Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 21,248
- 36,301
Habari ya muda huu popote pale ulipo wana jamvi.
Kama ulipo haijadondoka tarehe 25/12/2023 basi endelea kuvuta subira itafika tuu punde si punde.
Ni sikukuu leo ya kuadhimisha kukumbuka kuzaliwa kwa Kiongozi wa waumini wa dini ya Kikristo.
Heri ya Sikukuu na Maandalizi ya Mwaka Mpya 2024.
Mpendwa, kama hadi muda huu hujajua sikukuu inaendaje usipate msongo wa mawazo. Shukuru kwa uzima na afya uliyonayo, siku itapita na maisha yataendelea.
Imezoeleka sikukuu ni siku ya kula chakula kizuri, uvae nguo mpya, ukatembee mahala ambapo mtafurahia mandhari na chakula na vinywaji kishe mrejee nyumbani kulala au wengine kulala hukohuko, ama ualike wageni waje kula na kunywa au ualikwe mahala...
Ndugu, kama hukufanikiwa kusafiri, hukufanikiwa kuwa na gari jipya, hukufanikiwa kuwapa familia yako nguo mpya au mlo maalum (pilau nyama) wa sikukuu basi....
Kaa na familia yako mjadiliane kwa amani na upendo namna gani mnavuka mwaka mpya.
Inapendeza ukiwa na mahitaji yote hayo ila si lazima, ukipata sawa ila ukikosa basi usikumbatue huzuni.
Furahini katika Bwana tena Nasema Furahini....
Kila mwenye furaha ashiriki furaha yake na asiye nayo.
Sina mpangilio mzuri wa nini nataka kusema ila ikiwa huu ujumbe umekulenga. Amka, kaoge, kamshukuru Mungu, andaa kile ulichonacho jikoni basi furahi na nafsi, ndugu jamaa au marafiki walio karibu nawe hata kwa simu tuu.
Wale wanaopitia changamoto za ugonjwa, misiba, kesi mahakamani, polisi, nawaombea mpate ahueni.
Ntatupia picha baadae ya kile nilichobarikiwa nacho.
Kasinde Matata 🙂.