HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,566
Wana MMU, Heri ya Mwaka Mpya 2012!
Nimepata msukumo wa ndani ya Moyo wangu kuwaandikia waraka huu, kwa upendo mwingi sana, ninyi ndugu na rafiki zangu wakubwa wa MMU nikiwashukuru kwa ushauri na ushirikiano mkubwa mliouonyesha kwa mwaka huo tulioupoteza wa 2011.
Binafsi kuingia 2012 kwangu naona kama miujiza mikubwa sana. Leo hii nilikuwa nikitafakari ndugu kadhaa ambao TUMEWAACHA ktk mwaka uliopita. Ni siku chache tu tumewapoteza watangazaji Halima na John Ngayhoma. Siku kadhaa nyuma tuliwapoteza ndg zetu wengi kutoka Zanzibar kwa ajali ya Kuzama Meli. Wapo waliobaki mwaka 2011 kwa vifo vya kikatili mno kama walioteketea kwa moto kwa ajali ya basi huko chalinze! Wapo waliopoteza maisha kwa ajali mbaya za Pikipiki za kupondwa vichwa vyao! Wapo waliobaki mwaka 2011 kwa vifo vy ajali za gari na kukatwa vipande vipande kiasi cha kushindwa kutambulika. Wapo waliobaki kwa vifo vya wenzao kujilipua kwa kujitoa Mhanga. Pia wapo waliomezwa na mafuriko na wakafa vifo vibaya kabisa vya kunywa maji machafu mpaka kifo. Vita na maandamo ya kupinga watawala dhalimu iliwabakiza wengi! Magonjwa nayo hayakubaki nyuma! Vipo vikundi vya nyimbo na burudani ambavyo pia vilibaki kwa namna mbaya ya ajali isiyoelezeka!
Siwezi kutaja kila janga na namna ambavyo wenzetu wameshindwa kuingia 2012, lakini tujiulize sisi ni nani mpaka tupate neema hii ya kuuona mwaka huu mpya? Au tumefanya jambo gani zuri la kutubakiza kwa mwaka 2012? Hebu tafakari, na mshukuru Mungu wako aliyekulinda na mabaya yote ya 2011 na kukupa neema ya kuingia 2012!
Kipindi hiki cha kuanza mwaka mpya ni kizuri sana kutafakali yale ambayo uliyapanga mwaka uliopita ukashindwa kuyatekeleza. Kwa sasa chukua muda huu, kupanga malengo yako mapya na jitahidi kuhakikisha mwaka huu unamudu kuyatimiza, uliyoyapanga mwaka huu na yale yaliyosalia ya mwaka jana.
Waliobahatika kupata ndoa mwaka 2011, mzilinde ndoa zenu. Jiepusheni na watu wanaojifanya kuwapenda angali mna ndoa, hao ni hatari kwa maisha yenu ya sasa na baadaye, waogope kama ukoma. Kamwe msijihushishe na mambo ya kukumbushia enzi na wale wa zamani, mtaumia. Kataeni aina zote za mahusiano machafu na yale yasiyo halali, muogopeni Mungu.
Kwa wale mliopoteza ndoa zenu au wapenzi wenu, poleni sana. Nawaombea Mungu ayaponye majeraha yenu mliyopewa na wenzi wenu. Nawashauri kutulia, mkiyasahau yale ya 2011 na kuanza maisha mapya 2012. Naamini ukimtegemea Mungu, iko siku utampata wa kukufaa maisha yako yote.
Najisikia kuwashauri wale wote wanaofanya kazi, tujipange mwaka huu tufanye kazi kwa bidii. Wanafanyabiashara, Wakulima na waliojiajiri kwa namna yeyote ile tukaze buti, tuweze kuyatimiza malengo yetu.
Kwa wenye familia tukumbuke kuzitunza familia zetu kwa upendo mwingi. Tukumbuke kwenda kwenye ibada mara kwa mara kumuomba Mungu atulinde na kutukinga na mabalaa ya aina zote.
Niwatakie kila namna ya mafaniko katika mwaka huu Mpya. Upendo na amani vitawale maisha yako. Mikosi ya aina zote, ajali, magonjwa, kuchukiwa bila sababu, roho ya uvivu na mateso ya namna zote yakuepuke.
Happy New Year,