huu.

Pesa ni tamu aise, hata hawa majaji!
 
Kuna uwezekano mkubwa kampuni ya Mwananchi ilianzishwa kwania nzuri kabisa ila
ninapata wakati mgumu kuamini na kuheshimu kile anachosema mzee Warioba kwasababu kuu tatu.

{1}Jaji Warioba alihusika kupitia kampuni yake kutoa ushauri wa kuanzisha mwananchi.Mpaka hapo sina tatizo na mzee wetu Warioba kwasababu hiyo ni kazi yake.

{2}Jaji Warioba akawa mwanahisa wa mwananchi Gold.Hapa kiwingu kinaanza,naomba kuelimishwa hivi ukitoa ushauri wa kisheria kwa kampuni unakuwa mwanahisa au hii imekaa vipi.

{3}Jaji Warioba anakuwa chairman wa board.Sijui nani alimteua au labda alikuwa na hisa nyingi !!!!.

Conclusion Jaji Warioba ni mtu analiyebobea katika fani ya sheria na alikuwa anajua nini anafanya.Ajiandae kwenda kisutu asiwaambie waandishi wa habari yuko tayari kwenda mahakamani hizo ni dalili za woga,kama kweli yuko safi asubiri siku ifike.
 
Warioba afichua siri nzito

• Aitaka serikali iharakishe kumpandisha kizimbani

na Happiness Katabazi
Tanzania Daima~Sauti ya Watu​

Aliwataja wanahisa wa Kampuni ya Mwananchi Trust, ambayo ipo ndani ya Mwananchi Gold Company Ltd kuwa ni Umoja Entertainment, VNB, WM Holding inayomilikiwa na Yusuph Mushi, na CCM Trust Company.

Alisema katika Kampuni ya Mwananchi Trust, aliyekuwa na hisa nyingi ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichokuwa na hisa 15.


Watanzania tungependa kufahamu ili kupata hisa za 15% toka Mwananchi, CCM ilitoa kiasi gani ili kuchangia mtaji wa kampuni hiyo?
 
Judge Warioba first says that Mwananchi Gold was the brainchild and is owned by the Government. Later on he says that CCM is the major shareholder!! Does the Judge expect us to believe that CCM and the Sirikali are the one and same thing? He needs to be reminded that the era of a one party state is long gone!

If indeed this company is Government owned, then the Controller and Auditor General should tell us that he has audited the accounts of Mwananchi Gold and as is the practice with other parastatals, these should be made public.
 
Mwanakijiji said:
a. Kampuni ya Nyalali, Warioba na Mahula (mmoja aliwahi kuwa Jaji Mkuu, mwingine Waziri Mkuu, na mwingine Balozi) inaweza vipi kufanya biashara na taasisi kama Benki Kuu bila kuwa na aina fulani ya insider information n.k? At that time ilikuwa ni muda gani tanu Nyalali atoke Ujaji Mkuu?

Mwanakijiji,

..Chief Justice Nyalali alifariki 2003.

..kwenye hiyo Law Firm ya kina Warioba, kama sijakosea, yuko Justice Lameck Mfalila[rtd].
 
Mashtaka yatakuwa kujiandikisha kama wao ni CCM Trust wakati CCM haikuwapa ruhusa hiyo. CCM kama ingetaka kuwa na hisa au trust wangeweza kufanya kwa namna tofauti. Aulizwe Makalla kama wanaitambua CCM Trust Company ya kina Warioba na Mushi. I bet my last nickel kwamba CCM watawaruka!

Kwa sababu sidhani kama watapata dondoo za kikao chochote kilichounda au kuidhinisha CCM trust kufanya kazi na Mwananchi Gold.

SISI EMU Ni NANI? Mi nafikiri sisi emu ni pamoja na sisi wananchi. Ikifika uchaguzi wananchi ndiyo sisi emu, kwenye masuala ya pesa na miradi inayohusu pesa na maliasili yetu "wana sisi emu" wanakuwa wachache tu 'MAFISADI'. Wanatutenga wananchi wakishapata kura (kula). Mengi tutayajua nayakati hizi za mwisho, ndiyo maana kila mtu anakimbilia/anangángánia huko SISI EMU hata kama ni kwa kukopa saudi arabia.

Wanajua kuwa huko kuna biashara wanazozifanya bila kuwa na mtaji!!! Wanakula mpaka wanapasuka kwa kunyonya damu za wananchi. Laana ya Mungu iwajae, na panga la moto litawakata na kuwachoma. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WALALA HOI.

NAOMBA WIMBO WA TAIFA UREKEBISHWE SASA HATUHITAJI KUWABARIKI VIONGOZI TENA!

Endeleeni kuleta nyanga hapa.
 

".... serikali ilikuja kwenye ofisi yetu ya uwakili ya Nyalali, Warioba & Mahalu Law Associates ili tuisaidie kuipatia huduma ya kisheria kabla na baada ya kuundwa kwa kampuni hiyo."

Nani alikuja kwenye ofisi yako, kivipi, ulichaguliwaje?

Ufisadi huwa unaanza asubuhi.

Wakina Mkono nao ilibidi waeleze walivyopata tenda ya BOT. Waziri Ngeleja juzi juzi nae akataka kwenda kujinunulisha mashine za Dowans bila kufuata tararibu za tenda kabla hawajamstopisha. Mramba-Mgonja-Yona axis of corruption nayo ilivunja taratibu za tenda. Huyu msomali wa Dowans aliyemalizwa jana Kisutu nae tunaambiwa alifoji affidavits katika procedure za kupata tenda. Railways nayo ilivyopewa wahindi wasiojulikana nayo hivyo hivyo, taratibu za tenda, sasa hivi tunaambiwa ATC na TAZARA wanataka kupewa sijui wachina gani sijui. Baadae tutaanza kulizana. Tenda, tenda, tenda, tenda!

PUBLIC PROCUREMENT ACT 2004-21
Sect 44 (1), 66 (1), 67 (4), 63 (1), 56 (1)


Duties of procuring entities

44.-(1) Notwithstanding anything to the contrary contained in any written law, where any expenditure is to be incurred on any procurement of goods, works or services, it shall be the duty in respect of a head of expenditure to ensure that such procurement of goods, works or services is in accordance with the procedures prescribed by or under this Act or Regulations.

66.-( 1 ) The tender board … shall receive tenders using procedures set out in the Regulations made under this Act.

67.-( 4) The procuring entity shall prepare a detailed report on the evaluation and comparison of tenders, setting out the specific reasons on which its recommendations for the award of each contract are based.

63.-( 1) The procuring entity shall use the appropriate standard model tender documents specified in the Regulations for the procurement in question…shall be worded so as to permit and encourage competition and such documents shall set forth clearly and precisely all the information necessary for a prospective tenderer...

Records, Information and Notices

56.-( 1 ) Each procuring entity and each approving authority shall maintain a record of procurement proceedings in which each is involved, including decisions taken and the reasons for it and such record shall be kept for a period of not less than five years
 
...
{1}Jaji Warioba alihusika kupitia kampuni yake kutoa ushauri wa kuanzisha mwananchi.Mpaka hapo sina tatizo na mzee wetu Warioba kwasababu hiyo ni kazi yake.
.......hata kwenye hiyo namba {1} bado Warioba ana maswali mengi ya kujibu:

  • kwanini tangu awali hakumshauri mteja wake (Serikali) achapishe nia yake ya kutumia kodi ya wananchi kupitia Government Gazzete?
  • kwanini alikaa kimya ilhali akijua Serikali, ambayo tayari ilishakana Azimio la Arusha kupitia lile la siri la Zanzibar, inajiingiza kwenye biashara pasipo ridhaa ya wananchi?
  • Kwanini hakuwa muungwana kuweka bayana upatikanaji wa hisa za kampuni hiyo ili wananchi na vyama vingine vya siasa wapate hisa (kama anadai "CCM Trust Company" ni mali ya SSM?
Kama tutakuwa makini tutampata mbaya wetu kupitia kauli hii ya Warioba. Hata kama Serikali ikikaa kimya Warioba anapaswa kufikishwa Kisutu ili tumjue mdudu anayeimaliza Tanzania.
 
Huyu mzee ni JAJI mstaafu na ndo alikuwa Attorney General wa Jamhuri yetu, Kitu kinachonifanya niamini kwamba huyu mzee sheria anaijua vyema. Sasa kweli tangu lini Serikali/Dola ikaenda kuomba ushauri wa kuanzisha kampuni/mradi kwa Kampuni binafsi? (Yes its possible but in very rare and extreme case). Mwanasheria mkuu wa serikali na wanasheria wake wanalipwa pesa ya nini? This is pure comedy. Sioni sababu zozote zile kwa nini serikali iende kuomba msaada kwenye private Law firm wakati kuna substantial amount ya hela ya walipa kodi iko involved ($5M). I dont see compelling facts/reasons. Kwa sababu hii ni legal advice pure!

Ok, Assume Law Firm ya Warioba ilikuwa consulted kama experts wa sheria (which I think is wrong though because we have Attorney General who is supposed to be the Legal Advisor wa serikali)..sasa ilikuwaje Warioba akawa mwanahisa kwenye hiyo kampuni? I dont get it! Na anasema kabisa kwamba BOT WALITUKOPESHA DOLA MILLION TANO! Hakuona conflcit of interests hapa?

Well, hapa ukiangalia vyema this was a dirty deal na nadhani Warioba anataka kuplay VICTIM CARD kwamba anaonewa na wabaya wake kisiasa... Lakini kama wengine walivyosema, deal za chini ya meza matokeo yake ndo hayo. Huyu mzee he was in a position to know better. Na katika siasa, kila mtu anaubeba mzigo wake. Sana sana BOT itakuwa on the spot na ofcourse the usual suspect Mkapa atakuwa involved kwenye hili deal.

Hii kesi itaibua mengi, kama mwanakijiji alivyosema..CCM wataruka! na ndo yatatoka maswali mengi kuliko majibu...
 
Kampuni za sheria ziko nyingi, warioba anapaswa kuelezea kwa nini wao walipewa kazi ambayo hawajaomba?

Hivi warioba anatuona sisi ni watoto wa kuwadanganya kuwa wao walifuatwa na ''serikali'' kupewa deal ambayo ni nzuri na hawajaiomba na wao wakaamini kuwa huo ni utaratibu wa kawaida na kila kitu kikafanyika legally? warioba acha politics za miaka ya sabini this is 2009.
 
Naona kuwa Waryoba yuko matatani kabisa, na sidhani kama atakwepa. Ninaanza kuelewa kwa nini alikuwa akitetea watu wasimsakame Mkapa. Inaelekea Mkapa alimgawia kitu hiki ili anyamaze asiendelee kupiga kelele kuhusu ile ripoti yake ya rushwa halafu akaibugia bila hata kunawa mikono. Mkapa alikuwa na namna ya kuwanyamazisha wanasiasa wa aina yake kama akina Mzindakaya, na nadhani alitumia njia hiyo hiyo kumnyamazisha huyu Waryoba, lakini sasa atakuwa amekalia makaa ya moto.

Najaribu kufikiri jinsi gani Bwana Nalaila Kiula, George Mlingwa na Bwana Stephen Wassira (mgomvi wake wa kisiasa kwa kiti cha Bunda) watakavyofurahi kumwona jamaa akipelekwa keko!!

maelezo yake yamejikanganya sana halafu mtu ukipitia rekodi zilizoko kuhusiana na sakata hilo ndipo unagundua kuwa Mzee yuko matatani. Iweje kweli serikali "iiombe" kampuni yake binafsi ya sheria "kusaidia" uanzishaji wa kampuni hiyo ambayo baadaye ilipewa fedha na benki kuu katika "utaratibu usio wa kisheria" na baadaye kampuni hiyo inayeyuka bila kulipa fedha za umma kinyume cha sheria?

Halafu basi baada ya serikali "kumwomba" atoe huo ushauri wa kisheria kuisaidia kampuni hiyo mpya, inakuwaje kampuni hiyo iliyoanzishwa kwa maelekezo ya serikali inakuwa na wabia ambao ni makampuni ya watu binafsi tu, na tena mwenyekiti wa bodi yake akiwa ni yeye huyo huyo Waryoba?

Maswali ya kutatanisha yanazidi kuwa mengi, ngoja mimi niwahi kiti pale kisutu kusudi niweze kumsikiliza mzee wa sheria akijitetea.
 
Naona kuwa Waryoba yuko matatani kabisa, na sidhani kama atakwepa. Ninaanza kuelewa kwa nini alikuwa akitetea watu wasimsakame Mkapa. Inaelekea Mkapa alimgawia kitu hiki ili anyamaze asiendelee kupiga kelele kuhusu ile ripoti yake ya rushwa halafu akaibugia bila hata kunawa mikono. Mkapa alikuwa na namna ya kuwanyamazisha wanasiasa wa aina yake kama akina Mzindakaya, na nadhani alitumia njia hiyo hiyo kumnyamazisha huyu Waryoba, lakini sasa atakuwa amekalia makaa ya moto.

Najaribu kufikiri jinsi gani Bwana Nalaila Kiula, George Mlingwa na Bwana Stephen Wassira (mgomvi wake wa kisiasa kwa kiti cha Bunda) watakavyofurahi kumwona jamaa akipelekwa keko!!

maelezo yake yamejikanganya sana halafu mtu ukipitia rekodi zilizoko kuhusiana na sakata hilo ndipo unagundua kuwa Mzee yuko matatani. Iweje kweli serikali "iiombe" kampuni yake binafsi ya sheria "kusaidia" uanzishaji wa kampuni hiyo ambayo baadaye ilipewa fedha na benki kuu katika "utaratibu usio wa kisheria" na baadaye kampuni hiyo inayeyuka bila kulipa fedha za umma kinyume cha sheria?

Halafu basi baada ya serikali "kumwomba" atoe huo ushauri wa kisheria kuisaidia kampuni hiyo mpya, inakuwaje kampuni hiyo iliyoanzishwa kwa maelekezo ya serikali inakuwa na wabia ambao ni makampuni ya watu binafsi tu, na tena mwenyekiti wa bodi yake akiwa ni yeye huyo huyo Waryoba?

Maswali ya kutatanisha yanazidi kuwa mengi, ngoja mimi niwahi kiti pale kisutu kusudi niweze kumsikiliza mzee wa sheria akijitetea.

Warioba?? former prime minister? mwanasheria mahiri?

Si mramba huyu au Yona, pia sijaona bado alipojichanganya wapi, labda nisaidie!
 
Warioba?? former prime minister? mwanasheria mahiri?

Si mramba huyu au Yona, pia sijaona bado alipojichanganya wapi, labda nisaidie!

Waberoya,
Hata mie nimeanza kusoma nilikuwa sijui lolote. Ila nilianzia ukurasa wa kwanza na hadi kufika mwisho, nimeshaelewa kila kitu. NA WEWE NENDA UKAFANYE HIVYO. Vinginevyo, basi unaona kile tu unataka wewe ukione. Mzee kweli maji ya shingo. Mwanzo nilifikiri akina Mtanzania wanadanganya juu ya huyu Mzee.

Ila sasa nimeelewa na kwa kweli siasa kitu kibaya. Mkapa kalisha watu wengi sumu na ukichunguza sana, utagundua kuwa kuanzia juu hadi wabunge wetu, walikula ASALI hiyo ya mti wa kati.

Mtanzania nakubali sasa maneno yako. USIMWAMINI MWANASIASA.
 
- Hakuna jipya hapa sisi tumeyasema sana hapa kwamba huyu mzee ni another fisadi, sasa anajaribu kuwatisha serikali wait and see watakavyomfumulia mambo yake, yaani aibu tupu huyu ni fisadi tu hivi hiyo kampuni yao ya sheria ilikuwa ni lazima ianzishwe na Waziri Mkuu Mstaafu, Mwanasheria Mkuu Mstaafu, na Balozi wetu Italy ambaye ni rafiki wa karibu wa rais wetu Mkapa?

- Ni wanasheria wangapi Tanzania toka tupate uhuru wanaweza kusimama mbele ya public na kutuambia kua serikali iliwahi kwenda kwenye ofisi zao na kuomba msaada? What a nonesense? Haoni hata aibu kusema haya! Wanasheria wote tulionao serikalini ambao wamesoma mpaka mwisho wa elimu hawafai ila yeye Mahalu na Nyalali ndio waliokuwa wanafaa? Warioba amewahi kusimamia kesi ngapi kwenye mahakama zetu toka awe mwanasheria wa kujitegemea? Au nyalali aliwahi kusimamia kesi gani ya wezi wa kuku na mbuzi? au Mahalu ni lini aliwahi kusimamia kesi yoyote kwenye mahakama zetu? Hilo shirika wanaliendesha kwa hela kutoka wapi?

- Usafi wa Warioba unatokea wapi? Ni nani aliyekua akimlipia Wassira kusoma kule USA ili asirudi kumsumbua Warioba kwenye jimbo lake la ubunge?, wakati Warioba akiwa waziri mkuu? Kwa nini hawa viongozi wanapenda kutuchezea wananchi? Hivi Warioba kweli anaamini kuwa wanasheria wa serikali yetu ni wajinga kwamba wanaweza kumzushia kesi bila sababu huku wakijua wazi kwamba ni mtafutaji wa cheap popularity? Kama kweli sio fisadi kwa nini alipoona tu Mramba na Yona wako Kisutu, akaanza kuwapigia simu viongozi wanaohusika na sheria na kuanza kuwatukana kua hiyo kamata kamata wanawatisha viongozi kutoifanyia kazi nzuri serikali? Haya ni maneno ya kusemwa na Warioba, asiye fisadi? Na ambaye amekua akilia sana kuwa rushwa imezidi? Yeye ni msafi sasa leo wanakamatwa viongozi mafisadi halafu anatishia viongozi na maneno ya hovyo hovyo, WHY?

- Warioba anyamaze asubiri tu zamu yake ifike atinge Kisutu kama inakuja, lakini asitishie nyau serikali, I mean ninawaomba serikali yetu kutojiingiza kabisa na huu mtego wa Warioba wa kutaka kuigeuza sheria kua siasa, that is all he is trying to do sasa dawa ni serikali kuendelea na kazi yake kama kawaida bila kumjali na siku ikifika atinge tu Kisutu, lakini asilete ngebe, huyu Warioba si ndie aliyehesabu kura za mazishi zilizompa urais Mkapa mwaka 1995, leo anaweza kusimama mbele ya public na kutuambia kua matokeo aliyoyatangaza baada ya kuhesabu zile kura na kumpa urais Mkapa over Kikwete yalikua ni ya kweli? Hana hata aibu dhahabu inachimbwa wapi halafu yeye anashauri ikasafishiwe wapi eti?

Hivi kwa nini amekua akihangaika sana toka Mramba na Yona watinge Kisutu? WHY? Serikali haina sababu ya kumjibu, wamalize uchunguzi wao kama kuna kesi atinge tu, sio yeye tu kiongozi yoyote yule, wa sasa au zamani kusiwe na msamaha wala huruma,

Warioba anajaribu kudanganya toto hapa kwamba hatujui kuwa ukiona moshi maana yake chini kuna nini? Tena huyu inaonekana kuwa anajua mengi sana, ikibidi apewe immunity kwa masharti kwamba aseme yote anayoyajua, lakini muamuzi wa mwisho tutakuwa ni sisi wananchi sio yeye!

Finally, inaonyesha serikali iko kwenye the right track na hawa mafisadi, sasa hivi utawasikia na wegine, ingawa huyu Warioba anastahili sifa kidogo kwa kutokimbilia kupiga kelele jimboni, lakini serikali ikamate hapo hapo mpaka kieleweke!
 
Back
Top Bottom