Waraka wangu kwa JWTZ, Watanzania

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
2,436
4,429
Mniwie radhi kwa urefu wa makala hii, lakini nimeona ni muhimu wakati huu ambao Rwanda, Burundi na Kenya wanapoelekea kutufanya sisi mazuzu. Naomba wana JF mchangie bila jazba.

Safari hii ya Goma ihitimishiwe Kigali

Na Manyerere Jackton, JAMHURI

Meja Khatibu Mshindo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), amekufa katika mapambano nchini DRC. Amekufa kishujaa.

Amekufa akitekeleza maelekezo halali ya Umoja wa Mataifa (UN) yanayolenga kuwafanya wananchi wa Mashariki mwa DRC waonje tunu ya amani.
Kifo cha kamanda huyu kinapaswa kiwe chachu kwa Watanzania na wapenda amani katika Afrika na duniani kote.
Watanzania tuna historia iliyotukuka ya ukombozi wa wanyonge sehemu mbalimbali duniani. Ndugu zetu wa Msumbiji, Angola, Afrika Kusini, Namibia, Comoro, Ushelisheli, Angola na kwingineko wanatambua hilo. Bila kujali umasikini wetu, tulijitoa kwa hali na mali kuhakikisha wanyonge katika mataifa hayo tunawakomboa. Wakati tukihaha kutekeleza dhima hiyo ya kiutu, hatukujali kuachwa nyuma kimaendeleo na majirani zetu kama Kenya au Malawi ambao hawakuhangaika kwa namna yoyote.

Kifo cha Kamanda Mshindo kinapaswa kiwe chachu kwa wapiganaji na makamanda wa JWTZ katika kuhakikisha wananchi wa DRC wanapata amani, wanafaidi matunda ya uhuru, na utajiri wao unabaki kuwanufaisha wao kwanza.

Tumempoteza Mtanzania mwenzetu katika vita ambayo mwasisi wake ni Rais Paul Kagame wa Rwanda. Huyu ni mpenda vita, na ndiyo chimbuko la kundi la waasi wa Kihutu la FDLR. Hili ni matokeo ya ubabe wake alipoamua kushiriki kuwaua Rais Juvenal Habyarimana na mwenzake wa Burundi, Cyprien Ntaryamira. Aprili 6, 1994 ndege iliyokuwa imewabeba viongozi hao kutoka nchini Tanzania ilipigwa kombora wakati ikijiandaa kutua katika uwanja wa ndege wa Kigali, Rwanda.
Pamoja na marais hao, wengine waliouawa kwenye shambulizi hilo ni Bernard Ciza (Waziri wa Ujenzi wa Burundi), Cyriaque Simbizi, (Waziri wa Mawasiliano wa Burundi, Jenerali Deogratias Nsabimana (Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda), Meja Thaddée Bagaragaza (Msaidizi wa Rais wa Rwanda-masuala ya kijeshi), Kanali Elie Sagatwa (Mjumbe wa Sekretarieti ya Rais wa Rwanda), Juvénal Renaho (Mshauri wa Rais wa Rwanda wa Masuala ya Kigeni), na Emmanuel Akingeneye ambaye alikuwa Daktari wa Rais wa Rwanda.
Wana anga watatu, raia wa Ufaransa nao waliuawa. Nao ni Jacky Héraud (rubani), Jean-Pierre Minoberry (rubani mwenza) Jean-Michel Perrine (mhandisi wa ndege).
Damu ya watu hawa inamsumbua Rais Kagame.
Taarifa mbalimbali kutoka pande mbalimbali duniani zinamweka mbele kwenye orodha ya waliohusika kwenye mauaji hayo ambayo baadaye yalisababisha kile kilichokuja kujulikana kama mauaji ya kimbari.

Dola ya Bahima

Watanzania tuna sababu zote za kupigana vita ndani ya DRC. Hii ndiyo njia pekee sahihi ya kuvuruga mkakati wa Rais Kagame na rafiki yake, Rais Yoweri Museveni wa Uganda wa kuanzisha Dola ya Bahima. Hii ni dola ya watu wa kabila la Watutsi.
Marais hawa wanaamini Bahima inapaswa kusambaa Rwanda, Burundi, Uganda, sehemu za Tanzania na katika DRC. Tukiwaruhusu waimege DRC, nasi Tanzania tukae mkao wa kunyolewa! Hapa tunapaswa kutambua kuwa kwa huruma yetu tuliwakaribisha maelfu ya wakimbizi wa Kitutsi. Hawa wanajua mengi ya Tanzania. Haitashangaza siku moja wakijiunga na kuanzisha vita kwa madai ya kutaka watambuliwe. Tumeyaona juzi baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwaamuru wahamiaji haramu warejee kwao.

Kumetolewa maneno mengi ya vitisho na lawama, kana kwamba ni halali kwa mtu kuishi katika nchi nyingine bila kufuata taratibu. Waliingia nchini mwetu wakiwa na mifugo mingi. Wakajitwalia maeneo makubwa kwa nguvu na kwa hila. Wakawaua wananchi wetu. Wakachoma nyumba na mashamba ya wenyeji. Kama wameweza kufanya hivyo sasa, watashindwa nini hapo baadaye kudai Karagwe na Ngara kuwa ni yao? Tuwe macho sana.

Rais Kagame alihakikisha anaingiza nchi yake kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki, si kwa kutafuta kitu kingine, bali nguvu za kisiasa.

Chokochoko zake zimepamba moto baada ya ushauri wa Rais Kikwete wa kumtaka aketi na waasi ili wamalize tofauti zao kwa mazungumzo. Alichofanya Rais Kikwete ni kutoa ushauri, na si kumshurutisha! Kejeli, matusi na dharau vilivyotolewa baada ya kauli ya Rais Kikwete, vinaashiria kuwa kuna jambo kubwa zaidi ya hilo la kuchukizwa na ushauri aliompa.
Zipo sababu nyingi zinazomfanya Rais Kagame awe mbogo. Nitajaribu kuziainisha hapa kwa ufupi tu. Mosi, Tanzania tunakubalika sana kimataifa. Kwenye diplomasia tumeiacha mbali Rwanda. Hili linamuudhi sana kwani anaamini yeye ni bora na maarufu zaidi.

Kitendo cha Rais Barack Obama wa Marekani kuja Tanzania na kuziacha Rwanda, Uganda na hata Kenya kimewaudhi, na kwa kweli tunaweza kusema hii imekuwa nguzo imara iliyoibua mshikamano na mapenzi ya ghafla miongoni mwao. Rwanda ikijiona kuwa ndiyo nchi inayoinukia kiuchumi kwa kasi, ilidhani ina sifa zote za kuiwezesha kutembelewa na Rais Obama. Uganda ambayo ilikuwa mshirika mkuu wa Marekani, inaona Tanzania imechukua nafasi yake. Imeingiwa wivu! Kenya ambayo inaamini Obama ni wao kwa sababu babake ni Mkenya, imechukizwa kuona ikipigwa kumbo na Tanzania. Hawa watatu-Kagame, Museveni na Kenyatta-wameungana kuichukia Tanzania kwa sababu tu ya kumkosa Obama.

Pili, kinachomsumbua Rais Kagame na washirika wake ni uamuzi wa Tanzania wa kutaka Shirikisho la Kisiasa la nchi wanachama wa EAC liende hatua kwa hatua. Msimamo wa Tanzania umekuwa kwamba maoni ya wananchi ni muhimu mno kabla ya kuchukua uamuzi wowote. Kwao, Tanzania ndiyo kikwazo cha kuwa na serikali moja ya EAC. Hapa ni vema Watanzania wakakumbuka namna Rais Museveni alivyokuwa amejiandaa kuwa Rais wa Kwanza wa Shirikisho la Afrika Mashariki. Sidhani kama ameshaufuta mpango huo.

Baada ya kuona Tanzania tukitaka jambo hili liende hatua kwa hatua, watatu hawa wameungana sasa kutaka shirikisho lao la kisiasa, huku wakiiacha nje Tanzania na Burundi. Wanajidanganya bure. Lakini hapana sababu ya kulumbana nao. Kama wanataka kuanzisha, waanzishe tu. Hakuna haja ya ugomvi. Wakianzisha kutakuwa na nchi mbili-hiyo ya Shirikisho, na Tanzania kwa upande mwingine.

Hapa ni vema kwanza tukatambua kuwa Tanzania ni nchi kubwa. Ukichukua Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya, ukaziweka pamoja, bado ni ndogo kwa Tanzania. Hatuna sababu ya kuogopa.

Tatu, hawa jamaa kiu yao kubwa kabisa ni ardhi ya Tanzania. Ukiacha tamaa ya kutaka kuitawala kanda yote hii, kiu yao ya kweli ni ardhi ya Tanzania. Wamepambana kwa hali na mali kuhakikisha kuwa ardhi inakuwa moja ya mambo kwenye shirikisho. Wanataka Mkenya, Mganda, Mnyarwanda na mwanachama mwingine yeyote, akitaka kuingia Tanzania, basi apewe uraia wa kudumu na apata ardhi bila masharti!

Hoja yetu imekuwa kwamba wao wakija Tanzania watapata ardhi, je, Mtanzania akienda Rwanda au Kenya au Uganda ataipata? Chao chao, chetu chetu sote. Wao hawana mita ya mraba ya ardhi iliyo wazi kwa hiyo wanajua mlengwa na wa kuumizwa hapa ni Tanzania tu. Uroho wao wote ni ardhi ya Tanzania. Hilo tumeapa kuwa haliwezekani. Kama haliwezekani kwa ndugu wa tumbo moja, seuze kwa nchi na nchi? Tukianzisha shirikisho tutapeana nini? Hilo ndilo jambo wanalopaswa kutujibu kwanza. Janja ya kuja kuoa au kuolewa Tanzania haitawasaidia.

Wanachofanya sasa kinatokana na hasira tu

Shirikisho la Rwanda, Uganda na Kenya likianzishwa haliwezi kudumu. Watagombana tu. Rwanda watataka walitawale shirikisho. Hicho ndicho wanachokitafuta. Wakenya hawasumbuliwi na kingine, isipokuwa biashara. Wameingia kwenye mkakati huu kwa sababu wanadhani bandari ya Mombasa inaweza isiwe na maana endapo Rwanda, Uganda na Burundi wataamua kutumia bandari za Tanga na Dar es Salaam; na hiyo nyingine inayojengwa Bagamoyo. Bado ukweli unabaki kwamba kutoka Dar es Salaam hadi katika nchi za Rwanda na Burundi ni karibu mno kuliko kuanzia Mombasa.
Katika mpango huu sidhani kama Burundi itakubaliana nao. Burundi kuwa karibu na Tanzania kuna manufaa makubwa zaidi kwake kuliko kuwa karibu na hayo mafiga matatu.
Harakati hizi zote zinachochewa na Rwanda, na hapa ndipo ninapokuja na sababu ya nne ya Tanzania kuchukiwa. Rais Kagame amechukia mno kuona majeshi ya Tanzania yakiongoza mapambano ya kuwang'oa M23 ambao ni Wanyarwanda. Kwa miaka yote DRC imekuwa shamba la Rwanda. Kagame ameongoza harakati za kuliibia taifa hilo bila huruma. Ameanzisha vita ili amani isiwepo. Anajua DRC ikitawalika, hatapata mwanya wa kwenda kupora rasilimali, hasa madini. Kwa sasa adui yake mkubwa ni Rais Kikwete na Tanzania kwa sababu tunaziba njia yake haramu ya uchumi.

Kuachwa kwetu solemba EAC

Sioni kwanini tusianzishe Jumuiya yetu kwa kuwakaribisha DRC na Burundi. Sisi ni taifa kubwa. DRC ni taifa kubwa pia. DRC na Tanzania tuna rasilimali nyingi mno. Faida za kujitoa EAC ni kubwa kwetu kuliko kuendelea kuhangaika na hawa wapenda vita. Tuwaache waanzishe yao, na sisi tuanzishe yetu. La, hilo kama haliwezekani, tujikite zaidi SADC ambako kuna soko pana kuliko EAC.
Tukijitoa EAC atakayeumia zaidi ni Kenya maana bidhaa na uwekezaji wake mkubwa kauelekeza Tanzania. Soko lake kubwa lipo Tanzania. Wanajidanganya tu.

Tusiendelee kuwabembeleza watu wasiokuwa na shukrani. Tuwatakie heri katika ndoa yao hii mpya ambayo sioni uhai wake. Hizi ni hasira za mkizi ambazo mara zote humnufaisha mvuvi. SADC ni bora zaidi. Tupeleke nguvu zetu kwenye SADC.

Kagame na Museveni walisaidiana kuichukua Uganda. Museveni alimsaidia Kagame kuitawala Rwanda. Sasa wanasaidiana wachukue sehemu ya DRC. Museveni anamsaidia Kagame katika hili. Tutambue kuwa inayofuata ni Tanzania. Si ajabu wale Wanyarwanda waliokuja siku nyingi sasa wakadai wanabaguliwa, na kwa sababu hiyo wakaanzisha vita ya kutaka kutambuliwa au kujitenga na kuwa sehemu ya Rwanda na Uganda (Bahima Empire).

Njia pekee ya kumwondoa Rais Kagame ni hii aliyotusaidia kuiweka, yaani vita. Kuichokoza Tanzania ni njia ya kuelekea ukingoni mwa utawala wake. Amepigana kwa muda mrefu na wasiojua vita. Amejaribu kuitisha Tanzania akidhani atafanikiwa. Kinachotakiwa sasa ni kumwonyesha kazi. Safari iliyoanzia Goma inastahiki ihitimishiwe Kigali. Kama kasahau, arejee kwenye historia ili ajue kilichompata nduli Iddi Amin Dadaa. Buriani Kamanda Khatibu Mshindo.

manyerere@hotmail.com
 
Manyerere anazungumzia Dola ya Bahima wakati hajui hata hilo kabila ni akina nani!

Masikini mwandishi mjinga. Hajui kuwa propagandists wa hii dola walikuwa wanamwingiza hata Baba wa Taifa Nyerere kuwa yeye ndo kinara anaowatumia vijana wake Museveni na Kagame, sasa na wewe unadandia treni usiojua inakokwenda.

Sipendi kuona mwandishi makini anaandika upuuzi, sipendi kabisa. Nilidhani upuuzi unaandikwa na akina Mtikila au wanaotoa comment humu ambao ni watu tu wa kawaida, hata Manyerere? aliyelelewa na kula nafaka kwa Nyerere? Jamani, uandishi Tanzania unaelekea kubaya.

Manyerere ingia google, tafuta Tutsi, then Hima, then Bairu, then Hutu... then utajua tofauti. Kuhusu vita kuhitimishwa Kigali, nadhani Manyerere amevurugikiwa akiri. Vita Enzi hizi ambazo watu wanaangalia uchumi na kushirikiana?

Ona sasa unazungumzia kuingia EAC ikiwa ni mkakati wa Himaya, huoni Kenyatta ana take advantage ya matatizo yetu kujinufaisha? Wakati tunapiga kelele za empire, kupeleka majeshi kuwasaidi wacheza ndombolo, Kenyatta anazindua bandari na kuweka mpango wa kuhakikisha inatumiwa. We upo tu kwenye Hima empire.

Na hujui kuwa ili upigane vita Enzi hizi lazima ui-convice UN, Marekani, etc. Hujui kuwa Congo iko vile kwasababu kuna dola dhaifu, na kuna utamaduni wa uasi tangu Enzi za Mobutu? Sasa unaleta hadithi za Hima empire hapa, kweli nimekudharau, you are an empty basket.
 
"Waliingia nchini mwetu wakiwa na mifugo mingi. Wakajitwalia maeneo makubwa kwa nguvu na kwa hila. Wakawaua wananchi wetu. Wakachoma nyumba na mashamba ya wenyeji. Kama wameweza kufanya hivyo sasa, watashindwa nini hapo baadaye kudai Karagwe na Ngara kuwa ni yao? Tuwe macho sana,"
Manyerere,

Kweli una mawazo ya al-qiada. kweli kuna mfugaji ambaye amewahi kuchoma nyumba na mashamba? huu ni uchochezi kabisa, uliza mtu yeyote kutoka Kagera, hawa watu wanaishi kwa kuliwa. Wanaliwa na police, immigration, idara ya wanyamapori burigi, nk. Walikuja kwasababu kwao hakuna ardhi, huo ndo ukweli, wakati mipaka inawekwa walipewa ardhi kidogo, basi.

Lakini usieneze chuki eti wanachoma mashamba, etc, nenda kafanye utafiti ache jaziba, na usilifanye gazeti lako kuwa la itikadi la ki-nazi, we ni mwandishi wa habari una wajibu wa wananchi, wasomaji na kuleta utengamano wa kijamii na maendeleo sio kuchochea chuki, make makala yako imejaa jazba sana
 
Ruta, wapo wale wanaosoma neno moja kwenye biblia na kutoa tafsiri. Mara nyingi hao hupotosha. Nadhani soma maudhui yote, kisha utoe mchango wako. Raha ya JF ni mahali pa kupeana elimu, na si pa kutukanana, kukejeliana au kukashifiana. Watanzania tuna tabia nzuri za kujadili hoja kwa hoja. Ningependa tujikite zaidi hapo kwenye hoja. Haya ya Bahima yanasemwa, na si ya kupuuzwa.
 
Burundi unamwonea kumweka kwenye mpango huo. Burundi ya sasa haiko mbali na Tanzania. Hata hivyo ni bora vilevile tuboreshe miundo mbinu yetu ya bandari na vinavyoiunganisha hasa reli kuliko kuendelea kuamini tu kuwa hawa watu hawatakwenda Mombasa kwa sababu ya umbali! Tunaimba muno kwa kujiaminisha badala ya kutenda.
 
Manyerere leo nikupongeze kwa kuwa mwazi na kuacha uoga kama waandishi wengine walivyo waoga hasa wa IPP Media ambao kama vile wamerogwa kila siku kututangazia porojo za Rwanda ambazo hatuzitaki...! Ni vizuri pia na TFF wakapeleka CECAFA barua kutaka like kombe la ubingwa wa kanda kuwa Kombe la CECAFA sio kuita kombe la kagame....! Huyu jamaa ni Kagame na kagenge chake cha wahuni ni washenzi na dawa ya mshenzi ni kumminya p.u.m.b.u tu...! Kwa mtazamo wangu tatizo sio Watutsi bali tatizo ni Kagame na kagenge chake cha wahuni wasiozidi 2,000 wakiongozwa na hawa akina Kabarebe, Jack Nziza, Karake n.k....! As per your wishes kwamba safari ya Kivu iishie Kigali, hilo pia nami nimelisema mara nyingi hapa JF....inshallah tutakunywa chai Kigali....April 2014 mbali sana!
 
Manyerere, nilikuwa napenda sana kusoma makala yako Rai, na nilikuwa nakuona mwandishi mahiri sana, nilikupenda, ila leo ume-ni disappoint, najua hapa utapata kudos nyingi kwasababu ya aina ya watu wanaojadili mijadala hapa, lakini sikutegemea kuwa mwandishi wa hadhi yako achochee vita na nchi jirani, hii haipo duniani mwandishi wa habari kuchochea vita waziwazi, fanya utafiti. Kisha unakuja na himaya ideology, hii nimeifanyia utafiti na nita-post walaka original ambao umekuwa ukitumiwa kueneza hii campaign
Ruta, wapo wale wanaosoma neno moja kwenye biblia na kutoa tafsiri. Mara nyingi hao hupotosha. Nadhani soma maudhui yote, kisha utoe mchango wako. Raha ya JF ni mahali pa kupeana elimu, na si pa kutukanana, kukejeliana au kukashifiana. Watanzania tuna tabia nzuri za kujadili hoja kwa hoja. Ningependa tujikite zaidi hapo kwenye hoja. Haya ya Bahima yanasemwa, na si ya kupuuzwa.
 
Rudini nyumbani kwenu wanyarwanda, hamuwezi kuishi na majirani zenu vizuri.
Umepewa hifadhi kesho unasema hapa ni kwangu siondoki unaanza kupiga, kuuwa wenyeji na kudai Goma mara Kivu ni ya kwetu, mbona kila nchi inaheshimu mipaka iliyowekwa na wakoloni weupe??
Nchi yako ndogo ukitoka kwenda kutafuta hifadhi kwingineko nenda ila ufikapo huko nchi ya watu kaa kwa heshima na utii kwa kufuata sheria na tamaduni za ile nchi otherwise ndiyo haya yanawakuta, rudini kwenye hicho kibiriti chenu mbanane hapo muuwane vizuri sana siku mkipata akili mtasema wenyewe kwamba sasa tumekua.
 
Na hujui kuwa ili upigane vita Enzi hizi lazima ui-convice UN, Marekani, etc. Hujui kuwa Congo iko vile kwasababu kuna dola dhaifu, na kuna utamaduni wa uasi tangu Enzi za Mobutu? Sasa unaleta hadithi za Hima empire hapa, kweli nimekudharau, you are an empty basket.

Ni upuuzi kudhani kuwa wananchi wa Congo waendelee kuteseka na majirani zake hasa Tanzania tuendelee kubebe mzigo wa wakimbizi kisa ni Rwanda.......! UN na SADC zimesema sasa basi...! Hiyo convincing unayoona wewe kuwa haijafanyika ni kujidanganya, intervention brigade ina mandate ya kumtwanga RDF kwanza kwa kupitia proxy force yake ya M23 then akishambulia FIB, tunavuka mpaka kupitia Kagera na South Kivu...! Membe ameshatoa onyo kwa UNSC majuzi...!

Inshallah with JWTZ tutakunywa chai Kigali....!
 
Manyerere, nilikuwa napenda sana kusoma makala yako Rai, na nilikuwa nakuona mwandishi mahiri sana, nilikupenda, ila leo ume-ni disappoint, najua hapa utapata kudos nyingi kwasababu ya aina ya watu wanaojadili mijadala hapa, lakini sikutegemea kuwa mwandishi wa hadhi yako achochee vita na nchi jirani, hii haipo duniani mwandishi wa habari kuchochea vita waziwazi, fanya utafiti. Kisha unakuja na himaya ideology, hii nimeifanyia utafiti na nita-post walaka original ambao umekuwa ukitumiwa kueneza hii campaign


Ruta, unadhani tutakubaliana kwa mambo yote? Haiwezekani. Yapo mawili, matatu tutatofautiana. Wakati mwingine Kagame na rafiki zake watambue kuwa nasi ni Taifa huru tunaostahili heshima na utu. Atambue kuwa vurugu anazofanya DRC kwa ajili ya kupora madini hazikubaliwi na walimwengu wote. Kama una huruma, anza kuwahurumia mamilioni ya binadamu wanaotesema Mashariki mwa DRC kwa baraka za Kagame. Wala usikasirike ndugu yangu. Huu ni mjadala. Tunapeana mawazo. Unaweza kushinda kwa hoja yako ya kutaka mwafaka wa mazungumzo. Wengine tunaona kichapo kwa hawa M23 ambao ni uzao wa Kagame, ni muhimu zaidi. Tuendelee kubadilishana mawazo.
 
Wananchi tuna maisha magumu sana hatuitaji vita na mleta mada umeongea vita vya msingi lakini unakosea unapo sema tumalizie kigal ujue majeshi wengi wanakufa huko bila sisi kujua coz vita havichagui huyu mganda au mtz au mkenye kikiwaka sote tutakwenda na maji mpaka mkuu wa nchi ataingia mitini usione hao mapolis wetu wanakuwana mikwala na kuzunguka na magari barabarani vita vikija tz wote watakimbia hata wewe huto post kitu JF
 
@Manyerere Jackton nenda na wewe ukafe kishujaa! mnaniboa sana wabongo mnavyochochea huu ugomvi! ndugu zetu wanakufa, eti mnasema wamekufa kishujaa, kishujaa? "kishujaa my ass" kwanini na wewe usiende ukafe kishujaa!

Ukifa wakati ukiwatetea wanyonge wenzako ni thawabu kubwa. Mungu akipenda tutaushuhudia ukombozi wa Wacongo kabla ya kufa kwetu.
 
Mkuu mtazamo wako ni kama wangu kwa asilimia mia moja. Historia inaonyesha jinsi Kenya ilivo nufaika na jumuiya ya Africa Mashariki iliyo vunjika mwishoni mwa miaka ya 70.

This time wa Tz tuko makini zaidi na tunaenda step kwa step maana tuliisha umwa na nyoka nao hawataki. Naipenda DRC si kwa sababu nna interst la hasha kwa sababu nawahurumia kina mama na watoto wanao teseka kila kukicha sababu ya madini amabayo hata kidogo hayawafaidishi, ni vilio tu kila kukicha kisa ni utajiri alio wapa Mwenyezi Mungu.

JK plz fuata ushauri wa huyu mleta mada. Tz wil be more proud kudeal na wacongo kuliko hawa ma war mongers. Bandari zetu zina kazi za kutosha tu kwa DRC pekee kuliko ukijumlusha Rwanda, Burundi na Uganda.

Wahurumieni raia wa Congo plz, wamelia vya kutosha............after all JK senior ( Nyerere) alishaanza hivo JK junior (Kikwete) malizia. Tutawakomboa wa Africa. ......tunaweza
 
hahaa rutajumbu.... nshasahau, sikiliza ww mrwanda na ujifunze, kenyata karekebisha majirani zake somalia ndo katulia sasa anabase kwenye bizines, ww yakuwashia nn tukirekebisha congo nasi tusettle huh? learn from us & kenyans y'all tutsis, make peace wit yo neighbour so that u make a fair & prosperous busines, nyinyi na kiongozi wenu hamkuwaza hilo, mkadhani mtapora forever, za mwizi 40, mumekamatwa, sasa hakuna haja ya kutucompare na kenya eti bcoz wamebase kwnye biashara nasi tuige mfano, yule ana majirani wenye amani kusini kaskazini magharibi na mashariki,
about kagera walohamia kule kulikuwa na mbwa mwitu amongst kondoo, sasa kama unavojua tena samaki mmoja akioza inakuwaje,

mwandishi manyerere big up sana ndugu endelea na kazi yako ilotukuka, tz na wa tz kwanza mengine badae.
 
Back
Top Bottom